Handsome Rob
Senior Member
- Jan 12, 2017
- 157
- 525
Sawa mkuu.Mkuu kwahyo hela ungeanza kwanza na DLDM ambapo 5M inatosha kabisa, then baada ya kupata uzoefu wa kuendesha DLDM hata miaka 3 hv ndio ufungue Pharmacy.
Nasema hvyo kwa sababu kufungua Pharmacy ni very complicated na kwa mtaji wako utajikuta unatumia pesa ndefu kwenye Usajili na gharama zingne na usibakiwe na hela nyingi ya kuchukua Stock.
Anza na DLDM kwanza ukishaiva uko ndio uwaze Pharmacy. Kwa hela yako hyo utafungua DLDM na kui manage bila wasi wasi..
Kwa wabongo hii ni ngumu sana japo wapo watu wazuri ila ni bahati kukutana nao,zaidi utaonekana umetumwa na SerikaliEbu tembelea phamacy ya karibu au ambayo ipo standard unayoitika wewe na ujaribu kupata abc kupitia hapo unaweza kupata taarifa kamili. Najua ni ngumu mtu kukupa taarifa zote if possible toa kitu kidogo.
Hilo nalo neno, ila unaweza kumdodosa muuzaji, je anaweza kuwa msaada?Kwa wabongo hii ni ngumu sana japo wapo watu wazuri ila ni bahati kukutana nao,zaidi utaonekana umetumwa na Serikali
Muuzaji anaweza,ila inabidi pia awe mzoefu na anajua mambo yanaendaje ila weka mazingira akuamini na ajue una nia njemaHilo nalo neno, ila unaweza kumdodosa muuzaji, je anaweza kuwa msaada?
Uza jumla na rejareja inalipa.
Tenga vyumba viwili.
Sehemu 1 ya jumla sehemu nyingine ya rejareja.
Weka mfumo mzuri wa computer wa kuratibu mauzo.
Tangaza biashara yako.
Tembelea maduka ya dawa jitangaze
Wanajukwaa kwema.
Naomba nianze moja kwamoja kwenye hoja yangu ili nipate ushauri. Nimepata kasenti kadogo hivi kama 17m. Sasa nikawaza nifanye biashara gani na wazo likanijia nifanye biashara ya phamacy.
Nimetafuta eneo nimepata sehemu ambayo kodi yake ni laki 5. Sasa najiuliza nianze hiyo biashara kwa hayo mazingira na mtaji utarudi?Ishu ni hiyo kodi ndio inaniumiza kichwa sana. Ila eneo ni nzuri tu.
Naomba ushauri na mawazo zaidi. Ni mimi mpambanaji wa maisha.
Man Army
Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru sana kwa ushauri.
Ila mzigo sio lazima ninunue mwingi sana.
Naweza nunua mzigo wa 6m kwa kuanzia
6m nikalipa kodi
3m mambo ya ukarabati
Afu inabaki 5m.
Hapo vipi mkuu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwakuwa unaanza, unaweza kuongea na mfamasia ukampa hata 200K kwa mwezi.
Biashara ikiwa inakuwa na wewe unamuongezea.
Anaemlipa hiyo 1M ni mtu mwenye mtaji wa 50M na kuendelea na faida yake ni zaidi ya 5M kwa mwezi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli.Ha ha umpe Mfamasia laki 2 , mmh
Halafu ushauri; ukienda kwa hao wafamasia ukimwambia Unaanza Biashara Na mil 20 , honestly hutopata mtu .
Hatokubali hata siku moja , anauhakika mtasumbuana, Na for sure mtasumbuana.
maana wewe utakuwa na expectation zako na yeye utakuwa expectation zake.
Halafu nimesoma comment nyingi; wengi wanaandika kwa hearsay not buy realistic .kuna watu wataandika ukweli na kuna watu watakupa moyo pasipokuwa na knowledge. So ni wewe kuwa makini usijekujikuta unajichanga mil 17 ambayo unaweza ku invest kwenye Biashara nzuri na simple na ikazalisha pesa; badala yake unaenda kwenye business pasua kichwa kwa kuanza na mil 17 , totally impractical.
Nimeona mdau hapo anasema wewe fungua then utakopa dawa kwa wafanyabiashara wakubwa...... wapo wanaofanya hivo kwa riba na ni lazima uwe na advance . Sasa once unapowekewa riba maana yake unamfanyia mtu kazi. Maana dawa zikiexpire hiyo pesa utalipa tu. Unakula hasara mara 2.
Michezo hiyo hufanya maduka ambayo yapo kwenye game muda na wanajua movements ya biashara: Sasa wewe uanze na kuanza ukafanye michezo ya kukopa dawa .... my friend ...... !
Ndio maana nasema wengi humu wana comments kama zile inspirational speeches na mahesabu ya matikiti kwenye heka moja........
ukisoma mahesabu, unasema miezi 6 babake nimeuaga umaskini......
Nenda kalime Sasa ........ndio utajua kwanini ugali hauwekwi Chumvi LoL
utashinda na matikiti yako juani mwishoe uanze kuwapa majirani zako wale Bure.
Watizedi tujifunze kuwa realistic, tusipende sana blah blah