Na ndivyo watakavyofanya. Irani kuhalisia anaiogopa sana Israel na anajua nguvu yake. Anachokifanya ni kutengeneza katukio kuonyesha kuwa amelipa kisasi.
Na inawezekana huwa anawasiliana na Israel na Marekani kuwaomba kulipa kisasi kiaina na ndio maana Marekani muda wote hutoa taarifa ya muda . Tujikumbushe kisasi cha Iran dhidi ya Kambi ya Marekani kule Iraq ambapo hakuna aliyejeruhiwa hata mmoja, na juzijuzi alivyolipa kisasi kwa Israel kisasi kisichokuwa na madhara.
Kwahiyo ninaamini muda huu kamati imeundwa baina ya Israel, Iran na Marekani kupanga namna ya kulipiza ila malipizi yasiyo na madhara.
MTU MWENYE NIA HUWA HANA MATANGAZO MENGI
😂😂😂😂😂😂😂😂MKUU WEWE NI MUONGOO.
Embu nenda kahungame dhambi ya uongo kwanza.
Wewe nani kakwambia Iran anaiogopa Israel!?
Kama Iran anaiogopa Israel je angeweka jeshi Syria na Kuisaidia Hizbollah??
Hivi unajua kama Hizbollah inayoishambulia Israel tokea Oktoba 7 inasaidiwa na Iran!?
Kama angekua Iran anaiogopa Israel asingejisogeza Syria na Lebanon.
-Halafu uache UONGO kisasi cha Qassem Soleiman pale Iraq kililipwa kambi ya USA ilipigwa ikiwa na wanajeshi tena wengi wao wamepata ulemavu wa viungo na akili.Bahati yao walijificha katika mahandaki madogo ya ile kambi ndio pona yao wakapata ulemavu kwa kuumia viungo na wengine walemavu wa akili hadi sasa.
Ndugu wa hao wanajeshi walilalamika mitandaoni ndio Trump akajishaua kutuma battleships ziende Persian Gulf zikaishia pembezoni tu.
-Tukio la May lilihusisha kurushwa drone na makombora 300+ kama isingekuwa UK,USA na Jordan basi Israel ilikua inageuka majivu.
Maana ilikua ndio mara ya kwanza Iran anashambulia directly into Israel.
Hakuna mtu ambaye alitegemea,na Iran walisema kuwa it was the show of force not use of force.
-USA kujua kuhusu kushambulia ni kulingana na Intelijensia yake,maana hata uvamizi wa Russia ndani ya Ukraine USA wali predict na ikatokea vile vile.
Msitake kutudanganya hapa ilhali tunafahamu kila kitu huyo Israel anayemkingia kifua ni USA na UK.
Na kwa uwepo wa USA kunampa wakati mgumu Iran kwasababu anajua anatafutwa na maadui wengi huku akiwa na struggling economy yenye vikwazo vingi.