Dudu baya a.k.a mamba aichana chana clouds fm, amwagia sifa rubby

Dudu baya a.k.a mamba aichana chana clouds fm, amwagia sifa rubby

Wanoaribu mziki ni Babu tale na Fela wala sio clouds awajamaa wa ovyo sijawai kuona sana roho mbaya sana we fikiria mtu Kama MB dog kassim mganganga anajikongoja wanatoa pesa kwa Runge ngoma nyingine zisichezwe
Sasa Fela anahusiana nini na hao, bora ungemsema Juma Nature
 
Dudu baya kasema clouds ni wanyonyaji, kiki gani hapo

Anajuaje ni wanyonyaji, kaonyesha nini au kama msanii hajui kujituma kufanyikiwa na kusubiri kusukumwa ni ku blame Clouds? Wanataka kuimba then hujui kujisimamia na what unataka, hujitambui kikazi na kuweka mbele bosi au lala waelewe na msanii kujua pesa bila bidii na skills za nini nini. Si watoke waende kwingine no body anawalizimisha kukaa na Clouds.

Waache kutamani life na mafanikio ya wengine, bali wapige kazi na kuji promote vizuri.
 
Dah kiukweli dudu atapata tabu sana kurudi kwenye game, game imechange sa hv, hvo vinjia anavovitumia kurudi hatofanikiwa, kikubwa aingie studio atengeneze ngoma tamu ya kisasa then aone kama watu tujamuweka kwnye mistar! sio daily analalamika mpka hatak watu wajipe majina ya wanyama bhana, kha!
 
Wasanii wa bongo wengi kwa Ruge kila goti litapigwa leta jeuri urudi Igunga,Simiyu,Kibororoni..
Hukuna lolote, ni kutojiamini kwa wasanii tu, Sugu alimgusa kidogo tu akaishia kuomba suluhu kupitia Waziri Nchimbi na akina Tundu Lissu, kama alikuwa anaweza lile battle kilichomfanya akimbilie kuomba poo ni nini? Jide tu hapo wamemshindwa!!

Ukiangalia vizur utagundua ni kutojiamini tu kwa Wasanii wetu, kwa mfano huyo Ruby wanaosema kuwa walimbeba, mim nilisikia wimbo wake kupitia radio nyingine tofauti kabisa na nikamkubali, hali kadhalika hawa akina Raymond, Billnas na wengine waliochipukia majuzi, wote nilisikia nyimbo zao kupitia media nyingine na nikawaelewa.

Kitu ambacho wasanii wetu hawajaelewa ni kuwa, Wimbo mzuri ndio utambeba, promo ina nafasi yake ila kama unafanya nyimbo nzuri utatoboa bila hata hao watu!! Kuna nyimbo kibao kutoka mataifa mbali mbali zinapendwa sana hapa Tz, je hao mawingu ndio wanawabeba hao wasanii wa Kimataifa? Jibu ni hapana, Ubora wa Nyimbo zao ndio zinawabeba!! So kuwekeza tu kwny mziki wako ndio utakubeba na sio media fulani!! Kujitambua ni hazina kubwa sana!!
 
hivi hawa wasafi yani wcb wapo kwenye hizo tamasha?
 
Maombi yangu yanaanza kuzaa matunda maana hiyo redio ilikuwa kama shetani usipokuwa mfuasi wake anakufwata fuata hatari hadi usimame imara ndo umkomeshe wasanii wa bongo umoja wenu ndo ushindi maana hata wao hufaidika kwa kazi zenu!
 
Maombi yangu yanaanza kuzaa matunda maana hiyo redio ilikuwa kama shetani usipokuwa mfuasi wake anakufwata fuata hayari hadi usimame imara ndo umkomeshe wadanii wa bongo umoja wenu ndo ushindi maana hata wao hufaidika kwa kazi zenu!
Ulitaka kumaanisha nini?
 
Hukuna lolote, ni kutojiamini kwa wasanii tu, Sugu alimgusa kidogo tu akaishia kuomba suluhu kupitia Waziri Nchimbi na akina Tundu Lissu, kama alikuwa anaweza lile battle kilichomfanya akimbilie kuomba poo ni nini? Jide tu hapo wamemshindwa!!
Ukiangalia vizur utagundua ni kutojiamini tu kwa Wasanii wetu, kwa mfano huyo Ruby wanaosema kuwa walimbeba, mim nilisikia
wimbo wake kupitia radio nyingine tofauti kabisa na nikamkubali, hali kadhalika hawa akina Raymond, Billnas na wengine waliochipukia majuzi, wote nilisikia nyimbo
zao kupitia media nyingine na nikawaelewa.
Kitu ambacho wasanii wetu hawajaelewa ni kuwa, Wimbo mzuri ndio utambeba, promo ina nafasi yake ila kama unafanya nyimbo
nzuri utatoboa bila hata hao watu!! Kuna nyimbo kibao kutoka mataifa mbali mbali zinapendwa sana hapa Tz, je hao mawingu ndio wanawabeba hao wasanii wa Kimataifa? Jibu ni hapana, Ubora wa Nyimbo zao ndio
zinawabeba!! So kuwekeza tu kwny mziki wako ndio utakubeba na sio media fulani!! Kujitambua ni hazina kubwa sana!!
Uzuri umekiri mwishoni mwa uzi wako kuwa wasanii wengi hawajiamini na kujitambua hivyo umeelewa nilichokimaanisha
 
Clouds wanawafanya wasanii wakose kujiamini. Kila msanii anaona hawezi kujitegemea anapokuwa nje ya Clouds, inatakiwa wasanii wafunge mkanda ili kujinasua na huo ukoloni wa kifikra.
Wasanii wanatakiwa kuwa makini wataishia kutajirisha watu wengine ilihali wanakufa masikini.. media plz saidien wasanii msiwadidimize
 
Bila kuongelea Clouds Media naona watu hawana pa kupatia kiki

Kama wasanii wangekuwa wanalipwa pesa mbaya si wangeenda kwingine.

Mkubali kuwa Clouds kwa jina.wamejijenga na mengi hata iweje...wakongwe wa mengi nchini.
Cloooooooooooooooooooooouds fm,wale jamaa ndio Tbs na Tfda ya burudani hapa Bongo,kama wimbo wako hawajaupasisha basi katunge mwingine, nawapenda sana wazee wa burudani.
 
Hivi kuna ukweli kwamba wananyonywa??

Hao wanaonyonywa nao wamekubali kunyonywa.??

Ni vigumu sana kukubali mtu anaweza kunyonywa na kuendelea kukubali kunyonywa tu!!

Ndugu yangu wee,kwani kuna kuna anayenyonywa basi? Ni vile tu wabongo wanapenda sana udaku na maneno ya uongo na kuzushia watu ubaya na kama ujuavyo mara nyingi ubaya huvuma kuliko wema,kwa mfano huyu mtoto Ruby,awali hakuna aliekuwa akimfahamu Ruby,lakini Clouds fm kupitia fiesta hiyo hiyo wakamtoa ,ametoka wabongo wanamfahamu na shoo anapata,lakini kuna watu wamemjaza ujinga mtoto kajiona ana thamani kuliko clouds na tamasha la fiesta lililomtambulisha,amekataa,eti hataki kunyonywa,sasa najiuilza hataki kunyonywa nini alichonacho Ruby na kujifananisha na nani hata afikie kutamka hayo?Hivi Ruby ana thamani ya kumzidi Vanessa Mdee? mbona vanessa anahangaika na fiesta? jibu ni kwamba Vanessa anajitambua na anatambua thamani ya fiesta anajua fiesta ina maana kubwa kwake ndo maana yupo na anapanda hizo coaster bila nyodo wala kwere,Kwa taarifa yako wasanii wanaotaka kupanda kwenye jukwaa la fiesta ni wengi kuliko wasiotaka, na wasiotaka kiukweli wanataka ila wanajikaza kisabuni wasionekane masnitch yaani wanajiua kwa tai zao shingoni maskini,nawaonea huruma kujiumiza roho buree kwa kuichukia clooouds fm mabingwa wa burudani bongo.
 
Wasanii wanatakiwa kuwa makini wataishia kutajirisha watu wengine ilihali wanakufa masikini.. media plz saidien wasanii msiwadidimize
Dahh, mzee hawa watu wanawakamua kama unavyotafuna ganda la muwa halafu utamu ukiisha wanawabwaga kama hawawajui, hebu tizama watu kama Mabaga Fresh au Dully Sykes walivyo. Ni aibu kwa Dully kusota ofisi za Dangote lakini kwa kuwa hana jinsi inabidi ajibanze ili maisha yasonge.
 
Kwa uelewa wangu msanii unalipwa kutokana na idadi ya nyimbo zako zinazo het.unakuabalika vipi na jamii unayoenda kufanya shoo aiwezekan shalo mwamba akalipwa sawa na joh makin.navojua kuna laki nane.tano.na zaid sasa ww unanyimbo moja unalipwa laki tano.kula kulala kusafiri juu yao bado unapewa nafasi ya kupanda kuimba watu wakutambue bado unabenua poa ela kidogo.jitangaze nakapige shoo yako mwenyew sasa uone kma utapata hiyo hela.lazma ujue kutimia akili kucheza na watu ambao wameshikilia uu mzika
 
Haha bro ongea ukweli tu, ni kweli viongozi walimuomba ayamalize, but ni kwamba alilipwa chake alichokuwa anakidai then akakausha na kuyamaliza kimyakimya bila kuwashirikisha wenzake
Sina hakika kuhusu kulipwa
 
Naunga mkono hoja mkuu ila ninashangaa kuna watu humu mpaka leo wanamtetea sugu.
Sugu aliwageuka wenzake waliojotosa kupigana naye kama Rama D, mapacha.
Kwa upande wa jide pia naye uwa namlaumu kwanini hakuunga mkono wakati vinega wameanza harakati au kwakuwa bado alikuwa in good terms na clouds.
Hizi harakati mtu anazianza pale anapoona anaanza kuanguka au ameisha ndiyo maana naziona fake.
Ipo siku weusi wakiisha chat utasikia nao clouds wanyonyaji lakini kwa sasa ....
Mkuu sugu haijawahi kusaliti hiyo movement, bas ni jins tu media ilivyoweka ishu yenyewe
 
Back
Top Bottom