Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Tuwaulize nyie wapiga zumari wa chakubanga mlio kuwa mnamtukana leo hii sura zenu mtaziweka wapi?
Mkuu Rais wa mioyo yenu karudi kule alikotokaga...!

Nawaza tuu kama ni msafi bado au keshakuwa fisadi..? [emoji3][emoji3][emoji3]

In God we Trust
 
Hatimae safari ya matumaini imefika kikomo.
Hakika ni jambo jema la kujivunia katika siasa za nchi yetu.
Hongera,Comred Edward Lowassa.
 
Kuna mambo matatu:

1. Karudi kweli kweli kwa moyo wake wa dhati baada ya kuona chadema wanazingua, na hawana muelekeo

2.Ameona age inaenda, so angependa siku akifa azikwe kwa heshima zote sio kama Kingunge

3. Amekuja kwa issue maalumu ya kuivuruga ccm kwa next general election ya 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k



View attachment 1035375

View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums

Arejee asirejee it doesn't help the economy - shilingi inaendelea kufa kifo cha mende against dollar!
 
WALE WA ULIPO TUPO MNA HALI GANI JAMANI[emoji23][emoji23][emoji23] siasa hizi
 
Kama ilivyo kawaida, endapo atajitokezza kiumbe kumkashfu au KUMSEMA vibaya Lowasa Basi ajiandae kupambana na jeshi la polisi.

Awali maneno yake yalikuwa ya uchochezi ila leo Mhe. Dingilai kasema amefutiwa dhambi zake na amekuwa mpya.

Usimtamkie mabaya mzee wetu, Msukuma yule jamaa yako uliyemtusi amerudi kwao Sasa jiandae kumfanya rafiki ukigoma acha chama.

Nape mzee karudi so jiandae kumsujudia,

Makonda jiandae kumsalimia kwa heshima mzee baba la sivyo utapoteza ukuu wa mkoa.

Ridhiwan baba karudi, ulimkejeli Sasa amerejea jamvini

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu,maisha yataendelea kama kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wana wivu jamani! Yani wameona msiba wa Ruge umetikisa nchi wamenuna. Wanaogopa isijekuwa “Msiba wa Ruge ulikuwa mkubwa kuliko huu”

Hata hivyo nimejifunza, nilimpenda na kumuamini sana Lowassa nikasahau ni mwanasiasa tu ambaye maslahi yake binafsi ndio kipaumbele chake kikuu.

Sitaki kuwa shabiki wa mtu tena, nitafanya siasa huru pasi na kumuamini yeyote.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Dada nimekumiss lakini...!

Tutoe mioyo kwa wanasiasa.!
 
Mtu mzima kuonekana unayumba kiimani na msimamo ni changamoto ambayo inaweza kuzorotesha heshima yako kwa jamii.
Mh. Lowasa, Edward N. alikuwa mwachama wa CCM tangu enzi zake za uchipukizi mpaka kufikia kupata nafasi mbalimbali za kiutawala kama uwaziri na hata kuwa Waziri mkuu wa JMT. Mimi na wengine wetu wengi nahisi tuliungana katika ndoto mkakati za kimaisha za kutaka kuwa kama Lowasa siku moja maishani,
Kumuona Lowasa akienda upinzania kulinifanya nitafakari ziko wapi zile nasaha za hekima za wazee ambazo tumekuwa tukifunzwa? Niliweza hata kujiuliza ikiwa mheshimiwa huyu atafanya hivi vipi kuhusu vijana wanaochipukia si ndio chanzo cha kuwa na kizazi malaya cha siasa?
Kuamua kwake kurudi nyumbani kwake (CCM) kumenifanya niuone ukomavu wa hekima, utashi na hata busara za mzee huyu. Ni vigumu kwa yeye kusema anarudi kuunga mkono juhudi za Mh. Raisi bali cha msingi ni kwamba anarudi nyumbani kuendelea kukijenga chama cha mapinduzi hasa kwa kuwajenga vijana wa leo wafanane nao wa kizazi cha 'CCM imara' ambacho kilikuwa nyota kwa wote walikuwa ndani na nje ya CCM.
Kutokana na nafasi zake alizoshika kiserikali ameonelea umuhimu wa kushikamana na wale aliowaachia nafasi ili waweze kutimiza malengo yaliyowekwa kijamii kwani uongozi sio mwanzo wa kila kitu.
Nimpongeze pia Mh. Lowasa kwa kuweza kuwaonyesha kuwa binadamu huweza kubabaika kunakotokana na kutokuridhika ama kutotosheka ambako kunawez kumfanya binadamu huyo kuweza hata kukengeuka na kupoteza mwelekeo japo pia anakuwa na nafasi ya kujisahihisha endapo hatochelewa.
Hongera sana Mheshimiwa Edward N. Lowasa
Hongera sana Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.
Hongera sana Tanzania
 

Attachments

  • 1200px-Flag_of_Tanzania.svg.png
    1200px-Flag_of_Tanzania.svg.png
    5.1 KB · Views: 18
  • 52893188_2045096802192764_2698043531305418752_n.jpg
    52893188_2045096802192764_2698043531305418752_n.jpg
    43 KB · Views: 18
Leo nitakesha kwenye bar kwa furaha ya Lowassa kuondoka cdm. Alaaniwe Mbowe na genge lake kupokea hela ya Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais.
Nimekuwa nikifuatilia comments humu nimekuwa nikiamini ww ni MTU makini ila huu ujinga uliondikwa na hii account hufanani nao labda kama kijana wako ndio kaandika ....hebu tuthibitishie Hela aliyochukua Mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wana wivu jamani! Yani wameona msiba wa Ruge umetikisa nchi wamenuna. Wanaogopa isijekuwa “Msiba wa Ruge ulikuwa mkubwa kuliko huu”

Hata hivyo nimejifunza, nilimpenda na kumuamini sana Lowassa nikasahau ni mwanasiasa tu ambaye maslahi yake binafsi ndio kipaumbele chake kikuu.

Sitaki kuwa shabiki wa mtu tena, nitafanya siasa huru pasi na kumuamini yeyote.


Sent from my iPhone using JamiiForums
CCM imekushikisha adabu Ngoma ya watoto haidumu tuliwaambia mkatutukana . CCM chama kikongwe nyie vitoto tu vicheza Ngoma isiyokesha
 
#NUKUU "Hatuwezi kugombana na kuchukiana kwasababu ya Kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa hivyo, sisi ni Watanzania Kwanza.Lakini binafsi bado naamini Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM", - Edward Lowassa #NipasheMwangaWaJamii Nipashe Tanzania on Twitter
 
Shetani hajawahi kuongoka. Sasa timu ya wenyewe huko ccm imekamilika. 1. EDWARD LOWASA 2.ROSTAM AZIZI na 3 ANDREW CHENGE. ccm mbele kwa mbele wizi ni mila yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom