Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Huu uzi umeanzishwa saa kumi na moja jioni sasa hivi una repplies zaidi ya 850.kesho full day watu wengi wapo sijui utafika wapi.
Maskini Ruge katupwa kapuni.
 
Hapo kwenye kampuni hewa ya korosho 'kutoka Kenya' nazidi kukazia. Bongo lala Bongo nyoso.
Kagoda, Richmond nyingine inanukia ooh nimesahau kampuni ya korosho toka kenya
 
jiwe anamwisho mmbaya sana mbinu anazotumia.

mambo anayofanya hayana tija kwa taifa.

uchumi unakufa yeye anahangaika na hama hama.
 


Mimi binafsi sitadiriki kumlaumu Mzee Lowassa kwa uamuzi aliochukua. Kufanya siasa katika mazingira ya awamu hii iliyojaa "Hostility" na kwa umri wake ni ngumu sana.

Wapenzi na wanachama wa Chadema wanatakiwa wamshukuru Mzee Lowassa kwa kukiwezesha chama chao kupata madiwani wengi na wabunge ijapokuwa baadaye wale waliomfuata walirudi walikotoka.

Jambo lingine ambalo namsifu mzee Lowassa ni hekima na busara iliyotukuka ya kuvumilia kejeli na masimango ya CCM. Mwenyezi Mungu amemlipia hapa hapa duniani kwa kuwaabisha wabaya wake waliokuwa wanamwita fisadi; leo wamempokea kwa nderemo na vifijo akiwemo kubwa la maadui!

Ombi langu kwa vijana wa Chadema tuendelee kumpa heshima mzee wetu. Tusitoe maneno ya kejeli wala kashfa kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamua kutufungua macho kuwa kwa mwanasiasa kuitwa fisadi au msaliti au kibaraka wa mabeberu ni msemo wa kupita na unaweza ukabadilika muda wowote.
 
Achunguzwe tuhuma za Richmond
 
Watajipangaje na wakati wako jela,itabidi wawe majasiri kama late mzee Mandela.yaan upinzani unakufa,na uchaguzi serikali za mitaa hampati hata kiti kimoja,kwenye ubunge 2020 mkivusha wabunge watatu tu, mshukuru sana.
 
WANASIASA WOTE WATASEMA LOWASA SI FISADI NA MWANASIASA BORA WA KARNE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…