Duka la "Plea Bargain" lafungwa, Waliochukuliwa fedha zao waitwa kuhojiwa, uchunguzi waanza

Uko sahihi 100%. Nakumbuka kumsikia mwenyewe Rais Magufuli akitamka, yeyote ambaye atapuuza kwenda kwenye plea bargain, Shauri yake atakaa ndani hata miaka 20, kwa hiyo unaweza kuona wengi walijua nini kingewakuta wangebisha. Kwa ujumla ni ukatili wa kiwango cha juu sana, wenzetu walipitia. Udhaifu wa bunge na mahakama ni janga kubwa kwa utawala wa sheria. Naweza kusema mtu kama Kikwete hana sifa ya maana ya kukumbukwa kwenye utawala wake, kwani kwa sehemu kubwa alichangia sana mateso hayo ni kama alikuwa akifurahi, na alisikika akisema mlisema mimi mpole, Sasa nimewaletea tingatinga. Binafsi namuona kama msaliti tu, hata hizo nafasi za kimataifa hazimstahili hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…