EACJ: Vyama vya Upinzani vyashinda kesi dhidi ya Tanzania, kuhusu mabadiliko ya Sheria za Vyama vya Siasa

EACJ: Vyama vya Upinzani vyashinda kesi dhidi ya Tanzania, kuhusu mabadiliko ya Sheria za Vyama vya Siasa

Ila serikali yetu inaweza isifuate hayo maelekezo

Shida ipo hapo. Hiyo mahakama haina nguvu ya ku enforce.

Maana hata mtikila alishinda kesi ya mgombea binafsi ila mpaka leo hakuna mabadiliko.
 
Hii Chadema si mchezo , nimekutana na Mzee mmoja Mnyakyusa ananifahamu akaniuliza , hivi nyinyi Chadema mbona mnatulaza na viatu , mbona hamchoki ?

Mimi nikamjibu kwa kifupi tu , KATIBA MPYA .
Katiba mpya itawalaza usingizi murua sana, tatizo la haya makenge ya kijani mpaka yatoe damu ndio yataelewa SOMO.
 
‪ Mahakama ya haki ya Afrika ya mashariki (The East African Court of Justice - EACJ) katika shauri namba 3 la mwaka 2020 lililofunguliwa na Freeman Mbowe na wenzake watatu dhidi ya mwanasheria mkuu wa Tanzania, imetoa hukumu yake leo, 25/3/2022,

Katika shauri hilo, Freeman Mbowe na wenzake walikuwa wanalalamika kuhusu ukiukwaji wa mkataba wa Afrika Mashariki, ukikukwaji wa masharti ya utawala bora, na haki za binadamu ambayo mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa 2019 inaonekana kukiuka.

Mahakama ya EACJ imetoa hukumu kwamba Mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 2019 (the Political Parties Amendments Act 2019) yanakiuka mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika ya Afrika Mashariki (EAC) sehemu ya 6(9)(72),

Hivyo mahakama ya hiyo ya EACJ imeamuaru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurekebisha sheria ya vyama vya siasa haraka iwezekanavyo ili iendane na mkataba wa uanzishwaji jumuiya ya Afrika ya mashariki.

Pia, mahakama hiyo ya EACJ imeamuru gharama za kesi kwa kila mleta maombi kulipwa na serikali. Freeman Mbowe na wenzake katika shauri hilo waliwakilishwa kisheria na mawakili John Mallya, Jebra Kambole na Sheki Mfinanga.

#MMM‬
 
Ni jambo jema.

Lakini kushinda kesi ni jambo moja na kutekeleza hukumu ni jambo lingine!
 
Back
Top Bottom