Hiyo ndio maana ya proxy wars hata vita ya Armenia Vs Arzebeijan walioshangilia ni Uturuki ilihali hawakuwa Frontline!! ama vita ya Syria inayosifiwa ni Urusi kwamba imemshinda US licha ya kwamba hakuna Wanajeshi wa marekani huko Syria physically.
All out war siku hizi ni chache sana nyingi ni proxy lakini mwisho wa siku ndio zinaamua Mshindi hata kama umepeleka askari buku pekee.
Hata Tanzania huwa tunajisifia Kuzima mapinduzi Burundi, Seychelles, Comoros n.k ila je zilikua all out war? But we're still proud sababu technically tulishinda vita whether kwa askari 10 au 100.
2. Yes objective ni kumlinda lakini ukisema ni mji mkuu pekee hapana. Majeshi ya wageni yalikuwepo kuanzia Pweto na Kasai huko kusini mpaka Province Equator kaskazini hadi Bas Congo province huko magharibi na huko kote kulikua na engagement dhidi ya Kagame.
3. Kusema Angola ilikua na vita na waasi wa UNITA sio kisingizio hata Rwanda ilikua inapambana na FDLR, Burundi nayo kulikua na waasi, M7 naye alikua na waasi huko kaskazini na kasese n.k in fact Rwanda walitwangana na Uganda wakiwa katikati ya vita na Kinshasa!! Ila nguvu haikupungua na zaidi Uganda alipigwa in both battles.
Kusema haya kwa udogo wao ule bila kuwa na air cover walionyesha ujasiri wa hali ya juu, so hawako overrated ila they earned their status.

Mkuu, juhudi za Tanzania ktk kuzima mapinduzi huko Burundi, Comoro na kwingineko ni kukosea kuziita ‘Vita’ tutakuwa tunapoteza maana ya vita mkuu kwa sababu kuu moja, huko tuendako kuzima mapinduzi hatuendi pigana na jeshi zima la nchi hiyo, bali sehemu tu ya askari waloamua kuasi, hivyo si vita. Tanzania vita tulikuwa nayo mwaka 1977 dhidi ya Uganda. Pia mbali na kushinda machungu tuliyaona.
Ukirejea tena nilichoandika awali sikusema ni ‘Mji mkuu pekee’ nilisema focus kubwa ilikua huko, na hiyo haikuwa na maana kuwa walienda Kinshasa tu.
Bado naamini Rwanda wako overrated, Ndiyo walifanikisha kwa nafasi kuwa ktk kuipata Congo hii tuionayo leo. sababu tukiangalia Military objectives zao walizotazamia kuzikamilisha Congo si zote zilitimia pia napata ukakasi kuziita juhudi zao kuwa zilishindwa ila ni ukweli kwa kiasi kikubwa zilishindwa hiki ndicho kinanfanya nichelee kuipa Rwanda hadhi ya kana kwamba ni ‘invincible’ au kuiona kwa hadhi kubwa kama inavyooneshwa na waandishi kadhaa upande wa kijeshi.
Kumfurusha Mobutu walifanikiwa.
Kutwaa ardhi ya Congo hawakufanikiwa japo waliendelea kukwapua maliasili zake.
Kuongeza usalama mpakani mwao na Congo ili kuwaweka mbali interahamwe walifanikiwa.
Kuwa na ushawishi ndani ya Congo hawakufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Mwanzoni tu wakati Rwanda, Uganda na L. Kabila wanafanya oparesheni kumfurusha Mobutu na mpaka walipofanikiwa Rwanda alikua na ushawishi mkubwa ndani ya Congo kiasi hata Millitary chief of staff wa jeshi la L.Kabila alikuwa ni Mnyarwanda James Kabare, askari wa Rwanda pamoja na vikundi vinavyoungwa mkono nao walikuwa wakizunguka Kinshasa... wakati wote huo Rwanda waliweza ingia, toka na kufanya chochote ndani ya Congo mpaka alipotimuliwa bwana Kabare julai 1998.
Mwanzoni Vita vya pili vya Congo vya wenyewe kwa wenyewe Rwanda waliishika
karibu Congo yote, si mashariki si Magharibi. Waliweza kuviunganisha vikundi kadha wa kadha kupigana upande wao.
Hayo yote yaliwezekana kabla ya kuingia Angola na askari wao wazoefu, Zimbabwe na jeshi lao la anga takatifu, Sudan, Libya, Chad na Namibia.
Dhahiri kabisa askari wachache wa Angola walivirudisha nyuma vikundi na jeshi la Rwanda kutoka maeneo ya Magharibi mwa Congo, jeshi la Zimbabwe likavirudisha nyuma vikosi vilivyokuwa karibu kuizingira Kinshaza, Zimbabwe pia walifanya kazi nzuri kuvuruga mpangilio wa jeshi la Rwanda na wanamgabo wake kwa mashambulizi ya Anga hasa mashariki mwa Congo.
Mwisho nasistiza kuwa Rwanda walifanya nafasi kubwa, lakini si sawa kuichorea picha kuifanya kuwa ‘invincible’ machoni pa wengi hasa watanzania. Rwanda walinufaika sana na uwepo wa watu wa makabila yao mashariki mwa Congo, wakanufaika na madudu ya Mobutu yaliyowafungulia njia kuingia ndani ya Congo, wakanufaika na ukarimu wa Kabila kuwakaribisha, ikiwa Rwanda wakaingia vitani ktk mazingira tofauti kama ya Kenya au Tanzania ambako hakuna mazingira sawa na Congo basi jeshi la Rwanda litadhalilika sana.