Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…

Ule ujinga wa maigizo hatutaki,safi Sana Rais..

Haiwezekani kila mwenye tatizo amtafute Rais.
Uko sahihi Mkuu, huyo siyo Rais tena, bali, mjumbe serikali ya mtaa. Na nchii hii wenye shida wengi!

Halafu katika ya hotuba, unamsimamisha Mkuu wa nchi ili wewe uongee aisee!
Hata waliompanga walichagua bogus!
 
Rais amekosea kutomsikiliza ila mwenye shida amekosea zaidi kulazimisha kukatisha hotuba.

Mama Samia anatoa hutuba unamkatisha ili useme shida yako. Why usumsubiri amalize hotuba yake kwanza?
Kwa nini amngojee Mhe Rais mkutanoni kama jambo lake ni halali kuna mwakilishi wa Rais wa kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa ambao ni DC na RC kwa nini hakuwaona kwanza?? na kama aliwaona na wakalipima jambo lake aidha waligundua ni msanii au analazimisha haki ambayo sio yake. Mhe Piga kazi achana na hao wenye majungu wafuate ngazi!! Big up mama yetu Mhe Samia!!
 

Unalinganisha natural hazards na shida ya mtu binafsi inayokwamishwa na watendaji wa serikali…hv huu uchawa mtaacha lini
 
NA
 
Unatumia kigezo gani au point ipi kumlinganisha mama Samia na Magufuli?

Mama Samia ana njia zake za kutawala na Magufuli alikuwa na njia zake za kutawala.

Wacheni kulinganisha mambo ya hovyo kisa sukuma gang
 
kuna watu wanamuona samia kama mama wa kambo, hata afanye jema lipi bado wataona dosari moja tu. Si kwamba mimi ni mfuasi wake ila kutaka samia awape vibe ya mtangulizi wake ni kumuonea
Sema mama alilofanya ukiacha madarasa ya covid
 
It was staged, huyu raisi wenu nafikiri ana personal issues na Magu (RIP) kwa maana kila anachokifanya kimemlenga Magu, kwa nini ?

Get a life woman !
...Mhhh!... personal issues na mtu asiyekuwepo?...usimzushie Mh.Rais uongo.
 
Wewe mpumbavu unaona ujinga!
Ni ujinga kweli, njobege ujobege. Sikiliza mpaka amalize utaongea. Kwanini kuingilia kati maongezi muhimu ya raisi? Anashauri utaratibu mzuri kwa nchi nzima, yeye anapeleka ubinafsi.
 
Kwa nini asimwambie hata jaji mkuu msikilize hiyo mama?
Jaji mkuu wa nini bila evidence, wahusika wameisha msikia kaambiwa hivyo. Sasa alichotaka ni kumtoa rais katika mstari. Wakati alikuwa anaongea tatizo kitaifa.
 
Nyani Ngabu licha ya kukaa ughaibuni unashindwa kuelewa tukio hilo linaendana na anachoongea Rais?

Huoni kama kuna Dalili ya igizo Hilo lililofanyika😀😀

Au lengo la igizo hilo hujalielewa?
Nia ya huyu mleta mada pia ni kupiga propaganda za kumchafua rais. Mleta mada kujifanya anatetea wanyonge ni kuwajaza watu ujinga tu, lengo ni kumchafua rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…