DSTV yalamba hasara ya bilioni 122, gharama za vifurushi zawakimbizia wateja 486,000

Kitendo cha kifurushi cha compact kupanda toka 55k hadi 60k huku kukiwa hakuna huduma zilizoongezwa kilitukimbiza wengi.
Nililipia mwezi wa tano mwaka jana walipopandisha tu mpaka leo king'amuzi hata sijui kama kipo maana sijalipia tena. Mimi nanunua tu bundle basi maana kulipia king'amuzi ni hasara tupu.
 
Katika sababu walizoziweka wamesahau sababu moja ambayo ni ukuaji wa matumizi ya internet...

Ukishakuwa na internet ya kasi na yenye gharama nafuu, DSTV inakuwa kama option B...
 
Jibu ni moja tu.

  • Ujio wa Smart TVs
  • Watu kuwa na uelewa kuhusu FTA na IPTV. (Huko nibure kuanzia mpira mechizote hadi muvi, bure daima hadi kifo).
Naomba kuielewa hii mkuu.
FTA na IPTV ndio kitu gani hiki?
 
MultiChoice(DSTV) Malawi mwaka jana ilipoona inafilisika iliamua kufunga biashara lakini mamlaka ya mawasiliano ya Malawi ikawakubalia kwa sharti wanunue vifaa vyao vyote toka kwa wananchi ambao wanavyo kwa sababu havitakuwa na matumizi kwao, wakashindwa na kuendelea na biashara. Hapa Tanzania ingekuwa poa tu, watanzania wasikivu tu.
 

Streaming service multichoice wanayo ndo ile inaitwa SHOWMAX Sema watu hawashoboki nayo kivile kama netflix.
 
DSTV tayari wana streaming service kitambo sana zaidi ya miaka Nane sasa labda hujui tu..

WananPlatform wanaiita ShowMax, Wana DSTV Live Stream nk...
 
Mungu ibariki DSTV
 
Netflix ni nzuri zaid ya DSTV
 
Naomba kuielewa hii mkuu.
FTA na IPTV ndio kitu gani hiki?

FTA = Free To Air ( Hapo ukiwa na king'amuzi kinachoruhusu kupokea signals bila kulipia mfano " GTMEDIA RECEIVER DVB S2+T2" pamoja na kuwa na dish kubwa kuanzia ft 6 Cband utapata channels za bure kulingana na uelekeo wa satellite uliyotegeshea dish lako na zipo nyingi sana.)

IPTV = Internet Protocol Television ( Hapo ukiwa na uhakika wa internet iwe bure au kulipia bando bei rahisi tena ukipata fiber kama zuku na ttcl basi hapo mchawi anabaki kuwa Smart tv tu kuna apps za kustream channels za kimataifa tena zile kubwa kubwa kama zote bure.)
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
DStv
Ni nyumbani kwa F1 na MotoGP....

January hii tupo na Dakar rally
Mhh F1 iko premium! Mwanzo wa season wanaachia kidogo then wanarudisha premium. Kama wengi walivyosema inabidi washushe bei vinginevyo kila mwaka watapoteza wateja. Maisha yamekuw magumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…