DRC: Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23

DRC: Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23

Tuwe makini nchi yetu isijikute inaingia vita na tusiowajua sisi huku tukifikiri ni Rwanda! Russia ilipoivamia Ukraine haikujua kama itapambana na US na nchi za EU mpaka leo.
Natamani nchi yetu iendelee kuwa ya Amani,kama vipi wanajeshi wetu wajitoe katika kikosi cha kulinda amani huko Kongo warudi nyumbani.

Mkuu kama unaamini Russia hakujua kama atapambana na US na EU basi wewe ni mweupe sana.

Huwezi kuanzisha vita bila kufanya calculations za kutosha
 
Hayupo overrated jamaa aliwa face head-on Angola na Zimbabwe huko Katanga muda huo huo akipigana na Uganda huko Kisangani. Sio rahisi kwa nchi iliyokua umetoka vitani mwaka 1 nyuma kupambana na majeshi ya nchi karibu 7. Sasa miaka 20 baadae unadhani nguvu yake imekua mara ngapi?? As much tutampiga ila damage inaweza kuwa mara mbili haswaa kama M7 ataingia upande wake.
Mkuu Rwanda kwa uchumi wake sio rahisi kupigana na mataifa Saba , ila kilichowasapoti Ni kwamba walikuwa wanasaidiwa na USA government kipindi kile Cha bill cliton, na ndio waliwapasapoti.
1. Training
2. Weapons
3. Strategies
4. Equipment
Na 5. financial.
Na pia bindi wanapigana walikuwa wanachuka na madini pia.
Upo ushaidi rwanda ilipewa $ 1 billion na USA kuwasapoti kivita.
 
M 23 imewajeruhi wanajeshi wetu huko Kivu ya Kaskazini.

Ifahamike m23 ni wahuni wanaoungwa mkono na Serikali ya Kigali na ikumbukwe wahuni hao m23 kipindi cha Kikwete tuliwatwanga hali iliyopelekea mgogoro mkubwa wa kidipromasia baina ya Serikali ya Kikwete na Serikali ya Kigali.

Sasa baada ya Serikali ya Samia kuingia madarakani wahuni hao wamerejea kwa nguvu pengine wakiamini Samia hawezi kuwafanya lolote.Tusikubali aslani!

Tuwashughulikie hao wahuni kabla hawajaleta mgogoro mkubwa ndani ya Kanda yetu na Serikali ya Kigali ionywe wazi iache kuwakumbatia hao chawa wao.

Tusimchekee Kagame kwa sababu si mtu mwema hata kidogo.

Mzee Kikwete hakuwa mjinga ku deal naye kibabe huyo mwana- hizaya mpenda vya bure.

=====

Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23 DRC​

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, FARDC, limetangaza kuwa wanajeshi watatu wa Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO wamejeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia ngome yao iliyopo Rutshuru.

MONUSCO imethibitisha kuwa wanajeshi wake watatu wamejeruhiwa na kupelekwa kutibiwa katika hospitali ya mjini Goma uliopo mashariki. Katika tangazo hilo jeshi la serikali ya Congo limesema mmoja wa wanajeshi hao amejeruhiwa vibaya.

MONUSCO inasema kuwa wanajeshi hao wamejeruhiwa katika shambulio lililofanyw na wapiganaji wa M23 katika ngome yao iliyopo ivukatika eneo la Shangi -Rutshuru.

Kundi la M23 linasema kuwa majeshi ya FARDC na na MONUSCO ndio waliofanyanya mashambulio kwanza dhidi yao katika ngome yao iliyopo katika eneo la Jomba Jumatatu.

Hii inakuja wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya nne mfulurizo kati ya pande hizo yaliyoibuka baada ya mapigano hayo kusitishwa kwa muda wa wiki mmoja- mapigano yanayoendelea katika eneo la Rutshuru katika Kivu ya Kaskazini.

MONUSCO ilitangaza kuwa imo katika mapigano ikisaidia upande wa jeshi la Congo FARDC linalopigana na wapiganaji wa M23.

Tanzania ina wanajeshi zaidi ya 800 katika jeshi la MONUSCO kilichopo Mashariki mwa DRC.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano usiku, jeshi la DRC, FARDC linaishutumu Rwanda kutuma kikosi chake maalum cha wanajeshi 500 kuwasaidia wapiganaji wa M23, likisema kuwa walikuja wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi ya kijani kibichi na nyeusi.

Serikali ya Rwanda kwa imekuw aikikana mara kwa marakuwa inawasaidia M23, ikisisitiza kuwa tatizo lao liko ndani ya nchi yao wenyewe ya DRC.

Kikundi cha M23 Jumatano pia kilitoa tangazo kikiishutumu serikali kwa ‘’kuchagua njia ya vita’’, kwa vikosi vyake kushirikiana na wanajeshi wa MONUSCO na wapiganaji wa kundi linaloshutumiwa na Rwanda kufanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 la FDLR kuwashambulia.

Tangazo hil la M23linasema: “Kuchagua vita kwa serikali ya Congo badala ya kuchagua mazungumzo ya amani, ni tatizo katika kurejesha amani katika mashariki mwa DRC”.

Wakati huo huo, jeshi la DRC- FARDC limetangaza kuwa maazimio yakikao cha wakuu wa majeshi kilichofanyika Goma ya kubuni kikosi maalumu cha kupigana na makundi ya wanamgambomashariki mwa Congo.

Yatawasilishwa mbele ya kikao cha wataalamu wa masuala ya kijeshi na wakuu majeshiitakayofanyika kati ya tarehe 15 na 19 mwezi huu mjini Nairobi Kenya, kabla ya kuidhinishwa na maraisi wa Kanda.

Chanzo: BBC
Kagame haminiki.
 
Mara ya mwisho majeshi ya Rwanda na Uganda kupigana wakiwa Congo ilikua Ni eneo la Kisangani mwaka 2002.
Sio kweli... hufatilii tu. Watu walitwangana huko Mashariki ya Congo, wakafungiana hadi mpaka. Mwaka huu ndo wamesuluhisha
Screenshot_20220610-193407.png
 
Kagame ni kirusi ndani ya EAC. Siku ile tuliyomkaribisha EAC ndiyo siku tuliyokaribisha matatizo.
Tz nasikia walipiga kura ya kumkataa ila majinga kadhaa yalijifanya kutazama fursa za kiuchumi yaka waruhusu yajiunge na EAC
 
Mara ya mwisho majeshi ya Rwanda na Uganda kupigana wakiwa Congo ilikua Ni eneo la Kisangani mwaka 2002.
Sio kweli... hufatilii tu. Watu walitwangana huko Mashariki ya Congo, wakafungiana hadi mpaka. Mwaka huu ndo wamesuluhisha. Hiyo picha umeweka hapo ndo walikuwa wameenda kusuluhisha. Do your home work pleaseView attachment 2256677
 
Madini mkuu, DRC inategemea hizo Kivu zote mbili kwa survival yake maana huko western Congo hakuna rasilimali yoyote ya maana kulinganisha na Eastern.

Mwaka 1997 wangeweza ichukua kama sio Kabila kuwa mkali na kuwatimua; otherwise wangeigawa pasu kwa pasu.

Na walipotaka kuichukua 1998 walizingirwa na majeshi ya Angola na Zimbabwe, Namibia n.k hivyo ikawa ngumu kuziteka moja kwa moja.
mkuu Western drc kukatwa Ni ngumu sana, na ndo maana hata banyamulenge wanaoandama huko ulaya na USA wanasema wao Ni wakongo wanajua kukata Ni ngumu.
Kikundi Cha m23 battle yao inapiga Eastern huku mpakani mwa Rwanda na kidogo Uganda,
Na Mara nyingi tuu hua wanashidwa mapambana, wakishidwa wanapata urahisi was kukimbia.
Na Ni rahisi kwao kupata backup kutoka Kigali, ikiwepo askali na vifaa.
Na ndo maana hawaendi deep Sana Sana coz wakishidwa Ni rahisi kukamatwa na kukosa backup.
WhatsApp-Image-2022-05-28-at-23.56.32.jpeg

Hawa Ni wanajeshi wa rwanda walikamatwa ndani ya congo km 20 kutoka mpaka, walikamatwa na wanakijiji mwezi uliopita Kama 2 weeks zimepita Sasa.
 

Attachments

  • arton167063.jpg
    arton167063.jpg
    38.9 KB · Views: 9
Kwa Jeshi lipi walilonalo DRC? In fact M23 Ina malipo na silaha nzuri kuliko Jeshi la kitaifa!! So hao Wanajeshi wa DRC hawana morale ya kupigana wakikutana na waasi wapo tayari wakimbie kuliko kuuawa bila faida yoyote.

So hapo kilichopo either watimuliwe waende Rwanda/Burundi/Uganda kama enzi za Kabila Senior, ama wapewe Jimbo moja wajazwe wote humo then iwe nchi huru ama iende Rwanda n.k hapo ndio vita itaisha ila otherwise hiyo vita ni ya tokea miaka ya 90 na itaendelea mpaka siku ijitenge
Na sio rahisi watu watoke taifa jingine waje kuwapa msaada Kama nyinyi wenyewe hamko motivate na kupigana,
HAO MUNISCO wako huko kwa ajili ya kipato tuu, sio rahisi kuwa na morali ya kupigana.
Si unakumbuka UN peace keeping wa nchi ya MALI walikuwa wanaondoka wenyewe kwa sababu ya mashambulizi yalikuwa Ni mengi toka kwa jihad.
 
Kwani EA Kuna majeshi mkuu?Nachekaga sana nikiona nchi kama Uganda eti ndio inaongoza kwa Nguvu za kijeshi(kwa upande wa anga) kisa Ina ndege 6 zile Sukhoi SU-Mk30.Yaani ndege 6 tu,hahahah.Nikawa nacheki nchi Kama Ukraine mpk Sasa zimepigwa ndege zake zaidi ya 100,bado ma drones,maelfu ya vifaru etc .Sijajaribu kuzilinganisha nchi za EA vs Ukraine

Conclusion yangu Ni Kwamba hizi nchi za Kiafrica Zina mizaha hapa toa nchi Kama Tunisia,Algeria,South Africa,Misri hizi nchi nyingine zilizobaki zingepeleka Nguvu zao kwny kulima na kuondoa umaskini tu lkn Kati Yao wote wanafanana fanana kiuwezo tu.Nothing to Bragg about
Mkuu nilitaka kusema Nigeria ina nguvu ya jeshi nikakumbuka ,
Jihad, Boko Haram waliwatoa jasho Sana Sana mapaka kesho
😃😃😃😃
 
hahahahaha,cjui nisemaje, lakini M23 wako kulinda au kuzuia FDLR, wasiwe na nguvu,na wasifikie malengo yao ya kuangusha utawala wa kigali .

FDLR wanalengo la kurudi rwanda km nyumbani.na pia kuondoa utawala wa kigali

Kigali inachofanya ni kuonesha kwamba drc wamewahifadi maadui zangu.,hawezi peleka RDF ktkardhi ya congo. Ndo wakatengeneza ghost army wakatibue mipango yao. Mengine yanaendelea ni mengi huko
Kagame anasema kuwa Congo inawasaidia waasi was kihutu, na Ni madai ambayo haina ushaidi wowote, ila Ni kwamba hao wahutu wapo wengi wengi tuu huko drc na sio FDLR pekee yao vipo vikundi vingi Kama FLN na vingine.
Mimi siamini Kama FDLR kwa Sasa wanao uwezo wa kumpindua kagame , huo uwezo 100% hawana kabisa, kwa kawaida kikundi Cha waasi kuwa na uwezo wa kupigana na serikari Ni ngumu Sana.
Na hata wakiungana still Ni ngumu Sana. Ni uwoga wake tuu kagame huo uwezo hawana.
Ila anahofu Kama wakija kusaidiwa Kama yeye alivyosaidiwa na Uganda na USA kutoa juvenile. Alisaidiwa kila KITU.
 
Kuwa na uwezo wa kupigana Vita inategemea na uchumi wako Kwanza , Rwanda iliweza Congo kupiga na nchi 7 coz ya kupata msaada kutoka USA, hata watu wa haki za binadamu wanazungumza, Mtafute YouTube mtu anaitwa KAMBALE MSAVULI, kwa Sasa wanaweza kuwa na uwezo coz wana experience kubwa japo inaweza kuwacost Sana kwenye ishu ya fedha ndo inaweza kuwa shida kwao kumbuka walipigana first Congo war 1996 to 1997 na second Congo war 1998 to 2003, na second ndo ilikuwa Vita mbaya Sana na vilipigwa 5 years na Ni nchi 7 kwa nchi Kama Rwanda Ni ngumu Sana kutokana na uchumi wao, na ule ulikuwa Ni Mkono wa USA.
 
Kuwa na uwezo wa kupigana Vita inategemea na uchumi wako Kwanza , Rwanda iliweza Congo kupiga na nchi 7 coz ya kupata msaada kutoka USA, hata watu wa haki za binadamu wanazungumza, Mtafute YouTube mtu anaitwa KAMBALE MSAVULI, kwa Sasa wanaweza kuwa na uwezo coz wana experience kubwa japo inaweza kuwacost Sana kwenye ishu ya fedha ndo inaweza kuwa shida kwao kumbuka walipigana first Congo war 1996 to 1997 na second Congo war 1998 to 2003, na second ndo ilikuwa Vita mbaya Sana na vilipigwa 5 years na Ni nchi 7 kwa nchi Kama Rwanda Ni ngumu Sana kutokana na uchumi wao, na ule ulikuwa Ni Mkono wa USA.
Hio inaitwa African world war muanzilishi Ni Paul kagame na ndo maana Tunaimuita African hilter ilichukua maisha karibu wakongo million 6 , Ni Kama Adolfo hilter alivyoanzisha Vita vya dunia na kuua wayahudi 6 million.
 
Sio kweli... hufatilii tu. Watu walitwangana huko Mashariki ya Congo, wakafungiana hadi mpaka. Mwaka huu ndo wamesuluhishaView attachment 2256677
Si kweli wewe ndio hufuatilii,weka source yako hapa kuonyesha Uganda imepigana na Rwanda.Rwanda ilizinguana na Uganda kwa Sababu ilikua inawatuhumu wana-support Waasi wa Rwanda walioko Huko Congo.

Narudia tena weka source yako hapa hata 1 tu kuonyesha Rwanda na Uganda walipigana Huko Congo.
 
Sio kweli... hufatilii tu. Watu walitwangana huko Mashariki ya Congo, wakafungiana hadi mpaka. Mwaka huu ndo wamesuluhisha. Hiyo picha umeweka hapo ndo walikuwa wameenda kusuluhisha. Do your home work pleaseView attachment 2256677
Narudia tena kusema Rwanda na Uganda hawajipigana Congo na Wala hio source uliyoweka Hakuna sehemu imesema walipigana huko Congo.

Weka source hata 1 tu kuonyesha walipigana huko Congo,hautapata source hata 1 kuonyesha hilo.
 
mkuu Western drc kukatwa Ni ngumu sana, na ndo maana hata banyamulenge wanaoandama huko ulaya na USA wanasema wao Ni wakongo wanajua kukata Ni ngumu.
Kikundi Cha m23 battle yao inapiga Eastern huku mpakani mwa Rwanda na kidogo Uganda,
Na Mara nyingi tuu hua wanashidwa mapambana, wakishidwa wanapata urahisi was kukimbia.
Na Ni rahisi kwao kupata backup kutoka Kigali, ikiwepo askali na vifaa.
Na ndo maana hawaendi deep Sana Sana coz wakishidwa Ni rahisi kukamatwa na kukosa backup.
View attachment 2256679
Hawa Ni wanajeshi wa rwanda walikamatwa ndani ya congo km 20 kutoka mpaka, walikamatwa na wanakijiji mwezi uliopita Kama 2 weeks zimepita Sasa.
Hayo Ni mambo ya kawaida tu kwny medani boss,hata mwaka Jana wkt mahusiano ya Rwanda na Uganda yakiwa yamezorota mbaya kabisa wanajeshi wa Rwanda walimkamata mwanajeshi wa Uganda ndani ya mipaka ya Rwanda na akiwa na silaha zake.Mwisho wa siku aliachiwa huru akarud kwao.
Screenshot_20220610-211754.jpg
Screenshot_20220610-211811.jpg
Screenshot_20220610-211818.jpg
Screenshot_20220610-211831.jpg
Screenshot_20220610-211841.jpg
Screenshot_20220610-211856.jpg
Screenshot_20220610-211904.jpg
 
Mkuu nilitaka kusema Nigeria ina nguvu ya jeshi nikakumbuka ,
Jihad, Boko Haram waliwatoa jasho Sana Sana mapaka kesho
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Hahah kwa kweli u-superpower wa Nigeria kwny mambo ya kijeshi hapa Africa nilisha-udharau sana sababu ya hao al-shababu.[emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom