Dunia imechelewa mno kuishtukia Marekani kuhusu utawala wa pesa yake DOLA katika uchumi wa dunia. Angalau sasa wameishtukia

Dunia imechelewa mno kuishtukia Marekani kuhusu utawala wa pesa yake DOLA katika uchumi wa dunia. Angalau sasa wameishtukia

Unaupeo mdogo sana marekani ana nguvu sababu ya kuwa na GDP kubwa ndo sababu ya ela yake kuwa na nguvu na sio kingine
Kuwait hana Gdp kubwa na thamani ya Hela ipo juu mara kibao kuliko dollar. China ana uchumi mkubwa ila hela yao haina thamani kivile.

Jambo la Muhimu kiuchumi ni hela Kuwa stable, jinsi hela yako isiposhuka thamani ndio inakuwa na nguvu, ila kama hela hata kama ina thamani ila haieleweiki mara inapanda mara inashuka tegemea investors kuikimbia.
 
Inflation ipo Dunia kote hata Tanzania Kuna inflation kubwa sana ebu acha ushabiki
Kawaambie Usa wenyewe sio mimi, wao ndio wanalalamika. Wanalalamika policy za Biden ndio zinasababisha.

Marekani hakutakiwa kuathiriwa na Urusi kama Ulaya, Hategemei sana Gas na Mafuta Toka Urusi
 
Kuwait hana Gdp kubwa na thamani ya Hela ipo juu mara kibao kuliko dollar. China ana uchumi mkubwa ila hela yao haina thamani kivile.

Jambo la Muhimu kiuchumi ni hela Kuwa stable, jinsi hela yako isiposhuka thamani ndio inakuwa na nguvu, ila kama hela hata kama ina thamani ila haieleweiki mara inapanda mara inashuka tegemea investors kuikimbia.
Tofautisha thaman ya ela na ela kutumiwa sana kama USD nani ambaye ana angaika na hela ya Kuwait
 
Kawaambie Usa wenyewe sio mimi, wao ndio wanalalamika. Wanalalamika policy za Biden ndio zinasababisha.

Marekani hakutakiwa kuathiriwa na Urusi kama Ulaya, Hategemei sana Gas na Mafuta Toka Urusi
Utakua unakaa kwa baba ndo maana hujui kwamba Tanzania nako Kuna inflation, na kwakukusaidia tokea mwaka jana tatizo la inflation lilikuwepo Dunia nzima ni lilishababishwa na corona kabla hata ya vita ya urusi
 
China na Mrusi wana SWIFT zao ambazo kwa sasa wapo ktk kuona wana wezaje kuzifanya zifanye kazi duniani ktk masuala ya biashara za kimataifa za kutuma pesa...

sio kwamba hazikuwepo...

The Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunication, SWIFT ya mmarekani

System for Transfer of Financial Messages (SPFS) ya mrusi

the Cross-Border Interbank Payment System (CIPS) ya mchina...

hivyo mrusi anataka kutumia system moja na mchina ambayo ni CIPS kimataifa ila katka matumizi ya ndani ya nchi ataendelea kutumia SPFS
Nashukuru nimeongeza kitu kichwani
 
Utakua unakaa kwa baba ndo maana hujui kwamba Tanzania nako Kuna inflation, na kwakukusaidia tokea mwaka jana tatizo la inflation lilikuwepo Dunia nzima ni lilishababishwa na corona kabla hata ya vita ya urusi
Inflation ya double digit? Hebu tupe proof
 
Unaupeo mdogo sana marekani ana nguvu sababu ya kuwa na GDP kubwa ndo sababu ya ela yake kuwa na nguvu na sio kingine
Kama ni kuhusu usafirishaji wa bidhaa duniani, hakuna taifa linalouza bidhaa nyingi duniani kama China. Marekani wanategemea kuanzisha vita duniani ili wauze silaha. Marekani wana mgogoro wa kuchapisha dola!!! Arobaini yao imefika, mataifa mengi yameshaanza kuishtukia! Na inahaha kweli!!
 
Marekani iliipiga changa ya macho dunia kwa muda mrefu. Ikalazimisha dola iwe ndio pesa rasmi katika biashara za kimataifa na uchumi wa dunia. Wanachofanya ni kuchapisha noti tu za dola na kuipa thamani kwa kauli tu.

Dunia nayo ikawa imejikuta inakubaliana na changa hilo la macho. Lakini Urusi imeiamsha dunia na marekani imepaniki. Urusi imesema kila nchi inaweza kutumia pesa yake ya ndani kwenye miamala ya kimataifa.

Uamuzi huo ghafla ukairudishia thamani pesa yake ya ruble iliyokuwa imeshuka sana thamani kwa zaidi ya asilimia 90.

Kwa sasa mataifa kama india, China, Brazili tayari yamejifunza kitu na yataanza kutumia pesa za mataifa yao kwenye biashara baina yao na mataifa mengine yatakayokubali.

Urusi imeandaa mfumo wake kama ule wa SWIFT kwa ajili ya miamala ya kimataifa na nchi zimeshajiunga tayari na kwa kuanzia mataifa hayo (ukiacha mataifa ambayo hayaogopi kitu kama India na China) hayataainishwa ili kuyakinga na vitisho na vikwazo vya marekani.

Ndio maana Marekani inahaha kuongeza vikwazo kila siku na kupeleka silaha ukraine, si kwa kuwa inaipenda sana ukraine lakini inataka kuangusha kabisa uchumi wa urusi na kuipunguza nguvu kijeshi.

Japo mpaka sasa marekani inaonekana haijafanikiwa kwa hilo ila mambo yanaigeukia yenyewe kuwa mabaya!
Kama vile namuona J.Biden anavyozidi kuwa mwekundu...
 
Kama ni kuhusu usafirishaji wa bidhaa duniani, hakuna taifa linalouza bidhaa nyingi duniani kama China. Marekani wanategemea kuanzisha vita duniani ili wauze silaha. Marekani wana mgogoro wa kuchapisha dola!!! Arobaini yao imefika, mataifa mengi yameshaanza kuishtukia! Na inahaha kweli!!
Sio kweli asingekua na GDP kubwa na china anaoneka anauza sababu ana devalue yuan
 
Hii platform tunayotumia kubishana hapa. Ni product ya mmarekani
Iwe unatumia android , ios window linux etc
Nadhani hoja haijajibiwa $ kabla hata ya utandawazi ndio ilikuwa inatumika kama pesa ya manunuzi sasa product kama hii window unayosema imekuja dola inatumika. kumbuka pia hizi kampuni za kia america hata Google kuna watu wengi wana share humo hata sio watu wa USA. Lakini tukija kwenye point sababu kuu ya $ kuwa ilivyo leo ni makubaliano ya nchi 44 mwaka 1944 wanaita makubaliano ya Bretton woods agreement kuwa USA kama world reserve kutoka na kuwa na uchumi imara na uwezo wao mkubwa wa kulipa madeni yao. Miaka ya nyuma walikuwa wakilipwa dhahabu kufanya biashara na wakawa na akiba kubwa ya dhahabu duniani. baada ya dhahabu kuondoka kama sehemu ya malipo ikawa option $ kuwa pesa ya kutumika( kumbuka ni makubaliano) sababu za msingi ni utajiri wake na uwezi wa kuhudumia madeni yao, lakini hili linajulikana kuwa EURO ilipewa heshima yake ila hawakuwa na reserve moja kuu na hata wao wanakiri China ndio pekee anaweza kuireplace $ na sababu ziko nyingi akiba yake ya pesa na uchumi wao. Kikubwa wakati ule 1944 nchi tajiri duniani ilikuwa USA kwa mbali mpaka sasa ila gap limepungua sana sababu kuna utajiri mkubwa umeenea nchi zingine kama China. Kumalizia haikuwa kwa sababu wanazalisha sana hapana ila makubaliano na kulikuwa na sababu ya kuchagua $ walikuwa stable na akiba kubwa ya dhahabu duniani na pia security ya system yao reserve ilikuwa imara na mpaka sasa ila leo hata ukiwa na Yuan wanakubali ukiwa na Euro wanakubali ukiwa na na Yen wanakubali hata pound wanakubali kwa hiyo kuna ushindani sio kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
Kama ni kuhusu usafirishaji wa bidhaa duniani, hakuna taifa linalouza bidhaa nyingi duniani kama China. Marekani wanategemea kuanzisha vita duniani ili wauze silaha. Marekani wana mgogoro wa kuchapisha dola!!! Arobaini yao imefika, mataifa mengi yameshaanza kuishtukia! Na inahaha kweli!!
Unaposema sema ndio anazalisha na kusafirisha, kwani mkuu unajua mchango wa US na Ulaya ktk uwekezaji ktk Taifa la China?
 
Si kweli, thamani ya pesa inatokana na what you produce to the world. Kila kitu kinapatikana USA, kila nchi inahitaji kitu from USA, fedha yao itaabudiwa tu!
Kwa hiyo sisi tunaifanyia ibada ile ya china? mana kila kitu afrika tunatoa huko
 
Back
Top Bottom