Duniani kote usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote. SGR tulitegemea kuwa kiama cha usafiri wa mabasi na malori, imeshindikana

SGR haitafanya kazi wapiga dili wanashindana kununua mabasi balaa
 
Sio kweli...
Nimesoma heading tu ya bandiko pasi kusoma nyama yake!

Fanya utafiti tena, utanishukuru baadae...
 
Weka takwimu siyo kubwabwaja tu mambo ya vijiweni
 
Wapi duniani usafiri wa treni ya haraka bei rahisi? Tupe mfano wa nchi 3 tu duniani?

Mtu uko Chato huko hata Dubai tu hujafika unaleta uongo wako hapa.
Aweke takwimu siyo atuletee mambo ya vijiweni
 
Mwanzoni Viongozi wakati wanautetee huu Mradi, walikua wanasema Watu watasafiri kwa kulipa nauli kwa nafuu kuliko Ma bus!

Sasa naona Lugha imebadirika.

Wenye Ma bus na Maroli walikua na wakati Mgumu sana, lakini mara baada ya Mapendekezo ya Nauli kutoka, Wanaacheeeeeka kwa Dharauuuuu!!!
 
Kwan kuna tren ambazo zinaenda bila vituo kama ndege
Asante kwa swali nzuri.
Mfano china kuna High speed SGR ambayo inatokea Guanzhou kwenda Beijing ambapo ni almost Kms 3000.
Train inakimbia almost 360-450 kms/hr so inasimama vituo vichache sana ili kufika Beijing.na njia yake imejengwa juu kwa juu kama daraja .
 
Munashangaza kidogo munapotutolea mifano ya nchi kama za Afrika kusini, India na nchi zingine ambazo tuko nazo kundi moja la low income countries. Semeni ni nchi gani ya kundi la high income country utakuta reli za MGR kwa sasa? Walikuwa nazo lakini kwa sasa walisha zitupilia mbali. Nenda uingereza, ufaransa hata japan hutazikuta. Na sisi ndiko tunakoelekea kwenye uchumi wa juu. Ni miaka mingapi ijayo tutafika huko ni suala jingine lakini kwa sarakasi hizi za mafisadi na mabeberu, ni dhahiri kwamba inaweza kutuchukua hadi kiama!
 
Weka takwimu siyo kubwabwaja tu mambo ya vijiweni
Aweke takwimu siyo atuletee mambo ya vijiweni
Labda ya kijiweni
Natumaini vijana mnajua kusoma kimombo. Someni angalao hapa, halafu mtupe mrejesho.

 


Abiria ni nyongeza tu treni imetengenezwa kwasababu ya mizigo sio abiria. Kiuchumi kama ni abiria pekee ni hasara
 
Bw. Kamundu, habari za huko USA?
Utakubaliana na mimi kuwa USA, nchi yenye ukubwa wa eneo la 9.8 million square km (mara 10 ya eneo la Tanzania), ni kati ya nchi chache duniani ambazo usafiri wa reli siyo maarufu. Trains are not popular means of passenger and goods transportation. Ni tofauti sana na nchi kama za ulaya. Nchi ya China yenye ukubwa wa eneo sawa na USA (9.6 million square km) lakini lenye idadi ya watu mara 5 ya wale walioko USA, ndiyo magwiji wa usafiri wa reli. Reli zilizoko USA ni mali za makampuni za watu binafsi walizozijenga kwa ajili ya kusafirisha mizigo mikubwa kwenda nchi jirani, na hasa Canada ambayo ukubwa wake wa eneo unapita kidogo lile la USA lakini lina population ndogo sana sawa na ya Burundi. Hivyo usafiri wa ndani ya USA ni malori, mabasi na ndege. Domestic air travel in America is very cheap and more popular means of passenger travel than bus transport. Nadhani utakubaliana nami kuwa hakuna bullet trains huko Amerika. Usafiri wa reli si jadi wala utamaduni wa Amerika. Utamaduni wao ni usafiri wa anga ambao bei yake kwao ni nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu. Mathalani tulifikia nauli ya kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kuwa sawa na nauli ya kutoka Dar es Salaam hadi New York.

Hizo nchi za ulaya magharibi ni tu nchi tudogo dogo sana lakini tu tajiri sana. Yaani jumla la eneo lake combined halilifikii eneo la Tanzania lakini population yake ni zaidi ya mara 10 ya population ya Tanzania. Yaani kwa mfano nchi kama England eneo lake ni sawa na la mkoa wa Mwanza lakini population yake ni watu million 68 (zaidi ya population ya Tanzania ambayo ni 61 million) wakati population ya Mwanza ni watu million 3.8 tu. Hizi ndizo nchi ambazo most popular domestic mode of passenger and goods transportation is railway. Na treni zao ndizo hizo bullet trains zenye kasi kama ya ndege lakini gharama yake ya nauli zake ni ndogo kuliko ya mabasi. Yaani bullet trains ndiyo daladala zao za mijini na safari za kuunganisha miji na miji ambayo iko karibu karibu tu siyo kama ya kwetu. Kwa mfano kutoka mji wa London hadi mji wa Oxford ni kilomita 82, hadi mji wa Birmingam kilomita 163 na hadi mji wa Bristol ni kilomita 171 tu; yaani ni safari kama za kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze au kutoka Mwanza hadi mjini Magu tu ndiko unaenda kwa bullet speed na ndani ya dakika zisizozidi 15 unakuwa umeshafika huko. Unaweza pia kutoka London hadi mji wa Paris nchini Ufaransa ambao ni mwendo wa kilomita 344 kwa bullet train na kutumia kama saa mmoja tu. Huu ni kama mwendo wa kutoka Dar hadi Morogoro.

Hivyo mazingira na malengo yetu ni tofauti sana na hayo ya EU countries au USA na Japapan. Ya kwetu yanafanana na ya nchi kama ya Uchina.
 


Mimi tatizo langu ni wewe kutumia neno “Dunia nzima” kitu ambacho sio kweli. Mimi nimepita Europe hata mwezi haujaisha kuna treni zina bei zaidi ya ndege lakini naongelea treni mwendo kasi. Mimi naomba tu usitumie majina ya umoja kama Dunia nzima. Vilevile sema kwamba ni mawazo yako usi andike mawazo yako kama facts wakati ni mawazo!
 
linalowezekana kwingine dunia Tanzania huwa ni gumu sana na lisilowezekana kwingine duniani Tanzania huwa linawezekana... Tanzania ni nchi ipo Duniani hapa lakini inautaratibu tofauti kabisa na nchi yeyote katika dunia hii.
 
LATRA na Rushwa za wamiliki Wa mabasi ni Ndugu moja!!

Wamefunga vingamuzi kwenye mabasi Kwa ajili ya kudhibiti mwendo Kasi Badala ya kufunga kingamuzi pamoja na speed limit kama Kenya na nchi nyingine za Afrika ambapo gari za mizigo na Abiria speed zimedhibitiwa kwenye accelerator . Huwezi kutembea zadi ya speed iliyotajwa Kisheria. Ukichakachua speed limit Kingamuzi kinasoma unafungiwa KUFANYA Biashara hiyo.

Huku Tanzania LATRA inatunga kanuni Kila Siku za speed lakini kinachoendelea ni kuwekeana mikeka ya mamilioni kwenye vikampuni vidogo vya mabasi Ili vikome kushindana na Akina ESTÁ wanaokimbia kama treni ya mwendo Kasi.

Hata treni ya mwendo Kasi Kwa Sasa itakua ni mradi mfu mana wenye kulamba asali wamejipanga Kila eneo kuhakikisha utajiri Wa Nchi hii unamilikiwa na familia za watu Wa Chache waliopewa nchi kilaini kabisa na SIO Kwa kumwaga damu kama walivyofanya Akina Kenyatta Kule Kenya.

Ni Sanaa tupu Wenye Malory na mabasi ni wengi ni walamba asali. Wenye treni ni watanzania wanyonge wasio na mtetezi zaidi ya kuambiwa kuwa washukuru Kwa kile kinachofanywa na serikali mana baba ZAO hawajajenga Hata choo Cha shimo sembuse CHUO kikuu.
"CHUO ulichosoma amajenga baba yako"
 
Toeni CCM mtafikia malengo mnayoyategemea.....kikubwa wanachofanya Hawa ni low thinking na kukandamiza demokrasia kwa gharama za Kodi zetu
 
Hizo mantiki (logics) za ufikiri wa mtindo huo, huwa hazina mashiko na ni fikira potofu au fikira mgando.
Wacha wee...

Tuna Bush Lawyers, na bila shaka tunao Bush Economists!
Huoni aibu unavyojaribu kulinganisha labor intensive state vs highly advanced states?!

Unalinganisha nchi zinazozalisha malaki ya ajira kwa mwaka na hivyo kuwezesha labor movements among sectors of economy wakati nchi yako haina uwezo huo!!

Unalinganisha nchi ambazo zina malaki kwa malaki ya fursa huku nchi yako ikiwa na limited opportunities...

In short, as usual, uelewa wako katika masuala ya uchumi ni duni!!
Aina nyingi za kazi kwa sasa hazina tena soko la ajira duniani.
Acha kukariri... tunazungumzia Tanzania na sio kwingineko duniani!!

All economic practices zinazofanyika kwa kuangalia kwingine duniani badala ya kuangalia mazingira ya nchi husika kwa kawaida ni practices zinazoishia kufeli.

Na ndo maana, back in 1993, akihutubia Jukwaa la Uongozi, Afrika, Lee Kuan Yew, aliyeipaisha Singapore alielezea jukwaa hilo sera zake zilzoifanya Singapore kuwa ilipo. Baada ya kueleza mengi, kisha akasema haya:-

Hata vyuo vyingi vimeshasitisha au kupunguza sana ufundishaji wa kozi hizo.
Kozi zipi?

We jamaa mbona MUONGO SANA wewe?!
Leo hii kwa kubonyeza tu kitufe, komputa yako inaanza kutaipu unachokisema tena kwa spidi kali bila makosa kuliko typist au sekretare uliyemwajiri.
Kwahiyo hapo ndo tayari unadhani unafahamu vema masuala ya teknolojia na impact yake kwenye uchumi, ama?!

Before 2015 nimefanya sana kazi za freelancing, na moja ya lucrative gigs ilikuwa Translation kabla ya Wakenya hawajavamia.

Pamoja na kwamba zilikuwa translation softwares lakini bado ALL TIME Clients walilisisitiza Manual Translation!

Nalazimika kutoa hiyo mifano ingawaje hapakuwa na sababu za msingi kwa sababu hapa tunazungumzia ni namna gani unaweza kushabikia suala la kuondoa mabasi 500 kwenye mzunguko bila kuangalia economic impact. Hata hivyo, hapa unaishia kutoa mifano ambayo ni VERY IRRELEVANT.
Mfano mwingine IRRELEVANT... Jikite kwenye hoja!
Watatafuta kazi zingine hususani za kilimo kwani tuna ardhi tele hadi nusu ya ardhi yetu tumeachia wakae nyumbu zetu, tembo, fisi na wanyama wengine.
Sasa kwa akili zako hizo si utasema huko nako tutumie robot kwenye huu ambao tunaelekea kwenye Agricultural AI !
Hayo mafuta ya mabasi na malori yatakayo okolewa yatatumika sehemu zingine za kiuchumi hasa viwandani na kilimo.
Kwanini yasiendelee kutumika huko kwenye mabasi kisha tukaangiza mafuta mengine kwa ajili ya huko kwingine?
Huu ndiyo uchumi wa leo ambao tulitegemea hizi treni za kisasa zingalitusaidia kutuvusha.
Kausome uchumi, na uuelewe!

Uchumi ni moja ya nyanja ambazo hazitaki kukariri bali kuelewa!
Tusikubali kushindwa na mafisadi.
Ni wapi Mafisadi wanaweza kufaidika zaidi kati ya kuondoa mabasi barabarani na kuyaacha mabasi barabarani?

Kama reliable mode of transportation itabaki kuwa treni peke yake ina maana major players watakuwa Wanasiasa na Government Officials...

Hao ndio watatoa tenda za ku-supply nishati ili treni iendelee kuwa operational...

Hao ndio watatoa tenda za vyakula ili treni ziweze kuuza vyakula

Hao ndo watakamatia ajira kwenye sekta ya usafiri...

Hao ndo watakamatia tenda za kuagiza mabehewa mengi zaidi kwa sababu demand ni kubwa kutokana na monopoly..., and so on!

What about mabasi?

Kusoma
hujuji, ina maana hata picha ukutani huzioni?
 
Pole sana kama jina la title ya thread hii limekukwaza. Bila shaka kama ingaliandikwa, "Duniani kote isipokuwa nchi chache kama USA, usafiri wa reli ndiyo rahisi kuliko wote ....", bila shaka haungalikwazika.

Licha ya maneno kuwa mengi, title kama hiyo ingalikosa nguvu na kupuuzwa on the spot na hawa jamaa zetu walengwa ambao wamekuwa wakituzengua sana hapa nchini Tanzania kila siku kwa masilahi yao binafsi. Jamaa hawa ni pamoja na TRC, LATRA, wafanya biashara wakubwa wa usafiri wa mabasi, semi trailer lorries na baadhi ya wanasiasa. Jamaa hawa wamekuwa wakiwaaminisha wananchi wetu kila kukicha kwamba America na nchi za EU ndiyo dunia. Na kwamba kinachofanyika America na ulaya ndiyo nasisi tunapaswa kukifanya. Wamefika hadi kututishia kwamba tutashitakiwa kwenye dunia tukishindwa kile dunia inataka tukifanye au tuishi. Hawa jamaa wanajifanya ni waumini wa mwimbaji maarufu wa USA, Michael Jackson aliyeimba, "We are the world" akiimanisha USA ndiyo dunia. Nadhani nimeeleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…