Dudu baya, Mtoto wako Wile yupo na hali mbaya jaribu kumuokoa anateketea .

Kuna wakati wazazi wanalaumiwa tu ila mtoto akiamua kuchukua njia mbaya kachukua. Na hawa watoto wanajifunza bangi na pombe shuleni huku mzazi unajua anasoma.

Mtu akianza mibangi na pombe kumuokoa labda upeleke soba na hapo uombe sana maana nimeona waliokaa soba mwaka mzima na walivyotoka wakarudia.

Na mtu akiwa stage hiyo hata umnunulie simu atauza nguo atauza ukijikoroga umpe pesa ndio umemuua kabisa atalewa huyo. Kwahiyo inafika mahali inabidi muangalie tu. Kwahiyo tusione kama hawasaidiwi bali wengi wao hawasaidiki.
 
Kweli kabisa. Na bangi huwa wanaanzia shule ya msingi au akichelewa anaanzia O - level. Mdogo wangu akiwa darasa la 3 kuna mtu alinitonya kuwa dogo wako anakula ganja nikamwona kama snitch kwa sababu dogo mtulivu na ana adabu mno nyumbani. Tumekuja kujua kuwa ni kweli dogo yuko form 3. Ilikuwa too late.
 
Kwahiyo haikua na madhara kwake? Coz umesema dogo alikua mtulivu na ana adabu.
 
Kwahiyo wewe Kama s. Mom unatoa ushauri gani?
 
Poleni sana ila kama hajafikia stage ya kunywa hadi pombe mnaweza mkamsaidia.

Shule hizi ni nzuri ila watoto wanafundishana ujinga. Watoto wa shule wanakunywa hadi piwa.

Siku sio nyingi nilimkamata mwanafunzi na piwa kaweka kwenye chupa ya maji kumbe ndio anawaletea wenzake. Kuwabana vizuri wanavuta hadi bangi. Tumeita wazazi mimi nikawashauri wapelekwe kwenye matibabu kabla hali haijawa mbaya maana wakimaliza tu form four lazima wawe kama hawa tunaowaona.

Wameona watoto watapoteza muda ila wawili walielewa.
 
Alishafika hiyo stage ya pombe kitambo sana. Sasa hivi ni mtu mzima kashaoa single mama mwenye watoto wawili wakubwa.
 
Baba yupo bize kutukanana na waliomzidi kipato
 
Inasikitisha.

Piwa ni nini? Pombe ya aina gani hii?
 
Piwa ni nini madame?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…