DRC: Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23

M 23 imewajeruhi wanajeshi wetu huko Kivu ya Kaskazini.

Ifahamike m23 ni wahuni wanaoungwa mkono na Serikali ya Kigali na ikumbukwe wahuni hao m23 kipindi cha Kikwete tuliwatwanga hali iliyopelekea mgogoro mkubwa wa kidipromasia baina ya Serikali ya Kikwete na Serikali ya Kigali.

Sasa baada ya Serikali ya Samia kuingia madarakani wahuni hao wamerejea kwa nguvu pengine wakiamini Samia hawezi kuwafanya lolote.Tusikubali aslani!

Tuwashughulikie hao wahuni kabla hawajaleta mgogoro mkubwa ndani ya Kanda yetu na Serikali ya Kigali ionywe wazi iache kuwakumbatia hao chawa wao.

Tusimchekee Kagame kwa sababu si mtu mwema hata kidogo.

Mzee Kikwete hakuwa mjinga ku deal naye kibabe huyo mwana- hizaya mpenda vya bure.

=====

Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23 DRC​

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, FARDC, limetangaza kuwa wanajeshi watatu wa Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO wamejeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia ngome yao iliyopo Rutshuru.

MONUSCO imethibitisha kuwa wanajeshi wake watatu wamejeruhiwa na kupelekwa kutibiwa katika hospitali ya mjini Goma uliopo mashariki. Katika tangazo hilo jeshi la serikali ya Congo limesema mmoja wa wanajeshi hao amejeruhiwa vibaya.

MONUSCO inasema kuwa wanajeshi hao wamejeruhiwa katika shambulio lililofanyw na wapiganaji wa M23 katika ngome yao iliyopo ivukatika eneo la Shangi -Rutshuru.

Kundi la M23 linasema kuwa majeshi ya FARDC na na MONUSCO ndio waliofanyanya mashambulio kwanza dhidi yao katika ngome yao iliyopo katika eneo la Jomba Jumatatu.

Hii inakuja wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya nne mfulurizo kati ya pande hizo yaliyoibuka baada ya mapigano hayo kusitishwa kwa muda wa wiki mmoja- mapigano yanayoendelea katika eneo la Rutshuru katika Kivu ya Kaskazini.

MONUSCO ilitangaza kuwa imo katika mapigano ikisaidia upande wa jeshi la Congo FARDC linalopigana na wapiganaji wa M23.

Tanzania ina wanajeshi zaidi ya 800 katika jeshi la MONUSCO kilichopo Mashariki mwa DRC.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano usiku, jeshi la DRC, FARDC linaishutumu Rwanda kutuma kikosi chake maalum cha wanajeshi 500 kuwasaidia wapiganaji wa M23, likisema kuwa walikuja wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi ya kijani kibichi na nyeusi.

Serikali ya Rwanda kwa imekuw aikikana mara kwa marakuwa inawasaidia M23, ikisisitiza kuwa tatizo lao liko ndani ya nchi yao wenyewe ya DRC.

Kikundi cha M23 Jumatano pia kilitoa tangazo kikiishutumu serikali kwa ‘’kuchagua njia ya vita’’, kwa vikosi vyake kushirikiana na wanajeshi wa MONUSCO na wapiganaji wa kundi linaloshutumiwa na Rwanda kufanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 la FDLR kuwashambulia.

Tangazo hil la M23linasema: “Kuchagua vita kwa serikali ya Congo badala ya kuchagua mazungumzo ya amani, ni tatizo katika kurejesha amani katika mashariki mwa DRC”.

Wakati huo huo, jeshi la DRC- FARDC limetangaza kuwa maazimio yakikao cha wakuu wa majeshi kilichofanyika Goma ya kubuni kikosi maalumu cha kupigana na makundi ya wanamgambomashariki mwa Congo.

Yatawasilishwa mbele ya kikao cha wataalamu wa masuala ya kijeshi na wakuu majeshiitakayofanyika kati ya tarehe 15 na 19 mwezi huu mjini Nairobi Kenya, kabla ya kuidhinishwa na maraisi wa Kanda.

Chanzo: BBC
Poleni sana ndugu zetu Kwa UZALENDO mnaouonyesha kwetu na Africa nzima. Mungu awabariki na awaponye mrudie Hal zenu. Amen
 
Tuwe makini nchi yetu isijikute inaingia vita na tusiowajua sisi huku tukifikiri ni Rwanda! Russia ilipoivamia Ukraine haikujua kama itapambana na US na nchi za EU mpaka leo.
Natamani nchi yetu iendelee kuwa ya Amani,kama vipi wanajeshi wetu wajitoe katika kikosi cha kulinda amani huko Kongo warudi nyumbani.

Warudi Home Chap Idadi Yao Ni Kubwa Wapo 800

nani kawaambia mnatakiwa huko kama si kimbere mbere chenu? wenyeji wa huko wenyewe hawawataki huko, sibirini muanze kurejeshwa mkiwa kwenye ma jeneza……….
Lazima utakuwa umezaliwa JK akiwa madarakani. Uzalendo Bado unatakiwa ufundishwe Kwa vijana. Pole kwako.
 
Tuwe makini nchi yetu isijikute inaingia vita na tusiowajua sisi huku tukifikiri ni Rwanda! Russia ilipoivamia Ukraine haikujua kama itapambana na US na nchi za EU mpaka leo.
Natamani nchi yetu iendelee kuwa ya Amani,kama vipi wanajeshi wetu wajitoe katika kikosi cha kulinda amani huko Kongo warudi nyumbani.
issue sio kurudi home, sababu Leo no kwao Congo kesho kwetu, hao ni jirani zetu ,tusipokomesha hivi vitendo hao jamaa watazoea ni kudeal nao tu kama Panya road
 
Yapange majeshi ya EAC kutokana na nguvu zao kijeshi, kulingana na unavyofikiria tu (sitaki nikuombe ushahidi)
Kwani EA Kuna majeshi mkuu?Nachekaga sana nikiona nchi kama Uganda eti ndio inaongoza kwa Nguvu za kijeshi(kwa upande wa anga) kisa Ina ndege 6 zile Sukhoi SU-Mk30.Yaani ndege 6 tu,hahahah.Nikawa nacheki nchi Kama Ukraine mpk Sasa zimepigwa ndege zake zaidi ya 100,bado ma drones,maelfu ya vifaru etc .Sijajaribu kuzilinganisha nchi za EA vs Ukraine

Conclusion yangu Ni Kwamba hizi nchi za Kiafrica Zina mizaha hapa toa nchi Kama Tunisia,Algeria,South Africa,Misri hizi nchi nyingine zilizobaki zingepeleka Nguvu zao kwny kulima na kuondoa umaskini tu lkn Kati Yao wote wanafanana fanana kiuwezo tu.Nothing to Bragg about
 
Tunalinda amani. Hatuwezi kukaa tu hapa alafu mtaa wa pili kuna wahuni wanaua na kubaka waafrika wenzetu kwa maslahi ya mabwana zao wa huko ulaya, hatuwezi kamwe!
Hivi huko Congo kwanini miaka yote mnapasuliwa nyie tu(wanajeshi) wakati mapolisi wa nchi nyingi nao wapo?
 
Huu mgogoro wazungu wanafaidika nao sanaa...!!
 
Sio rahisi, Rwanda wana intelligence madhubuti na iliyoenea sana East Africa. Kuingia kwenye vita ya moja kwa moja na Rwanda na kutarajia kuwapiga kirahisi ni kujidanganya. Usiongopewe na udogo wa eneo lao.
Dah,kwamba Rwanda wanaweza kutuchapa??[emoji1][emoji1]

Basi tutakuwa kubwa jinga.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo mawazo ya CDM na wafuasi wake hayo?

Ndo maana nasema ni wachanga mno Bado kupewa Nchi.
Samia kafanya nini ambacho CHADEMA hawawezi? Kwamba Samia ana vigezo kuliko wanasiasa wote upinzani? Get serious.
 
hakuna kikundi kisicho na ufadhili au wafadhili.iwe wa wazi au wakificho,tatizo m23 wanataka kuangusha serikali? Kigali hapana, kinshansa ? hahahaha,hy ni ndoto na wala si lengo lao.
Lengo lao ni lipi Sasa?..je ni kupata tu 'attention' kutoka kwa viongozi wa Kinshasa kwamba bado wapo ?...

Au ni mkono wa nchi jirani tu (Rwanda) kuwakumbusha watawala wa Drc kwamba bado wana ushawishi huko mashariki ? ,hivyo maslahi yao yazingatiwe ?
zitto junior
Richard
 
Sioni fact yoyote uliyoongea hapa, hizo story za Rwanda kuwa na intelejensia kali ndani ya Tz ni hoja unayoweza kuithibitisha au ni story za kusikia?

Kama ni hoja usiyoweza kuithibitisha basi na mimi ninao uwezo kwa kusema kwamba Tz ina intelejensia kali ndani ya Rwanda, na unapaswa usinibishie.

Rwanda hawezi kufanya lolote kwa Tz unless uwe ni Mnyarwanda unaeishi ndani ya Tz na umeamua kuleta ushabiki tu[emoji1].

Kwa hapa EAC jeshi la kuipa presha Tz labda ni lile la Kenya.
"There are no facts, only interpretations " Nietzsche.
 
M 23 imewajeruhi wanajeshi wetu huko Kivu ya Kaskazini.

Ifahamike m23 ni wahuni wanaoungwa mkono na Serikali ya Kigali na ikumbukwe wahuni hao m23 kipindi cha Kikwete tuliwatwanga hali iliyopelekea mgogoro mkubwa wa kidipromasia baina ya Serikali ya Kikwete na Serikali ya Kigali.

Sasa baada ya Serikali ya Samia kuingia madarakani wahuni hao wamerejea kwa nguvu pengine wakiamini Samia hawezi kuwafanya lolote.Tusikubali aslani!

Tuwashughulikie hao wahuni kabla hawajaleta mgogoro mkubwa ndani ya Kanda yetu na Serikali ya Kigali ionywe wazi iache kuwakumbatia hao chawa wao.

Tusimchekee Kagame kwa sababu si mtu mwema hata kidogo.

Mzee Kikwete hakuwa mjinga ku deal naye kibabe huyo mwana- hizaya mpenda vya bure.

=====

Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23 DRC​

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, FARDC, limetangaza kuwa wanajeshi watatu wa Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO wamejeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia ngome yao iliyopo Rutshuru.

MONUSCO imethibitisha kuwa wanajeshi wake watatu wamejeruhiwa na kupelekwa kutibiwa katika hospitali ya mjini Goma uliopo mashariki. Katika tangazo hilo jeshi la serikali ya Congo limesema mmoja wa wanajeshi hao amejeruhiwa vibaya.

MONUSCO inasema kuwa wanajeshi hao wamejeruhiwa katika shambulio lililofanyw na wapiganaji wa M23 katika ngome yao iliyopo ivukatika eneo la Shangi -Rutshuru.

Kundi la M23 linasema kuwa majeshi ya FARDC na na MONUSCO ndio waliofanyanya mashambulio kwanza dhidi yao katika ngome yao iliyopo katika eneo la Jomba Jumatatu.

Hii inakuja wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya nne mfulurizo kati ya pande hizo yaliyoibuka baada ya mapigano hayo kusitishwa kwa muda wa wiki mmoja- mapigano yanayoendelea katika eneo la Rutshuru katika Kivu ya Kaskazini.

MONUSCO ilitangaza kuwa imo katika mapigano ikisaidia upande wa jeshi la Congo FARDC linalopigana na wapiganaji wa M23.

Tanzania ina wanajeshi zaidi ya 800 katika jeshi la MONUSCO kilichopo Mashariki mwa DRC.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano usiku, jeshi la DRC, FARDC linaishutumu Rwanda kutuma kikosi chake maalum cha wanajeshi 500 kuwasaidia wapiganaji wa M23, likisema kuwa walikuja wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi ya kijani kibichi na nyeusi.

Serikali ya Rwanda kwa imekuw aikikana mara kwa marakuwa inawasaidia M23, ikisisitiza kuwa tatizo lao liko ndani ya nchi yao wenyewe ya DRC.

Kikundi cha M23 Jumatano pia kilitoa tangazo kikiishutumu serikali kwa ‘’kuchagua njia ya vita’’, kwa vikosi vyake kushirikiana na wanajeshi wa MONUSCO na wapiganaji wa kundi linaloshutumiwa na Rwanda kufanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 la FDLR kuwashambulia.

Tangazo hil la M23linasema: “Kuchagua vita kwa serikali ya Congo badala ya kuchagua mazungumzo ya amani, ni tatizo katika kurejesha amani katika mashariki mwa DRC”.

Wakati huo huo, jeshi la DRC- FARDC limetangaza kuwa maazimio yakikao cha wakuu wa majeshi kilichofanyika Goma ya kubuni kikosi maalumu cha kupigana na makundi ya wanamgambomashariki mwa Congo.

Yatawasilishwa mbele ya kikao cha wataalamu wa masuala ya kijeshi na wakuu majeshiitakayofanyika kati ya tarehe 15 na 19 mwezi huu mjini Nairobi Kenya, kabla ya kuidhinishwa na maraisi wa Kanda.

Chanzo: BBC
Sasa kama mnajua tatizo ni Kagame yanini Kupeleka Vijana wetu Congo na kuishia Kuuawa na M23 ?
Si Bora tungeingia Kigali Straightway, yaani shina la tatizo twalijua halafu bado twahangaika na Matawi ?
Unless Kuna Mengi huyafahamu ndugu
 
Back
Top Bottom