Nadhani hoja haijajibiwa $ kabla hata ya utandawazi ndio ilikuwa inatumika kama pesa ya manunuzi sasa product kama hii window unayosema imekuja dola inatumika. kumbuka pia hizi kampuni za kia america hata Google kuna watu wengi wana share humo hata sio watu wa USA. Lakini tukija kwenye point sababu kuu ya $ kuwa ilivyo leo ni makubaliano ya nchi 44 mwaka 1944 wanaita makubaliano ya Bretton woods agreement kuwa USA kama world reserve kutoka na kuwa na uchumi imara na uwezo wao mkubwa wa kulipa madeni yao. Miaka ya nyuma walikuwa wakilipwa dhahabu kufanya biashara na wakawa na akiba kubwa ya dhahabu duniani. baada ya dhahabu kuondoka kama sehemu ya malipo ikawa option $ kuwa pesa ya kutumika( kumbuka ni makubaliano) sababu za msingi ni utajiri wake na uwezi wa kuhudumia madeni yao, lakini hili linajulikana kuwa EURO ilipewa heshima yake ila hawakuwa na reserve moja kuu na hata wao wanakiri China ndio pekee anaweza kuireplace $ na sababu ziko nyingi akiba yake ya pesa na uchumi wao. Kikubwa wakati ule 1944 nchi tajiri duniani ilikuwa USA kwa mbali mpaka sasa ila gap limepungua sana sababu kuna utajiri mkubwa umeenea nchi zingine kama China. Kumalizia haikuwa kwa sababu wanazalisha sana hapana ila makubaliano na kulikuwa na sababu ya kuchagua $ walikuwa stable na akiba kubwa ya dhahabu duniani na pia security ya system yao reserve ilikuwa imara na mpaka sasa ila leo hata ukiwa na Yuan wanakubali ukiwa na Euro wanakubali ukiwa na na Yen wanakubali hata pound wanakubali kwa hiyo kuna ushindani sio kama ilivyokuwa huko nyuma.