Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Kwa haraka haraka unaweza Dhabi yamefanywa au kuamuliwa na mtu mmoja.
 
Aende, tunamshukuru kwa kututengenezea upepo wa kimbunga ulio wazoa akina mwanry, anna kilango, Arfi wa mpanda, madabida, Idd Azan, yule mama wa kibamba aliyewahi kuwa naibu waziri, zungu aliponea chupuchupu kupeperushwa na huo upepo
 
The best option was to retire with honour from politics instead of going back . shame
Hizo akili hawezi kuwa nazo. Huyo ndio kioo cha/mfano wa siasa za kibongo na ambazo zinarithishwa kwa kizazi kipya cha uvccm. Tutahitaji miaka mingine 100 jamii hii (simaanishi nchi) kujikomboa kifikira.
 
Aruhusu siasa sasa aone hiyo njia nyeupe ikoje. Alimchukua Dr. Slaa na njia haikua nyeupe, huyo Lowassa njia itakuwaje nyeupe?
 
I respect Kingunge, hakutaka kula matapishi. Alipokuwa kalazwa Magufuli alimlazimisha awe ccm lakini jamaa alikomaa mpaka kaenda kaburini.
CCM wanaogopa na huyu asije akawafia akiwa chadema.
 
Baada tu ya uchaguzi CHADEMA ilimpa Regina Lowassa nafasi ya Ubunge wa viti Maalumu. Yeye alikataa.

Sina chama chochote, lakini pale mimi akili linicheza na kilichotokea jana kwangu ilikuwa ni suala la muda tu, tena wamechelewa kweli.
 
1551483338336.jpeg

Hawa walioko kwenye picha ni watu makini sana katika siasa za Tanzania. Picha hii inaonekana wakati tumebakiza takriban mwaka mmoja na nusu kuingia kwenye uchaguzi mkuu.

Jana balozi wa Uingereza alitoa neno kuhusu kufungiwa kwa gazeti la The Citizen. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza aliongezea kuwa katika mkutano wa waandishi wa habari utakaofanyika Canada wataliongelea swala la uhuru wa habari Tanzania.

Wakati huohuo Tundu Lissu ameieleza duniawkuhusu shambulio lake la kupigwa risasi 38 akiwa katika mapumziko ya mchana bungeni. Alieleza piawjukosekana kwa ulinzi wakati wa shambulio, kunyimwa stahiki yake ya matibabu, na ku pia kusimamishiwa mshahara wake wa ubunge. Na aliekeza waziwazi nia yake ya kugombea u raisi 2020 kwa tiketi ya CHADEMA.

Kule kusini kwa yakiyotokea baada ya sakata la korosho. CCM inahitaji nguvu ya ziada kupata kura.

Ninavyoona rais amaeamua kuunganisha hekima za watu makini katika kukabiliana na changamoto za sasa kuelekea uchaguzi 2020.
 
Dr slaa naona Leo anacheka kweli asset au liability majibu yameonekana Leo .
Kwa ukumbusho tu...

Dr. Slaa alihamia Chadema akitokea CCM baada ya jina lake kukatwa kwa namna ile ile Lowassa alivyohamia Chadema kutoka CCM baada ya jina lake kukatwa.

Dr. Slaa baada ya kukaribishwa Chadema alipewa fursa ya kugombea nafasi ile ile aliyoikosa CCM na hivyo hivyo Lowassa naye baada ya kukaribishwa Chadema alipewa fursa ya kugombea nafasi ile ile aliyoikosa CCM.

Tofauti ni kwamba Dr. Slaa alishinda uchaguzi lakini Lowassa alinyimwa ushindi. Naomba tu tuweke kumbukumbu sahihi...wote wawili waliikuta Chadema ikawasetiri na hakuna ajabu wakiamua kwa nyakati tofauti kurudi nyumbani CCM.

Wote wawili hakuna aliyeonja ladha ya kupigania mageuzi nchini, walikuwa wanakula kivulini wanamageuzi wakihangaika juani. Wote wawili hawajui gharama za kudai mabadiliko waliyolipa wana mageuzi.
 
Ruge huyu jamaa itakuwa ameuwawa na sumu kali sana sana kama polonium-210 tena itakuwa alikula, aliivuta au alikunywa huenda ilikuwa ni dozi ndogo aliyopewa na mtaalam wa hali ya juu. Mazingira yanaonyesha kabisa maana tangia mwaka jana alipoanza kujisikia vibaya akiwa kwenye hafla fulani.

Dalili za kupewa sumu ndo hizo kujisikia vibaya kuharisha, kutapika na baadhi ya organ za mwili kushindwa kufanya kazi vizuri na mwishowe kifo. Anyway hii inaonyesha serekale tuliyonayo ni ya aina gani.

Kwenye kumuaga Ruge kuna watu watalia sana kuliko wenye msiba ila ili ku shift attention wakaona wafanye wanamleta mzee Lowassa ila watambue CCM makada ipo siku watakuwa wakimbizi. Waanze kuandaa sehemu z kukimbilia maana sasa mambo yamekwiva

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kauawa na boss mmoja wa jiji la Dsm hakufa kwa mapenzi ya mungu cha ajabu waliomuua wanajidai kuwa na majonzi utadhani mungu hawaoni
 
Back
Top Bottom