Edwin Mtei aliposikitishwa na Tundu Lissu kumtusi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Hujaonesha neno gani ni tusi, tulijadili.

Hujaonesha.
 
Unapimaje na kujua factually kwamba "Mwalimu is the most intelligent Tanzanian?".
 
Tatizo kubwa la baadhi ya watu ni kufikiria kuwa watu wengine ni miungu watu na wanafaa kuabudiwa tu bila kukosolewa pamoja na makosa mengi wanayoyafanya kama binadamu.

Hili halikubaliki kwani hakuna mwanadamu yeyote aliyeumbwa kufanya mema tu siku zote. Hivyo Tundu Lissu kama alimkosoa Nyerere, (Japo hakumtukana kama waongo wengine wanavyodai humu), ni sawa kabisa kwani Nyerere hakuwa Mungu bali alikuwa ni binadamu tu kama wengine na ndio maana hatunaye humu duniani leo hii.

Nyerere kama binadamu yeyote alikuwa na mapungufu yake na ndio maana hakuweza kuishi milele sasa leo wengine kutaka kumtumia kama mtaji feki wa kisiasa ni ujinga tu na ufinyu wa mawazo.

Mfano tu ni kuwa kuna makosa makubwa matatu ambayo aliyafanya na athari zake zimekataa kuondoka hadi leo na inaonekana itachukua muda mrefu sana kwa hizo athari kuondoka.

1. Alilazimisha sera yake ya Azimio la Arusha na matokeo yake kudumaza kabisa uchumi na kuua uwekezaji.

2. Alibuni siasa mbovu ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kumuiga dikteta Mao wa China na kupelekea kusondeka watu kwenye vijiji vya ujamaa kwa nguvu na kusababisha watu kupoteza mali na wengine kufariki dunia.

3. Alilazimisha vita na Uganda ili kumrejesha madarakani rafiki yake dikteta Milton Obote na matokeo yake kutia kitanzi uchumi wa nchi isipone hadi leo hii.

Hayo mapungufu yanatuonyesha vizuri kuwa Nyerere alikuwa ni mtu mwenye mapungufu tena sana tu na kuwa wasioweza kumkosoa ni wanafiki tu na wachumia tumbo kwani hakuwa Malaika.

Kwa sisi tunaoamini ktk ukuu wa Mungu kamwe hatutakubali ujinga au upumbavu wa mtu yeyote kuabudiwa kwani kufanya hivyo ni sawa na kuabudu sanamu na ni dhambi kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu.

You should not worship idols: Exodus 20:3; Leviticus 19:4; 26:1; Psalm 16:4; Isaiah 45:20; Jonah 2:8; Matthew 4:10; Luke 4:8; 1 John 5:21; Corinthians 10:14; Colossians 3:5; and Revelation 9:20 etc.

Wanadamu tumezidi sana kumchezea Mungu kwa kuwa hatumuoni kwa macho tunafikiri hayupo na badala yake watu tunaowaona kwa macho ndiyo tunafikiri ni yeye na tunathubutu eti kuwaabudu hadi viongozi wa kidini leo hii wanaabudu watu (Sanamu) tena mbele za waumini wao, very stupid. Tuache huu Upumbavu.
 
Reactions: Pep
Kwamba unafikiri makubaliano tuliyoyafanya na sheria A yangekua nullfied na sheria B ambayo tungeitunga kama Lisu alivyotaka?

Alisema tutashtakiwa. Umesikia tuna kesi yoyote kwa ajili ya makinikia?

Chanzo cha vita ya Kagera haiwezi kua hicho kisa wewe umeamua. Kuna official docs zipo. Andika na wewe official doc ya kupinga hizo official docs.

Mimi sijaandika vitu 2 katika kuaddress hii ishu. Umechagua hivi 2 na yet unaviaddress hovyo. Hakua perfect, Nyerere, lakini at least hakufutuka kama Lisu baada ya kupata madaraka.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu katika Hilo huna hoja,hakina mahali Lissu alimtukana Mwalimu,weka hiyo Clip hapa Kama ushahidi,alichofanya no kuchallenge like Mwalimu alifanya hasa kuhusu vijiji vya ujamaa.Lakini sio uongo kuwa Nyerere yeye alijiona Kama Alfa Omega kwenye nchi hii kitu ambacho kilikuwa sio sawa.Wakina Sokoine na kawawa na wengineo walikuwa hawamchallenge,yeye anaagiza tu Kama MFALME ,aliiongoza Tanzania Kama MFALME na yeye Ndio chanzo hata Leo unaona ninyi CCM mnashindwa kuitofaitisha CCM,serikali na vyombo vingine vya dola,raia anakuwa MFALME kitu ambacho sio sahihi.

Nyerere alikuwa Kiongozi mzuri lakini alikuwa na.madhaifu mengi tu makubwa ambayo mengine historia haisemi wazi.Operation ya kuwenga nguzo za Ujamaa ziliambatana na ukatili mkubwa sawa na leo Magufuli anavyowatesa wapinzani.
Vita ya Uganda ya kumrudisha obote ambapo majeshi yetu yalienda mpaka ndani ya ardhi ya nchi nyingine kinyume na masharti ya UN,yalileta balaa kubwa kwa nchi lakin mabalaa hayo huwezi kuta yameandikwa au kusemwa na media yoyote Tz.
Kuna Mambo mengi Sana siwezi kuyamaliza.japo mazuri ni mengi Ila na mabaya yapo,na lazima yasemwe,kusema yeye ndio mwasisi wa taifa kwa hiyo asisemwe vibaya huo ni ufinyu wa fikra.
 
Nyie madogo kuweni na heshima kidogo japo hata kwa Baba Wa taifa, hizo schoolboy politics zitawaletea shida,
Suala sio schoolboy ama la,Tundu Lissu hakuwahi kumtusi Mwalimu Bali alijaribu kuchallenge Basi ya maamuzi yake.Na anao huo Uhuru.Lakini matusi No.
nNyerere ana mazuri mengi lakini kumwona Kama Mungu hiyo sio sawa,ana madhaifu yake kibao tu.Na lazima tuseme.
Wengine hata kusema Mwalimu alikuwa mvutaji aliyekubuhu wa Sigara na Tumbaku hawasemi wanaogopa.Sasa huo uoga unaturudisha nyuma hapo baadae kwenye Mambo mengine.

Japo hatupaswi kumwongelea Mwalimu madhaifu yake in personal,Bali maamuzi yake tunaweza kuhoji na isiwe kosa la kuvunja katiba
 
Kamalizie shule kwanza ili ujue vyema historia na kuelewa kile kinachoongelewa hapa.
Ninyi watoto, repeat, nasema watoto mliozaliwa juzi, hamjui wala hamjaweza kuona scenario ya yale aliyoyafanywa na Mwalimu na watanzania kwa ujumla.
 
Unanivunjia heshima mkuu.
Mimi mwana CCM damudamu na siwezi linganishwa na Musiba wala Polepole, watu ambao kiitikadi hawana msingi wala muelekeo.
Inakuwa vigumu kuamini kuwa ni wewe uliyeandika hayo uliyoandika. Mimi si pekee wala wa kwanza kuwa na shaka kama ni wewe. Sasa tumeamini ni wewe. Hivyo unajivunjia heshima mwenyewe!
 
Inakuwa vigumu kuamini kuwa ni wewe uliyeandika hayo uliyoandika. Mimi si pekee wala wa kwanza kuwa na shaka kama ni wewe. Sasa tumeamini ni wewe. Hivyo unajivunjia heshima mwenyewe!
Ni ulemavu wa kifikra kufikiri kuwa hakuna mwana CCM ambaye ni liberal.
A spade I call a spade, fuatilia posts zangu.
I argue with a principle not hearsay!
 
Ni ulemavu wa kifikra kufikiri kuwa hakuna mwana CCM ambaye ni liberal.
A spade I call a spade, fuatilia posts zangu.
I argue with a principle not hearsay!
Umenoa. Mwenye principle anaeleweka. Dunia nzima itajua. Leo kuna mutation imetokea. Si wewe. Umeamua kujivunjia heshima mwenyewe. Usitafute mchawi. Ni wewe mwenyewe!
 
nimefafanua mkuu, go back to my comment!
Comment yako haijaeleza umejuaje Nyerere ndiye most intelligent.

Unawajua Watanzania wangapi?

Unawezaje kusema Nyerere ndiye most intelligent katika wote hao?

Intelligence ni nini?
 
Comment yako haijaeleza umejuaje Nyerere ndiye most intelligent.

Unawajua Watanzania wangapi?

Unawezaje kusema Nyerere ndiye most intelligent katika wote hao?

Intelligence ni nini?
nimeiedit comment yangu mkuu, paragraph ya kwanza na ya pili naeleza mambo aliyofanya Mwalimu kuonesha sisi sote ni wajinga mjanja ni yeye tu ( my contextual definition of intelligence) go back itafute ukaisome upya!
 
Taifa limejaa mang'ombe kila Kona unategemea nn mwana?
 
Umenoa. Mwenye principle anaeleweka. Dunia nzima itajua. Leo kuna mutation imetokea. Si wewe. Umeamua kujivunjia heshima mwenyewe. Usitafute mchawi. Ni wewe mwenyewe!
Sasa kama hata hizo principles huzielewi uta argue vipi mkuu.
Usitetee dogmas ambazo hazina logic.
 
Mkuu baba yako , msiyelingana hata kidogo kwa umri, wadhifa na hata disposition, kumfananisha na matapeli wa mitaani,si kuudhi tu bali tusi baya sana.

Na ndio maana post yangu ya kwanza kabisa nimemquote mzee Mtei akiwa anaonyeshwa kukerwa na tabia hiyo ya Lissu KUMTUSI Mwalimu.

Mdomo wa Lisuu unaweza kuwa ni asset katika ku argue a case na kudraw precedence mahakamani, lakini kwenye siasa kuna un written laws, na anaonekana kuwa na mdomo mchafu, usio na staha kwa wakubwa.
Na kumtusi Mwalimu ni dharau kubwa kwa watanzania.

Busara , hekima na adabu kwa waliokuzidi hata kama ni mtu ambaye hukubaliani naye ni kitu muhimu.

Kwa heshima aliyojijengea Mwalimu kwa Watanzania, Afrika na dunia nzima, kwa Lissu kumwita ati ni tapeli sawa na kina Massawe au Papaa Msofe wa mitaani, ni tusi na kosa lisilosameheka kisiasa.

Na leo tamko hilo linamrudia Lissu, ati yeye ni msafi kuliko na kuzidi Mwalimu na anautaka urais!
Over my dead body.

Na naamini kuna wanasiasa watakuwa wameapa Lissu si lolote wala si chochote katika kugombea urais Tanzania.
Na pengine huko aliko aombe uraia na agombee Urais huko maana huko kuna demokrasia ya kutosha.
 
Reactions: Pep
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…