Duniani kote usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote. SGR tulitegemea kuwa kiama cha usafiri wa mabasi na malori, imeshindikana

~ Hivyo ndivyo ingalikuwa kwa usafirishaji wa abiria. Trip moja ya passenger train yenye urefu wa si chini ya kilomita 3 ingalikuwa sawa na mabasi yasiyopungua 500 na wangalisafirishwa kwa raha kwa spidi ya 170 kph.
Sasa ulijaribu kufikiria economic impact ya kuondoa hayo mabasi 500 barabarani?!

Ni madereva wangapi hao ambao utaondoa ajira zao?

Utakuwa umeondoa ajira za makonda wangapi?

Utakuwa umeondoa ajira za wakata tiketi wangapi?

Itakuwa umeathiri soko la Mama Lishe wangapi?

Turudi kwenye macroeconomic...

Utakuwa umepunguza lita ngapi za mafuta ambazo zingetumika na hayo mabasi 500... mafuta ambayo yangeleta kodi?!

Ungeathiri kodi ya kiasi gani ya uagizaji mabasi kwa siku za baadae?!

Uchumi hauendi hivyo...
 
Mkiu hebu nitonye jina la huyo mmiliki maana amanikwaza natamani niruke nae
Watoa maamuzi wengi ndo wenye makampuni ya usafirishaji. Wapo kuanzia bungeni na kwingineko.

Hivi unategemea mtu kama huyu atasema nini when it comes to kuamua nauli na uebdeshaji wa reli?
 
Aliyekudanganya nani hiyo MGR itaondolewa, huoni reli imeboreshwa na kuzidi kuboreshwa kutoka 45,56, 60 pounds hadi 80 pounds huoni zinanunuliwa advanced diesel electric locomotives, huoni yananunuliwa mabehewa mapya ebu acha kupotosha watu.

South Africa wana meter gauge, cape gauge na standard gauge hadi leo hii, ukitazama India wana standard gauge, broad gauge na bado hiyo meter gauge hawajaicha.

Kuna haja gani ya kufanya maboresho makubwa ikiwa wanahitaji kuiacha hiyo reli fuatilia kwanza ndo uandike siyo unakurupuka.
 
Yale mabehewa hayajawa adjusted katika Axle. Yametoka huko South Korea hivyo hivyo na axle yenye 1000mm kwa ajili ya kuhudumu katika reli ya meter gauge. Hao viongozi wenu tu ndiyo wamejichanganya namna ya kuuleza umma wa watanzania.

Manufacturer yeye anapewa specifications anakutengenezea kitu kwendana na hitaji lako yapo ya meter gauge na yapo ya standard gauge vile vile, uliyoyaona yanafanyiwa test juzi kati yale ni ya meter gauge Mzee.
 
Yamekuja ya SGR na pamoja na ya MGR ila rang za behewa zinafanana na muundo ndo mana watu wanachanganya fatlia page za TRC utaona utofauti
 
Reli ya Uhuru aliyotujengewa mkoloni tumeishidwa itakuwa hii SGR.

Tanzania tunatumia 1% ya uwezo wetu wa kufikiri...hii yaweza kuwa kweli.
Akili hizi ndiyo napenda kuzisikiliza maoni yake, mfano reli ya TAZARA tu ilikamilika ikiwa advanced kuliko ile ya kati ya mkoloni kaitazame leo inasikitisha mno.

Sasa tunajengewa reli ambayo ipo very advanced kuliko ile katika mambo mbali mbali ngoja Korail wamalize muda wa kuisimamia waachiwe wabongo uone shoo yake.
 
Wapi duniani usafiri wa treni ya haraka bei rahisi? Tupe mfano wa nchi 3 tu duniani?

Mtu uko Chato huko hata Dubai tu hujafika unaleta uongo wako hapa.
Hebu usiwe mjinga ww nimepanda Treni kutoka hongkong mpaka china lakin pia nimepanda train za under ground kama dala dala duniani pote trein ndio usafiri rahisi sio kila kitu kupinga Pinga tu na aslimia kubwa hizo treni wanafanya kama huduma kwa jamii sio biashara
 
Yamekuja ya SGR na pamoja na ya MGR ila rang za behewa zinafanana na muundo ndo mana watu wanachanganya fatlia page za TRC utaona utofauti
Yah sijakataa yapo SGR na MGR ila ambayo yameanza test ni ya MGR kwa 400km yani kutoka Dar to Moro (200km) na kurudi.
 

Hilo jina ulilotaja baada ya Kadogosa kuna mzee mmoja rafiki yangu sana msukuma ni contractor mnene sanaaaa halafu huwa havai suruali akiwa home anavaa shuka tu halafu anavaa kandambili kubwaaa, na hua hanywi chai anakunywa uji tu halafu ananywea kwenye sufuria, na mwisho kabisa ana mapengo, hana meno matatu matatu juu na chini ndo hua nae hilo jina analitaja hivyo kama wewe sasa nimejisikia kumkumbuka sana, nashukuru sana kwa kuipendezesha siku yangu.[emoji1317][emoji1317]
 
Watoa maamuzi wengi ndo wenye makampuni ya usafirishaji. Wapo kuanzia bungeni na kwingineko.

Hivi unategemea mtu kama huyu atasema nini when it comes to kuamua nauli na uebdeshaji wa reli?
NImekuelewa mkuu, na sasa naona kuna mzigo mpya wa majenereta umeingia
 
Watu kama wewe, mwendazake aliwapenda sana , maana bila hata kutumia common sense mnaleta suluhisho
Reli ni usafiri nafuu sana , ila inategemea na yo topography ya nchi husika , kuna muda reli inakuwa ni expesiive option .
Kwa nchi kama Tanzania ambapo kuna mazao kusini na soko lipo kanda ya ziwa , bandari mashariki inayohudumia kaskazini kusini na magharibi, makaa ya mawe kusini ambayo yanasafri kwenda pande zote, Reli haiqezi.kuleta suluhisho la kudumu wala unafuu, pendekezo la nauli za sgr zimewastua usingizini, the elites walishajua kuwa sgr haiwezi kuwa reli nafuu
 
Wapi duniani usafiri wa treni ya haraka bei rahisi? Tupe mfano wa nchi 3 tu duniani?

Mtu uko Chato huko hata Dubai tu hujafika unaleta uongo wako hapa.
Hata shuleni tumesomea hivyo,usafiri wa treni na meli ni bei rahisi na rafiki wa mazingira ulilinganisha na barabara,sema wewe unareta uchawa kwenye mambo ya msingi
 
So far so good, SGR popote duniani ni almost 3/4 ya tiketi ya ndege ila sio SGR ya kusimama simama kila mahali .

Pili SGR ya kusimama kila mahali bei ni bei ni ndogo zaidi
Kwan kuna tren ambazo zinaenda bila vituo kama ndege
 
Nchi hili ni la kipumbavu! Wamiliki wa malori na mabasi ni hao hao vingozi wa serikali sasa wanaona kabisa wakiiacha SGR ifanye inavyotaka watakosa wateja ndiyo maana wanafanya kila liwezekanalo kuihujumu! Na hili li maushungi linalaza mimacho tu! Bure kabisa!
 
Dr Akili naona unalitendea haki hilo jina lako. Naona kabisa unawajibu kwa facts hawa wanaokujibu kwa dhihaka. Wakati wenzako wanataka upanic ili muanze kutukanana mpigwe ban hii thread ionekane takataka [emoji23][emoji23][emoji23].. Akili nyingi [emoji848]
 
Bahasha zinaangamiza Taifa ndugu yangu!
 
Mi naona tunatoka kwenye ujamaa taratibu na tunatakiwa tutoke uko kabisa ili watu wawe serious na Maisha. MTU unakuta anazaa watoto 11 alafu Kwa mke mmoja alafu anawake watatu bhado wa njee alafu ni maskin wa kutupwa sasa hao matoto Yao ndo yanata kilakitu serikali iweke vya burebure lakin hawaangali matrilioni ambayo serikali imetumia zikiaribika utawaona uku jfee wanatukana serikali. Kama MTU unaona ni gali panda basi zako ulizozoea kwan kuna mkoa ambao bhas alifiki, siyo lazma upande Tu kwasababu ni kitu kipya kimekuja panda basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…