DRC: Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23

Suluhisho labda wamege kipande Cha kivu na Bunia kiende Rwanda ama wawatimue Jamii zote za Kinyarwanda huko DRC otherwise M23 ni muendelezo tu wa RCD-Goma na vikundi vingine vya Rwanda huko DRC.
Sasa kwa nini hao Banyamulenge wanashindwa kujimegea hivyo vipande vya Kivu & Bunia maana backup wanayo kutoka kwa Rwanda,Uganda & mabeberu mbona south Sudan waliweza
 
Sasa nimeelewa. Hata wale vijana wetu waliuawa na Kigali
 
Sasa kwa nini hao Banyamulenge wanashindwa kujimegea hivyo vipande vya Kivu & Bunia maana backup wanayo kutoka kwa Rwanda,Uganda & mabeberu mbona south Sudan waliweza
Madini mkuu, DRC inategemea hizo Kivu zote mbili kwa survival yake maana huko western Congo hakuna rasilimali yoyote ya maana kulinganisha na Eastern.

Mwaka 1997 wangeweza ichukua kama sio Kabila kuwa mkali na kuwatimua; otherwise wangeigawa pasu kwa pasu.

Na walipotaka kuichukua 1998 walizingirwa na majeshi ya Angola na Zimbabwe, Namibia n.k hivyo ikawa ngumu kuziteka moja kwa moja.
 
Vp
Vipi 2012 na 2022 kipi kinawazuia halafu kwa nini DRC wanashindwa kupeleka askari wa kutosha huko ili kuwatawala hao wanyarwanda wa mchongo kwa mkono wa chuma mbona JK aliweza kupeleka askari wa kutosha kule mtwara mpaka akaweza kuihamishia gesi yote Dar
 
Acheni Kila lawama kuwapa wazungu? Hivi mfano Tanzania tulikua tunaingia mikataba ya kiuonevu kwani tulikua na vita au CIA walitushurutusha tusign Ile mikataba? Sasa nchi kama Congo kuporwa madini inahitaji vita au CIA??

Kipindi Cha Mobutu nchi ilitulia huko Kivu ikitokea vita basi asubuhi tu Mobutu ashatuma FAZ Kuizima!! Ila he madini yalikua hayaporwi?

Tatizo ni kukosa uongozi, kuendekeza ukabila, kukosa uzalendo n.k ndio vinarudisha nyuma DRC. Ukitaka kujua Hilo Harare na Luanda zilipeleka majeshi kumsaidia Kabila dhidi ya Kagame ila nao wakapewa migodi huko Katanga kufidia gharama za Vita!! Sasa unadhani hapo kulikua na beberu au hata hao wanaojiita wakombozi ni mafisadi tu wote??
 
Vita vimekuwa modernised siku hizi vifaru ni mzigo tuu siku hizi ni artillery, missiles na well trained infantry with help of drones.
[emoji1][emoji1] Kwamba vifaru ni mzigo sio?nenda kawaulize wale mercenaries Kule Ukraine waliokimbia Vita wanasemaje khs vifaru vya Warussi.Sniper hatari wa kutoka Canada aitwae Wali anakwambia mizinga inapigwa non-stop mwisho wa siku ameishia kupiga risasi 2 tu na kukimbia Vita [emoji1][emoji1][emoji1].
 
Kwamba majamaa ya Urusi yamegundua dawa ni kutuma missile tu hao masniper wataambulia vumbi na miripuko
 
M23,FDLR etc hivyo vikundi kufa Ni impossible vitaendelea kubadili majina na viongozi tu.Kwa sababu ya Ideology wanazoziamini bado ziko/zina-survive.
 
Sioni fact yoyote uliyoongea hapa, hizo story za Rwanda kuwa na intelejensia kali ndani ya Tz ni hoja unayoweza kuithibitisha au ni story za kusikia?

Kama ni hoja usiyoweza kuithibitisha basi na mimi ninao uwezo kwa kusema kwamba Tz ina intelejensia kali ndani ya Rwanda, na unapaswa usinibishie.

Rwanda hawezi kufanya lolote kwa Tz unless uwe ni Mnyarwanda unaeishi ndani ya Tz na umeamua kuleta ushabiki tu😄.

Kwa hapa EAC jeshi la kuipa presha Tz labda ni lile la Kenya.
 
Kwa Jeshi lipi walilonalo DRC? In fact M23 Ina malipo na silaha nzuri kuliko Jeshi la kitaifa!! So hao Wanajeshi wa DRC hawana morale ya kupigana wakikutana na waasi wapo tayari wakimbie kuliko kuuawa bila faida yoyote.

So hapo kilichopo either watimuliwe waende Rwanda/Burundi/Uganda kama enzi za Kabila Senior, ama wapewe Jimbo moja wajazwe wote humo then iwe nchi huru ama iende Rwanda n.k hapo ndio vita itaisha ila otherwise hiyo vita ni ya tokea miaka ya 90 na itaendelea mpaka siku ijitenge.
 
Vita ni experience na strategy hivi kuna Jenerali bongo ana track record ya James Kabarebe? Kenya Wana vifaa ila hawana strategy otherwise wasingekuwa weak hivyo.
 
Vita ni experience na strategy hivi kuna Jenerali bongo ana track record ya James Kabarebe? Kenya Wana vifaa ila hawana strategy otherwise wasingekuwa weak hivyo.
Hoja yangu ya msingi ni kwamba kuliko kuifikiria Rwanda kama babe kwa Tz ,ni bora uwafikirie hata Kenya (KDF).

Rwanda ni toothless mbele ya Tz.
 
Hebu tupeane taarifa Kenya imeshawahi kupigana Vita na jeshi la nchi ipi ukiachana na kukimbizana na wale Al-shabab?

Tangu niwaone KDF wakiiba chocolate kwny Ile Westgate Mall,baadae wakaenda Somalia wakaanza kuiba mkaa na kuuza [emoji1][emoji1] hua nawacheki tu nasema Hiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kagame ni kirusi ndani ya EAC. Siku ile tuliyomkaribisha EAC ndiyo siku tuliyokaribisha matatizo.

Mzee Moi alikataa sana kuwakaribisha watu wasiojielewa. Alisema ni ku import troubles in our lovely jumuiya. Kina mzee mkapa na mzee Mseven wakasema hawa ni ndugu zetu. Ona sasa wanavyosumbua. Saa hizi ni kuwapiga suspension tu.
 
Yapange majeshi ya EAC kutokana na nguvu zao kijeshi, kulingana na unavyofikiria tu (sitaki nikuombe ushahidi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…