Mkuu punguza hasira umekula mchana? by the way wabongo ni waoga hata tukisafiri huko nje ya mipaka safari za mbali unajikuta uko peke yako, wabongo wanaenda dubai na china na uturuki kwa uchache, ila wenzetu majirani na wa afrika ya magharibi wanajilipua sana sisi waoga mno.
Sio waoga mkuu .
Fursa zinatafutwa na serikali kwa niaba ya wananchi wake.
Tuna viongozi wachuuzi wa rasilimali za nchi sio kuwainua wananchi .
China wanakuja mpaka wafungwa kufanya kazi bongo na wa anafadhili wa na nchi zao.
Jiulize nani alifungua geti kwa wachina kuja kuchoma mpaka mahindi.
Watoto wa wakubwa badala ya kusafirisha tangawizi kwenda Dubai wanaosafirisha unga wa kubwia.
Badala ya Waziri wa kilimo kwenda Vietinam na wakulima kutoka mbalizi kujifunza kilimo cha kisasa katika mazingira ya wakulima wa chini anasafiri na wachekeshaji wakajifunza na wasanii wa kupamba.
Mkuu wa nchi anaonoka na umati wa wasanii waandishi wa habari na machawa kwenda Thailand badala ya kuondoka na wamachinga hamsini wakapate connection na uzoefu wa safari za nje na ujasiri.
Mpaka leo kuna watu hawana hata kitambulisho cha Taifa achilia mbali Passport .
Mikopo yenye riba nafuu inatolewa kwa machawa wa 5 tena, badala ya wafanyabiashara wadogo.
Take masoko ya Mipakani yako wapi?
Angalia jinsi wafanyabiashara wa kibongo wanavyosumbiliwa mipakani tena zaidi wanasumbuliwa na watanzania wenzetu wa uhamiaji?
Kama Dubai wananunua Wanyama hai kwa nini watanzania wasipewe vibali vya kubeba swala na kwenda kuuza wenyewe kwa bei ya kule au ni Waarabu wanaopewa mbuga nzima wahamishie wanyama uarabuni kisha waje waturithishe misikiti ambayo tungeku na fedha tungejenga wenyewe.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya kilimo wanwezeshwaje kutumia elimu yao ? Ardhi yote wanapewa wageni kwa rushwa ili walime wao na kusafirisha wao sawa mtanzania ataenda wapi na atapeleka nini huko ugenini ?
Hao watanzania wenye mitaji ya kwenda China na Thailand mbona wengi ni wale wale wake na waume na mahawara wao tu. Watanzania Watangayika walipotaka kuifanya kariakoo kuwa Soko kubwa la bidhaa kwa nchi za Kongo na Ukanda wote wa maziwa makuu walikuja madalali wakauza mpaka bandari ziwe mali ya Waarabu ili wapate pesa wakajenge Kwao Dubai wabongo wabaki kupiga kura za marehemu mana waliopo hai hawahitajiki kwenye hii nchi.
Kama wetu wanahujumiwa kwenye kuchagua viongozi wao itakuaje kwenye mali zinazosimamiwa na hao hao wanaonunua uongozi ?
Bila kuondoa hili janga linaloitwa CCM watanzania watabagi kama walivyo na nchi na uchumi wake utatawaliwa na Wachina ,wahindi na waarabu huku wakisingiziwa kuwa ni wavivu na waoga kumbe kuna kundi dogo limeamua kuigeuza nchi kuwa ya wasanii ,waandishi wa habari wa online TVs na wachekeshaji ili baadae nchi iwe kama Kongo na muziki na ushirikina huku rasilimali zikiwa zinachotwa kwenda Ulaya na Uarabuni.
Mitano tena lakini hatujui ni ya nini kama sio ya kumaiza kuwakabidhi na hati ya Muungano wawekezaji😂😂😂😂😂😂😂😂