Nilipigwa hivyo hivyo 🤣🤣... Show yangu ilikuwa hivi
Bidada hatukuonana muda Sana Pindi chuoni nilimpenda Sana akanikazia ana mahusiano nikaelewa Maisha yakaendelea. After 5years naona namba ngeni kupokea yeye aka yangu ilikuwa famous chuoni aliniita hivyo, Kwanza alianza na sorry nyiiiingi then she told me "kitumbua kimeingia mchanga" sikumuelewa bana kumbe anamaanisha ana mtoto, akataka tuonane ikawa hivyo na kuna sehemu patuliivu tuonane 😅😅 kila kitu juu yake, Mimi nikawaza Hawa watu wanaweza kukuabisha ukiwasikiliza hata kama wako njema 🤣🤣. Siku imefika nimefatwa na Bolt yeye akiwemo, tumefika as gentleman nikatoa Hela ya usafiri. Stori za hapa na pale mara menu hiyo baada ya order, I miss you kibaoo nilienda na Akili mbili 😅😅, sasa huwa sitembei na wallet maana huwa na msemo wangu za wallet hazikai nyingiii, huwa nasikia raha Sana nikitoa rubber band na huwa sina hulka ya kutoa pesa nyingi mbele ya mwanamke so natenga kiasi kadhaa pembeni. Nikaenda washroom nikiwa nimehaidiwa Leo ntapewa nilivyonyimwa miaka ileee, we bana ile sehemu tuliyoenda ina garden so ukitoka washroom naiona Meza yetu, nikamwona mhudumu anaweka bill pale wakati naongea na simu huku naangalia vinanyofanyika pale Mezani bi dada kaangalia bill hakuweka chochote akafunika kitabu 🤣🤣, nimefika anajifanya haoni kama bill basi nikalipa, stori zikaendelea mpaka tunaondoka nacheka moyoni..😂😅, kwake nilimshusha ahadi yake alidai anaenda mchukua mtoto wake nikasema poa. All in all nilifurahi kumuona ila alikuwa na yake kichwani, later alianza vizinga Kwa njia ya mkopo hapo ana Kazi nzuri tu, nikamfutilia mbali alijua nitamzingatia Sana. Baadhi ya wanawake Mungu anawaona asee 😂😂😂