Dunia ni ya ajabu sana. Hadi Sasa sielewi hii dunia imeanza wapi na lengo la watu kuletwa hapa ni nini?

Ila boss mbona mtu akiombewa mchungaji akisema Toka mtu anarudi kwenye Hali yake ya kawaida
Majini hayapo mkuu.

Wachungaji na waumini wao ni waigizaji tu.

Hakuna chochote hapo, wanataka hela tu. Ndio maana wanafanya maigizo yote hayo.
 
Wewe ni mmoja kati ya hao uliowataja?
 
Sasa kwani lazima kila mtu apandwe na majini?
Mbona mimi sijawahi kupandwa na majini?
Umaskini ukikolea sana unageuka uwendawazimu, Hao wanaoanguka Angalia aina ya maisha yao ndo utaelewa.
Ushawahi kuona tajiri, viongozi, watu waarufu wakianguka mapepo?
Hapana, kwa sababu hawana ule uwendawazimu wa umasikini
 
Hilo haliwezekani.
Unabisha kwa sababu haijawahi kukutokea ila mimi nina ushahidi na hilo
Nakusihi tafuta mwenye majini ya ukweli sio ya kuigiza halafu ujaribu kumuuliza kuhusu mambo yako uone atajibu nini halafu uje utoe ushuhuda
 
Umaskini ukikolea sana unageuka uwendawazimu, Hao wanaoanguka Angalia aina ya maisha yao ndo utaelewa.
Ushawahi kuona tajiri, viongozi, watu waarufu wakianguka mapepo?
Hapana, kwa sababu hawana ule uwendawazimu wa umasikini
Au labda tuseme majini wanachagua watu maskini?
Ila kuwa na majini sio lazima upandishe
 
Majini hayapo mkuu.

Wachungaji na waumini wao ni waigizaji tu.

Hakuna chochote hapo, wanataka hela tu. Ndio maana wanafanya maigizo yote hayo.
Miaka ya nyuma kidogo Kuna jirani Yetu ilikuwa inasemekana ana majini ikifika tarehe fulani anakamata kuku ananyonya damu na Kuna wakati alitaka kujidhuru na kisu lakini akiombewa anakuwa sawa.

How do you explain such a scenario?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…