DRC: Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23

DRC: Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23

Mkuu kama unaamini Russia hakujua kama atapambana na US na EU basi wewe ni mweupe sana.

Huwezi kuanzisha vita bila kufanya calculations za kutosha
Calculation zipi wakati hazikwenda sawa? Russia ilijua kama itakutana na upinzani mkali namna hiyo?
 
Sio rahisi, Rwanda wana intelligence madhubuti na iliyoenea sana East Africa. Kuingia kwenye vita ya moja kwa moja na Rwanda na kutarajia kuwapiga kirahisi ni kujidanganya. Usiongopewe na udogo wa eneo lao.

Kwani kipindi cha Kikwete hao m23 walifanywa nini?!

Huyo kagame intelijensia haikuwepo
 
Na wanapigwa hukoo, poleeeeh [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kama hujui kitu bora usiongee, yaani unaongea ujinga halafu wajinga wenzio wanakusapoti! Hujui vita ni nini ,hujawahi kushika silaha, hujawahi kwenda vitani! Halafu unaropoka mtandaoni watu wakuone unajua sana!
Mpuuzi wahedi!!
 
Porojo tu sioni facts ulizileta, kuishi uraiani ndio kujua uwezo wa kijeshi?? Ongelea missions za Manqueal De Zombo huko Angola ama Kisangani II n.k ndio utaelewa uwezo wa kijeshi wa Rwanda, sio silaha au ukubwa wa Jeshi ndio Una determine ushindi.
mawazo ya kipumbavu na sifa kijinga za wanyarwanda, tendeni haki kwanza nchi kwenu muache kuwabagua na kuuwa wahutu. Mission gani hizo za kisangani hakuna kipya wala cha jabu chochote. Mlikutana na wachovu tu nyie maskini mna nguvu gani kijeshi bana? unatusumbua hapa na misifa ya kijinga ya kitusi.Unapoteza muda wangu sijidili tena na wewe wala sitakujibu tena utumbo wako kijinga na kuoenda misifa wakati maskini tu nyie. mmekalia kuiba tu Congo
 
Mkuu kwenye takwimu huwa tunafanya estimations kupitia previous data. Mfano kama Rwanda alipambana na hizo nchi tajwa ilihali katoka kwenye civil war na umaskini mzito Ndio tuna estimate miaka 20 baadae atakua na nguvu mara dufu ya pale irrespective ya hizo nchi zingine zilivyojipanga.

Uchumi sio issue maana wakati wa vita walipora sana Mbao na madini ku fund vita na hapo lazima watasaka support ya kifedha kutoka Kwa washirika wake n.k so it can be sorted.

Tanzania inaweza kuwa vizuri mara 100 ila hoja ni kwamba Rwanda sio wadhaifu that's all I'm saying.
Kwenu ni Ngara sehemu gani Mkuu?
 
Tatizo lenu mnakuwa too theoretical, hata nikikuiliza utoe ushahidi wa kwanini JWTZ ni bora kuliko RDF najua hauna. Mimi naongelea RDF sababu ya milestones zake, kuanzia campaign za kule Uganda, hadi kuiteka Rwanda mpaka kuivamia DRC mpaka kujipenyeza Angola na Jamhuri ya Afrika ya Kati hizo sio milestone ndogo tena ndani ya mwaka mmoja tu toka watoke kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Recently tu wamezima magaidi wa Mozambique!!

Na ambacho hufahamu nchi inayoongoza kuwa na majeshi kwenye foreign land na peacekeeping mission ni Rwanda. Licha ya udogo wa jeshi imeweza kusambaa nchi nyingi sana mpaka Leo so tusidharau sababu hatuna taarifa za kutosha.

Sasa kwa faida ya mjadala na wewe njoo na counter arguments for JWTZ maybe mission za Seychelles, Darfur n.k ila sio kuita wengine wanachekesha huku hauna milestone hata moja ya kushare hapa.
Nedna kwenu sasa TZ ynafanya nini? kaka na wazee wa mission nyingi za nnje wababe wa vita Africa hahahahahahahahah
 
Tatizo lenu mnakuwa too theoretical, hata nikikuiliza utoe ushahidi wa kwanini JWTZ ni bora kuliko RDF najua hauna. Mimi naongelea RDF sababu ya milestones zake, kuanzia campaign za kule Uganda, hadi kuiteka Rwanda mpaka kuivamia DRC mpaka kujipenyeza Angola na Jamhuri ya Afrika ya Kati hizo sio milestone ndogo tena ndani ya mwaka mmoja tu toka watoke kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Recently tu wamezima magaidi wa Mozambique!!

Na ambacho hufahamu nchi inayoongoza kuwa na majeshi kwenye foreign land na peacekeeping mission ni Rwanda. Licha ya udogo wa jeshi imeweza kusambaa nchi nyingi sana mpaka Leo so tusidharau sababu hatuna taarifa za kutosha.

Sasa kwa faida ya mjadala na wewe njoo na counter arguments for JWTZ maybe mission za Seychelles, Darfur n.k ila sio kuita wengine wanachekesha huku hauna milestone hata moja ya kushare hapa.
Ningekusimulia nilichoambiwa na ndugu yangu ambaye walienda kutrain jeshi jipya la Congo baada ya Kabila Senior kushika madaraka, hao jamaa zako walijaribu kujipenyeza yaliwakuta ya kuwakuta wanaijua habari ya JW vizuri kabisa sio kwa kusimuliwa bali kwa vitendo.
 
Hayupo overrated jamaa aliwa face head-on Angola na Zimbabwe huko Katanga muda huo huo akipigana na Uganda huko Kisangani. Sio rahisi kwa nchi iliyokua umetoka vitani mwaka 1 nyuma kupambana na majeshi ya nchi karibu 7. Sasa miaka 20 baadae unadhani nguvu yake imekua mara ngapi?? As much tutampiga ila damage inaweza kuwa mara mbili haswaa kama M7 ataingia upande wake.

Hebu inyooshe hii habari vizuri Mkuu. Nikiri wewe unafahamu vizuri hizi habari.
 
Ningekusimulia nilichoambiwa na ndugu yangu ambaye walienda kutrain jeshi jipya la Congo baada ya Kabila Senior kushika madaraka, hao jamaa zako walijaribu kujipenyeza yaliwakuta ya kuwakuta wanaijua habari ya JW vizuri kabisa sio kwa kusimuliwa bali kwa vitendo.
😄😄 Rwanda wao wanajua lengo la FARDC Ni kuwaharibia mkutano wao wa CHOGM,Sasa tusubiri CHOGM ipite(na hii Ni endapo tu Kama Rwanda itaweza kuvumilia bila kumwaga Moto kipindi hiki hiki) tuone Ni Nani ataanza kuomba cease fire,nitaku-tagg.
 
Kama hujui kitu bora usiongee, yaani unaongea ujinga halafu wajinga wenzio wanakusapoti! Hujui vita ni nini ,hujawahi kushika silaha, hujawahi kwenda vitani! Halafu unaropoka mtandaoni watu wakuone unajua sana!
Mpuuzi wahedi!!
Mbona umepanic?
 
Mkuu, juhudi za Tanzania ktk kuzima mapinduzi huko Burundi, Comoro na kwingineko ni kukosea kuziita ‘Vita’ tutakuwa tunapoteza maana ya vita mkuu kwa sababu kuu moja, huko tuendako kuzima mapinduzi hatuendi pigana na jeshi zima la nchi hiyo, bali sehemu tu ya askari waloamua kuasi, hivyo si vita. Tanzania vita tulikuwa nayo mwaka 1977 dhidi ya Uganda. Pia mbali na kushinda machungu tuliyaona.

Ukirejea tena nilichoandika awali sikusema ni ‘Mji mkuu pekee’ nilisema focus kubwa ilikua huko, na hiyo haikuwa na maana kuwa walienda Kinshasa tu.

Bado naamini Rwanda wako overrated, Ndiyo walifanikisha kwa nafasi kuwa ktk kuipata Congo hii tuionayo leo. sababu tukiangalia Military objectives zao walizotazamia kuzikamilisha Congo si zote zilitimia pia napata ukakasi kuziita juhudi zao kuwa zilishindwa ila ni ukweli kwa kiasi kikubwa zilishindwa hiki ndicho kinanfanya nichelee kuipa Rwanda hadhi ya kana kwamba ni ‘invincible’ au kuiona kwa hadhi kubwa kama inavyooneshwa na waandishi kadhaa upande wa kijeshi.

Kumfurusha Mobutu walifanikiwa.
Kutwaa ardhi ya Congo hawakufanikiwa japo waliendelea kukwapua maliasili zake.
Kuongeza usalama mpakani mwao na Congo ili kuwaweka mbali interahamwe walifanikiwa.
Kuwa na ushawishi ndani ya Congo hawakufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Mwanzoni tu wakati Rwanda, Uganda na L. Kabila wanafanya oparesheni kumfurusha Mobutu na mpaka walipofanikiwa Rwanda alikua na ushawishi mkubwa ndani ya Congo kiasi hata Millitary chief of staff wa jeshi la L.Kabila alikuwa ni Mnyarwanda James Kabare, askari wa Rwanda pamoja na vikundi vinavyoungwa mkono nao walikuwa wakizunguka Kinshasa... wakati wote huo Rwanda waliweza ingia, toka na kufanya chochote ndani ya Congo mpaka alipotimuliwa bwana Kabare julai 1998.
Mwanzoni Vita vya pili vya Congo vya wenyewe kwa wenyewe Rwanda waliishika karibu Congo yote, si mashariki si Magharibi. Waliweza kuviunganisha vikundi kadha wa kadha kupigana upande wao.

Hayo yote yaliwezekana kabla ya kuingia Angola na askari wao wazoefu, Zimbabwe na jeshi lao la anga takatifu, Sudan, Libya, Chad na Namibia.

Dhahiri kabisa askari wachache wa Angola walivirudisha nyuma vikundi na jeshi la Rwanda kutoka maeneo ya Magharibi mwa Congo, jeshi la Zimbabwe likavirudisha nyuma vikosi vilivyokuwa karibu kuizingira Kinshaza, Zimbabwe pia walifanya kazi nzuri kuvuruga mpangilio wa jeshi la Rwanda na wanamgabo wake kwa mashambulizi ya Anga hasa mashariki mwa Congo.

Mwisho nasistiza kuwa Rwanda walifanya nafasi kubwa, lakini si sawa kuichorea picha kuifanya kuwa ‘invincible’ machoni pa wengi hasa watanzania. Rwanda walinufaika sana na uwepo wa watu wa makabila yao mashariki mwa Congo, wakanufaika na madudu ya Mobutu yaliyowafungulia njia kuingia ndani ya Congo, wakanufaika na ukarimu wa Kabila kuwakaribisha, ikiwa Rwanda wakaingia vitani ktk mazingira tofauti kama ya Kenya au Tanzania ambako hakuna mazingira sawa na Congo basi jeshi la Rwanda litadhalilika sana.
Laurent kabila kosa jingine alilolifanya BAADA ya kuchukua nchi alianza kuchukua watu wa kabila lake na kuwaingiza kwenye jeshi la taifa, KITU hiki kiliwachukiza watu wengi kule Congo nilimsikia James kaberebe aliongea kwenye documentary ya INVASION OF CONGO YouTube ipo.
Kumbuka kulikuwa na kundi kubwa la uasi liliitwa RCD ilikuwa linakikosi Cha Askari 40,000 mwaka 1998 second congo war
Second Congo war makabila mengi yalikuwa yakimpinga kabila kutoka na kuwaweka watu wake kwenye jeshi Kama nilivyosema.
Na ndio maana alizialika nchi nyingi kwenda kumpa support.
 
Yes mkuu,
Rwanda lilikuwa Ni jeshi la kitutsi Tena walikuwa Ni waasi RPA( Rwanda Patriotic Army) wale walikuwa hawalipwi walikuwa wanajitolea kutoka rwanda civil war mpaka Congo war. RPA walikuwa wapo 26,000. Nilisikia kutoka kwa JAMES MUNYANDINDA kagame former bodyguard. Na pia BAADA ya kuchukua nchi kutoka Rwanda alichukua Genocide survivor akawapa mafunzo na wengi wake aliwapeleka congo Sasa hii inamaana waliongeza idadi. Na hata kwenye first Congo hawakuwa pekeao kumbuka kulikuwa na Uganda, Baadhi ya wanajeshi wa kitutsi kutoka Burundi, na Banyamulenge na waasi wa Congo senior kabila. So hawakuwa pekeao.
Tena kwenye second Congo war
Kulikuwa majeshi ya rwanda ya kitutsi na vikundi vya uhasi vya Congo hasa Banyamulenge na Askari wa mabotu seseko,
Nimewahi kumsikiliza Laurent nkunda batwale alisema kuwa alikuwa na vijana zaidi ya 10,000 kwenye second Congo war. Na alikuwa upande wa rwanda, na vikundi vilikuwa Ni vingi na idadi ya Askari wa rwanda Ni kweli walikuwa wengi.
Ila Ni KWAMBA WANAMOYO WA KUPIGANA HASA. Japo walikuwa wengi ila walishidwa kukimaliza kikosi Cha Angola na Zimbabwe ambavyo viliwasumbua Sana.
zitto junior
Dah !.. una ufahamu mzuri Sana wa siasa za maziwa makuu...👊👊👊
 
Back
Top Bottom