Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Msukuma mwili umemkauka sababu ya kutusi watu wazima na roho mbaya nadhani atayakana maneno yake.Siasa ni upepo sio hesabu sipati picha lowasa ndo akawa mgombea wa ccm 2020 ataweka wapi USO wake
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni muda mzuri kwa upinzani kustaw sasa EL alikuwa akiwatesa sana na kuua vipaj kama wakina Mnyika sasa tutegemee kuona wakina Mnyika wale wa zamani hakika patakuwa patamu sasa.
Mbona hamkusema siku zote ? Iweje leo
 
Msukuma kuna vitu viwili alikuwa anafanya hivi ili kuthibitisha kweli lowasa kaenda upinzani kutuliga changara macho tusione kilicho nyuma ya pazia au msukuma alikuwa anamtukana hajui ukweli ni upi aibu inategemea yuko upande gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio kilichobaki hicho kujipa moyo hivi unafikiri zile kura milioni 6 walizopata chadema 2015 zilikuja kwa lisu na kina mnyika hakika ule kwa asilimia kubwa ni mtaji wa lowasa kiukweli hili ni pigo kwa chadema kilichobaki kujikaza tu kwa maneno kama yako.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Sometime tupunguze Ujuaji Na tuheshimu Wake zetu Na Watoto zetu

Akina Fred Na Regina walishauri Mzee abaki CCM akaacha kufuata ushauri wa Familia akaenda kuwa sikiliza Wajanja wa Mjini kina Hamis Mgeja Na Freeman Mbowe

Wamempulusa hela zote Wahuni wale mpaka Jumba la ubalozi wa SA limeyeyuka ndio anakumbuka ushauri wa Familia

Pamela atandike kitanda karibu ataacha kukumbatia Mto usiku

Hussein Bashe Uteuzi unanukia
 
Mh mzee Lowassa ni mjanja sana anajua kucheza na akili za viongozi wa Tanzania

Ameamua kurudi mapema baada ya kuona mambo siyo mambo pia nyumbani kumenoga
kale kamsemo mwenye nyumba hawezi kukimbia nyumba yako nimekakumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu damu ni nzito kuliko chama wataachiwa na kufutiwa kesi, sishangai nililitegemea ili lakini ameacha mtaji mkubwa. Ninachoshauri wanachadema msimtukane kama ccm walivyomtukana sasa sijui aibu wataziweka wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa ni mchezo mchafu, huwa haina aibu mkuu, ni sawa na msemo mmoja unaosema, '......haina makombo', na mtalaka hatongozwi.
 
Msiba wa Ruge?

Hapana. Hakuna sababu ya msingi kwa Lowassa "ku-divert attention ya Watanzania kutoka kwenye msiba wa kitaifa wa Ruge."

Hata hisia kuwa "kuna mkono wa mtu kwenye kifo cha Ruge" hazijapata umaarufu kiasi cha kupelekea Lowassa akurupushwe leo ili "azime" suala hilo.

Kuwatenga waliomtosa Lowassa?

Uwepo wa Rostam Aziz katika tukio unaweza kuwa ishara ya uhusika wake katika uamuzi wa Lowassa kurejea CCM. Na uhusika wake unaweza kumaanisha kuwa "mapacha wawili kati ya watatu" wa MTANDAO wa JK (JK mwenyewe, Lowassa na Rostam) sasa wapo kwa Jiwe.

And where does that leave JK? Well, he was the major force behind kutoswa Lowassa. With him were Mkapa na Mwinyi. Sio siri kuwa wote watatu have fallen out of favour with Jiwe.

Nadhani katika hili labda tuache muda uongee.

October surprise?

Katika siasa za uchaguzi huko Marekani, "October surprise" ni tukio la makusudi linalolenga ku-influence matokeo ya uchaguzi.

Ninaazima political jargon hiyo kumaanisha kuwa huenda tukio hilo la leo linalenga ku-preempt tukio jingine kubwa ambalo "mtu flani" anatarajia linaweza "kupozwa" na ujio wa Lowassa huko CCM pindi tukio hilo likitokea.

Ugumu wa kuongelea tukio hili kama ule uliojitokeza katika kujadili uwezekano wa Lowassa kurejea CCM. Kila baadhi yetu tulipofungua mdomo sio tu kubashiri kuwa Lowassa angerudi CCM bali pia kumtuhumu kuwa huenda anakihujumu chama hicho, tuliishia kutukanwa



Kwahiyo to be on the safer side, si vema kuongelea kitu ambacho huenda kikatafsiriwa kuwa ill wish if not sedition. But something is indeed cooking.

Nafsi inakataa sio kuamini kuwa kweli Lowassa karudi CCM (lilikuwa suala la when na sio if) bali kuamini kuwa kurudi kwake CCM LEO ni kwa vile "leo ni siku kama nyingine."

Time will tell.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom