Tetesi: Edward Lowassa kuongea na vyombo vya habari kesho kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Status
Not open for further replies.
Wala sitaki hata kumsikia huyu mtu kuanzia leo. Kaniharibia siku hakuna kunacholika wala kunyweka mpaka muda huu. Heri nikapumzike kambi za alshababu!!

Mkuu cdm walipokea makapi, na waliambiwa kabisa kuwa ni makapi, ila hawakusikia!! Lowassa toka amekuja, hakuna lolote aliloongeza, zaidi ya upole. Huyu hayawan alifanya Dr Slaa kuondoka, sasa anaenda kujikomba kwa wakuu wake! Bastard!!
 
Kwa akili zako ukajua kabisa kwamba 2015 Chadema inaaminiiika na wa Tz kiasi cha kuweza kukabidhiwa dola?!
Ni suala la muda tu utaelewa kama in chama cha siasa au cha upatu
Mambo 2015 yamekujaje hapo ?

Upo ok upstairs ?
 
Mkuu hii ni zaidi ya mtu aliyepata Cannabis, labda uichanganye kidogo na cocaine halafu ushushie gongo ndio unaweza kufikia level ya mkanganyiko utakaoupata ukizichukulia siasa za bongo serious sana😀
Hahahahahaaaaa
"Mkuu Cannabis, you made my day”
 
Mimi KAYEKE kuanzia leo siingii tena jukwaa la siasa. Byeeeee.
 
Lowasa ni Mzee wa maamuz magumu akiwa raisi huyu anaweza tunduma
 
Ngoja aunge mkono juhudi za Magufuli, sijui makamanda watamuita fisadi tena, halafu wale wakijani watamsafisha, hapa patamu, akivuka upande wa pili hamna aliye salama wote wataonekana wanafiki, yetu macho😀
Nimetulia natafuna kashata zangu apa...naangalia movie inavyoendelea
 
Nimelia!!! Sio sabab ya lowasa ila sabab ya nchi yangu inavyopotea kizazi cha kina swalehe kinaniuma!!! [emoji22]
 
"Muda" tu ndio kitu pekee ndio kitakacho ponya vidonda na majeraha yetu kwa sasa.
Yale maneno yao ya faraja si dhani kama bado yananafasi tena katika ngoma za masikio yetu.
Ndimi zetu zilishazoea radha ya "siki" chungu. Ila hakika upo muda unakuja utafuta yote hayo na tutakuwa na "furaha".
THIS TOO SHALL PASS.
 
Duh, stori za lissu zote zimezikwa leo, hamna anaeongea ya kamanda lissu for presidence wala sijui kaenda Brussels.
Njia nyeupe kwa TL kugombea sasa 2020, kuna vitu huwa vinatokea naturally, this is one of them!
 
Nakumbukia kale kawimbo tuna imani na EL. Tanzania oyee
 
CDM Vigeu geu kweli..leo hii wanamponda Babu yangu aliyewapatia viti vyingi vya udiwani!hehee subirini dawa iwaingie hamjielewi.
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Leo katibu mwenezi wa CCM Ndugu Polepole aliutangazia umma wanatarajia kumpokea kiongozi mkubwa toka chama cha upinzani.Tena mapokezi hayo yangeongozwa na Makamu wa Mwenyekiti Bara Ndugu Philipo Mangula.

Tangu hama hama au nunua nunua ya wapinzani kuanzia ngazi za uduwani na hata ubunge sijapata kusikia Makamu wa mwenyekiti akitumika kupokea wapinzani.

Ajabu leo Makamu wa Mwenyekiti kampokea mpinzani aliyeshindwa ubunge Ilala !!!.

Nafsi yangu inaniambia Muslim Hassanal hakuwa kiongozi mkubwa aliyetarajiwa kupokelewa leo.

Kiongozi mkubwa kutoka upinzani aliyetarajiwa kupokelewa leo alikuwa Ikulu ya Magogoni na kesho pale hotel ya Serena tusitarajie mapya zaidi ya Ng'ombe aliyekatwa mkia kurejea zizini lakini akihakikishiwa kurejeshewa heshima yake na utukufu alioukosa kwa kipindi cha miaka miwili.

Makamanda tujiandae kisaikolojia,ukweli utabaki ukweli Mbowe alicheza karata mbovu anastahili kubeba lawama zote.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…