Dunia imechelewa mno kuishtukia Marekani kuhusu utawala wa pesa yake DOLA katika uchumi wa dunia. Angalau sasa wameishtukia

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Marekani iliipiga changa ya macho dunia kwa muda mrefu. Ikalazimisha dola iwe ndio pesa rasmi katika biashara za kimataifa na uchumi wa dunia. Wanachofanya ni kuchapisha noti tu za dola na kuipa thamani kwa kauli tu.

Dunia nayo ikawa imejikuta inakubaliana na changa hilo la macho. Lakini Urusi imeiamsha dunia na marekani imepaniki. Urusi imesema kila nchi inaweza kutumia pesa yake ya ndani kwenye miamala ya kimataifa.

Uamuzi huo ghafla ukairudishia thamani pesa yake ya ruble iliyokuwa imeshuka sana thamani kwa zaidi ya asilimia 90.

Kwa sasa mataifa kama india, China, Brazili tayari yamejifunza kitu na yataanza kutumia pesa za mataifa yao kwenye biashara baina yao na mataifa mengine yatakayokubali.

Urusi imeandaa mfumo wake kama ule wa SWIFT kwa ajili ya miamala ya kimataifa na nchi zimeshajiunga tayari na kwa kuanzia mataifa hayo (ukiacha mataifa ambayo hayaogopi kitu kama India na China) hayataainishwa ili kuyakinga na vitisho na vikwazo vya marekani.

Ndio maana Marekani inahaha kuongeza vikwazo kila siku na kupeleka silaha ukraine, si kwa kuwa inaipenda sana ukraine lakini inataka kuangusha kabisa uchumi wa urusi na kuipunguza nguvu kijeshi.

Japo mpaka sasa marekani inaonekana haijafanikiwa kwa hilo ila mambo yanaigeukia yenyewe kuwa mabaya!
 
si kweli, thamani ya pesa inatokana na what you produce to the world. Kila kitu kinapatikana USA, kila nchi inahitaji kitu from USA, fedha yao itaabudiwa tu!
Pesa hutiwa nguvu na hasa na mali asili zinazomilikiwa na nchi na nchi kuwa tayari kuziingiza soko la kimataifa. Kwa kigezo hicho marekani huwezi kuilinganisha na nchi kama Urusi na China.

Biashara kubwa ya marekani ni silaha! wakati wa amani hakuna anayehitaji silaha, na ni mataifa mengi yanayozalisha silaha kwa bei nafuu zaidi. kwa hiyo silaha haiwezi kuwa na mchango kwenye thamani ya silaha. Ndiyo maana marekani wanachochea sana vita duniani.
 
China na Mrusi wana SWIFT zao ambazo kwa sasa wapo ktk kuona wana wezaje kuzifanya zifanye kazi duniani ktk masuala ya biashara za kimataifa za kutuma pesa...

sio kwamba hazikuwepo...

The Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunication, SWIFT ya mmarekani

System for Transfer of Financial Messages (SPFS) ya mrusi

the Cross-Border Interbank Payment System (CIPS) ya mchina...

hivyo mrusi anataka kutumia system moja na mchina ambayo ni CIPS kimataifa ila katka matumizi ya ndani ya nchi ataendelea kutumia SPFS
 
Thamani ya fedha inategemea na utegemezi wa bidhaa na mahitaji ya nchi yako.

USA thamani ya fedha yake ni kubwa kwa sababu anazalisha bidhaa nyingi zinazotegemewa na watumiaji wengi duniani

Sasa wewe ulazimishe itumike fedha katika mauzo ya bidhaa ipi?
 
Si kweli, thamani ya pesa inatokana na what you produce to the world. Kila kitu kinapatikana USA, kila nchi inahitaji kitu from USA, fedha yao itaabudiwa tu!
No
Huu mchezo wa kuchapa pesa ndio mchezo wao.
Marekani inaweza kuchapa pesa na kuzitia kwenye mfuko kisha kuja direct Tanzania kununua dhahabu , rubi n.k
Ila wewe huwezi kuchapa pesa zako za Kitanzania na kuzibeba kama zilivyo kwenda kununua kitu US.
 
China na Mrusi wana SWIFT zao ambazo kwa sasa wapo ktk kuona wana wezaje kuzifanya zifanye kazi duniani ktk masuala ya biashara za kimataifa za kutuma pesa...

sio kwamba hazikuwepo...

The Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunication, SWIFT ya mmarekani

System for Transfer of Financial Messages (SPFS) ya mrusi

the Cross-Border Interbank Payment System (CIPS) ya mchina...

hivyo mrusi anataka kutumia system moja na mchina ambayo ni CIPS kimataifa ila katka matumizi ya ndani ya nchi ataendelea kutumia SPFS
Nimeongeza kitu hapa kichwani SPFS na CIPS.
 
Marekani iliipiga changa ya macho dunia kwa muda mrefu. Ikalazimisha dola iwe ndio pesa rasmi katika biashara za kimataifa na uchumi wa dunia. Wanachofanya ni kuchapisha noti tu za dola na kuipa thamani kwa kauli tu.

Dunia nayo ikawa imejikuta inakubaliana na changa hilo la macho. Lakini Urusi imeiamsha dunia na marekani imepaniki. Urusi imesema kila nchi inaweza kutumia pesa yake ya ndani kwenye miamala ya kimataifa.

Uamuzi huo ghafla ukairudishia thamani pesa yake ya ruble iliyokuwa imeshuka sana thamani kwa zaidi ya asilimia 90.

Kwa sasa mataifa kama india, China, Brazili tayari yamejifunza kitu na yataanza kutumia pesa za mataifa yao kwenye biashara baina yao na mataifa mengine yatakayokubali.

Urusi imeandaa mfumo wake kama ule wa SWIFT kwa ajili ya miamala ya kimataifa na nchi zimeshajiunga tayari na kwa kuanzia mataifa hayo (ukiacha mataifa ambayo hayaogopi kitu kama India na China) hayataainishwa ili kuyakinga na vitisho na vikwazo vya marekani.

Ndio maana Marekani inahaha kuongeza vikwazo kila siku na kupeleka silaha ukraine, si kwa kuwa inaipenda sana ukraine lakini inataka kuangusha kabisa uchumi wa urusi na kuipunguza nguvu kijeshi.

Japo mpaka sasa marekani inaonekana haijafanikiwa kwa hilo ila mambo yanaigeukia yenyewe kuwa mabaya!
Unaupeo mdogo sana marekani ana nguvu sababu ya kuwa na GDP kubwa ndo sababu ya ela yake kuwa na nguvu na sio kingine
 
Si kweli, thamani ya pesa inatokana na what you produce to the world. Kila kitu kinapatikana USA, kila nchi inahitaji kitu from USA, fedha yao itaabudiwa tu!
Mkuu US anachapisha Note, ni scandal ya Biden na ipo verified na source za kimarekani pia, wana inflation kubwa sasa hivi na naona wanataka kuanzisha pesa mpya Digital Usd.
 
Back
Top Bottom