Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…

Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…

==========

Mama mmoja amesikika akimuomba Msheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassani kuwa anaomba atendewe haki, mama huyo amerudia mara 3 kusema anaomba atendewe haki, Lakini Rais Samia alimjibu kuwa hawa hapa wapo umeshatuandikia litanifikia nenda kakae. Rais Samia Aliendelea kusema kuwa ona yanajitokeza hata hapa. Hivyo kusisitiza mahakama zitende haki kwa kuangalia utu wa mtu.

Amekaa kikazi tu hana uchungu wa moyoni na shida za wanyonge. Mwenda zake angetaka kujua shida ya huyo mama na angefanya uamuzi.
 
Kwa hiyo Rais aache kushugulika na mambo makubwa ya nchi kama sera, ulinzi, mikataba aanze kutatua migogoro ya viwanja vijijini, mirathi, matatizo ya ndoa ? Akili za wapi hizi!
Mbona kura anakuja kutuomba na kutuahidi atatua changamoto zetu? Tena mnapota nyumba kwa nyumba jana kimemshinda nini kumsikiliza mwanadamu mwenzie? We unafikiri yule mama anaweza akampenda Samia kweli kwa yale ya jana? Atamtaia kheri?
 
Rais amekosea kutomsikiliza ila mwenye shida amekosea zaidi kulazimisha kukatisha hotuba.

Mama Samia anatoa hutuba unamkatisha ili useme shida yako. Why usumsubiri amalize hotuba yake kwanza?
Mkishiba Mnakuwa Na Viburi. Lini Raisi Magufuli alisubiriwa Amalize Hotuba.
 
Nikweli unalosema ila haijawahi kukutokea ukapitia changamoto,wajanja wanawapiga makofi ya nyani watu wote hadi RC.na Mahakama.....Utaenda wapi? Nchi hii dhulma ni waziwazi, inawezekana nikweli JPM kulikuwa na kasoro hizo,ila Kuna machozi ya watu wengi na hakuna pa kupata haki yao
Sasa afanye utaratibu rasmi akamuone kwa njia zinazotakiwa ofisini kwake ila sio maigizo ya Majukwaani,Rais atahudumia wangapi Kwa staili kama hiyo?
 
Rais anaendelea Na hotuba kumwambia wape hao makaratasi yako utasaidiwa!

Think this way, what if ana sikiliza and then wakatokea wengine 10 atamaliza speech?
Yeye ni Raisi na hafla aliyokuwa anaihutubia ni ya mahakama ambao ni mhimili mwingine pia hoja ya yule mama ilikuwa haki nadhani busara ilikuwa kumsihi jaji asimamie swala lake hilo kwani sio wote wenye shida wanao huo uthubutu na hata walionao ni wachache wanaoweza kumfikia raisi mbaya zaidi ni lugha (tone) aliyoitumia
 
Hatuwezi elewana maana tunaishi kwenye uhalisia tofauti
 
Sasa afanye utaratibu rasmi akamuone kwa njia zinazotakiwa ofisini kwake ila sio maigizo ya Majukwaani,Rais atahudumia wangapi Kwa staili kama hiyo?
Raisi anamhudumia nani kwa njia hizo sahihi za kwenda kumuona mtanzania wa kawaida hana namna yoyote ya kufikisha ishu yake kwa Raisi directly mbali na hiyo
 
Mkiambiwa nchi inatakiwa iwe na mifumo imara yakufanya kazi na taasisi zinazojisimamia mnaona wanaosema hivyo hawajielewi ila kila siku kulia lia.Tungekua na taasisi imara na mifumo ya uwajibikaji mambo madogo madogo kama hayo yangekua yanamalizika ngazi ya chini.Rais ni cheo kikubwa sana na ni cheo cha mwisho kimamlaka sasa ni aibu rais kuangaika kujibu vitu ambavyo vilipaswa vifanywe na watendaji.Tupambanie katiba mpya na bora ili kila mtu awajibike kwenye nafasi yake badala yakutaka kumlundikia rais kila kitu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwahyo unataka Rais akawe hakimu ama Judge kwa muda huo huo mfupi hapo na atoe maamuz!!?
Sasa hamuoni kama atakuwa ameingilia muhimili mwingine!?! Halafu kesho muanze tena kumsema vibaya
Kwani ni sawa chadema wanapotaka awe hakimu na jaji kwenye kesi ya gaidi aingilie mahakama amwachie mtuhumiwa ni sawa?
 
Acha basi ale kuku wa ikulu, alale, anye, aoge.

Umefurahi ee!

Maana unaona kuwasikiliza wananchi ni shida.
Acha akili zakitoto wewe.Inaonekana kinachokusumbua ni chuki sio kitu kingine ndo maana umerukia kwenye ujinga badala yakusimamia hoja.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Acha akili zakitoto wewe.Inaonekana kinachokusumbua ni chuki sio kitu kingine ndo maana umerukia kwenye ujinga badala yakusimamia hoja.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sasa kama tunakuelimisheni kwamba rais anajukumu la kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao wewe hutaki.

Unataka Rais afanye nini sasa?.

Acha basi ale kuku wa ikulu, alale, anye, aoge.
 
Rais amekosea kutomsikiliza ila mwenye shida amekosea zaidi kulazimisha kukatisha hotuba.

Mama Samia anatoa hutuba unamkatisha ili useme shida yako. Why usumsubiri amalize hotuba yake kwanza?
Prime time......
 
Watu wako desperate. Ukiona hivyo ujue huko kwingine wanaona kama vile hawapati haki zao.
uko sahihi kabisa nchi kwa sasa imerudi one step behind.mahakama hazitendi haki pia wenye mamlaka hawatendi haki so wananchi hawana pa kukimbilia.nadhani taratibu watapata akili ya kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi ili wajue nani sahihi wa kumchagua.
 
==========

Mama mmoja amesikika akimuomba Msheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassani kuwa anaomba atendewe haki, mama huyo amerudia mara 3 kusema anaomba atendewe haki, Lakini Rais Samia alimjibu kuwa hawa hapa wapo umeshatuandikia litanifikia nenda kakae. Rais Samia Aliendelea kusema kuwa ona yanajitokeza hata hapa. Hivyo kusisitiza mahakama zitende haki kwa kuangalia utu wa mtu.
Nyani ulipotelea wapi?
 
Back
Top Bottom