Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Nguruvi3,
Mkuu mimi sii mjuzi wa kuandika makala japo vitu vipo kichwani na kwa bahati mbaya kila napokusoma nakuona hukunielewa hivyo najiuliza jinsi gani niwepe sawa picha hii. Labda nijaribu kwa lugha nyepesi isokuwa fasaha na kwa wale wanaojua watakueleza vizuri. Na sintoweza kukujibu yote naomba twende kwa kituo tukianza na nini maana ya JMT na mamlaka yake. Nini serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mamlaka yake.

Mkuu maelezo yangu yote yanazungumzia hapa TULIPO sasa na sii pendekezo wala sijagusia serikali 3. Labda niweke hivi badala ya kutumia neno NCHI niongezee langu la UTAIFA (Nation) ili kutofautisha baina ya NCHI na TAIFA.
Toka kuzaliwa kwake Tanzania ni TAIFA moja (One Nation) lenye bendera na wimbo wake wa Taifa. (sijui kama ndio kiswahili safi maana sijawahi kusikia tukisema tuna wimbo wa nchi au bendera ya nchi ila watu wote husema - wimbo wa TAIFA, bendera ya Taifa, Nationality yako kadhalika) anyway tuachane na huko. Nisikilize kwa makini na kwa lugha yangu ambayo nadhani itakuwa nyepesi Zaidi ukizingatia nachokisema badala ya tafsiri fasaha na matumizi ya maneno haya NCHI na TAIFA.

Na katika Taifa hili kuna nchi 2 (countries) zilizoungana (Tanganyika na Zanzibar) zikaunda TAIFA moja. Kila ardhi inayoitwa nchi huwa na mihimili mitatu 1. Serikali 2. Mahakama na 3. Bunge.. Hivo mihimili mitatu Zanzibar wanayo na ndio maana tunasema Zanzibar ni nchi. Tanganyika yetu haina na sio nchi isipokuwa tuna JMT, hivyo mamlaka yote ya mihimili mitatu 3 ya JMT inawahusu Tanganyika na Zanzibar ktk maswala ya Muungano.

Wazanzibar hawali huku na kule isipokuwa ni sehemu ya JMT. Hata sisi tunakula huku na kule maana katika mambo yote muhimu 22 ya JMT yanatuhusu sote hivyo hata sisi tunafaidika kutokana na kuwepo kwa Zanzibar yaani tunaingia moja kwa moja.. na kama sikosei mambo mengine kati ya hayo 22 yameongezwa kinyemela hayakuwepo zamani wakati wa makubaliano na kuzaliwa Tanzania, kulingana na madai ya Wazanzibar. Bahati mbaya sina orodha kamili ya mambo ya muungano yalokubaliwa mwaka 1977 nasikia tu kwamba yalikuwa 11 sijui 12. Mambo yasiyokuwa ya Muungano ni yote yaso orodheshwa ktk makubaliano ya muundo wa serikali ya JMT. Hivo ni serikali ya Zanzibar, mahakama yake na bunge lake ndio wenye mamlaka na wajibu wa utendaji na utekelezaji wa haki kwa jiamii yao na sio serikali ya Muungano.

Hivyo kimsingi ina maana Watanzania bara tumeweka nyavu zetu Znz pia na tunakula huku na kule kwa sababu hakuna vitu muhimu ktk uendeshaji wa serikali kama vilivyoorodheshwa ktk hayo maswala 22 na kero zilikuwepo tu juu ya maswala hayo 22 ambayo Wazanzibar waliona wamebanwa sana pasipo uhuru kamili wa kujiamria mambo yao, na sii swala la kula zaidi bara au nani analiwa. Kumbuka tu kuwa mihimili ya serikali, mahakama na bunge haizailishi utajiri wala sii source ya maendeleo bali majukumu yake ni hutunga policy, sheria na kusimamia utekelezaji ndio kusema Wazanzibar wamefungwa kamba miguu yote miwili kubanwa na policy za kwao na zile za JMT na sio wanakula huku na kule. Kula huku na kule tunakulla wote. Na Usipokubali kuliwa, hutakula - JMK

Ni majibu ya Mheshimiwa Pinda tu ndio yaloleta vuguvugu jipya kla Uzanzibar ikafikia wao kudai bendera yao, wimbo wao na kadhalika kwa sababu hawataki historia ipotoshwe kuwa Zanzibar sio nchi ktk muungano huu. Hivo hii ni retaliation ya kijinga waloifanya na kama nilivyosema JK ni dhaifu hakuweza kuwachukulia hatua ama kumsimamisha Pinda kama alivyofanya Nyerere kwa Malecela. Tulopoteza nchi ni sisi Bara. Tumepoteza tu jina la Tanganyika lakini kila kitu kipo ktk muundo wa JMT.
 
Last edited by a moderator:
Si kweli! kwa tafsri ya nchi, Tanganyika ni nchi.
Rejea bandiko lililotofautisha kati ya nchi, serikali na taifa la ! Mchambuzi
Huu ndio upotoshaji unaofanywa kuficha ukweli. Mkandara, Tanganyika ni nchi.

Kwa msomaji yoyote wa maelezo yako atakuuliza swali moja, kama muungano ni zao la Tanganyika na Zanzibar, halafu unasema Tanganyika siyo nchi! unaa maana gani.

Pili, kama Tanganyika iliungana na Zanzibar,na Znz ina mihimili yake, ile ya Tanganyika ipo wapi? Kwanini mihimili ya Tanganyika iwe ya muungano na ile ya znz iwe kwa wazanzibar? Si kweli, Tanganyika haiunufaiki kwa kuwa na muungano.

Katika mambo 22 yaliyoongezwa kinyemela hakuna hata moja ambalo Tanganyika inanufaika nalo. Nimekuuliza mara 4 hujaweza kuja na hata moja.

Mimi kwa uhakika nimekuonyesha mambo yote yanainufaisha znz kuliko Tananyika.
Ndilo chimbuko la neno Mzigo na ndicho Watanganyika wancholalamikia.

Uwepo wa znz katika muungano ni sawa na zigo usilojua lina nini ndani.
Tumekupa takwimu za kiuchumi ambazo hakuna sehemu hata moja Tanganyika inafaidika Hakuna!

Lakini pia nimekuuliza mara 4, kama kuna mambo yasiyohusu muungano, Tanganyika itayaweka wapi? Umesema hakuna nchi ya Tanganyika, sasa yale yasiyo ya muungano tuyaweke wapi ili Tanganyika isifadike zaidi ya Znz!!

Nimekuuliza tena, kwanini kusiwe na urahisi wa kuwa na mambo 7 ya pamoja na mengine kila mmoja ashughulike nayo.

Ni kwanini unadhani Tanganyika inapaswa kubeba muungano peke yake.
Maswali yote huna majibu, unarudia kueleza kile kile usicho na majibu. Mkuu hapa sikuelewi.

Unafahamu wazi kuwa serikali 2 zinatengeneza mazingira ya utegemezi wa znz kwa Tanganyika bila gharama.Sisi tunasema sasa basi waachwe wasimamie mambo yao.

In fact serikali 3 ni best option kwa mznz, kinyume chake tuvunje muungano, Tanganyika haina cha kupoteza zaidi ya kupunguza furushi la mzigo.
Mkuu mtu abebwe halafu acheze msewe mgongoni wewe unaona sawa sawa kabisa. Hapa ndipo unajichanganya mkuu, kama wamebanwa kwanini wasiungane nasi ili wapate fursa ya kutanua?

Mambo 22 sasa ni 7 na practically ni 4 kwanini znz wasiunge mkono serikali 3 ili, kwanza wasinyonywe na Tanganyika, na pili waweze kujiamulia mambo yao.

Ndio maana nasema utetezi wako unajichanganya sana, na hakika mtu akikusoma vizuri wewe ni muumini wa serikali 3 kwasababu hoja zako kutetea serikali 3 ni nzito kuliko zangu Pinda ni mwanadamu na si mara moja amepotoka kusema kauli. Kauli ya Pinda bungeni ina ukweli. Kumbuka hulka ya wznz ni kuchukua mambo out of proportion

Jumbe alisema serikali 3, wznz hao hao wakamkana akiwemo aliyemshataki amabye leo anataka serikali 3 ndani ya chama na mkataba akiwa na uamsho.

Kauli ya Pinda haikuwa na sababu zozote za maana za kuifanya znz ikimbilie kutafuta kitambaa na kuita bendera, kwaya na kuita wimbo wa taifa n.k.

Bendera ipo new York na Wimbo ni mungu ibariki.
Kama wanataka kinyume chake basi njia ni moja vunja muungano.
Hawawezi kwasababu ya utegemezi. hilo wanajua, sisi tunasema utegemezi sasa basi.

Nimekusoma bandiko lako la jana na kushangaa sana. Mkandara anasema ili tuwe na muungano lazima tuhakikishe tunawafurahisha wznz kwa kila jambo.
Tufunge mahoteli bara ili znz inufaike. Tuhamishe AICC Arusha kwenda znz.
Tufunge bandari zetu ili znz iwe bandari huru bidhaa ziingie bila kodi.
Tuachie znz waendelee kusajili meli kihuni kwa jina la Tanzania
Tuwalipie bill zao bila wao kufanya lolote

Mkuu anasema muungano haupo kama Mtanganyika hatagharamia znz na kwamba lazima mzanzibar afurahi ili tuendelee kuwa nao.

Mkandara, yaliwezekana huko nyuma kwasasa basi!
Kama serikali itatumia mabomu kulazimisha muungano tutakuwa tumepata ruhusa ya kutenda tunachokijua. Madole ya macho yameanza, baada ya muda itakuwa mbaya zaidi ya hapo.
 
Nguruvi3,
Twende kwa kituo, unapotosha sana kauli zangu (bandiko) kiasi kwamba nashindwa kufuatilia.
1. Mkuu wangu Tanganyika haipo na wala sii nchi (haina mihili yake)na kama madai yako ni kweli kuwa Tanganyika ipo kwa nini leo mnadai KURUDISHWA kwa Tanganyika (serikali 3) ktk katiba hii mpya?

2. Katika maswala 22 ya muungano nambie moja ambalo Zanzibar wamenufaika nalo,japo ilani za Mkapa na JK ni kuijenga bara (hesabu yake haina kiimo). sasa wewe nambie mradi wowote mkubwa wa maendeleo ulojengwa Zanzibar na serikali ya Muungano toka enzi ya Mkapa.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara;8972131]
Mkuu hili suala la nchi, serikali, , taifa na state linaonekana kukusumbua, hebu pitia mabandiko haya ujiridhishe kwanza
sijui kama nitakuwa sahihi sana ama kama nimekuelewa sijui, nafikiri NCHI ni eneo lenye mipaka yake (country =is a region legally identified as a distinct entity in political geography)
na TAIFA ni watu wenye tamaduni, lugha na historia katika eneo husika, (NATION =a large body of people united by common descent, history, culture, or language inhabiting a particular state or territory )
na serikali ni muundo
 
Tukubaliane kimsingi kuwa huna jibu kwa ukweli kuwa swali hujibiwa kwa jibu siyo swali.

Pili, kumbuka kuwa mambo 22 hayahusu ujenzi wa barabara au viwanda ni zaidi ya hapo.

Tatu, umeniomba nieleze moja tu lililowanufaisha wznz.
Mimi nitaeleza zaidi ya moja kati ya yale 100 yaliyopo.

Ulinzi na usalama:
Znz haina wizara hiyo na wala bajeti ya wizara hiyo. Bajeti ya wizara ya ulinzi ni trilioni 1, bajeti ya znz ni bilioni 700. Utasema znz ni sehemu ya muungano, well ni kweli lakini kufuatana na Prof Humphrey znz haijachangia hata senti tano tangu 1969 na miaka 5 iliyopita haina mchango wowote. S
asa kama mchango ni jina, upo sahihi mkuu.

Mambo ya ndani:
Znz haina bajeti ya mambo ya ndani. Na hoja zingine zinabaki kama nilivyokueleza hapo juu.

Elimu ya Juu:
Hili liliingizwa kinyemela na hivyo tutarajie Tanganyika ilinufaika.
Guess what! Znz imepewe nafasi za upendeleo kujiunga na vyuo.

Hata kama mtu ana div 4 zipo nafasi kwake. Mwaka 2012 wanafunzi 1000 walipewa zawadi za kusoma bure. Uwezo wa SMZ kusomesha katika mwaka huo likuwa wanafunzi 800.

Yaani Tanganyika ambayo ni JMT ilichangia zaidi ya SMZ.
Kumbuka hili sijambo la muungano, nitashangaa ukisema wznz wana haki.
Huko nyuma umeeleza ni la kinyemela hivyo kila wanachokipata ni zawadi si haki yao.

Chuo Kikuu:
Mwaka jana Muungano umetoa bilioni 5 kujenga chuo cha Nyerere. Pesa hizo si mkopo ni zawadi kwasababu znz haikuchangia chochote katika muungano mwaka huo huo lakini imechota bilioni 5.

Umeme:
Nyaya za kwenda Pemba ni mradi wa muungano. Well, pamoja na hayo umeme haulipiwi ni bure.
Narudi ni bure kwasababu wznz hawajui mita za umeme zinafananaje.

Mihahara:
Sijui hili linaingia wapi lakini JMT iimekuwa inalipa mishahara ya SMZ.
Hata hivyo tusiliongee sana maana ni kawaida limeanza wakati wa Salimin hadi sasa.

Hayo ni mifano tu baada ya kuona kuwa katika 22 na zaidi hakuna hata moja lililomnufaisha Mtanganyika. Hakuna!

Hivyo Mtanganyika anapswa kulalama si mznz. Mznz anapaswa kutafuta mamlaka kamili.
Huu mpango wa Mkandara wa SMZ na JMT umelenga kumnyima mznz mamlaka kamili, na ataishia kulalamika.

 

Nguruvi3.

Mawazo yako ni mazuri sana nimeyapenda sana ILA TATIZO LAKO LIPO PALE PALE Unachanganya Serikali na Chama. Siku zote unapojenga hoja jaribu ku hit sehemu moja IMA SERIKALI au CHAMA, japo Serikali ni zao la Chama kilichoshinda uchaguzi.

Kwani tunaamini huwezi hit two targets at the same time.

Hongera sana.

 

Nguruvi3,

Kama utapunguza USHABIKI na JAZBA kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa MKANDARA, kwani ametoa darsa zuri sana kwako na wasomaji wengine katika POST YAKE Na. 81.

Kumbuka kuwa popote pale HAKUNA NENO TANGANYIKA BALI KUNA TANZANIA BARA. Na hii imejificha chini ya Muungano wa JMTz.

Nakusihi ahali yangu Nguruvi3 , punguza ushabiki na jazba kwani hivi vinaharibu haiba yako ya uandishi.

Hongera sana Mkandara kwa darsa lako.

 
kwa sababu Tanganyika ipo usingizini!
 

NGURUVI3.

Mimi naamini hakuna kitu MUHIMU KATIKA MAISHA KAMA ILMU au UJUZI wa jambo. Kwani hili ndili litakalokupelekea kuweza kutumia DATA kama Reference katika kuhalalisha hoja zako. KWANI KWA MTU YOYOTE MCHUMI NA ANAYEJUA NCHI HIZO ANAKUONA KABISA UNAELEA KATIKA BAHARI YA CHUNGU.

Kumbuka kuwa kuna wengi wajuzi wanasoma uzi au maandiko yako hivyo kuwa makini kuonyesha umahiri wako.

MIMI KWA KUKUSAIDIA TU KWA HILI LA UCHUMI nakushauri PITIA RIPOTI ZA WATAALAMU WA UCHUMI WA NCHI HIZO MBILI TZ BARA NA ZNZ WANAZOZITOA KILA MWAKA KUPITIA JOINT FINANCE COMMISSION (JFC) utajiona unavyoelea katiba bahari ya uongo na ushabiki. website yao ni Joint Finance Commission.

Afisi zao zipo pale SUKARI HOUSE, Dar .Tembelea ili wakupa bayana badala kuandika bila kuwa na evidence. Kumbuka uchumi ni fani, na sio bla bla.

Pole sana.

 

Mchambuzi
Naona ngoja nikusaidie hapo kidogo kujadili historia ya mkataba wa mvungano wenu kw jicho la kisharia .

Sio lazima kila mkataba uwe ni wa maandishi, lakini mkataba wowote wa ardhi, land au pango, lazima uwe wa maandishi!. Wewe unaweza kununua gari na kumzawadia mpenzi/mke/ ndugu au mzazi kwa kauli tuu na ukawa ni mkataba halali!.

Lakini kama una land yako, ukiamua kumzawadia yoyote, hata ukimzawadia kwa kauli, lazima maandishi yafuatie ndio yatakayo halalisha hiyo kauli!.

Mzizi asili haswa wa muungano ni kauli, ya Nyerere na Karume.

halisi ya mkataba wa muungano.

Nyerere " Sisi ni ndugu, kwa nini tusiungane?".
Karume " Tuungane, wewe rais. mimi makamo".

Shughuli ilianza na kumalizika in a split of a second!.

Kilichofanyika ni kwa Nyerere na Karume tu kufikia makubaliano ya msingi (kwa hati ya dharura) na mambo mengine yakaburuzwa. Aidha, Mkataba huo wa Muungano ulitoa mwelekeo tu na kuacha mambo mengine muhimu kushughulikiwa baadaye na Tume ya Katiba ambayo chini ya Mkataba huo, ingeundwa katika muda usiozidi miezi 12 kuandaa Katiba ya Muungano. Katika kipindi hiki, Muungano uliendelea kutumia Katiba ya Tanganyika (kama ilivyorekebishwa) hadi hapo Muungano utakapopata Katiba yake.

Tunachofahamu ni kwamba, si Tume ya kupendekeza Katiba wala Bunge la Katiba (Constituent Assembly) lililoundwa au kuitishwa katika muda wa makubaliano hadi miaka 13 baadaye ilipotungwa Katiba ya kudumu ya 1977, kinyume na utaratibu unaotajwa kwenye Mkataba wa Muungano na Sheria ya Muungano.

Madhumuni ya kuunda Tume ya Katiba na Bunge la Katiba kipindi kile, yalikuwa ni kutoa nafasi kwa raia wa nchi hizi mbili kushiriki, kutoa maoni yao kuhusu aina ya Katiba ya Muungano wanayotaka, Muundo wa Muungano na mgawanyo wa madaraka ya kiutendaji ndani ya Muungano.

Kuna utata namna Katiba ya 1977 ilivyotungwa. Utaratibu unaotajwa katika Mkataba wa Muungano na Sheria ya Muungano unaelekea ulivunjwa kidogo, kwamba badala ya kuundwa Tume huru mahsusi kwa ajili ya kupendekeza Katiba, Tume ya vyama vya TANU na ASP ya watu 20 (ambayo haikuwa na Mwanasheria hata mmoja, bali wakereketwa wa siasa watupu), iliyoundwa mahsusi kuunganisha vyama hivyo viwili, iligeuzwa kuwa ndiyo Tume ya Katiba ya Chama na kupendekeza Katiba.

Mapendekezo ya Tume hiyo na ya Bunge la Katiba kama ilivyotakiwa, badala yake yaliwasilishwa na kujadiliwa kwenye Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama na baadaye kwenye Bunge la kawaida. Pamoja na hayo, Bunge hilo halikuyajadili mapendekezo ya “Tume” kwa sababu alizozitaja Waziri Mkuu wa wakati huo, Rashidi Kawawa, kwamba “Kwa kuwa NEC ilikuwa imeijadili, Bunge halikuwa na mamlaka ya kujadili wala kubadili kitu”.

Utata wa Muundo wa Muungano ulijitokeza tena kama hoja wakati wa Tume ya Jaji Nyalali na kupatiwa suluhisho kwa njia ya mapendekezo ya kurekebisha Katiba. Lakini badala ya mapendekezo ya Tume hii makini kufanyiwa kazi, yalitiwa kapuni na hivyo kupoteza nafasi nyingine nzuri ya kutibu ugonjwa unaousumbua Muungano wetu.

Lakini, kwa nini Tume ya Katiba haikuundwa kwa mujibu wa Mkataba na Sheria ya Muungano? Moja ya sababu ni kwamba waasisi wa Muungano huo, Nyerere na Karume, walianza kugundua kwamba walikuwa tofauti mno kwa kila hali; kuanzia maumbile, kitabia na kifikra, elimu na mtazamo juu ya Muungano waliotia sahihi.



Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisharia ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisharia liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisharia, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.







 
Barubaru,

Hapa mkuu wangu unapotosha. kwa sababu hakuna nchi zilizoungna kwa makubaliano ya raia ama kupitia wawakilshi wake iwe wabunge ama BLW -hakuna. Nchi zote zilizoungana kuunda TAIFA moja ilitokana na makubaliano ya watawala ama vita, utekwaji na kadhalika.Mpango wa kuunda muungano wa nchi yetu ulikuwepo hata kabla ya Uhuru bandia wa Zanzibar. Tanganyika ama niseme TANU na AFRO SHIRAZ walikuwa na mpango wa kuunganisha nchi hizi toka wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa nchi hizi na mikutano mingi ya Afro shiraz party ilifanyika bara miaka ya 50.

Kumbuka tu kwamba Hiyo Yanga na Simba zilikuwa sehemu za wapambanaji na chimbuko la timu hizi ni kutoka Zanzibar. Viongozi wa TANU ,AFRO SHIRAZ na UMMA PARTY walikuta wala sii mara moja kabla hata ya Mapinduzi na ndio maana baada tu ya Mapinduzi mlishtukizwa na Muungano. Umoja wa nchi za kafrika uliisha paniwa hata kabla ya Uhuru wenyewe kuatikana kwa nchi zote.

Ukitazama vizuri historia ya Zanzibar utagundua kwamba hata yale Mapinduzi yasingekuwepo kama waziri mkuu Shamte angesikia ombi la Afro Shiraz Party waunge nguvu dhidi ya chama cha Sultan lakini Shamte akachagua upande wa Sultan akitarajia kupewa uongozi wa nchi (Waziri mkuu). Hivyo, baada ya uchaguzi Umma party na Afro shiraz wakaunda chama kumuondoa Sultan huku nyuma wakipigiwa debe na TANU maana wajkati huo hakuna kitu kikubwa kiichokuwa kikizungumziwa zaidi ya UHURU wa nchi za Kiafrika toka mikononi mwa wakoloni, ikifuatiwa na kuundwa muungano wa nchi zote za KIAFRIKA.

Kwa hiyo hata Nyerere na Abdulrahman Babu walipokuwa Ghana walipingana na dhana ya kuunganisha Afrika yote mara moja isipokuwa hatua kwa hatua.Hivyo kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni hatua ya mwanzo ya kuunganisha bara la Afrika. Kifupi hata sisi hatua ilokuwa ikifuatiwa ni kutoka serikali 2 kwenda serikali 1. Na bahati mbaya sana mara tu baada ya Tz kuungana na Zanzibar balaa likazuka la EAC, nchi nyingine za Kiafrika zilizoungana pia zikaanza kujitoa ktk muungano kutokana na UMASKINI ulozaa mfumo binafsi.

Hii imedhihirisha wazi kwamba adui mkubwa wa mwafrika ni UMASKINI wetu, kila kiongozi aloshika madaraka kitu cha kwanza hufikiria kujenga kwao akasahau kuwa yeye ni kiongozi (rais) wa nchi nzima. Na tazama basi, Mungu akawajaalia wale wanyonge wasokuwa na elimu wala Ustaarabu kulingana na tulivyoelimishwa, ardhi zao akazirutubisha na mali asili tele madini, mafuta na kadhalika.

Na tazama basi, mzungu alipoingia Afrika akajenga urafiki na yule asokuwa nacho ili kuunda nguvu dhidi ya maskini mwenye utajiri. Wakasomeshwa na kupewa kila zuri ili tu wamtumikie mzungu dhidi ya ardhi tajiri. Hivyo mzungu hakutumia jeshi lake kupambana na waafrika wengine isipokuwa alitutumia sisi wenyewe kupigana na kuteka maeneo kwa faida yake. Hawa walosomeshwa na mzungu ndio wakaja kuwa viongozi marais baada ya Uhuru. Kila rais aloingia madarakani alikuwa mbaya kuliko hata mkoloni, alitaka kuchota toka kwa hawa maskini na kuineemesha nchi yake hii ikawa mwanzo wa nchi za Kiafrika kusambaratika. Ndoto ya Afrika moja ilikufa toka Nkurumah alipokufa!

Hivyo nasi Muungano wetu unakumbwa na tatizo hili kubwa, Vingozi wote wa Bara wamekuwa wakiitazama Bara zaidi ktk ujenzi wa miundo mbinu ama miradi mikubwa ya maendeleo, tena pasipo aibu wanajenga majimboni kwao ama kwa wake zao. Viongozi wetu wa Kiafrika ndio sababu kubwa ya kushindwa kuunganishwa kwa Afrika na kama itafikia hata muungao huu ukafa basi tujue hapatakuwa na Afrika moja isipokuwa hata hiy mikoa itaanza kutaka kujitenga. Ndiko tunakoelekea.

Watu wengi sana wanachukulia huu muungano wa Tanzania na Zanzibar kama vile ni kuunda Jumuiya iwe EAC ama EU wakati muungano huu ni kuunda TAIFA moja lenye kiti chake UN (Umoja wa MATAIFA)Huku UN unakuta MATAIFA wanachama na sio NCHI wanachama, na ndio sababu pakaitwa UMOJA wa MATAIFA na sio Umoja wa NCHI, hii ndio sababu hata mimi natumia tafsiri ya TAIFA kuwa juu ya nchi. Kwa maana hiyo napingana pia na Tafsiri ya katiba yetu inaposema Tanzania ni NCHI yenye mipaka yake blaa blaa ila Tanzania ni TAIFA lenye kuunganisha nchi 2 na mipaka yake ni eneo lote la blaa blaa blaaa.

Tume huundwa tu ktk kuunda shirikisho,jumuiya na kadhalika ambazo nchi zote vina viti vyake UN kama TAIFA huru. Hivyo unaposema Tanzania huru ni eneo lote la Tanganyika na Zanzibar wakati ukiitazama EU kila nchi ina UHURU wake, serikali kuu yake, kiti chake UN na kadhalika. Kupotosha maana ya muungano wetu kwa makusudi ukifananisha na kuunda jumuiya nadhjani hapa tunafanya makosa makubwa sana na sielewi kama ni ya makusudi ama ni kutokuelewa asili ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
 
Barubaru, hili tumelijadili siku zote tukiwa na akina JokaKuu. Data unzosema tumeziweka hapa jamvini.
Hakuna sababu ya wewe kutoeleza kile unachojua kiuchumi unaweza kufanya hivyo.

Mara nyingi katika mijadala yako huwa huelezi nini hasa unakusudia kuonyesha katika joint finace commission. Lakini kw auchache tu nikukumbushe tunzaotakwimu.

Prof Humphrey kaja na takwimu, zipinge kwa takwimu. Nimngeomba sana kama huna jambo la maana la kueleza basi ukae kimya. Nadhani unaona eneo lilivyotawaliwa na usatarab. Kama una data ziweke, imaa huna soma zilizowekwa.
Narudia nadhani unaona jinsi eneo lilivyotawali na ustaarabu ni vema ukawa katika mpangilio huo. Matusi hayana nafasi na si mahala pake. Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu, nadhani unapotoshwa sana kwa kutoelewa nini maana ya serikali 1, 2 au 3. Bajeti ya serikali ya Zanzibar ni kitu kingine kabisa nje ya bajeti ya Muungano, Hivyo ukisikia bajeti ya Zanzibar ni bajeti kama ya mkoa kama ingetokea kila Mkoa una serikali yake. Kwa hiyo wakisema bajeti ya Zanzibar ni bil. 700 ina maana ni sawa na bajeti ya kimkoa ama nikwambie kwa mfano fasaha ni sawa na Bajeti ya state ya New York huwezi kuitazama na kuipima na mahitaji ya bajeti ya Usalama wa TAIFA (USA). Hivyo unaweza soma kuwa bajeti ya Usalama homeland security) ni Trillioni 1 na bajeti nzima ya state ya New York ni bil.700 ukasema New York wanafaidika na hawachangii bajeti ya usalama wa Taifa kwa saabu ktk wizara zake hakuna wizara ya usalama wa Taifa..

Kuhusu Mchango wa Zanzibar, mkuu wangu nitarudia tena kusema huyo Profesa anakosea sana anaposema hivyo kwa sababu hakuna kitu Tanganyika wala Bara. Makusanyo yote ya Mapato nchini hutoka kwa watu, wananchi wake hivyo maadam kodi inakusanywa pande zote mbili, mikoa yote na kupelekwa serikali kuu huwezi kuitenganisha Zanzibar na Bara. Labda rudia tena kusoma hayo mambo ya Muungano ndio utajua kwamba Ushuru na forodha imo ktk muungano, mambo ya nje na kadhalika. Hivyo fedha zinapotoka nje au kukusanywa ndani hazipiti mkono wa serikali ya Zanzibar ama Bara bali JMT na zinakusanywa na TRA.

Unaposema Zanzibar haina bajeti ya mambo ya ndani ina maana Zanzibar inaingia moja kwa moja ktk serikali kuu, fedha zinazopatikana kuendesha wizara hiyo zinatokana na bajeti ya serikali ya Muungano ambayo fedha zake zimepatikana kupitia nchi mbili na mikoa yake. Serikali haina miradi wala haikusanyi fedha zake kwa kufanya biashara isipokuwa kupitia kodi za wananchi. Hivyo huwezi nambia Zanzibar hawachangii kitu wakati Tanganyika haipo ila tuna Tanzania ambayo ni bara na Zanzibar.

Mkuu siju hta a nikwambie vipi iiiwa hujui muundo wa serikali hii uko vipi. Kama tungekuwa na serikali 3 ndio ungeweza kutenganisha. Yaani serikali ya bara ina makusanyo yake na serikali ya Zanzibar ina yake kisha wote wamechangia kiasi kadhaa ktk serikali kuu lakini kwa jinsi muundo wa nchi hii ulivyo, zanzibar inachangia moja kwa moja kama bara na ndio maana nilikupa mfano wa Bakhresa, ni Mzanzibara lakini mchango wake ktk kodi ni mkubwa kuliko Wadanganyika mil. 2. Utaweza vipi kuukataa ukweli huo?


Niongezee kidogo,

kama nilivyosema kuhusu Bandari, hi ni moja ya mambo ya muungano inapojengwa Zanzibar makusanyo ya mapato yanakwenda moja kwa moja serikali ya muungano kama ilivyo leo na bandari zetu, haitazuia pato la bandari za Dar, Tanga wala Mtwara na hakika hakuna kitu kitachoweza kufika nchini tusihitaji bandari za Dar, Tanga na Mtwara bado bandari hizo zitahitajika kupokea mizigo kutoka Zanzibar ili isambazwe mikoani. Uzuri wake ni kwamba kila meli itakayo tua bandari ya Dar tayari mzigo uliisha lipiwa Zanzibar TRA kwa bara hivyo mizigo haita kaa dry dock yoyote Bara kwa muda mrefu ili kusambazwa kwa waagizaji wetu.

Tatizo lako unapenda sana kutazama na kuhukumu maandishi yangu pasipo kuingia ndani zaidi ya maoni yangu. Mchango wowote wa mambo yalokuwa ktk muungano nazinufaisha pande zote mbili, ni mfano wa Utalii sasa hivi Zanzibar wanachanga kiasi kikubwa kuliko bara lakini inafaidika na Utalii na pato lake linatangazwa kama pato la Taifa (tanzania) sio Zanzibar.
 
Mkuu Mkandara

Unaposema SMZ ni sawa na mkoa hapo wznz hawatakuelewa. Wao wana rais, bendera, wimbo wa taifa na kila chombo cha dola.

Ningemualika mkuu Mchambuzi atupe takwimu za michango ya mikoa na mgao wa pato la taifa kwa mikoa. Nakumbuka aliwahi kuweka takwimu maridhawa sana. Hapo ndipo utaelewa ninaposema mchango nina maana gani.

Na pia ningemwalika mkuu JokaKuu atupe data za JFC ambazo aliwahi kuzionyesha kwa undani sana ili tuone mchango wa kila mmoja.

Kuhusu kuelekea serikali 1 hapo napo unatafuta ugomvi na wznz. Tulianza hivyo, mwaka 1984 wakaanza kujiondoa na kuhitmisha 2010 kwa katiba inayaowatambua kama nchi Na wznz hawajitambulishi kama Watanzania hata siku moja.
Hivi ulishawahi kusikia mtu anajitambulisha kama Mcalifornia?


Kuhusu bandari, mapato yanaingiaje JMT wakati wznz wameondoa bandari katika mambo ya muungano?
Kumbuka katika yale 11 bandari ilikuwa muungano, sasa hivi siyo.

Na mwisho hebu nielimishe kuhusu utalii, Tanganyika inafaidika vipi?
 
Haya sasa umeanza jipya!.. nimetumia Zanzibar kama Mkoa ili ufahamu vizuri makusanyo ya mapato na mchango wa Zanzibar ktk serikali ya JMT. Kwa maana hiyo huwezi kuitenganisha Zanzibar na Bara ktk tafsiri ya JMT kwa takwimu ambazo hakuna utaratibu mzuri ulowekwa kuitenganisha Bara na Zanzibar ndani ya muungano huo. Hivyo, ndio maana nimekupa pia mchango wa Zanzibar ktk Utalii ambao wao pia wanaweza dai Bara tunafaidika.

Swala la serikali moja ndiko lengo la awali lililokusudiwa, yaani tumeanza kwa hatua ya serikali 2 kutokana na mazingira yalotangulia. Hivyo maadam tumeshindwa ku deal na kero za muungano kwa sababu kila upande unaanza kufikiri kimaskini, uroho na uchu wa changu changu ndio tumefikia hapa. Binafsi yangu kila anayeitaka serikali ya Tanganyika ni fikra za kimaskini na utawajua kwa madai yao kuwa Zanzibar wanafaidika na hivi ama vile badala ya kuzitazama kero zenyewe. Kuna ubaya gani miradi ya maendeleo ikijengwa Zanzabar ilihali pato lake linaenda moja kwa moja mfuko wa Taifa?.

Haya Tazama swala la Elimu ya Juu kuna haja gani ya sheria kupitishwa ati Wazanzibar kadhaa waje kusoma bara ikiwa elimu hiyo ya juu ingepatikana Zanzibar? Kwa nini hatukujenga shule hizo kule hadi leo inajengwa moja kisha tunadai ni msaada kutoka bara. Hizi fedha zimetoka mfuko wa TAIFA na sio mfuko wa bara ambayo haipo. Hiyo bara mnayoijengea hema iko wapi au mnaipata vipi ikiwa makusanyo yote ya mapato yanapatikana ktk mambo ya muungano? Hivyo ni hii dhana ya kuwepo nchi ya Bara ilojengewa nguzo kiasi kwamba Zanzibar wameiona. Na kila mnapotumia maneno haya ya kuinufaisha zanzibar ndio mnadhihirisha kkuwepo kwa serikali ya 3 ilojificha nyuma ya pazia la Muungano.

Wazanzibar wameondoa bandari kutokana na jeuri yetu sisi wenyewe kusema Zanzibar sio nchi. Na ndio maana nikasema JK alikuwa dhaifu sana kumwachia Pinda angefanya kaa alivyofanya Nyerere kwa Malecela na Jumbe.. mawazo yoyote ya kuhujumu Mapinduzi, kubeza Muungano wetu hayavumiliki ila inakubalika tu kutafuta suluhisho la kero zake. Na hakika kutungwa kwa katiba mpya ya Zanzibar kinyume cha katiba ya Taifa, ni utovu mkubwa wa nidhamu na uhaini mkubwa ambao usingepewa nafasi kabisa kama mzee wetu Nyerere angekuwa hai.

Utalii imo ktk mambo ya Muungano toka 1977 sijui ya sasa!
 
Tutajenga shule wakati wao wanasema hilo si suala la muungano? Umesahau kuwa halipo katika 11 na wewe unaita yameongezwa kinyemela hadi 22 ili kuwaumiza wao.

Pili, SMZ inafanya kazi gani? Kwanini wasubiri kujengewa shule wasifanye maamuzi ya haraka kama kuondoa gesi na mafuata, kuunda baraza lao la mitihani, kuondoa bandari na anga?

Yote hayo hawakuhitaji kibali, walikaa na kuamua wenyewe vipi wasiamue kujenga chuo chao hadi wasubiri handout?
Kwani walipojenga SUZA nani alihoji?

Hili la utalii naomba sana msaada wako, hebu tuelemishe wznz wananyonywa vipi.

Na kila ninapokusoma unaelekea serikali 3, kwasababu umeshaamini 1 haiwezekani, 2 ni mazingaombwe.
Kama 3 haziwezekani kuna option nzuri sana vunja jahazi tugawane mbao na misumari.

Kuna tatizo gani tugiwana umasikini kwa raha kuliko kuishi kwa chuki kama ilivyo sasa?
 
Mkuu wangu nimesema yaloongezwa kinyemela ni kulingana na madai ya Wazanzibar tena wasokuwa ktk BLM. Sasa suluhu ya jambo hili ilikuwa nini? ilikuwa turudishe makubaliano ya awali yale mambo 11 tu maana yaloongezwa ndio yamezua kero.Je, hilo BLM linaafiki kutengua yaloongezwa? sidhani! Hivyo sidhani kama wangeweza kujitegemea, lakini pia kumbuka swala la ELIMU ya Juu walitaka kusaidiwa na OIC, sisi tukaingilia kati kwa sababu linahusu mambo ya nje hivyo hawana mamlaka kamili ktk hilo, likaingizwa kinyemela huku.

Hivo basi, kero zote za muungano zinatokana na tafsiri mbaya ya muungano wenyewe pia hizo kero za mambo yaloongezwa kinyemela japo binafsi yangu naamini kabisa kuwa Baraza la Mapinduzi ndio wenye mamlaka ya kutengua mambo hayo na sio BLW ambalo lina wawakilishi wengi pinzani na Mapinduzi yenyewe. Jua tu ya kwamba CUF ina wanachama wengi kutoka ZNP na ZPPP wakati CCM ni wanachama wa Afro Shiraz na Umma Party - Kero nyingine..
 
Mkuu usitumie suala la OIC kupotosha umma. OIC ilikuja miaka 1990..Suala la elimu ya juu lilikuwepo kuanzia miaka ya 1964.

Kwa taarifa yako suala la elimu ya juu halikuingizwa kinyemela, liliombwa na SMZ. Muulize Nasor Moyo.
Narudia tena suala hilo liliombwa na wznz wenyewe.

Wakati wznz wanaomba ilikuwa ni miaka 20 kabla ya OIC. Hivyo kutumia OIC ni kujenga hoja kwa kisingizio.

Mkuu, hapa ndipo unapoungana nami kuhusu serikali 3.
Kama wanataka OIC basi tuwe na serikali 3, tume ya Warioba imetoa uhuru kwa washirika kujiunga na taasisi wanazotaka kama ni hivyo serikali 3 ni muafaka kabisa ili wajiunge na OIC na kupata maendeleo.

Kwasasa kuna uwezekano wa nchi kujiunga, kisichokubalika ni kuiunga kwa kutumia jina la Tanzania halafu matatizo yanakuja Tanganyika in general.

Nimekuonyesha mfano wa kuondoa Maritime na kuunda ZMO.
Ilipoibuka issue ya znz kusajili meli za Iran kibano kilikuwa Tanzania ambayo ni Tanganyika. Pesa lakini 4 dola zimechukuliwa na SMZ tena wajanja madhara yutapate sisi.
Hilo uliangalie kwa jicho angavu.

Unachotaka wewe ni znz kufanya mambo inavyotaka.
Katika nchi zenye muungano hilo haliwezekani.

Ni kwa msingi huo tunasema wakitaka uhuru wa kufanya watakacho wana option mbili
1. Kuvunja muungano
2. Kama hawakubali wasi wakubali mambo 7 ya Warioba

Kinyume chake wakubali kuwa ndani ya ndoa kuna kutoa, kama wanapoke lazima wawe tayari kukubaliana na mambo wasioyataka kwasababu ni sehemu ya msharti ya ndoa.
 
Nguruvi3,
Mkuu wangu tunazungumzia muungano ama kitu gani? hiyo ya mwaka 1964 imeipata wapi. Je, unaweza nambia mambo 11 ya shughuli za Muungano wa awali ni yapi? maana nasoma hapa nayaona kuwa ni Mambo yafuatayo
1. Mambo ya nje, 2.Jeshi na Polisi, 3. Mamlaka ya dharura, 4. Uraia, 5 Uhamiaji, 6 Biashara ya nje, 7. Utumishi wa umma. 8. Kodi ya mapato na forodha, 9 Bandari,10.Usafiri wa anga, 11. Posta na Simu.

Sioni swala la elimu. wewe umelipata wapi?
 
Last edited by a moderator:
Mbona tupo pamoja mkuu! Nimesema elimu ya juu halikuwa suala katika yale 11.

Zanzibar iliomba baada ya muungano miaka ya 1969 kwenda 1970 liongezwe. Mh Sitta alisema bungeni , Nasor Moyo analijua vema. Halikuingizwa kinyemela lilikuwa ni ombi la SMZ. Huo ni ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…