Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema


Mchambuzi naona ni vizuri tukiendelea kuelemishana. Kuna baadhi hapa hata hawajui kuwa mchakato wa Katiba ulianza na serikali ya awamu ya tatu.

Nakumbuka sana siku marehemu Rushagara alivyokuwa anaeleza jinsi alivyoona watu hawaelewi hata umhimu wa katiba. No wonder baadhi yetu wanaanza kumrushia mawe mzee warioba.

Issue ya serikali tatu imewaondoa wengi tu, na issue hii nusura iiparaganyishe CCM, nadhani kuna haja ya kuwakumbusha watu kuhusu G55, na tuwaulize watu wakati huo Warioba alikuwa wapi na anafanya nini. This time inaonekana CCM haitaparaganyika, lakini kuna mwelekeo wa Tanzania kuparaganyika.
 

Hadi dakika hii tukiwauliza baadhi ya watu kuhusu kwanini tuliungana, na kwanini tuendelee kuulinza muungano, majibu yanayotolewa ni ya kitoto sana.

Sasa hivi imefikia wakati hata wabunge wenyewe wanashindwa kuelewa kwanini tumeungana.

Mzee Sitta nadhani lengo lake kubwa ni kuangalia hadhi yake ndani ya CCM, na sio maslahi ya Taifa.
 

Swala la serikali tatu limekuwepo kwa miaka mingi, najua tume kadhaa zilikuja na mapendekezo ya serikali tatu mzee nyalali akiwa mmoja wao. That is not the issue, the issue ni kwamba kwenye swala sensitive kama hili huwezi kuja na solution ya kwamba tuna implement tatu and it's over.

The approach was total wrong just like the idea, huwezi kuwa na swala linalogawa nchi katikati halafu ukaja na approach ya kuwapa nusu moja, then what will happen to nusu nyingine? Go to hell au?

Mnapokosea mnaotaka serikali tatu ni kwamba hamtaki kingine chochote zaidi ya serikali tatu.
 

Nashukuru angalau umekubali Kwamba suala la serikali Tatu linaligawa nchi nusu; maswali yetu kwako:

1. Je ni kwanini nusu yenu Ndio nusu yenye kupewa Haki kuliko nusu nyingine?

Matamshi yako ni Yale Yale ya Balozi Sefue, Katibu Kiongozi Kwamba ambae amenukuliwa akisema hivi:
"Ni sahihi kwa bunge maalum kuweka Kando mjadala wa muungano kwa vile umeligawa taifa". Sefue anaenda Mbali zaidi na kusema: " muundo wa sasa wa muungano utabaki Kama ulivyosasa kwa kuwa bunge maalum la katiba limeshindwa Kupata maridhiano juu ya Jambo Hilo."

Swali letu la pili kwako:

2. Ikiwa serikali Inasema Kwamba hakuna muafaka Katika muundo wa serikali Tatu:
•Muafaka wa muundo wa serikali Mbili upo wapi?
•Maridhiano yake yanatokana na nini?
•Maridhiano yalifanyika lini
•Maridhiano yalifanyika wapi?







Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Kwa mbali tunaona matumaini, mwamko wa watz wa sasa sio ule wa zamani, ipo siku hata watoto wa primary watahoji uhalal wa muungano.
 
Kwa mbali tunaona matumaini, mwamko wa watz wa sasa sio ule wa zamani, ipo siku hata watoto wa primary watahoji uhalal wa muungano.

Wasi wasi wangu, watakapotambua kuwa hakuna majibu yamaswali muhimu, na watakapotambua kuwa muungano unawabebsha mzigo, asubuhiinayofuata muungano utakufa.

Tena, kwa njia mbaya sana maana hawana majibu yamaswali yao na hawataona sababu za kuhoji.
 


Bongolander ,unapoona serikali na bunge la CCM wanashindwa kutoa ufafanuzi wa vifungu,wanavikimbia ujue lipo jambo. Ukuliza kwanini trumeungana, majibu ya wengi na hapa namnukuu mwenzetu Mkandara ni kuwa watu wameoleana!!!

Imefika mahali Rais anashangilia katiba inayojibu kero za znz na wala si matatizo ya Watanganyika wanayoitumia.

Znz wanatumia katiba ya JMT kidogo sana, hii iliyoandikwa na akina Chenge/Sitta haina jipya bali kuwapendeza wznz kwa gharama zaWatanganyia.

Ninakuhakikishia 90 ya wabunge wa BMK-CCM hawajui muungano huu au mingine.
 
Last edited by a moderator:

Ndio maana tunasikiiza utuambie, kama Warioba alikosea, weweunadhani angefanya nini? Hebu tuanzie hapo
 

Mkuu kNguruvi3, nadhani uko sahihi. Slowly watu wanaamka. Kwa sasa inaonekana uwezo wa CCM kulunda Muungano kwa hoja umekwisha, kadiri watu wanavyoendelea kuamka kimawazo ndivyo hoja walizokuwa wanazitumia kuwadanya watu zamani hazina nguvu tena.

Nakukumba kuna wabunge niliwauliza kuhusu muungano majibu yalikuwa yanachekesha sana. Moja lilikuwa ndio hilo undugu wa damu na kuoleana, which in my view is absurd kwa kuwa ukiangalia jinsi tulivyooleana na wakenya basi maana yake ni kuwa tuungane nao, wanyarwanda waliojazana kule kagera na kuoleana na wenzetu wahaya basi nao tuungane nao.

Nashindwa kuelewa kwanini wafanya maamuzi ndani ya CCM hawataki kuangalia economic sense.

Katika hali ya kawaida mtu mwenye akili timamu au anayefikiri kwa usahihi ataangalia economic sense kwenye muungano kabla ya yote. Kuna mengine kama ya usalama. Inawezekana kuna sababu ya msingi sana ambayo ni muhimu kuliko uchumi, lakini bahati mbaya hawatuaambii ni sababu gani.
 
Ninachoona ni kuwa ndani ya CCM kuna watu wanaoogopa kupoteza mikate yao kwa kukubali kufuata misimamo ya chama huku wakijua kuwa sio sahihi.

Mfano mzuri ni kukubali kuondoa vipengele vyote vilivyowalenga mafisadi na viongozi wababaishaji. wanaCCM wa kweli waliona kuwa misingi na miiko ya uongozi inarudishwa, lakini wabunge wamekubali iondolewe ili kulinda vityumbua vyao.
 
Uwezo wa kulindamuungano kwa hoja hakuna, ndicho Sitta alichodhihirisha kwa wizi walipobaki wenyewe.

Hilo lilianza kuonekana CCMilipowafunga midomo wabunge wake. CCM iliujua hoja zakiuchumi, kijamii na kisiasa hazina mashiko . Aliyefunguapandora box ni Rais Kikwete. Kitendo cha kuachia katiba ivunjwe na wazanzibarakidhani anaweza kuanzisha mchakato na kupiga marufuku mjadala wa muunganondicho kimeafungua macho Watanganyika.


Kama utakumbuka, wznz wamelalamika kuonewa, kunyonywa na kila aina ya upuuzi wakinyamaziwa. Walitishia kuvunja muungano kama silaha ya kupewa. Nadhani umeona walivyofunga midomo na kubaki na ngumi kule Dodoma.

Kuoleana ni hoja ya mitaani kama mifano yako uliyoonyesha hapo juu kuhusu Rwanda, Kenya, na ninaongezea Malawi na msumbiji. Hata Norway, Uingereza na Marekani tumeoleana, hatuna muungano. Ni hoja kama ya gharama za S3 ilivyotumika na ilivyofutika

Kiuchumi, muungano unamuumiza Mtanganyika na kumjengea ‘pepo' mznz bila sababu za maana. Mfano, tumeuliza,kwanini Mtanganyika aliyebeba muungano kwa kodi zake, bado abebe makando kando mengine yanayotokana na uzembe wa wazanzibar? Nitoe mfano, shirika la umeme znz lina deni la bilioni zaidi ya 67 kutoka Tanesco.


Wznz walikataa kuwa sehemu yaTanesco kama nchi huru kwa mujibu wao. Zeco imekusanya bilioni 20 mwaka2013 ambazo hazikwenda SMZ, zimetafunwa na wazanzibar. Badala ya SMZ kuwabana wezi, SMZ imeleta deni hilo kwa JMT lilipwe na kodi za Mtanganyika, kwa umeme uliotumika znz na pesa kuliwa nawznz.


Ndivyo ilivyo sasa hivi, kwamba denila znz la nje asilimia 88 inadhaminiwa na JMT ambayo ni Tanganyika. Hakunamahali bajeti ya znz ya 2014/2015 inaonyesha madeni yao ya ndani na nje yanalipwaje.

Hii maana yake deni la znz kama lile la kununua mchele anayelihudumia ni Mtanganyika. Kuna justifications gani za mtu wa Mtimbira au Nkapanya kulipa gharama za wazanzibar ambao katiba ya JMT ya 1977 kwao silolote si chochote?


Na rasimu ya Chenge/Sitta inasema znz inaweza kukopa nje na dhamana itatoka JMT. Kwamba wanaweza kukopa na kununua vitumbua na zingine kula kama zile za Zeco, anayelipa ni Mtanganyika aliyechukua dhamana ya deni. Hivi sasa tuna deni la mchele wa znz ulioagizwa na SMZ yenye kila chombo lakini anayelipia ni Mtanganyika.

Kiuchumi, hakuna mahali ambapoMtanganyika anaonekana kufaidika na znz kwa namna yoyote ile. Hata pale Mtanganyika alipojitwika mzigo wa Muungano kwa ‘kuoleana'' wazanzibar wamegeuza fadhila kuwa haki yao

Hivi, wznz wana haki gani ya kupata21 ya ajira za Tanganyika, na 79 za ajira za Watanganyika tena, ikiwa haki za ajira kule kwao kwa Mtanganyika zimeundiwa sheria maalumu ya kuwazuia.

Hivi mznz anasababu gani za kupata4.5% inayotokana na makusanyo ya Tanganyika. 4.5 ya pato la Tanganyika ni kubwa kuliko pato la znz. Hapa tunawafanyia kazi hawana sababu za kufanya kazi.

Hivi wazanzibar wana haki gani na gesi ya Tanganyika ikiwa wao hawataki yao iwe yetu?

Zilipopendekezwa S3 kwa maoni ya wznz, CCM wakakaimbilia hoja ya gharama. Hoja hiyo umeungwa mkono na wasomi tuwengine wakiwemo jamvini kama Kobello , Mkandara .
Leo rasimu ya Chenge imetoka wote wamepotea. Kwamba Warioba alikuwa na mantiki kuliko.


Wanachosema CCM kuwa S2 zinapunguza gharama, maana yake zinawapunguzia waznz gharama na kupitisha gharama hizo kwa Mtanganyika. Leo kwa rasimu ya Chenge Mtanganyika anaumia zaidi ya ilivyokatiba ya 1977.

Maswali yasiyo na majibu ni kuwa,tuna invest znz kwa gharama za Watanganyika ili kupata return gani?
Kwanini CCM inaongopa uwepo wa muungano wa nchi ya Tanzania na znz?
Kuna tatizo ganiTanganyika ikiwepo kama ilivyo znz?

Na kuna uhalali gani wa kumtwisha Mtanganyika gharama zinazotokana na mambo ya nchi jirani ya znz?




 
Na haswaa!

Bunge la katibalilipoanza, wabunge wa CCM wengi hawakujua Chenge alikuwa na rasimu yakeiliyoandikwa kwa kushirikiana na akina Asha. Aliyepewa kazi ya kuhakikishamambo yanafanikiwa ni Sitta.

Ujanja uliotumika ni wa kuwafungawabunge wa CCM kwa kura ya wazi.

Akina Chenge walijua ndani ya CCM wapowabunge wanaoujua ukweli, njia rahisi ni kuwawekea makufuli.
Nao wakaachama,wakasokomezwa matambara ili Chenge atakapomaliza kazi, matambara yaoondolewekitumbua kiingie.


Nina ushahidi wa haya. Abod Jumbe niCCM, Nyalali alifanya kazi wakati CCM ikiwa na hatamu.
G55 ilikuwa CCM. Malecelani CCM tena makamu wa mwenyekiti.

Tume ya Kisanga iliundwa na CCM Mkapa. Hakuna tume hata moja ukiacha ya juzi yaWarioba iliyokuwa na watu wengine. Wote walikuwa CCM na walikuwa na jibu moja,mufaka wa muungano ni S3.


Kwasasa hivi nusu ya wabunge wa CCMwanaujua ukweli na hawakubaliani na CCM yao.
Tofauti na huko nyuma, sasa hiviCCM si chama kile cha watu.
Ni chama kinachodhibitiwa na kundi la wahafidhinaili kulinda masilahi yao.


Wahafidhina wameteka chama. CCM wana muda, wahafidhina hao ndio wenye saa.
Hivi huoni weziwakipewa kazi ya kuandika maadili ya taifa?
Wale walioitwa na halmashauri kuu Butiama nakuambiwa wachukuliwe hatua, hakuna hata mmoja.


NEC ya butiama, wazee wenye chamawalisema bila kificho, wezi na wabadhirifu wafukuzwe.
Aliyenusuru hali ni JKkwa kuahirisha mada hiyo.

Wahafidhina waliporudi Dar wakamuondoa Sitta kwanza,halafu wakamwambia JK ni marukufu wazee wa zamani ndani ya chama. Ndichochanzo cha wazee wa CCM kutengwa hadi leo.


Wahafidhina wakamtisha mzee zaidi,na sasa wamepewa kazi ya kuandika rasimu ya CCM wakisema ni ya taifa.
Hii rasimuya Chenge ilikuwepo na tulisema mapema sana tena tukieleza watafanya nini.


Sitta anachokifanya ni kuombamsamaha kwa wahafidhina akijua ndio wamekamata faili lake siyo CCM.
Jitihada zoteza Sitta ni kuwalamba wahafidhina miguu kwa matayarisho ya mwakani.
 

Mkuu mpaka sasa najiuliza bila majibu. Labda tuweke pembeni suala la muundo wa muungano ambalo tunalijadili sana hapa. Miiko ya uongozi ni muhimu sana mkuu, na CCM imeikataa kabisa and no body within the party seems to care.
Rasimu ya pili ilijitahidi sana kuangalia suala la rushwa na wanasiasa kuwatumia wananchi bila kuwatumikia.

Halafu cha ajabu of all the people wamemweka Mzee Chenge mwenye kashfa kubwa, na matokeo yake amebomoa vipengele vyote vinavyowalenga watu kama yeye.

Mzee Sitta mwenyewe alikuwa anajidai kuwa anapambana na mafisdi, na sasa amejionesha wazi kuwa anaweka mechanism ya kuwalinda mafisadi.
 

Kama alivyojadili Nguruvi3,

Aliyetia sahihi Kama Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi, uadilifu wake umejaa mashaka, wananchi watarajie nini zaidi ya haya.

Ukiangalia sehemu ya kwanza ya rasimu ya Chenge, ibara ya tano, maadili Kama moja ya tunu za taifa imeondolewa na kupachikwa mwenye ibara ya Sita ambayo Inahusu "misingi ya Utawala bora". Huu ni ujanja wa kitoto sana, kuondoa maadili ya viongozi kutoka kwenye TUNU na kuipeleka kwenye MISINGI YA UTAWALA BORA.

Kuhusu Sitta, ameshapoteza credibility kwenye fronts zote zilizompaisha kwenye medani ya siasa za nchi:

1. Uongozi Stadi wa bunge akiwa spika wa bunge la JMT (2005-2010).
2. Ukiranja wa kupambana na mafisadi.

Ni Vigumu sana kuelewa iwapo kuna Siri nzito juu ya haya. Je has he traded in uzalendo wake na usimamizi wake wa maslahi ya wananchi for urais? Uwaziri mkuu?

Tukijaliwa uzima tutaona mengi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Suala la maadili ni zito sana kwa CCM. Wanafahamhawawezi kuendelea kuwepo kama kuna maadili ya viongozi. Wanafikiria yakiwepomaadili yanayowabana hivi Sitta angeweza uiba kura za CCM achilia mbali zawananchi?

Kama utakumbuka, Mkapa alimteua Warioba kushughulikia mianya ya rushwa.

Taarifa ya Warioba ndio iliondoka na mtu mmoja , Nalaila Kiula kwasababu aliwapingana wahafidhina kutolewa kafara. Rasimu ya Warioba ilikuwa inaeleza uzoefu kuhusu maadili na iliziba mianya hiyo.

CCM wanafahamu hakuna njia itakayowawezesha kudumu kama sikupinga maadili na kuyaweka katika utawala badala ya tunu. Maana yake wanayarudisha watakapoweza kufanya manoeuver. Tunu huwezi kuzifanyia upuuzi.

Pia kuna hofu maadili yanaweza kutumika kuwahukumu wahalifu siku za baadaye. Ni kwa msingi huo mkakati ukawekwa na wahalifu kwa kumtumia mhalifu'' ili kuzuia maadili.

Hivi uadilifu wa Chenge unaweza kumpa nafasi yakuzungumzia maadili achilia mbali kuandika.

Kuhusu Sitta, kwanza alijipambanua kama mpiganaji dhidi ya mafisadi.Baadaye aligundua mafisadi ndio wenye chama, ilibidi atafute njia nyingine.Lengo lake lilikuwa kutumia uspika wa Bunge JMT kama ngazi ya kuelekeaMagogoni.

Bahati mbaya, wenye chama wakamwita wakamweka pembeni na aliyeshirikini akina Chenge. Mbinu ya pili, ilikuwa kutumia bunge la katiba kama platform ya kwenda Ikulu.

Kwa bahati mbaya, amevurunda na ndio imekuwa mwisho wake kisiasa.
Alichotaka BMK ni kuwafuhisha wahafidhina kama tunavyoona, hilo sasa nihistoria, wahafidhina bado wana kinyongo naye.
 
Mchambuzi huyu Mzee hakuwahi kuwa na uzalendo,na hana uzalendo na hatokuwa nao kamwe!This Mzee ni mroho wa madaraka pengine kupita hata hao kina Lowassa aliokuwa kila mara anawabrand kuwa Mafisadi.

Kwake yeye ulafi wa madaraka kwanza,maslahi ya wananchi baadae.unakumbuka akiwa Spika alivyokuwa anashona "joho la Uspika"Uingereza tena bila aibu anawaringishia bungeni.Rejea pia ujenzi wa "ofisi ya Spika" Urambo as if alikuwa kajimilikisha cheo hicho milele.

Narudia kusema huu mchakato wa Katiba ndio umemfunua tabia yake halisi ya ubinafsi na kupenda Makuu.Remember alivyoitelekeza CCJ na kina Mpendazoe baada ya kuona future yake kwa siasa itakuwa mashakani nnje ya CCM.
 
Last edited by a moderator:
TARATIBU YAMEANZA KULE ZNZ,WAMERUDI NA KUKUMBANA NA MASWALI MAZITO

CCM NA HARAKATI ZA KUFICHA UKWELI KWA KUTUMIA VIJANA, AKINA MAMA

Bandiko la juu tumeeleza unafiki unavyoisumbua znz.
Tumeeleza jinsi walivyo na msimamo mmoja dhidi ya adui yao Tanganyika.
Hata hivyo, adui huyo hugeuka kuwa rafiki pale maislahi yao yanapokuwa matatani.

Hali inaanza kuwa tete kule visiwani. Waliopitisha katiba ya Chenge na kuitungua ya Warioba wamekumbwa na kihoro.

Wamerudi znz,hoja iliyopo ni namna gani ya kukubaliana na Chenge bila kuathiri katiba ya znz ya 2010 wanayodai imewapa nafasi zaidi kwa kuchukua uamuzi wakiwa wenyewe.

Ugumu unafahamika, ni pale itakapobidi wabadilishe katiba iwiane na katiba ya Chenge.
Ugumu ni kuwa yale waliyosema si ya muungano sasa itabadi wayakubali.

Kile walichosema kodi zao kuliwa na Tanganyikaitabidi wakikubali. Na ule uhuru wa Rais wa znz sasa itabidi uminywe kwani katiba ya Chenge/Sitta itakapokubalika kama wanavyoinadi basi Rais wa znz atakuwa makamu wa pili wa rais wa JMT.

Hilo tu, linamuondolea ule wigo wa uhuru. Lazima atafanya kazi zake akiwa na Tanganyika mgongoni kwa jina la Tanzania. Mamlaka kamili yanazidi kuyoyoma.

Na itakapotokea hamkani, Rais wa znz ataweza kuwajibishwa kwa mujibu wa katiba ya Chenge/Sitta.
Ndivyo ilivyomkuta Aboud Jumbe na sasa historia inajirudia.

Kitendo cha CCM kuwazogoa wapinzani wao kinaodoa kabisa uwezekano wa maafikiano ya kubadili katiba ya 2010. Hapo ndipo tunaanza kusikia maswali ya kama katiba ya Chenge itakuwa na athari au la dhidi ya znz.

CCM NA MBINU MFU

Baada ya kubaini hali ya mapokezi ya katiba ya Chenge/Sitta ni tata, wamebuni njia mpya.
Njia zile za wasomi na waandishi wa habari zinaonekana kuwa na ‘ganzi'.
Inahitaji kujitoa fahamu ili uweze kutetea katiba ya kihuni iliyoandaliwa kihuni, kupitishwa kihuni na iliyojaa uhuni.

CCM wameanza ziara za kurudi majimboni ili kuwalaghai wananchi wa kawaida.
Hoja zao si zile za kuongezeka kwa gharama tena, katiba ya Chenge/Sitta inaonyesha kuwatwisha wananchi mzigo mzito.

Hoja sasa ni uzuri wa katiba kwa vijana na akina mama wakijua hao ndio wapiga kura.

Inavyoelezwa, itadhaniwa kuwa tatizo la katiba tulilokuwa nalo ni vijana na akina mama.

Hilo halijawahi kuwa tatizo hata siku moja. Ni ulaghai tu wa kutowaambia wananchi ukweli.


Inaendelea...
 
Inaendelea...

Ukweli ni ule wa jinsi katiba ilivyopitishwa bila muafaka wa kitaifa.
Pengine hilo ni tatizo kubwa kuliko katiba yenyewe.

Matatizo mengine ni kama ya kutokuwa na uwiano wa serikali, kutoeleza muundo wa serikali 2 umetatua vipi matatizo hasa kwa Tanganyika.

Wanachokifanya ni kuwaambia Watanganyika mambo ni mazuri, bila kuwaambia kuwa sasa watabeba mzigo wa Zanzibar katika bega la pili, wakihudumia marais wa znz 4 wasiowachagua, wakilipa kodi za wabunge zaidi ya 100 kutoka znz kwa mujibu wa Chenge, wakitoa 4.5% ya pato la Tanganyika kwenda znz, wakihudumia madeni ya mikopo na misaada inayokwenda znz peke yao n.k.

Wakati hayo yakiendelea, wznz hawajui gharama zozote na wamepewa hata wasichostahili.
Mtanganyika anazidi kupinda kibyongo, huku walaghai wakisema katiba imewajali.

Hivi unaweza kumjali mtu kwa kumuongezea mzigo.

Wasichowaambia wananchi ni kuhusu maswali muhimu yasiyo na majibu.
1. Je mfumo wa utawala utaweza kuwalatea wananchi tija wanayokusudia?
2. Je mfumo wa muungano ni haki kwa pande mbili
3. Je, Tanganyika imejivua koti la Tanzania lenye gharama kubwa ya kulihudumia?
4. Je, yale matatizo yaliyotokana na mfumo wa S2 yamepatiwa ufumbuzi?
5. Kuna dhambi gani Tanganyika ikiwepo, ikiwa znz ipo tena kama nchi huru?
6. Kwanini Mtanganyika abebe mzigo wa kuendesha muungano na SMZ isiyomhusu?
7. Je, katiba itatua matatizo ya kiuchumi yakiwemo, wizi ubadhirifu na ufaujaji?
n.k.

Lugha wanazotumia ni tamu sana, matatizo yanayowasubiri wananchi ni machungu sana.

Kwa mwendo huu wa ulaghai, muungano utavunjika siku moja kama glass iliyojaa maziwa

Tusemezane
 
Wanajamvi
Kwa wale mnaofuatilia hapa, tuliandika bandiko likieleza jinsi ambavyo makundi ya kijamii yatatumika katika kuhalalisha uharamu uliofanywa Dodoma. Tulitaja makundi haya
1. Wasomi, tukasema hawa watatumia TV na magazeti kueneza propaganda. Tulieleza 'kwa vile bei yao inajulikana, hilo ni suala la muda tu''

2. Tukazungumzia kundi la wanahabari ambao nao pia tulisema bei yao inajulikana.

3. Tukaeleza kuhusu makundi ya dini, na tulisema haya yana utata. Kwasasa bei yake ina matatizom hawajulikani wanasema nini au wanasimamia nini. Matamko ya kupinga uhalifu yanatoka, baraka kwa katiba ya Chenge zinaendelea

Tlichokisema ndicho mdau alichokieleza kinatokea sasa hivi

Kwa Hisani ya gazeti la Raia mwema
 
LITAIBUKA KUNDI LA KUJENGA HOJA
HUO NDIO UTAKUWA MWANZO WA KUVUNJIKA MUUNGANO


Tunaona jinsi CCM wanavyotumia ulaghai wa vijana na akina mama kama ndilo tatizo kubwa la katiba.
Wanaficha ukweli ikiwemo maadili yanayowahusu na mambo yanayolikabili taifa kwa hoja laini tamu tamu.

Mbinu hii ni kama ‘big G'. Haina muda thamani yake itakwisha.
Mfano, kuna wizara maalumu inayoshughulikia akina mama na watoto
Kwa miaka zaidi ya 10 wizara hii imekuwa sehemu ya ajira tu ikiwaacha akina mama huko vijijini hoi.

Laiti ingekuwa na mashiko, basi hoja ya akina mama isingekuwepo kwasababu chombo kinachoshughulikia tayari kipo.
Pamoja na uwepo wake akina mama bado wanajifungua katika matenga ya baiskeli, vifo vyao wakati wa uzazi ‘maternal death' ni vingi na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5 ni vingi sana.
Ukiangalia kwa undani vifo hivyo vinazuilika.
Kwanini basi serikali isianzie hapo hadi kuweka usawa wa jinsia kikatiba? Hao wabunge sawa wanasaidiaje akina mama wa vijijini endapo sasa hawawezi kusema wanabaki na misimamo ya CCM ?

Kwani tatizo la akina mama ni haki au ni usawa wa jinsia? Inakuwaje basi akina mama ambao ni wapiga kura wengi hao hao wachague wanaume kuwaongoza endapo mfumo uliopo unawanyima haki kwa kutokuwa na usawa?

Hoja kubwa hapa si uaswa wa jinsia, ni kueleza tu kuwa katiba ni sukari guru wanayopewa.
Baada ya mradi wa Chenge/Sitta kukamilika, sheria zitakazowahusu hazitatiliwa maanani.
Katiba itatamka, hawatetenda kwa sasbabu hawajaweza kutenda leo hii, na mradi wao utakuwa umekamilika

Kuhusu vijana, nako kuna tatizo. Kwasasa tuna mbaraza ya vijana.
Vijana hao hao wanaosemwa katika mradi wa Chenge/Sitta hawjaweza kuwa kitu kimoja.

Tunaona wakitumika kama karatasi za maliwato kama wapiga debe na si watu wanaotazama siku za mbeleni ''shape their future''

Kuwatengenezea baraza ni kutafuta kuungwa mkono. Hakuna kitakachofanyika zaidi kwasababu hata sasa hivi hawana haki ya elimu. Wangapi hawana mikopo au uwezo wa kulipa ada za kumaliza masomo ya sekondari?
Wangapi hawana ajaira na je, baraza tamu waliloahidiwa na Chenge linamaliza vipi matatizo yao?

Hoja kubwa hapa ni kuonyesha jinsi nao watakavyotumika na kutupwa kama walivyotumika viongozi wa dini katika mchakato.

Pamoja na matamko na jitihada za kuunga mkono mradi wa Chenge/Sitta, mwisho wa siku Sitta kawaita wapuuzi.

Mbinu za kutoa peremende kwa wazanzibar na Big G kwa vijana na akina mama ni hafifu sana.

Litatokea kundi lenye weledi litakalohitaji majibu ya maswali ambayo CCM hawana kwa sasa na wala hawatakuwa nayo. Miongoni mwa maswali hayo ni ya kiuchumi na hata kugusa muungano wenyewe.

Mathhalani, vijana watakapohoji nini faida za muungano.
Kwanini hakuna uwiano katika kuubeba muungano. Kwanini wao walipe gharama za muungano ikiwa tuna muungano.
Kwanini upande mmoja wa muungano upewe kipaumbele na ufumbiwe macho katika kuwajibika kitaifa.
Nini maana ya investment kubwa zznz na return yake ni nini

Ikifika hapo itatafutwa hoja ndogo tu ya kuhalalisha madai yao.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Jumbe, Nyalali n.k. Kwamba, G55 ilipopata mwanya wa passport na IOC basi Tanganyika ikadaiwa kwa nguvu hasa.

Haikuwa nguvu ya mbavu au wizi wa kura wa Sitta, ilikuwa nguvu ya hoja inayozizima hadi leo.
Na hapo ndipo sababu ndogo tu itahitimisha muungano.

Sijui kama wanaolitakia taifa hili mema wanaona hatari hiyo.

Tusemezane


cc
Alinda gfsonwin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…