Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

Mkuu gfsonwin,nimefurahi kukusoma kwa mara nyingine tena,nafarijika sana...
Unajua kwa nchi za wenzetu,hizi tunazoziita dunia ya kwanza huwa wanavipaombele vya taifa ambavyo huwa haviyumbishwi na siasa zao,
Kwa mfano Bill clinton(Democrat) alipoiacha nchi ile kwa George Bush(Republican) na kisha G Bush kuondoka na kuiacha nchi hiyo hiyo tena Barack Obama wa Democrat hawatofautiani katika kusimamia vipaombele vya taifa lao,
Ima iwe ni uchumi,usalama na kadhalika,
Huku kwetu inashangaza sana,kila anaekuja huwa anakuja na sera zake na ajenda zake na kuacha kuangalia lipi ni la msingi na la kitaifa la kuliendeleza na lipi la kulipa muda,suala la Mtwara Corridor JK kalipuuza ili hali suala hili lilikuwa na umuhimu kitaifa na si kikanda,mwezangu yeye nadhan kaja kulichukulia kuwa sual hili chinga Mkapa alifanya katika kutafuta kujikomba na kuwasaidia wamachinga wenzake na sio taifa na ndio kwa maana hatushangai kwa yeye kulipuuza na kuhamishia akili yake kwao bagamoyo kwa kipindi hiki cha miaka miwili ilyobakia,najiuilza sana huyo rais ajaye atakuwa na misimamo ipi??sijajua kama atatokea CCM au la,

Ila kikubwa kinachonishangaza ni kwamba wenzetu hawa nchi zao hizi huwa wanabadilishana badilishana,
Msimu huu chama hiki,msimu ujao chama kingine,lakini linapokuja suala la national interests siasa na ubabaisha huwekwa kando na kufanya kazi,sasa hawa jamaa hupokezana vijiti wenyewe kwa wenywe,sasa najiuliza tatizo linatokea wapi??
Kwanini huyu anakuja kulipindisha la yule hali ya kuwa wote ni wamoja??na huwa wote kwenye meza moja za maamuz kichama na kiserikali??
Inashangaza sana kwa kweli...

Karibu sana kaka yangu THE BIG SHOW.
Naomba sasa nijibu hoja yako na ya ndugu yangu , kaka yangu Zinedine kama ifuatavyo;

Nimeona hoja iliyoibuka katika mabandiko yenu #278 na #280 ni kwamba HATUNA NATIONAL PRIORITIES ambazo zinatakiwa ziwe AMONG THE FIRST PRIORITIES kwa pesident candidate. na baraza lake la mawaziri.

Kwangu mimi naona sasa umefika wakati wananchi tuamue kwenye katiba hii mpya of which sijui kama itakuwepo kweli ama la kwamba among other things, ni kwamba rais anayechaguliwa lazima ahakikishe kwamba anafwata national interest na hizi zinatakiwa zipangwe na Katibu mkuu Kiongozi akishirikiana na watu wa sera na mipango ya ofisi yake.

hapa nina assume kwamba huyu CHIEF PERMANENT SECRETARY sio mwanachama wa chama chochote cha siasa na huyu tunaweza kumfkukuza na kumshtaki iwapo atakwenda kinyume na matakwa ya katiba yetu.

Binafsi kuna siku nilishiriki kwenye mjadala wa rasimu mpya ya katiba, nilishangazwa sana kuona pale hatukujadili mambo kama haya ila tulijadili sijui eti katiba iwe inasema mwanaume/mwanamke badala ya mwananchi...........ghhhhhhhhhhhhh nilikasirika sana, yaani sijui na wale waliokuja walitudororesha na nini......................

mara tunajadili ooh! kwenye katiba tuondoe ulazima wa mtu kuimba wimbo wa taifa, kwasabbau uko biased kwa mtu asiye mwamini Mungu.............. mimi niliboreka sana nikajiondokea manake niliona sina cha kuongea. Kumbe kuna mambo ya msingi kama haya ambayo tunatakiwa tuyajadili kwa kina kabisa.

napenda sana niwashukuru Zinedine, THE BIG SHOW Nguruvi3 na Mchambuzi kwa kunishirikisha katika mjadala huu na kujibu hoja zangu. Lakini pia napenda niwasisitize kwamba we are the voices of soo many people tusikae kimya lets talk am sure ipo siku tutasikika tu.

Binafsi sijapata muda mzuri wa kujadili rasimu ya katiba ila when given chance ningependa sana nishiriki mjadala wenu wa aina hii.

once again thanks.
 
Last edited by a moderator:

Kabisa gfsonwin, uko sahihi. Hakuna hicho kitu kinachoitwa priorities katika nchi hii wala kufuatwa utaalam. Nikiunga mkono juu ya uimarishwaji wa kitaasisi, nadhani vyombo viwili vilitakiwa viundwe na vitambulike na Katiba. 1. National Economic Advisory Council(NEAC, Baraza la Taifa la Ushauri wa kiuchumi), na liwe huru na wajumbe wake watokane na merits na maadili na lisiwe biased na upande wowote, pamoja na majukumu ya kuishauri nchi katika masuala ya kiuchumi lakini pia Baraza hili liwe linapitia na kupitisha Ilani za vyama vyote vya siasa ili kubaini kama ziko in line na vipaumbele vya nchi bila kutoka katika mstari. Chombo cha pili ni Baraza la Taifa la majadiliano ya mikataba (National Council on International Negotiation) likichukua nafasi pia ya GNT ambayo imeonekana kujali personal interests zaidi. Vyombo hivi viwe huru, na viwe wazi katika masuala yote ya vipaumbele na mikataba ili kuepusha wanasiasa kutekeleza mipango ya maendeleo unaotokana na utashi, ukabila, ukanda, udini au any personal interests. Sikubaliani na mfumo wa majadiliano unaotumika hivi sasa ambapo mambo yakiharibika hakuna wa kumkamata, na majadiliano yanahusisha watu either wasio na uwezo wa kujadiliana au wenye maslahi binafsi. Kinyume chake, maamuzi makubwa ya nchi hii yataendelea kufanywa na watu wenye upeo duni na kuleta maisha duni daima-dawamu. Nami pia niwashukuru Mchambuzi na Nguruvi3, kwa muda mrefu nimekuwa nikijifunza mengi sana kwa watu hawa hasa namna wanavyoweka pembeni ushabiki wa kisiasa katika mijadala yao. Mungu awalinde na azidi kuwaongoza.
 
Nguruvi3 rejea bandiko lako #279 , umenieleza kitu cha ajabu sana toka kukua kwangu sijawah kukiskia. How comes mradi mkubwa kama huu hauna EIA?? JE NEMC, na ofisi ya makamu wa rais mazingira wanacho cha kujitetea??

WHO knows kutattokea nini as a result?? je inamana serikali yetu licha ya kwamba ni mshirika wa makubaliano ya utunzaji wa mazingira duniani na kila mwaka inalipa membership fee na ikakubali kuwepo na penalties kwa kila mshirika atakayekiuka maswala ya utunzaji mazingira lakini bado yenyewe inashindwa kutekeleza makubaliano??

je serikali unless inatuficha lakini kwa jinsi nijuavyo mimi ni kwamba kwa kutokuwa na EIA kwenye mradi kunapelekea taifa kulipa kiasi kikubwa sana cha fedha kama faini sasa hili lingeweza kuepukika tu.

tizama swala la KIHANSI TOADS lilivyoigharimu nchi hii fedha nyingi sana na bado mpaka leo mtu nayewalea vyura hawa hapa UDSM analipwa pesa nyingi sana ishu ni kwamba hakukuwa na EIA sasa je bado serikali inarudia makosa haya haya??

angalia mradi wa kakobe na mpaka leo umeme bado hauwaki licha ya kwamba serikali imezika na kusmamisha mabilion ya hela pale lakini wapi je hatujifunzi??

sasa jamani tunaze sisi wananchi kuamka na kulazimisha mabadiliko ya kweli kwenye hili taifa. kama mradi wa gesi huu hauna EIA hauna sera ya gesi je tunafanya drilling ya nini??

ngoja ni kwambie kwenye nchi walizoendelea ungekuta mradi kama huu watu wamesha study in real cost benefit anaylsis. watu wangekwisha kujua mradi utaigharimu nchi sh ngapi kama matumizi ya mwezi na nchi ingepeta sh ngapi kama mapato yake. tungekwisha kuproject gesi bila wataalam ingegharimu expert importation kwa kiasi gani, lkin pia tungeweza kuinvest kwenye human resource wakati hawa wagen wakiwa kwenye contract.

unajua kuna mambo mengi sana ndani ya hii nchi yanafanyika kisanii sana, mfano mwingine ni huu unakuta donors wamekuja hapa na bonge la mradi na mapesa yao, lkn cha ajabu unakuta mradi unaanza mbeleni unakutana na mapungufu ndipo eti wanasema watu waende short courses sasa najiuliza huo muda wakiwa short courses kazi za mradi wanamwachia nani?? je kwann wataalam wako wasiwe updated kila mara na sio kipindi cha miradi tu?? leo hii muulize procument officer yyte guidelines procurement za WB/IDA uone atakavyo kushangaa. lakini serikali itasubiri hadi IDA walete mradi ndipo wapeleke wataalam wakati vitu kama hivi hawa wangetakiwa wapewe since wakiwa vyuoni na mwajiri alazimishwe atleast kila baada ya miaka 3 amfanyie training huyu mtumish ili awe aware na standards za kimataifa.

utashangaa sana kuona vitu kama M&E eti ni watumish wa serikali wa muda mrefu lkn bado hawawez na ni managers wa taasisi unajiuliza hivi huyu meneja anafanyaje kazi zake?? hivi kweli inamaana sisi hatuna standars??

ukitaka kichekesho nenda kwa internal auditors utashangaa yaani zaid ya kujua audit za kitanzania hawana ujuzi wowote kuhusu international auditing unashangaa mpaka uje mradi mkubwa watu waanze kuona ugumu ndipo waseme tumwombe huyu donor tupeleke watu short course sasa kama ni short course kwann usipeleke kabla hao watu wako??

mimi narudia tena kusema kama wataalam wa RISK MANAGEMENT, FINANCE &AUDIT, M&E, PROCUREMENT,GAS DRILLIN ENGINEERING, MECHANICAL ENGINEERING, ENVIROMENT protection EXPERTS, NA CIVIL ENGINEERING hawajaanza kufikiriwa na hii serikali basi huu mradi utakuwa ni wa maangamizi kwa taifa as hakuna kitakacho kuwa kinafanyika zaid ya hasara tu. tena uje uskie bomba la gesi limepasuka ama sijui limeibwa.
 
Last edited by a moderator:
.

Leo tunawaacha Wamtwara kwasababu tuliwaacha wa Nyamongo, Geita na Bulyamhulu.
Kesho tutawaacha wa Mchuchuma na Kiwira kwasababu tuna uzoefu wa kuwaacha wenzetu.
Kikundi cha watu wachache kinazidi kutumaliza eti kusimamia haki ya kujua haki yako ni uchochezi, eti ni ukorofi, udini na upinzani.

Tukifanikiwa kugoma kugawanywa na kusimamia haki hapo tutakuwa na jibu la swali la Zinedine.

Mkuu Nguruvi3 umenena mambo mazito sana lakini hii tabia ya watanzania ie wanasiasa,raia wa kawaida,vyombo vya habari kuacha kuungana na watanzania wengine wenzao wenye matatizo imekuwa sehemu ya utamaduni wetu.Ni kama vile Nyumbu anavyosambuliwa na Simba 3 au 4huku kundi kubwa la Nyumbu zaidi ya elfu 1 ,2 wakimtazama mwenzao anavyoteketea bila kutoa msaada.Ni kweli tuliwaacha wa Nyamongo,Geita na Bulyamhulu bila kusahau wamasai wa Loliondo.
 
Last edited by a moderator:
CCM NA WARAKA WA RASIMU YA KATIBA

Wanajamvi, baada ya kuona jinsi gani tumewatosa wenzetu wa Mtwara kama livyosema Ngongo(mfano wa nyumbu na simba) turejee katika suala la rasimu ya katiba wakati huu mabaraza ya kata yakikaa.

Inasikitisha kuona hoja ya muungano imechukua sehemu kubwa ya majadiliano na kuacha vipengele vingi muhimu vinavyoathiri maisha yetu ya kila siku.

Kwa mfano, kuna kipengele cha rasimu kinachosema ni marufuku mtu kulazimishwa kufanya kazi kama sehemu ya haki za binadamu. Kipengele hicho hakiongelei wafungwa wa magereza wanaangukia sehemu gani.
Je, kuwalazimisha kufanya kazi ni kukiuka haki zao?

Pili, kuna kipengele kinampa rais uwezo wa kutangaza hali ya hatari bila kuainisha ni kwa msingi gani.

Upo uwezekano rais kutumia kipengele hicho kuziba haki za binadamu, kwa mfano kuzuia harakati za wapinzani au wanaharakati, au kuzuia wananchi kuipinga serikali pale wasipokubaliana nayo

Hata hivyo suala la muungano ni jambo zito linaloamua mustakabali wa taifa.
CCM wametoa waraka kwa wanachama wao kushinikiza uwepo wa serikali 2 na si tatu au vinginevyo.

Sijjui kama viongozi wa CCM wanaopigia debe hali hiyo kama kweli wana weledi wa mambo au nia njema na taifa hili.

Serikali 2 zimekuwa ni tatizo kwa muda mrefu kukiwa na malalamiko kutoka kwa wazanzibar kuwa Tanganyika inawanyonya kwa kujificha katika muungano.

Tanganyika wanalalamika ndio wamebeba gharama za muungano kwa asilimia 100, wakitoa fursa kwa wazanzibar wakati hawana fursa hizo wakiwa huko kwao.
Tanganyika wanaona hawana cha kupoteza hata kama muungano utavunjika.

Hoja ya serikali 3 inaonekana kuwa na afadhali kwa Tanganyika na kuwa mwiba kwa wazanzibar.
Mathalani, uwepo wa serikali ya Tanganyika utaziba mianya ya fursakwa wazanzibar na kufungua fursa kwa watu wake.

Hivyo nao kwa kuzingatia lawama wanazotupiwa na wazanzibar wameamua kukomalia hoja ya serikali 3.

CCM inaangalia rasimu kwa kutumia Zanzibar , kwamba wao wakiwa walalamikaji wana uwezo wa kuamua serikali za aina gani ziwepo. Kosa ambalo CCM inalifanya ni kutosoma mazingira ya Zanzibar na hivyo hoja yao itajiua yenyewe bila mkono wa mtu.

Zanzibar wanataka utaifa wao ndio maana wanataka uwepo wa rasi wao bila kujali jambo lingine.
Wao wanaamini kuwa na bendera, wimbo wao wa taifa na kiti katika jumuiya ya kimataifa.
Ili kuweza kufikia lengo hilo wazanzibar wanashinikiza uwepo wa serikali ya Tanganyika ili kuwe na usawa wa washirika wa muungano.

Ingawa wamefundishwa na CCM kusema serikali mbili hasa kule Unguja, tatizo linakuja kuwa serikali mbili zinaondoa uwezekano wa wao kuwa na bendera yao, wimbo wa taifa na hata kiti katika jumuiya yoyote kama ilivyo sasa.

Kwahiyo wanaposema serikali 2 wanasahau kuwa watakuwa wamepoteza 3/4 ya mambo wanayotaka.

Kujichanganya kwa CCM ni kuwaambia watu waseme serikali 2, wakati wazanzibar wanataka serikali ya Tanganyika irudi kama ilivyokuwa mwaka 1964.

Maana yake ni kuwa wanaimba serikali 2 wakati wanataka muundo wa serikali 3.
Sijui hapa inaeleweka! Yaani wakitaka serikali 2 lazima waue madai ya uwepo wa Tanganyika.
Ni lazima wakubali kuwa Tanganyika ndiyo itakuwa Tanzania na kurudi hapa tulipo.

Hata hivyo wale wanaosema serikali 2 wanashindwa kujiuliza kuwa iweje seikali 2 zimekuwepo nusu karne na zimeshindwa kutafuta suluhu ya muungano?

Tume zimeundwa na hakuna jibu sijui rasimu hii itawezaje kutatua tatizo wanaloliona sasa hivi.
Hapa ndipo tunahoji kama CCM na wakaraka wake viliandaliwa na watu wenye akili timamu?

Watanganyika wanataka serikali yao ili washughulikie mambo yao na waondokane na lawama zisizo na msingi licha ya ukweli kuwa wao ndio wameubeba muungano kwa gharama.

Ingawa CCM imetoa waraka wa serikali 2 zinazoimbwa na baadhi ya Watanganyika waliofundishwa, swali linakuja je, Watanganyika hao wameridhia kwa kuangalia mustakabali wa taifa lao?

Je, kitendawili cha uwepo wa Tanganyika kama taifa na utaifa kimetenguliwa? Hapo CCM wamejichanganya maana hoja zitajiua zenyewe

Kumekuwa na madai ya kupotosha kuhusu serikali 3. Wana CCM wanasema serikali 3 zitakuwa mzigo.
Ni kituko na ufinyu wa kufikiri kwasababu serikali 3 zina maana kuwa kutakuwa na serikali ya shirikisho ambayo itakuwa ndogo na lazima ichangiwe sawa na wabia bila kujali idadi ya watu au eneo.

Hii ni kwasababu wazanzibar wamedai usawa katika kila jambo lisilohusu gharama na wakati wa gharama wamejificha katika kichaka cha udogo na watu wachache.

Uzumbukuku huo wa wazanzibar lazima uwekwe wazi. Hawawezi kudai ajira na mambo lulukiki wakakimbia gharama.

Lakini ni ukweli kuwa hata kama serikali ya shirikisho itakuwa na bajeti ndogo sana bado kwa wazanzibar itakuwa mzigo kwao. Kwa mfano tu wa mjadala huu, gharama zikiwa trilioni 1 maana yake ni bilioni 500 kila upande. Wakati znz ikiwa na bajeti ya bilioni 700 hilo halitawezakana na bado Mtanganyika atabeba mzigo tu.

Upotoshaji wa serikali 3 ni kutokana na ukweli kuwa uwepo wa serikali ya Zanzibar utailazimu serikali hiyo kuhudumia watu wake kwa mambo yasiyo ya muungano na hivyo kupunguza mzigo kwa Tanganyika.

Na Tanganyika itabidi ihudumie watu wake bila kupunguza chochote Zanzibar.
Maaana yake ni Tanganyika na Zanzibar kila moja itakuwa na gharama zake kulingana na mhitaji yake bila kutegemeana. Hapo tutakuwa tumepunguza gharama.

Kwa mfano uendeshaji wa serikali ya Tanganyika utazingatia uchumi wake kama ilivyo Zanzibar.
Yoyote miongoni mwao atakayeamua kuwa na serikali kuubwa haitahusu upande mwingine.

Kusema kuwa serikali 3 ni mzigo ni upotoshaji kwasababu mzigo huo utabebwa na kila mshirika peke yake.
Unless CCM waseme kuwa uwepo wa serikali 3 utahusu serikali ya Tanganyika kuhudumia SMZ jambo ambalo si kweli.

Tunapoongelea serikali 3 hatupaswi kuangalia serikali zote kwa pamoja, tunapaswa kuangalia serikali ya shirikisho ambayo itakuwa ndogo yenye vyombo vichache na isiyo na gharama kubwa.
Hivyo jicho la gharama za serikali 3 lipelekwe kwa serikali ya shirikisho na wala si serikali za washirika.

Hoja ya CCM kuhusu serikali 3 nayo inakufa yenyewe kwasababu lazima tuangalie serikali ya shirikisho, mfano kama Tanganyika itakuwa na serikali yenye wizara 3 hilo litaathiri vipi gharama za serikali ya mapinduzi au kama SMZ itakuwa na wizara 20 hilo litaathiri vipi serikali ya Tanganyika?

Kila mmoja atapanga serikali kutokana na uchumi wake ndio maana rasimu imesema mapato yote yatabaki kwa nchi husika.

Nimalizie kwa kusema CCM na serikali yake vimeteka hoja ya muungano bila kuwa na mkakati wala kujua nini kitatokea na hatima ya taifa hili. Viongozi wa CCM wamejikita katika kutafuta nafasi za uongozi na si muafaka wa kitaifa. Hili ni jambo la hatari sana kwa maendeleo na demokrasia ya nchi.

Tume ya Warioba nayo inabeba lawama. Haiwezekani tume iliyosheheni wasomi kama hii ikashindwa kuelewa kuwa jambo la kwanza ilikuwa kutafuta ridhaa ya wananchi kwa kura ya maoni endapo wanahitaji muungano au wakati umefika tuachane kwa amani.

Kama kungekuwa na kura ya maoni maana yake wananchi wa pande zote wangeridhia kutoa kwajili yake, na kwavile hakuna nani atatoa kwa ajili ya mwenzake.

Ni kwa msingi huo tunaona tume inakuja na proposal za jina la Tanzania bara na hakuna Tanzania visiwani. Wameshindwa kuwa na muafaka kama uwepo wa mawaziri wakuu wamebaki na marais 3 n.k.

Suala hili litasumbua sana na inawezekana ndio ukawa mwanzo wa kuvunjika kwa muungano.
Kuvunjika kwa muungano kuna athari kwa upande wa Zanzibar kuliko Tanganyika.
Kijiografia, kisiasa na kiuchumi bado Zanzibar inategemea Tanganyika, ni kanuni za asili (natural law) zinazoamua na si kundi la watu. Na hiyo ndiyo itakuwa nafuu kwa Tanganyika.

Wakati huu wa mabaraza Watanganyika wazingatie utaifa wao kwanza na yatokanayo na utaifa huo.
Muda wa kubebana sasa umefika kikomo, na nchi zote mbili kama zinahitaji muungano ziwe tayari ku-sacrifice.
Ni ujuha kwa Tanganyika kutoa kwa ajili ya nchi jirani na ndio maana tunawausia wana mabaraza waukatae waraka wa CCM na wasimame na taifa na utaifa wao kwanza.

Tusemezane
 
Nguruvi3 rejea bandiko lako #279 , umenieleza kitu cha ajabu sana toka kukua kwangu sijawah kukiskia. How comes mradi mkubwa kama huu hauna EIA?? JE NEMC, na ofisi ya makamu wa rais mazingira wanacho cha kujitetea??

WHO knows kutattokea nini as a result?? je inamana serikali yetu licha ya kwamba ni mshirika wa makubaliano ya utunzaji wa mazingira duniani na kila mwaka inalipa membership fee na ikakubali kuwepo na penalties kwa kila mshirika atakayekiuka maswala ya utunzaji mazingira lakini bado yenyewe inashindwa kutekeleza makubaliano??

je serikali unless inatuficha lakini kwa jinsi nijuavyo mimi ni kwamba kwa kutokuwa na EIA kwenye mradi kunapelekea taifa kulipa kiasi kikubwa sana cha fedha kama faini sasa hili lingeweza kuepukika tu.

tizama swala la KIHANSI TOADS lilivyoigharimu nchi hii fedha nyingi sana na bado mpaka leo mtu nayewalea vyura hawa hapa UDSM analipwa pesa nyingi sana ishu ni kwamba hakukuwa na EIA sasa je bado serikali inarudia makosa haya haya??

angalia mradi wa kakobe na mpaka leo umeme bado hauwaki licha ya kwamba serikali imezika na kusmamisha mabilion ya hela pale lakini wapi je hatujifunzi??

sasa jamani tunaze sisi wananchi kuamka na kulazimisha mabadiliko ya kweli kwenye hili taifa. kama mradi wa gesi huu hauna EIA hauna sera ya gesi je tunafanya drilling ya nini??

ngoja ni kwambie kwenye nchi walizoendelea ungekuta mradi kama huu watu wamesha study in real cost benefit anaylsis. watu wangekwisha kujua mradi utaigharimu nchi sh ngapi kama matumizi ya mwezi na nchi ingepeta sh ngapi kama mapato yake. tungekwisha kuproject gesi bila wataalam ingegharimu expert importation kwa kiasi gani, lkin pia tungeweza kuinvest kwenye human resource wakati hawa wagen wakiwa kwenye contract.

unajua kuna mambo mengi sana ndani ya hii nchi yanafanyika kisanii sana, mfano mwingine ni huu unakuta donors wamekuja hapa na bonge la mradi na mapesa yao, lkn cha ajabu unakuta mradi unaanza mbeleni unakutana na mapungufu ndipo eti wanasema watu waende short courses sasa najiuliza huo muda wakiwa short courses kazi za mradi wanamwachia nani?? je kwann wataalam wako wasiwe updated kila mara na sio kipindi cha miradi tu?? leo hii muulize procument officer yyte guidelines procurement za WB/IDA uone atakavyo kushangaa. lakini serikali itasubiri hadi IDA walete mradi ndipo wapeleke wataalam wakati vitu kama hivi hawa wangetakiwa wapewe since wakiwa vyuoni na mwajiri alazimishwe atleast kila baada ya miaka 3 amfanyie training huyu mtumish ili awe aware na standards za kimataifa.

utashangaa sana kuona vitu kama M&E eti ni watumish wa serikali wa muda mrefu lkn bado hawawez na ni managers wa taasisi unajiuliza hivi huyu meneja anafanyaje kazi zake?? hivi kweli inamaana sisi hatuna standars??

ukitaka kichekesho nenda kwa internal auditors utashangaa yaani zaid ya kujua audit za kitanzania hawana ujuzi wowote kuhusu international auditing unashangaa mpaka uje mradi mkubwa watu waanze kuona ugumu ndipo waseme tumwombe huyu donor tupeleke watu short course sasa kama ni short course kwann usipeleke kabla hao watu wako??

mimi narudia tena kusema kama wataalam wa RISK MANAGEMENT, FINANCE &AUDIT, M&E, PROCUREMENT,GAS DRILLIN ENGINEERING, MECHANICAL ENGINEERING, ENVIROMENT protection EXPERTS, NA CIVIL ENGINEERING hawajaanza kufikiriwa na hii serikali basi huu mradi utakuwa ni wa maangamizi kwa taifa as hakuna kitakacho kuwa kinafanyika zaid ya hasara tu. tena uje uskie bomba la gesi limepasuka ama sijui limeibwa.

Mkuu wengine tunaalikwa/tunaombwa kwenye nchi za watu tukatoe ushauri kuhusu mazingira.....na tunapotoa maoni kwa serikali husika wananzingatia......tena mijadala ya mazingira huwa ni ya wazi sana.......wananchi hushirikishwa kwa sana.......kuanzia kuelimishwa mpaka kutoa maamuzi.......

Kwa nchi mbali mbali ambazo nimepita......NGO za mazingira ziko so ACTIVE.....vitu haviendi kiholela holela....hata kama serikali imeamua.....na kama vinaharibu mazingira basi ndio mwisho wa mradi........Ndiyo tuilaumu NEMC.....lakini kusema ukweli sijawahi kusikia NGO ya mazingira huko nyumbani iliyo ACTIVE.....tunategemea kusikia kelele za Dr. Terezya peke yake....HAWEZI....na yeye keshasema...unfortunately!!

kuna nchi zingine zina Marine National Parks sijui kama kwetu sisi kuna hizo parks!........
 
Ogah;6938615]Mkuu wengine tunaalikwa/tunaombwa kwenye nchi za watu tukatoe ushauri kuhusu mazingira.....na tunapotoa maoni kwa serikali husika wananzingatia......tena mijadala ya mazingira huwa ni ya wazi sana.......wananchi hushirikishwa kwa sana.......kuanzia kuelimishwa mpaka kutoa maamuzi.......

Kwa nchi mbali mbali ambazo nimepita......NGO za mazingira ziko so ACTIVE.....vitu haviendi kiholela holela....hata kama serikali imeamua.....na kama vinaharibu mazingira basi ndio mwisho wa mradi........Ndiyo tuilaumu NEMC.....lakini kusema ukweli sijawahi kusikia NGO ya mazingira huko nyumbani iliyo ACTIVE.....tunategemea kusikia kelele za Dr. Terezya peke yake....HAWEZI....na yeye keshasema...unfortunately!!

kuna nchi zingine zina Marine National Parks sijui kama kwetu sisi kuna hizo parks!........
Ogah ,gfsonwin hatuna upungufu wa taarifa wala watalaam. Tunaupungufu wa viongozi na uongozi.

Nadhani mnafahamu kuwa mradi wa umeme wa Stiegler gorge uliobuniwa na wajerumani miaka ya 1930 ulikuwa na kila kitu. Ukisoma ripoti ya mradi wakati utagundua wenzetu wanatumia wataalamu.

Hakuna kiongozi anayefikiria tunayoongelea hapa, fikra zao ni 10% ya uhalifu wa nchi.
Tulidhani ujio wa vijana wasomi ungeweza kuleta mabadiliko, nakuhakikishieni ni maafa tu

Katika wabunge 20 vijana ukiwauliza kuhusu Stiegler gorge au Songo songo gas kama wameshawahi kusoma taarifa, nasema kusoma taarifa tu za miradi hiyo, hakuna katika sample ya 20. Labda sample ya 50 unaweza pata mmoja au wawili

Tukitaka tuondoke hapa tulipo lazima tuchukue radical measures.
China, Korea kusini ,Asian Tiger, Japan waliliona hilo.
Kwa mfano, china ukichukua rushwa utakula risasi tu. Waliohusika na kutengeneza maziwa yenye melanin yaliyoharibu soko la bidhaa za china wote ni marehemu.

Japan watu walioandaa taarifa ya uchumi baada ya Tsunami hakuna mwenye kazi.
Huko Japan rushwa au ubadhirifu mtu anakula kitanzi na mara nyingi hujinyonga kabla . Hakuna pa kutokea

Tanzania tunatakiwa tuanzie hapo, kwamba kiongozi anawajibika au kuwajibishwa na umma kwa namna yoyote inayowezekana iwe kwa hiari au kwa lazima na gharama yoyote.

Kama hututakuwa radical kwa hatutafanikiwa.Tuwe radical na si viongozi watengeneze mazingira hayo, sisi wananchi lazima tuchukue ownership ya nchi na kuwatia adabau watawala.

Wiki mbili zilizopita zimeibiwa bilioni 8 za mkutano wa partneship. Taarifa ipo wazi ,katibu mkuu kiongozi amekiri kutokea. Kwa nchi yenye Rais, Makamu na Waziri mkuu hakuna aliyetegemea jambo hilo kufichwa chini ya kapeti. Linafichwa kwasababu msisimazi wa mradi ambaye ni katibu kiongozi ameshindwa kuwachukulia hatua wahalifu anao wajua kwasababu wana mtandao na wakubwa. Wizi wa viongozi tunawaowahudumia

Kwa nchi za magharibi Rais na waziri mkuu wangekuwa katika wakati mgumu sana na vibarua vyao.
Pengine kashfa kama hii ingeondoka na mmoja kama si wote.
Kwa nchi kama china wote waliohusika na wizi huu wangeshakula risasi kitambo.

Ndivyo wenzetu wanavyoweza kusonga mbele, leo china ni uchumi namba 2 duniani.
Angalia miaka 30 iliyopita uone tofauti kati yetu na China na tofauti iliyopo sasa.

Hakuna utawala wa sheria unaoruhusu mtu kufa kwa kukosa 1,500 ya antibitic kuruhusu genge la watu wakilindwa na viongozi wa nchi kiuba bilioni 8 liachiwe.

Hakuna kosa kama kuna radical measures za kuhukumu vifo watu hawa kama China na Japan wanavyofanya kwasababu kupitia wizi wao watu hao wamehukumu vifo vya mamia ya Watanzania wasio na hatia.

Leo utawala umesimama kunyoosha mitutu ya silaha kwa wananchi wa Mtwara kwasababu tu wanataka kujua ushiriki wao katika mradi na thamani zitokanazo na mradi kwa maisha na jamii zao!! Mabomba yanalazwa kwa mtutu, wananchi wantandikwa viboko kuhoji gas na si pesa, gas iliyopo ardhini.! bila kuiba chochote wanachapwa mijeledi na kurushiwa risasi! kwa kuhoji tu.

Serikali hiyo hiyo imeshindwa kujua nani kaiba mapesa ya miradi kibao ambayo hadi leo hakuna majibu na hata za wiki mbili zilizopita wameiba bilioni 8 hadharani Rais, makmu waziri mkuu na katibu mkuu kiongozi wakiona na wakijua, wanalindana. Hawaelekezeani mitutu kwasababu wanafadika na wizi wa mabilioni.

Haiwezekani serikali iweze kukabiliana na watu wa Mtwara ambao ni milioni 2 na kushindwa kukabiliana na genge la wezi wa bilioni 8 wasiozidi 10.

Viongozi wanashirikiana katika kuiba na kudhulumu ndio maana tunasema bila kuwa na kanuni za kuwajibishana ikiwa ni pamoja na kunyongana na kuchapana risasdi kama China au Japan hatutaondoka katika umasikini.

Soma rasimu ya katiba, viongozi wamejitengenezea utaratibu kuwa hawatashitakiwa kwa makosa waliofanya wakiwa katika uongozi. Kwamba hata tukijua waliiba bilioni 20 kwa kushirikiana na watoto wao si wao au watoto wao watakaoshtakiwa!!!

Tunatakiwa tukatae kipengele hiki kwanza, kwamba Rais au kiongozi mwingine akibainika na makosa aadhibiwe. Tubadili kanuni za adhabu, kwamba hukumu ya rushwa za kimadaraka ni risasi tu.

Kwamba mradi umefeli kwasababu ya 10% basi watafutwe wote kwa kulitia taifa hasara wasomewe mashitaka na hukumu na walambwe risasi. Period!

Ndio njia rahisi ya kuinusuru nchi.

Tisemezane
 
UNAFIKI WA VIONGOZI WA DINI NA UDHAIFU WA SERIKALI YETU

Wengi wenu mtakuwa mumeshika midomo kwa mshangao kusoma kicha hapo juu.
Pengine mwisho wa mjadala huu mtaweza kuelewa kusudio la bandiko na kuwafungua katika 'kadhia'

Unafiki ni kutenda, kusema au kusimamia kitu katika hali ya undumila kuwili. Kwamba, kuna nyakati mtu au watu wanaamini jambo fulani wakati huo huo wakikinzana na jambo hilo kwa mgongo mwingine.

Viongozi wetu wa dini zote kuu wamekuwa na undumiliwa kuwili huo.
Imekuwa ni kawaid kusikia katika maadhimisho yawe ya Krismasi, Pasaka, Idd alhaji au Idd filtri, maulidi, warsha, semina, vikao vya utakaso n.k. viongozi hao wakiongelea amani ya nchi na umuhimu wake.

Viongozi hao wamehusisha imani za kidini,kwa kutumia misahafu na biblia na kila aina ya matoleo, hadithi, sunna, mapambio, maandiko n.k. kusisitiza kuhusu amani na jinsi gani mungu angependa watu waishi kwa utengamano, amani na utulivu.

Tumewasikia wakiandaa makaongamano, sala za kuombea taifa amani n.k. ili kuwa usia waumini wa dini zao kuhusu kujenga na kulinda amani ya nchi. Wamekwenda mbali hata kuhusisha mambo ya utawala na siasa kama sehemu ya uovu uliotamalaki katika jamii.

Viongozi hao wamelaani ten percent, ufisadi, ufujaji wa fedha na kushindwa kuhudumia masikini.
Tena wakisisitiza kuhusu haki za mwanadamu, utawala bora na wakisheria kwa matamko mazito yanayosimumua na hata kufikirisha.

Miaka ya karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la wanasiasa kutumika katika shughuli za kidini tena wakipewa hadhi kubwa utadhani wao ndio wasomi na manguli katika dini.

Hali hiyo imekuwa mbaya na kuhusisha viongozi wa kisiasa katika harambee za makanisani na misikitini kwa kuwatumia wanasisa.

Aghalabu ni rahisi kusikia mbunge, meya, waziri, katibu mkuu n.k. wakiongoza harambee za mamilioni kuchangia mambo kadha wa kadha katika dini zao.

Viongozi wa kisiasa ni wanadamu ambao kazi yao haimaanishi kuwaondoa katika mambo ya kiroho. Lakini hawa si viongozi wa dini na wala hawapaswi kupewa hadhi katika safu za viti vya mbele.
Wao ni waumini kama walivyo wengine na hiyo ndiyo haki yao.

Kwakutambua kuwa siasa ni mchezo mchafu viongozi hao wanatumia nafasi wanazopewa katika kufikia malengo yao ya kisiasa. Michango yao na jitihada zao si za kiuumini bali zimefungamanishw na matakwa ya kisiasa. Kwamba huko ndiko wanakotaka waungwe mkono kwa kutumia viongozi wa dini

Tunaelewa kuwa viongozi wa dini wana nguvu kubwa sana katika ushawishi wa waumini wao.
Mara zote wamekuwa wanasikilizwa hata kama hoja zao hazifikirishi. Si kiongozi kasema!!!!

Hivi karibuni kuna kiongozi maarufu amekuwa akipita makanisani na misikitini kuchangisha harambee.
Inasemwa kisias alicho changa hadi sasa ni mabilioni ya pesa.

Kiongozi huyo anyehusishwa sana na uchaguzi wa 2015 kupitia chama tawala amejitetea kuwa michango na pesa zake zinatokana na michango ya marafiki zake.

Utetezi huu dhaifu na wa kipuuzi unatupelekea kuamini kuwa kiongoz huyo eti amejivika wadhifa wa kufikisha michango ya waumini wenzake kwa mungu kama yeye na si kama wao.
Kwamba yeye amechukua jukumu la kidini la kuwafikishia michango hiyo.

Hali ni kama hiyo kama tunavyoshuhudia kila siku. Mara utasikia waziri wa imani fulani ameongoza harambee kanisani, mara meya fulani, mara katibu mkuu fulani n.k. Wote hawa hufanya hayo kama sehemu ya mtaji wa kisiasa.

Viongozi wa dini wanafahamu hali hiyo wazi na wanajua kuwa hilo litazaa balaa siku za baadaye na kupekekea uvunjifu wa utangamano wa taifa na imani kwa waumini.

Tumeshuhudia kukiwa na mijdala mikali hadi bungeni ambako wabunge wameasi vyama vyao ili kutetea imani na wala si wananchi waliowapeleka. Tumeona mivutano ya kidini ikiendelea na tumeona vurugu ambazo chanzo chake ni sababu za dini.

Viongozi hawa dini wanaowakaribisha wanasiasa kuwagawa wananchi wanafahamu madhara ya kile wanachokifanya. Wanafahamu kuwa mungu hapendezwi na unafiki wanaoufanya wa kuhubiri amani kwa mlango mmoja na kuchochea uvunjifu wa amani kwa upande mwingine.

Ikifika hapo nadhani wasomaji watakubaliana na duru za siasa kuwa viongozi hawa ni wanafiki kama kichwa cha habari kianvyosema.

SERIKALI DHAIFU
Katika siku za nyuma viongozi walikuwa waumini kama wengine huko misikitini au makanisani walikwenda kama waumini. Kama ilitokea kupewa hadhi basi ni kwa heshima ya nafasi zao na wala si kwasababu ya nyadhifa za kisiasa au ushawishi wa kutaka kuungwa mkono na viongozi wa dini.

Hata ilipotokea viongozi hao wakaombwa kushiriki katika mambo hayo mara zote wamekuwa wakiongelea mambo yanayolihusu taifa kama afya, umasikini elimu, umoja wa kitaifa, kutobaguana n.k

Siku hizi serikali imekaa pembeni kana kwamba imetoa ruhusua kwa mwenye dini au dhehebu fulani ni ruksa kutumia mwanya huo kujinufaisha kisiasa.

Ni serikali hiyo hiyo inayohubiri amani imekuwa mstari wa mbele kuachia hali ya uvunjifu wa amani kutamalaki.

Kuwaachia viongozi hao kutumia nafasi zao za kisiasa katika mambo ya kiimani ni jambo la hatari ambal serikali yoyote duniani haiwezi kufumbia macho.

Kiini macho ni pale matatizo yanapotokea, utasikia viongozi wakisema hata wao hawajui chanzo ni nini.
Tena wanasisitiza kutumia silaha za moto kukomesha wahalifu hao. Inashangaza kwasababu kwanini serikali itumie silaha za moto na si kuzia uhalaifu kabla haujatokea?

Kuachia hali za kuchangisha mabilioni huko miskitini na makasnisani ni kutengeneza mazingira ya uvunjifu wa manani na ni ujinga na upuuzi has kwa mtu mwenye dhamana kuamuru kutumika silaha kukomesha hali hiyo.

Huu ndio udhaifu mkubwa sana wa serikali ya JK katika miaka 50. Hatukuyaona haya siku za nyuma na serikali hii inalipeleka taifa mahali pabaya sana.

Serikali imeshindwa kuwakemea viongozi wake au wadini huku kwa unafiki ikisema haina dini.
Kama haina dini kwanini wanasiasa wanapita katika sehemu za dini kueneza siasa zao uchwara?

Duru za siasa zinawatahadharisha wananchi kuwa katika kutafuta muafaka wa kitaifa kwa mambo muhimu kama elimu, afya na umasikini kiongozi hupatikana kwa sifa na si imani.

Hawa wanaonunua uongozi kwa kutumia harambee wanawekeza na pindi wakipewa dhamana watautumia umasikini wa wananchi kurejesha fedha zao.

Ni vema kuwauliza kwani hawajengi shule na vituo vya afya eti ni hadi wapitie misikitini na makanisani?
Huu uumini wa siasa za makanisani na miskitini umeanza lini na una lengo gani.

Ni wakati umefika sasa kuwakemea viongozi wa dini kwa unafiki na kuikemea serikali kwa udhaifu.
Duru za siasa tunalaani hali hiyo kwa nguvu zote, tunawalaani viongozi wa dini na wansiasa wao kwa kutaka kulitumbukiza taifa katika janga kubwa

Tusemezane

Mgeni wa leo Kimweri
 
TUNATAKA MADARAKA NA HESHIMA, HUTUTAKI HESHIMA KUTOKANA NA MADARAKA

Huko nyuma tumesikia wabunge wakitaka kuitwa waheshimiwa na si ndugu, kaka, dada, baba au mama. Walitumia kikao cha bunge kujadili hilo kama tatizo kubwa sana la kitaifa.

Kwamba wao kuitwa waheshimiwa ni kuwatendea haki na wala si wao kuwatendea haki wapiga kura wao kwa kujadili matatizo makubwa yanayofunika taifa kuliko mafanikio.

Kama ilivyokawaida ya historia kujirudia baada ya muda fulani, kituko hicho kimetokea tena wiki hii lakini kwa njia nyingine. Mwanasheria mkuu wa serikali ya Tanzania ameagiza mawakili wa serikali kupigiwa saluti ili kuleta heshima ya dola.

Jaji Werema anaamini kwa dhati ya moyo wake kuwa kupigiwa saluti, heshima ya dola itakuwa imerudi. Ni mwanasheria mkuu!

Moja ya matamko ya TANU ni ile isemayo '......heshima ya mtu itatokana na huduma yake kwa jamii''
Kwamba ni huduma mtu anayotoa ndiyo itamletea heshima kwa jamii na wala si saluti amri au vitisho.

Kwa wakati huu nchi ipo katika kipindi kigumu cha kukandamizwa kwa haki za wananchi, kukiukwa kwa haki za kibindamu na kutofuata utawala wa kisheria achili mbali makando kando mengine.

Tulidhani mwanasheria mkuu atasimama kidete kuhakikisha kuwa haki za rai zinalindwa, utawala wa kisheria unadumishwa na ukuaji wa demokrasia unasimama.

Tofauti na hayo Mwanasheria amekuja na hoja 'nzito' sana ya kupigiwa saluti.
Kwamba saluti zitaweza kumaliza matatizo tuliyoyasema.

Huu ni uzumbukuku na ujinga wa hali ya juu sana. Mwansheria mkuu kutoa kauli hiyo tena kama tamko ni aibu kwake, taasisi anazowakilisha na hata alimyemteua.

Nia aibu ambayo haiwezi kuelezwa kwa kurasa 999 kwa uzito wake.
Ni wakati mzuri wa kulaani aina hii ya viongozi ambao pengine ulevi wa madraka au upeo wao finyu umefikia tamati na hivyo hawaoni kingine kilichobaki kumsaidia mtanzania bali saluti.

Ni upofu huu wa viongozi unaopelekea hali katika hospitali zetu iwe ya kutisha.
Marehemu anapoachwa wodini kwa siku mbili, wagonjwa wanapolala sakafuni kama mbuzi zizini ni matokeo ya kuwa na viongozi aina ya Werema.

Wao wanadhani kuwa wana haki kwenda India na Afrika kusini kutibiwa kwasababu ni waheshimiwa na wanapigiwa saluti na hiyo ndiyo sehemu yao ya huduma kwa jamii.

Nimesikitika kuona hospitali ya taifa ambayo inatakiwa iwe sehemu ya kinga ya maradhi (disease control centre) inakuw kituo cha kusambaza maradhi. Eti wagonjwa wanakwenda hospitali na ndoo za maji kwasababu bomba la maji limekatwa na wajenzi wa barabara.

Mkurugenzi wa Muhimbili haonekani kuguswa na tatizo hilo na ni kama ni kitu cha kawaida tu ilimradi masilahi yake na wenzake wanaomzunguka yanalindwa.

Hivi ujenzi wa barabara unawezaje kufanyika bila wadau kushirikishwa na kuhakikishiwa kuwa huduma hazitaathirika hasa kwa kutambua kuwa Muhimbili ni hospitali ya taifa?

Hivi mradi huo haukuwa na mchakato (analysis) uya kugundua kuwa ujenzi wa barabara utaathiri upatikanaji wa maji na hivyo kuwepo na mbadala wa kupiisha bomba la muda ili kutoathiri huduma?

Majibu yake ni rahisi kuwa hakuna kiongozi aliyekaa chini na kufikiria hilo kwa kujua kuwa yakiwawakuta, kodi za walala hoi zitatumika kuwapeleka India kwa matibabu na hata kama watakuwa Muhimbili basi watakuwa katika vyumba maalumu kule MOI na wala si Sewhaji, Mwaisela au Kibasila.
Ndivyo wanavyotaka sasa wanataka saluti hata wakati wanapanda first class kwenda kutibiwa India.

Ni kwa kuangalia muktadha huo,sisi wananchi tunasehemu muhimu sana ya uzembe huu.
Mwenzetu Mchambuzi alishuhudia tukio la mtu kufariki na kuachwa wodini, wagonjwa kujitafutia mlo kwa kuchaguana kama mabolizi n.k.

Kwa hulka zetu watanzania hilo halionekani kuwashughulisha watu na tumebaki tukijadili mambo yasiyogusa maisha yetu kabisa. Tumeacha kupaza sauti za kuwakemea waheshimiwa na wapenda salauti kana kwamba ni haki yao kututendea hivyo. Tumekubali kugeuzwa watumwa hata baada ya biashara hiyo kukomeshwa karne nyingi zilizopita.

Vipi tungewaita wabunge wa Dar kwa kuanzia na kuwaonyesha kwa macho yao madhila tunayopata? Vipi tungekuwa tumeshika viboko na kuwaambia ima watatue matatizo yetu au tuwapigie saluti halafu tuwacharaze bakora na kuwataka wajiuzulu mara moja?

Vipi tungeiambia serikali izuie pesa za kwenda kuwatibu India au south Africa ili tushirikiane nao katika kualala sakafuni kule Mwaisela na Kibasila? Je, wangeweza kufikiria saluti badala ya huduma za jamii?

Vipi tungemwambia Werema atuambie nani kachukuliwa hatua dhidi ya ufujaji, ubadhirifu na ufisadi nchini? Vipi tungemwambia Werema wale wanaolipua watu kwa mabomu mikutanoni na nyumba za ibada wamechukuliwa hatua gani?

Je, Werema angekuwa na akili ya kufikiria saluti kama tungekuwa tumememsimamia na viboko ijiuzulu au atende anayopaswa kuyafanya kama Mwanasheria?

Kwa vile tuliruhusu wakajiita waheshimiwa sasa wanataka saluti.
Mungu jalia ipo siku wataidhinisha wapewe haki za kuzini na kujamiana na wake zetu.
Na sisi tutakaa kimya kwasababu tunaamini hawa ni manabii walioletwa na mungu kutuhudumia na wanapaswa utukufu na wala si utukufu wa huduma zao kwa jamii.

Ifike wakati Watanzania tuangalie mabali na tufanye maamuzi magumu hata kama wakaofaidika ni vizazi vyetu. Leo tupo huru bila kujua kuna watu walitoa nafsi zao kwa ajili yetu.

Watu hao wanpotuangalia kutoka huko waliko hakuna kinachobaki zaidi ya wao kutikisika kwa hasira kutoka makaburini walikopunzika. Wanatuona kama kizazi cha majuha, wajinga na wapuuzi.

Wao walikabiliana na mkoloni ili kupata heshima ya huduma bora,sisi tunashindwa kukabiliana na kundi hili dogo linaloturudisha katika ukoloni wa salauti na uheshimiwa.

Ni aibu na dhalili wakati umefika tuseme enough is enough.

Tusemezane

Mgeni wa leo Matola
 
Last edited by a moderator:
UNAFIKI WA VIONGOZI WA DINI NA UDHAIFU WA SERIKALI YETU

Miaka ya karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la wanasiasa kutumika katika shughuli za kidini tena wakipewa hadhi kubwa utadhani wao ndio wasomi na manguli katika dini.

Hali hiyo imekuwa mbaya na kuhusisha viongozi wa kisiasa katika harambee za makanisani na misikitini kwa kuwatumia wanasisa.

Aghalabu ni rahisi kusikia mbunge, meya, waziri, katibu mkuu n.k. wakiongoza harambee za mamilioni kuchangia mambo kadha wa kadha katika dini zao.

Viongozi wa kisiasa ni wanadamu ambao kazi yao haimaanishi kuwaondoa katika mambo ya kiroho. Lakini hawa si viongozi wa dini na wala hawapaswi kupewa hadhi katika safu za viti vya mbele.
Wao ni waumini kama walivyo wengine na hiyo ndiyo haki yao.

Kwakutambua kuwa siasa ni mchezo mchafu viongozi hao wanatumia nafasi wanazopewa katika kufikia malengo yao ya kisiasa. Michango yao na jitihada zao si za kiuumini bali zimefungamanishw na matakwa ya kisiasa. Kwamba huko ndiko wanakotaka waungwe mkono kwa kutumia viongozi wa dini

Tunaelewa kuwa viongozi wa dini wana nguvu kubwa sana katika ushawishi wa waumini wao.
Mara zote wamekuwa wanasikilizwa hata kama hoja zao hazifikirishi. Si kiongozi kasema!!!!

Hivi karibuni kuna kiongozi maarufu amekuwa akipita makanisani na misikitini kuchangisha harambee.
Inasemwa kisias alicho changa hadi sasa ni mabilioni ya pesa.

Kiongozi huyo anyehusishwa sana na uchaguzi wa 2015 kupitia chama tawala amejitetea kuwa michango na pesa zake zinatokana na michango ya marafiki zake.

Utetezi huu dhaifu na wa kipuuzi unatupelekea kuamini kuwa kiongoz huyo eti amejivika wadhifa wa kufikisha michango ya waumini wenzake kwa mungu kama yeye na si kama wao.
Kwamba yeye amechukua jukumu la kidini la kuwafikishia michango hiyo.

Hali ni kama hiyo kama tunavyoshuhudia kila siku. Mara utasikia waziri wa imani fulani ameongoza harambee kanisani, mara meya fulani, mara katibu mkuu fulani n.k. Wote hawa hufanya hayo kama sehemu ya mtaji wa kisiasa.

Viongozi wa dini wanafahamu hali hiyo wazi na wanajua kuwa hilo litazaa balaa siku za baadaye na kupekekea uvunjifu wa utangamano wa taifa na imani kwa waumini.

Tumeshuhudia kukiwa na mijdala mikali hadi bungeni ambako wabunge wameasi vyama vyao ili kutetea imani na wala si wananchi waliowapeleka. Tumeona mivutano ya kidini ikiendelea na tumeona vurugu ambazo chanzo chake ni sababu za dini.

Viongozi hawa dini wanaowakaribisha wanasiasa kuwagawa wananchi wanafahamu madhara ya kile wanachokifanya. Wanafahamu kuwa mungu hapendezwi na unafiki wanaoufanya wa kuhubiri amani kwa mlango mmoja na kuchochea uvunjifu wa amani kwa upande mwingine.

Ikifika hapo nadhani wasomaji watakubaliana na duru za siasa kuwa viongozi hawa ni wanafiki kama kichwa cha habari kianvyosema.

SERIKALI DHAIFU
Katika siku za nyuma viongozi walikuwa waumini kama wengine huko misikitini au makanisani walikwenda kama waumini. Kama ilitokea kupewa hadhi basi ni kwa heshima ya nafasi zao na wala si kwasababu ya nyadhifa za kisiasa au ushawishi wa kutaka kuungwa mkono na viongozi wa dini.

Hata ilipotokea viongozi hao wakaombwa kushiriki katika mambo hayo mara zote wamekuwa wakiongelea mambo yanayolihusu taifa kama afya, umasikini elimu, umoja wa kitaifa, kutobaguana n.k

Siku hizi serikali imekaa pembeni kana kwamba imetoa ruhusua kwa mwenye dini au dhehebu fulani ni ruksa kutumia mwanya huo kujinufaisha kisiasa.

Ni serikali hiyo hiyo inayohubiri amani imekuwa mstari wa mbele kuachia hali ya uvunjifu wa amani kutamalaki.

Kuwaachia viongozi hao kutumia nafasi zao za kisiasa katika mambo ya kiimani ni jambo la hatari ambal serikali yoyote duniani haiwezi kufumbia macho.

Kiini macho ni pale matatizo yanapotokea, utasikia viongozi wakisema hata wao hawajui chanzo ni nini.
Tena wanasisitiza kutumia silaha za moto kukomesha wahalifu hao. Inashangaza kwasababu kwanini serikali itumie silaha za moto na si kuzia uhalaifu kabla haujatokea?

Kuachia hali za kuchangisha mabilioni huko miskitini na makasnisani ni kutengeneza mazingira ya uvunjifu wa manani na ni ujinga na upuuzi has kwa mtu mwenye dhamana kuamuru kutumika silaha kukomesha hali hiyo.

Huu ndio udhaifu mkubwa sana wa serikali ya JK katika miaka 50. Hatukuyaona haya siku za nyuma na serikali hii inalipeleka taifa mahali pabaya sana.

Serikali imeshindwa kuwakemea viongozi wake au wadini huku kwa unafiki ikisema haina dini.
Kama haina dini kwanini wanasiasa wanapita katika sehemu za dini kueneza siasa zao uchwara?

Duru za siasa zinawatahadharisha wananchi kuwa katika kutafuta muafaka wa kitaifa kwa mambo muhimu kama elimu, afya na umasikini kiongozi hupatikana kwa sifa na si imani.

Hawa wanaonunua uongozi kwa kutumia harambee wanawekeza na pindi wakipewa dhamana watautumia umasikini wa wananchi kurejesha fedha zao.

Ni vema kuwauliza kwani hawajengi shule na vituo vya afya eti ni hadi wapitie misikitini na makanisani?
Huu uumini wa siasa za makanisani na miskitini umeanza lini na una lengo gani.

Ni wakati umefika sasa kuwakemea viongozi wa dini kwa unafiki na kuikemea serikali kwa udhaifu.
Duru za siasa tunalaani hali hiyo kwa nguvu zote, tunawalaani viongozi wa dini na wansiasa wao kwa kutaka kulitumbukiza taifa katika janga kubwa

Tusemezane

Mgeni wa leo Kimweri

Ndugu Nguruvi, Kuna mwerevu mmoja aliwahi sema maneno yafuatayo.namnukuu, "you can not solve problems using the same level of thinking,when you created them".

Wanachotufanyia viongozi wetu wa dini ni kutuaminisha kuwa kiongozi wakisiasa aliyeshindwa kutatua matatizo ya jamii wakati akiwa madarakani,ataweza kuyatatua kwa kuchangisha michango kupitia kwenye taasisi za dini.Mbaya zaidi haya yanafanyika katika hali isiyo na uwazi,na lugha za ujanja ujanja zikitumika.

Viongozi wetu wa dini nao,wameamua kutu-take for a ride.Halafu waumini wakiacha kuwafuata kwa weledi waliokuwa wanafanya hivyo zamani wanapanda juu ya membari na kulalamika maadili yanamong'onyoka.yataacha vipi kumong'onyoka wakati wewe kama kiongozi wa dini hauna "moral authority".Leo hii makanisani na misikitini ndio kimbilio la wauza unga,kimbilio la wanasiasa wenye kashfa lukuki.Imefika wakati sasa wazee wa makanisa na misikiti hawapewi heshima inayostahili na heshima hiyo wanapewa wenye nacho,kwa kuwa tu ndio wachangiaji wakuu wa hafla za makongamano ya kidini.

Suala lengine ambalo inabidi litazamwe kwa jicho la 3 ni uingiaji wa Taasisi za kidini kwenye shughuli za kibishara zilizopitiliza,sasa hivi hasahasa makanisa,ndio mabepari wakuu wa nchi hii,ndio wanamiliki mapande makubwa zaidi ya ardhi,ndio wamiliki wa shule nyingi za sekondari,ndio wamiliki wa vyuo vingi zaidi ambavyo si vya serikali,ndio wamiliki wakubwa wa kumbi za harusi pamoja na majengo kwenye miji yetu.Katika hali ya kawaida,complexity ya aina hii ya shughuli za taasisi za kidini inazifanya zifikirie kibiashara zaidi,kwani priority zao ziko kwenye kupata faida,kufanya investment na kutunza investment zao,kwa matiki hii tutegemee kuona mapadri na maaskofu wanao-act kama ma-CEO wa makampuni makubwa,kwani wana -vast interest za kutake care of.Dini ile tuliyozoea ya miaka nenda rudi inaelekea kupuuzwa,ukichanganya na uwepo wa serikali dhaifu isiyoweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo si jambo la ajabu viongozi wa dini waki-act kama wanasiasa/wafanyabiashara na watawala vilevile.,kwani serikali inayopaswa kuchora mstari juu ya mipaka ya viongozi wa dini iko bize kufanya harambee za kuchangia visima vya maji ambaavyo wao walishindwa kuvichimba.

hali tuliyokuwa nayo sasa kama taifa ni ushahidi ulio wazi kuliko wa aina yoyote wa "a failed state". nchi ya kusadikika haswaa
 
Nguruvi, Kuna mwerevu mmoja aliwahi sema maneno yafuatayo.namnukuu, "you can not solve problems using the same level of thinking,when you created them".

Wanachotufanyia viongozi wetu wa dini ni kutuaminisha kuwa kiongozi wakisiasa aliyeshindwa kutatua matatizo ya jamii wakati akiwa madarakani,ataweza kuyatatua kwa kuchangisha michango kupitia kwenye taasisi za dini.Mbaya zaidi haya yanafanyika katika hali isiyo na uwazi,na lugha za ujanja ujanja zikitumika.

Viongozi wetu wa dini nao,wameamua kutu-take for a ride.Halafu waumini wakiacha kuwafuata kwa weledi waliokuwa wanafanya hivyo zamani wanapanda juu ya membari na kulalamika maadili yanamong'onyoka.yataacha vipi kumong'onyoka wakati wewe kama kiongozi wa dini hauna "moral authority".

Leo hii makanisani na misikitini ndio kimbilio la wauza unga,kimbilio la wanasiasa wenye kashfa lukuki.
Imefika wakati sasa wazee wa makanisa na misikiti hawapewi heshima inayostahili na heshima hiyo wanapewa wenye nacho,kwa kuwa tu ndio wachangiaji wakuu wa hafla za makongamano ya kidini.

Suala lengine ambalo inabidi litazamwe kwa jicho la 3 ni uingiaji wa Taasisi za kidini kwenye shughuli za kibishara zilizopitiliza,sasa hivi hasahasa makanisa,ndio mabepari wakuu wa nchi hii,ndio wanamiliki mapande makubwa zaidi ya ardhi,ndio wamiliki wa shule nyingi za sekondari,ndio wamiliki wa vyuo vingi zaidi ambavyo si vya serikali,ndio wamiliki wakubwa wa kumbi za harusi pamoja na majengo kwenye miji yetu.Katika hali ya kawaida,complexity ya aina hii ya shughuli za taasisi za kidini inazifanya zifikirie kibiashara zaidi,kwani priority zao ziko kwenye kupata faida,kufanya investment na kutunza investment zao,kwa matiki hii tutegemee kuona mapadri na maaskofu wanao-act kama ma-CEO wa makampuni makubwa,kwani wana -vast interest za kutake care of.Dini ile tuliyozoea ya miaka nenda rudi inaelekea kupuuzwa,ukichanganya na uwepo wa serikali dhaifu isiyoweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo si jambo la ajabu viongozi wa dini waki-act kama wanasiasa/wafanyabiashara na watawala vilevile.,kwani serikali inayopaswa kuchora mstari juu ya mipaka ya viongozi wa dini iko bize kufanya harambee za kuchangia visima vya maji ambaavyo wao walishindwa kuvichimba.

hali tuliyokuwa nayo sasa kama taifa ni ushahidi ulio wazi kuliko wa aina yoyote wa "a failed state". nchi ya kusadikika haswaa
Oh! Kimweri! Shukran ndugu yangu kwa kugusa nafsi zetu.
Naomba nikazie sehemu chache tu za maeneo uliyoyazungumzia zinazoshangaza, stusha na kutia kinyaaa kwa viongozi wa dini ambao mimi nawaona waovu zaidi ya waovu wanowapelekea fedha.

Viongozi wa dini mbele ya madhabahu na membari wakihuburi dhambi za maovu kama wizi, kushiriki kudhulum,ulevi, kusenganya n.k. Wanasema ni haramu kula mali iliyotokana na haramu.

Wakishuka kwenye hizo membari na madhahabu wanapeana mikono na wanasiasa waliokimbilia nyumba za dini baada ya kuiba, kudhulumu, kuhujumu na kufisadi mali za walipa kodi.

Tena viongozi hao wanakubali ichango hiyo na kutoa sala na maombi kwa wezi eti mungu awazidishie zaidi! Mungu awazidishie wazidi kuiba, na kuleta pesa makanisani na misikitini!!!

Hukumu ya moral authority(mmomonyoko wa maadili) imebaki kwa wale wanaova vi min skirt kanisani na wasiovaa hijabu misikitini.

Wauza unga hawamo kwasababu baada ya kuuza unga wao hutoa zaka na matoleo na hujitakasa mbele ya Masheikh na Maaskofu. Kama huu si unafiki ni nini hasa?

Wazee wa makanisa na misikiti wamebaki kusikiliza matatizo ya ndoa tu, linapokuja suala la pesa kuna kamati maalumu zisizowahusisha.
Kamati hizi zinaundwa na ndugu wa wanasiasa, wauza unga na majambazi ili kutengeneza 'Chanel' kwa wazee wako na kuwapa habari nini kinaendelea au kinahitajika.

Umegusia suala la biashara, hili ni tatizo kubwa sana ambalo serikali hii isiyo makini imeliacha tu. Kama kawaida rais JK hutaka kumpendeza kila mtu hata kama kufanya hivyo ni kulivuruga taifa.

Leo taasisi za dini zinaongoza kwa kufanya biashara kuliko kuhubiri dini zao.
Taasisi zipo katika ushindani na private firms, na kibaya zaidi zinapewa msaada na serikali kufanikisha malengo yao ya kibiashara.

Taasisi za dini zimepewa nafasi ya misamaha ya kodi eti zinatoa huduma kwa jamii.
Nenda uone gharama za shule hizo na zile za binafsi. Utashangaa hizo shule za taasisi za dini zinagharama kubwa sana licha ya ukweli kuwa zinapewa misamaha na serikali.

Siku hizi taasisi zimekuwa machaka ya kukwepa kodi. Masheikh na Maaskofu ndio walio mstari wa mbele kuingiza magari na kuyauza baada ya miaka 2 tena kwa thamani kubwa kuliko waliyonunulia kwasababu walipewa misamha ya kodi. Imekuwa ni machaka ya kukimbia kodi halafu wamekamata biblia na misahafu wakizungumzia mtoza kodi wa Jerusalem.

Tayari viongozi wa dini wamekuwa ma CEO, mwaka jana waliungana kwa pamoja na kutunisha misuli serikali iondoe kifungu kinachohusu misamaha ya kodi ili iendelee kubaki wazi.

Nilitarajia wao ndio wangeongoza katika kuonyesha mfano wa maadili ya kulipa kodi hata pale wasipoonekana ili kuonyesha woga wao si kwa mwanadamu bali mungu anayewaona kila kona.

Wenzetu nchi za ulaya na Marekani wameshagundua uchafu huu, taasisi zao kama CAG na zile za kodi zinaingia ndani ya makanisa na miskiti kukagua nyaraka za fedha na uchumi, miradi inayoendelea na ufadhili wake, hakuna huruma wala haya.

Sisi serikali yetu haijui nani anafanya nini, kwa njia gani na sababu zipi.
Imekaa kando eti inatoa uhuru wa kuabudu.

Na wajanja kama majambazi, wauza unga, wakwepa kodi na wanasiasa wameamua kwenda kujificha huko wakikingiwa kifua na maaskofu na masheikh kwasababu tu wanawezesha dini kujenga miradi hata kama ni kwa fedha chafu mbele ya mungu.

Ulaya na Marekani dini zimekufa, makanisa yanafungwa na kuuzwa na vijana wanakumbatia sifa ya kutokuwa na dini kwasababu dini zimeonyesha 'immoral' ya hali ya juu sana na hazina tena moral authority ya kuongelea uovu.

Sijui Afrika kitatokea nini na wala sina sababu za kutaka kujua hilo.
Concern yangu ni kuhusu serikali inayoachia dini ziwe sehemu na kinga za wahalifu.

Kwamba mtu aniibiea kwa 10% akiwa kiongozi au kuruhusu unga uwanja wa ndege uue vijana wetu halafu akimbilie makanisani na misikitini kwenda kutoa sadaka na harambee ili anunue waumini wampigie kura arudi serikali kuendelea kunidhulumu, that's the point I'am sick to my stomach.

Narudia tena udhaifu huu wa serikali ya JK unajenga mazingira ya majanga makubwa mbele ya safari. Hawa viongozi wa siasa wanaotumia pesa za 'cartel' wizi na ufsadi na kusafishwa na viongozi wachafu wa dini hawapaswi kupewa nafasi ya kumhudumia mwanadamu achilia mbali mwananchi.

Lazima tusimame kidete na kuiambia serikali iache unafiki kwa kushirikiana na viongozi wa dini wanafiki kuudanganya umma. Wao ni tatizo la mmomonyoko wa maadili siyo mini skirt au hijabu.

Tuwalaani viongozi wa dini wanaohubiri uwazi, ukweli na upendo huku pembeni wakishirikiana na wanasiasa na wauza unga kuliangamiza taifa.

Wewe unayekwenda msikitini au kanisani na kushindwa kumkemea kiongozi wako kwa kuleta wanasiasa miskitini na makanisani kuchangisha fedha tena ukijua ni haramu na wewe pia ni sehemu ya uhalifu na uharamu na uwepo wako katika nyumba hizo za ibada ni kupoteza muda kwasababu unashirikiana na wahalifu kwa unafiki ukidhani kuwa mungu hakuoni.
Unakuwa sehemu ya uchafu wa serikali dhaifu na imani chafu na za kinafiki za dini siku hizi.

Simama umwambie kiongozi wako unahitaji huduma ya kiroho na si huduma za kisiasa na pesa za wanasiasa na wauza unga.

Mwambie kiongozi wako aache unafiki na mkemee ikiwezekana usiende tena huko kanisani au msikitini na tafuta eneo lingine takatifu umeuombe mola wako.

Ukiwa unashangilia wakati pesa za unga na za wizi wa wanasiasa zinakusanywa wewe ni muovu tu kama kiongozi wako, mwanasiasa wako na muuza unga wako anayekuchangia

Tusemezane
 
MHESHIMIWA RAIS KAMA SI WEWE NI NANI?
WANAOSEMA SERIKALI YAKO NI DHAIFU WANAKUONEA?

Rais hula kiapo cha kuitetea katiba ambayo ndio msingi wa sheria za nchi, kuwalinda watu na mali zao.
Siku zote mkuu wa serikali awe waziri mkuu kwa nchi zingine au rais, huwa na maamuzi yanayogusa maisha ya watu. Maamuzi yake huwa ni sehemu muhimu ya maisha ya wananchi.

Siku za nyuma tumeshuhudia serikali ikichukua maamuzi magumu kwa manufaa ya nchi na wananchi.
Mfano, awamu ya kwanza iliamua kupambana na wahujumu uchumi na walanguzi.

Hututkusikia onyo lolote bali hatua zikichukuliwa. Iwe ilikuwa sahihi au la, jambo moja muhimu ni kuwa hatua zilichukuliwa na serikali.

Awamu ya tatu ilichukua hatua kama ile ya kukabiliana na serikali ya Burundi iliyokuwa inasababisha hali ya usalama katika mikoa ya Kigoma. Serikali ilifanya hivyo bila rais kujua wengine hadi leo.

Awamu ya nne imekuja na mambo yanayoshangaza. Kwanza tulimsikia rais akiwataka walioiba pesa za EPA warudishe kwa hiari yao. Kwamba, walikuwa na hiari na wala si sheria kuchukua mkondo wake.

Tumesikia mambo mengi kama ya rais kusema hajui tatizo la udini chanzo chake ni nini.
Pamoja na kuwa na vyombo vyote vya usalama mkuu wa nchi bado hakupata chanzo cha tatizo.

Yeye kama sisi tumebaki tukilalama huku hali ikizidi kuwa mbaya ikiwa ni pamoja na wanasiasa kushiriki katika shughuli za dini kwa kofia zao bila aibu wala haya. Rais kama sisi, analalamika.

Tukio la kushangaza na kutia wasi wasi ni hili la majuzi. Rais alipodhudhuria sheria za mashuja kule Bunazi, Kagera, alitumia fursa hiyo kufanya ziara wilaya za mkoa huo ambazo zimeathirika sana na ujambazi, migogoro ya ardhi, kuvamiwa na raia wa Kigeni hasa kutoka Rwanda na kuvurugika kwa usalama

Tulimsikia rais akitoa siku kadhaa kwa raia wa Rwanda kwalioingia nchini kwa njia haramu kuondoka na mifugo yao kurejea makwao. Rais alisema hao ni wahamiaji HARAMU kwa kauli yake.

Duru za siasa tunajiuliza, hivi inakuwaje wahamiaji haramu wapewe muda wa kuondoka?
Kwamba,hata kama wamefanya uhalifu wa kupindukia sasa ilikuwa ni wakati wao kurejea makwao (wazungu wanasema get way) bila sheria kuchukua mkondo wake.

Tulidhani kuwa wananchi wa Tanzania hawajui na hawana sababu za kujua operesheni za kijeshi zitafanyika lini na kwa mukusudio gani. Wao wanachokitaka ni kuishi katika hali ya usalama kwa kutegemea utendaji wa vyombo vya usalama. Hatujui ilikuwaje rais kutangaza operesheni wakati huo huo akiwataka wahamiaji haramu waondoke baada ya kufanya uhalifu.

Tunajiuliza kama rais naye ataomba wahamiaji haramu waondoke kama sisi raia, ni nani na kwa njia gani anaweza kupambana nao? Nani miongoni mwetu ana uwezo juu ya vyombo vya dola kuzidi rais? Na je huu si udhaifu unaosemwa wa serikali hii.

Inapofikia mkuu wa nchi na Amir jeshi anaomba wahalifu waondoke bila kuchukuliwa hatua za kisheria nani atasimamia sheria za nchi?

Lakini pia lazima tujiulize wahamiaji hao haramu wameingiaje nchini tukiwa na vyombo vyote vya usalama pamoja na maafisa uhamiaji?

Ni nani mwenye dhamana na uteuzi wa wakuu wa vyombo hivyo kama si rais, na kama vimelegea katika utendaji nani wa kubeba lawama za udhaifu huo kama si serikali anayoiongoza rais?

Ndiyo maana tunauliza, mheshimiwa rais kama si wewe ni nani? na je huu siyo udhaifu wa serikali yako unaosemwa?

Tusemezane

mgeni wa leo HAMY-D
 
Mkuu Nguruvi3 huyu amejikita kumjadili Dr W.Slaa nadhani atapata taabu sana ukimwondoa katika uwanja wake wa kujidai tumsubiri labda anaweza kuja na kitu tofauti kidogo.

Ni mgeni wetu ambaye anaweza kutusaidia kwa undani nini mwenyekiti anafikiria.
Tunataka kusikia kutoka kila sehemu zina maoni gani.
 
TUKIO LA MOROGORO (SHEIKH PONDA)

Habari zilizopo katika vyombo vya habari ni kuhusu kushambuliwa kwa sheikh Ponda huko Morogoro wakati wa kongamano la Idd. Sheikh,ambaye mara nyingi amezua mitafaruku amelazwa hospitali.

Tayari watu binafasi na taasisi zimeitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya Polisi waliohusika.
Wakati huo huo Polisi wamekuwa wakitoa kauli za utata zisizoeleweka kama ilivyo kawaida yao.

Hakuna anayeweza kuamini taarifa ya jeshi la polisi la Tanzania kwasababu jeshi hilo limeacha majukumu yake ya kisheria na kuwa tawi la chama au sehemu ya serikali.
Jeshi la polisi ni chombo cha dola cha kulinda raia na mali zao na kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

Tatizo lililopo katika jeshi letu ni kupoteza nguvu za kufikiri katika kupambana na uhalifu.
Mbinu wanazotumia za kubadili kauli au kubambikia watu makosa ni ni mbinu hafifu na dhalili sana.

Kutokana na udhaifu huo wa jeshi kesi nyingi zimetupwa mahakamani na wahalifu kuachiwa huru.
Sheikh Ponda aliyekuwa anatumikia kifungo cha nje, jeshi limeshindwa kumkamata kwa matamshi yake hatarishi.

Sheikh Ponda ana nguvu tusioijua katika nchi hii. Si mara moja au mbili amekuwa katika mitafaruku ambayo yeye ni sehemu ya uchochezi.

Hata pale penye ushahidi bado amekuwa anakwepa viunzi. Mathalan, hivi karibuni alikuwa na kesi ya uchochezi wa kiwanja cha Chang'ombe lakini ameishia kuhukumiwa kifungo laini kabisa kama mtu aliyepigana baa na mwenzake.

Sheikh Ponda inasemwa ni raia wa nchi jirani ambaye si rahisi kujua anasimamia nini hasa.
Yeye ni mwenyekiti wa kamati ya kutetea mali za waislam, na sasa amechukua jukumu la kisiasa la kuchochea mambo ya udini akishirikiana na wenzake.

Hata hivyo Ponda anabaki kuwa hana hatia hadi pale atakapothibitishwa na vyombo vya sheria kuwa ana hatia kama ilivyotokea hivi karibuni. Ni wajibu wa serikali na jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria ili ajibu tuhuma zinazomkabili bila kumdhuru.

Tunakumbu kumbu ya Dr Ulimboka, Kibanda, Mwangosi, mabomu Arusha n.k. ambayo serikali haijayatolea majibu.

La Dr Uliomboka aliyetaja hata washiriki linatoa picha isiyo na shaka kuwa njia hii ya kudhuru wananchi inaratibiwa na vyombo vya usalama. Haiwezekani mwendesha mashtaka wa serikali DPP aseme Ulimboka hakutoa ushirikiano wakati afisa aliyehusika yupo na wala hajachukuliwa hatua zozote.

Ni vigumu sana kuamini kuwa Ponda alishambuliwa na mtu mwingine kama si Polisi kwasababu historia ya jeshi la Polisi kuhusiana na matukio ya aina hii inatoa ushahidi usio na shaka kuwa ni Polisi unless aje mtu na ushahidi mwingine,kazi ambayo ni ngumu sana kuifanya katika ukweli ulio wazi wa historia

Kitu cha muhimu katika bandiko hili ni kuwaeleza wananchi kuwa jeshi a Polisi na Serikali vimechukua udhaifu wetu (take for granted) wakijua hakuna mwananchi atakayechukua hatua.
wameendelea na mauaji au mateso bila wasi wasi wakifahamu wananchi wamegawanyika.

Lilipotokea tukio la marehemu Mwangosi, Dr Ulimboka, Absolon Kibanda, bomu la Chadema Arusha, umwagiwaji wa tindikali kwa watu n.k. wananchi walidhani kuwa hayo ni matukio yasiyowahusu.

Kwa mfano CUF walisema bungeni kuwa Chadema ni wahalifu tena wakiomba serikali iwape nafasi ya chama rasmi cha upinzani. CUF haikufikiri hata siku moja kuwa mchezo huu mchafu unaweza kuingia hadi chumbani kwa mtu binafsi. Haikujua kuwa tunahitaji nguvu ya pamoja kukabiliana nao.

Leo mwenyekiti wa CUF na naibu katibu mkuu wametoa matamko ya kutaka ziundwe tume za uchunguzi. Huu ni upuuzi wa hali ya juu!

wamesahau miezi miwili iliyopita waliunga mkono Chadema kupigwa mabomu tena bungeni.
Hawakudai kuundwa tume na hata CDM walipoomba tume ya kimahakama iundwe si CUF wala taasisi za dini zilizoona jambo muhimu.

Leo kila mmoja ana hamaki kana kwamba ni tukio baya.
Hili la Ponda si tukio baya kabisa ukilinganisha na la Kibanda, Mwangosi, Ulimboka na raia waliouawa Arusha. Hakuna haja ya kulalamika kwasababu kwa muda wote hatukulalamika, leo kipi cha ajabu?

Duru za matukio tunawaasa wananchi kuacha kucheza michezo ya kisiasa katika mambo yanayohusu maisha yetu. Jambo linalotugusa sote lazima tusimame pamoja kama taifa na kulikemea tena tukiweka shinikizo ili hatua zichukuliwe wala si kungoja mtu mmoja akipigwa na jiwe tuhamaki.

Ni funzo zuri sana kuwa kama hatutasimama pamoja tutaendelea kupopolewa kwa risasa kwasababu hawajali na wala hawana hofu ya kufanya hivyo. Wanajua sisi ni mazezeta, yatapita na upepo.

Tusemezane

Mgeni wa leo Remote
 
MASHAMBULIO YA TINDIKALI , MADHARA NA MATOKEO YAKE KIUCHUMI

Kumekuwepo na wimbi la umwagiwaji wa tindikali kwa raia wa nchi yetu. Matukio haya yanayolenga kuumiza yametokea Zanzibar na Tanzania bara yakihusisha viongozi wa dini, wafanyabiashara,wanasias na raia wa kawaida. Hata kama ni tone la tindikali haliondoi ukweli kuwa matukio ya haya ya mtindo wa uhalifu 'kigaidi' yameikumba Zanzibar zaidi.

Leo nikiangalia CNN nimeona taarifa ya waingereza waliomwagiwa tindikali ikitolewa na wao kueleza kilichowasibu. Mmoja wa waliojerhiwa amesema aliyemwagia alionekana kutabasamu baada ya tukio.

Ikumbukwe kuwa gaidi wa shambulio la ubalozi wa Marekani Dar Mohamed Ghailan ni mzawa wa Zanzibar, mauaji ya padre yametokea zanzibar, sheikh kumwagiwa tindikali ni zanzibar na padre mwingine kunusurika kifo ni huko huko zanzibar.

Tofauti na zanzibar mashambulio ya sehemu nyingine yanaonekana kama uhalifu,ya zanzibar yanabeba sura ya udini. Huu ni ukweli, na duru za siasa tunaubainisha hata kama tunakinzana.

Kuuawa kwa padre hukukuwa na sababu nyingine zaidi ya kuhusishwa na imani yake kwa kuzingatia uchochezi na chuki dhidi ya Nyerere imefungamanishwa na imani yake ya kwa njia ya mapinduzi.

Waingereza waliomwagiwa tindikali tukio limetolea ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani jambo ambalo si rahisi unless kuna upotoshaji wa dini kwa kutumia kauli ya thawabu . Tumeshuhudia
maeneo yenye vita au vurugu yakionyesha uvumilivu kwa wakati huo.

Shambulizi za tindikali kwa sheikh, mzawa na kiongozi linafungamanishwa na tofauti za kimtazamo kuhusu dini na siasa pia. Mtiririko wa matukio ni mwingi na haya ni kwa uchache tu wa mifano

Ukiyaangalia matukio ya akina Ghailan (ubalozi), vurugu za mwaka 2001 zilizotoa wakimbizi, na haya yanayoendelea hakuna shaka Tanzania inakuwa katika international spot.
Hata hivyo zanzibar kama sehemu ya historia muhimu na kituo cha utalii inabaki kutajwa kama zanzibar na si Tanzania kama ilivyoonekana leo CNN.

Uchumi wa zanzibar unategemea sekta ya utalii na watalii wengi hutoka magharibi kuliko mashariki. Watu kutoka mashariki ya kati au mashariki wengi wao ni wafanyabiashara

Matukio haya kuzunguzwa vyombo vya habari si jambo jema kwa zanzibar. Ipo athari katika sekta ya utalii zanzibar, jambo litakaloathiri pia maisha ya watu wa kawaida

Aghalabu kutatokea madai ya muungano kuzorotesha utalii tukijua wazanzibar ni wazuri wa kutunga habari na wabovu wa kutafuta chanzo.

Zanzibar haiwezi kusimama yenyewe kiuchumi duniani,inahitaji kufungamana na dunia yenye watu na tamaduni tofauti. Huko Dubai, Saudia Arabia, Misri n.k. wanategemea mashirikiano na nchi nyingine ni ujinga kudhani kuwa zanzibar itaweza kufanya tofauti na wengine.

Ni upuuzi kuamnini kuwa Imani na Amani vinaweza kuwepo katika mazingira yanayojengwa Zanzibar.
Kuna ushahidi usio na shaka kuwa utulivu ni chachu nzuri ya utangamano wa jamii na ustawi kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Wazanzibar wanapasw kujiuliza endapo wanapenda kuishi kwa mujibu wa tamaduni, mila na imani zao iweje basi wao kwa maelfu wawe wamejaa nchi za mgharibi kule wasikokubali utamaduni wao?

Lakini pia tusisahau athari za yanayotokea znz yanaikumba Tanzania kwa ujumla.
Tunakumbuka meli zilizosajiliwa znz na kufanya biashara na Iran yenye vikwazo ni Tanzania ndiyo ilikuwa katika spot. Ndivyo ambavyo ubalozi wa Tanzania unawajibika kueleza nini kimetokea kwa raia wa Uingereza.

Mbele ya safari huenda kila mmoja akabeba mzigo wake, lakini kwasasa huu ni mzigo ambao tumeweka bega na lazima tuungalie kwa jicho pevu.

Tusemezane

TATIZO LA UHAMIAJI HARAMU

SEHEMU YA KWANZA

Wiki hii imegubikwa na mjadala kuhusu kurudishwa kwa wahamiaji haramu wa nchi za jirani kufuatia tanganzo la rais JK alilowapa siku 14 kuhakikisha wameondoka wenyewe kabla ya nguvu ya dola haijaingilia kati.

Tatizo la uhamiaji haramu ni la kimataifa na hakuna taifa dunia lisilokabiliana na hali hiyo. Mipaka ya nchi imewekwa na wanadamu na hakuna kizuizi cha kuzuia wahamiaji. Hata nchi kama Marekani iliyojenga ukuta kwa maelfu ya kilometa bado ina tatizo kubwa.

Kuna taratibu za uhamiaji zinaroruhusu mwanadamu kutambuliwa na kuishi sehemu nyingine nje ya dunia aliyozaliwa.
Zipo taratibu za kupata uraia (citizenship) na ile ya ukaazi wa kudumu (permanent resident), ya muda (temporary resident) na utembeleaji (visa), masomo (studies), ukimbizi (refugees status) na nyingine nyingi kutokana na mikataba kati ya nchi na nchi.

Katika hizo uraia huwa ni hatua ya mwisho kwa mtu ambaye amefuata tartibu zingine zilizotajwa.hapo juu.
Ukiwa na haki ya ukaazi wa kudumu (permanent resdient) mtu hupewa haki sawa na raia pengine pungufu ya zile za kisiasa kama kugombea au kupiga kura ingawa sehemu nyingine huweza kufikiriwa.

Kuna sheria za uhamiaji zinazotofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Zipo nchi zinaruhusu kuoa au kuolewa na kupata uraia, zipo zinazolazimu mwombaji apewe hadhi ya ukaazi wa kudumu kwanza kabla ya uraia na nyingine haziruhusu chochote.

Zipo nchi zinaruhusu mtoto anayezaliwa kuwa raia wa nchi hiyo bila kujali uraia wa wazazi na zipo zinakataa kutoa Uraia.
Kuna program nyingi zinazofanyika katika nchi za dunia ili kupata wahamiaji kwa minajili ya shughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii zao.

Marekani ina mpango unaojulikana kama rottery na kila mwaka inachukua malaki ya watu wanaotaka kwenda kuishi huko na kupewa hadhi ya ukaazi wa kudumu. Pia ina utaratibu wa kuchukua wakimbizi kama ilivyotokea kwa raia wa Burundi, Rwanda na Somalia.

Nchi za Canada na Australia pia zina program za aina hiyo. Nchi hizo mara nyingi huwa na maeneo makubwa na zinahitaji watu (population) kukidhi haja za kijamii na kiuchumi. Hata nchi ndogo kama Norway, uswiss na Sweden nazo zinatoa huduma hizo kwa misingi ya ubinadamu(refugees).

Nchi za ulaya zimeelemewa na mzigo na nyingi zimesitisha program zao.Mataifa haya yamefikia hatua za kuweka sheria za kubana wahamiaji haramu kama kuzuia kwa njia za visa, kupunguza idadi ya wanafunzi n.k.
Uingereza hivi karibuni imetangaza kuwa mtoto anayezaliwa wazazi wake wakiwa si waingereza basi hapewi uraia wa nchi hiyo.
Imeweka taratibu ngumu za visa za masomo na muda wa kufanya kazi kama njia ya ku-discourage wahamiaji halali na haramu

Marekani nayo inapendekeza hatua kama hizo huku sweden na Norway zikibana idadi ya watoto wa kuzaliwa kwa wahamiaji kutokana na wengi kuwa mzigo katika kuendesha shughuli za kijamii.

Nchi za mashariki nyingi hazitoi uraia au ukaazi wa kudumu. Ni ngumu sana kupata uraia wa India kama siyo Mhindi, vivyo hivyo Saudia Arabia na kwingineko.

Pamoja na hatua hizo za uhamiaji halali bado mataifa makubwa yanapambana na wimbi la wahamiaji haramu.
Marekani ipo katika mjadala mzito sana wa namna ya kukabiliana na wahamiaji haramu kutoka nchi za Latino Amrica kama Mexico n.k.

Mtu atauliza swali moja, endapo nchi hizi zina program za kukaribisha watu na kuwapa hadhi za ukaazi wa kudumu na mwisho uraia kwanini basi zisikubali wahamiaji haramu ambao tayari wapo ndani ya nchi hizo?

Jibu la swahili si rahisi kwasababu kuna mambo mengi yanaangaliwa na sababu za kuwa na program hizo.
Tuangalie mifano michache katika uhalisia.

1. Usalama :
(a)Nchi zinazochukua watu hufanya uchunguzi wa kubaini aina ya watu wanaotarajiwa kuhamia huko, rekodi zao za uhalifu, ugaidi, umri wao na matarajio ya matiafa hayo kutoka kwa wageni.

Kwa msingi huo rais Obama wa Marekani anasema ni vema kuwapa wahamiaji haramu vitambulisho wajulikane ili serikali iweze kupanga mipango kulingana na idadi ya watu lakini pia kujua ni akina nani waliopo na wapo wapi hasa nyakati hizi za ugaidi.

(b)Wapo wahamiaji wanaotoka maeneo yenye vita, mara nyingi huingia na silaha na kuwa chanzo cha uhalifu hasa kwa kuzingatia kuwa uwepo wao haujulikani.

(c)Gharama za ulinzi na usalama hutegemea idadi ya wakaazi. Uwepo wa wahamiaji haramu hupunguza ufanisi kwasababu rasilimali zinaotolewa hazilingani na idadi ya watu, wengi wakiwa wamejificha na hutokea wakati ikibidi.

2. Huduma za Jamii
(a) Afya: Wahamiaji haramu wamekuwa mzigo katika kutoa huduma za afya. Kwa vile wengi hawajulikani uwepo wao tatizo la rasilimali linabaki pale pale kwamba zinaelekezwa mahali pasipolingana na idadi ya wakaazi. Mathalani, hakuna taifa litakaloacha watu wafe kwasababu tu si raia au wakazi. Hata Marekani ambapo ubepari umeshamiri bado suala hilo limebaki kuwa la maadili 'moral authority'.
Matokeo ni kujazana watu katika mahospitali, upungufu wa madaktari na huduma zingine za kawaida.

(b)Elimu, suala hili linalingana na la afya. Tofauti kidogo ni kuwa wahamiaji haramu wanaweza kutumia rasilimali za elimu na kubana nafasi za wazawa au wakaazi wa kudumu. Lakini pia kuna tatizo la kuwa na jamii ya wajinga kwavile wahamiaji haramu wanaweza kutopeleka watoto wao shule kwa kuogopa au kubanwa na tartibu za eneo husika.

3.Mipango ya maendeleo ya jamii hutegemea mipango na moja ya vigezo vinavyotumika ni kuangalia idadi ya watu na huduma wanazohitaji ikiwa ni pamoja na kodi zao katika jamii. Wahamiaji haramu wamekuwa tatizo kwasababu nchi hushindwa kupanga maendeleo yake kulingana na idadi ya watu kwa vile hawajulini walipo

4. Kiuchumi: Mara nyingi wahamiaji haramu hufanya shughuli zao chini ya meza (under the table) kwa malipo hafifu kwa mategemeo kuwa nao hawatadai kingine zaidi ya ujira. Kutokana na hali hiyo waajiri wamekwpa kodi na malipo mengine kwasababu wahamiaji haramu hawakuandikishwa na wala hawajulikani uwepo wao.

Kwa kuangalia mifano hiyo mchache tunaweza kuona tofauti iliyopo kati ya makundi yaliyotajwa ya wahamiaji na kundi la wahamiaji haramu. Jambo la kuzingatia ni kuwa unapokuwa na wahamiaji haramu unakuwa 'una deal na uknown' kwamba hujui nani yupo wapi anahitaji nini au anachangia nini. Serikali haijui nani ni salama nani ni hatari, lakini linapotokea la kutokea serikali husika hubeba mzigo kwa asilimia 100.

Tutaendele sehemu ya pili kuangalia
Mtafaruku uliozuka kuhusu Rwanda
kwanini Tanzania inahitaji kuwaondoa wahamiaji haramu
Ni zipi haki za wahamiaji hao zinazobaki au kuhamishika
Kuna madhara gani kama wataendelea kuachwa
Haki zipi za watoto, wake au waume wa wahamiaji haramu
Tuna mikataba gani au mashirikiano yapi na majirani zetu

pamoja na mengine yatakayojitokeza katika mjadala

Tusemezane

mgeni wa leo Mikael P Aweda
 
Back
Top Bottom