Kama umenisoma vizuri utakuwa umenielewa. Nchi zote duniani mwananchi usikilizwa. Na ikishindikana unaruhusiwa kumuona mtu wa juu au chombo maalum kinachosikiliza wananchi wenye malalamiko. Kwa Tanzania hatuna huo mfumo. Rais Ana madaraka yote.
Nilishawahi kuandika humu ndani, mfano. Kuna bibi haki ya mtoto wake alicheleweshwa kwa miaka 20 toka mwanae afariki kwa ajali. Yule bibi aliishi mikoani. Alikuwa bibi maskini na aliachiwa familia ya mtoto wake. Bibi alifuatilia haki ya mwanae kwa miaka hiyo bila mafanikio.
Huko wizarani alizungushwa. Alifikisha malalamiko kwa mkuu wa mkoa.
Mkuu huyo alijitahidi kushughulika lkn kwa kuwa yeye awezi mwamuru katibu mkuu wa wizara, mambo bado yalikuwa ni magumu. Katibu wa Wizara alikuwa anakubali atafatilia lakini mama hapati haki yake.
Mpaka hapo Rais alipotembelea mkoa ule, huyu mama alipewa nafasi ya kuonana na rais aeleze tatizo lake. Rais alitoa maagizo, na haki ya huyu mama ikashughulikiwa baada ya mika 20 kupita. Si yeye tu wapo wengi. Hao maDC na ma Rc unaosema kwa muundo wa mfumo wa serikali yetu kuna sehemu wanakwama hawawezi kumaliza kila kitu.