Mkuu Jidu kwanini umeamua kubomoa reputation ambayo for years umejijengea humu?
I have never seen you giving biased opinions as on this post.
Umekua mtu wa kuruka ruka huku na kule, tena kwenye thread yako mwenyewe.
Funny enough, aina ya maneno aliyotumia Lisu (sio matusi, but maneno ya kuudhi) ndiyo unatumia kuwajibu wachangiaji wanaoleta hoja fikirishi ama wanaokua tofauti ya maoni yako.
Bado nashawishika kuamini huyu sio Jidu, na hata kama ni Jidu basi sio la Mabambasi
Mkuu baba yako , msiyelingana hata kidogo kwa umri, wadhifa na hata disposition, kumfananisha na matapeli wa mitaani,si kuudhi tu bali tusi baya sana.
Na ndio maana post yangu ya kwanza kabisa nimemquote mzee Mtei akiwa anaonyeshwa kukerwa na tabia hiyo ya Lissu KUMTUSI Mwalimu.
Mdomo wa Lisuu unaweza kuwa ni asset katika ku argue a case na kudraw precedence mahakamani, lakini kwenye siasa kuna un written laws, na anaonekana kuwa na mdomo mchafu, usio na staha kwa wakubwa.
Na kumtusi Mwalimu ni dharau kubwa kwa watanzania.
Busara , hekima na adabu kwa waliokuzidi hata kama ni mtu ambaye hukubaliani naye ni kitu muhimu.
Kwa heshima aliyojijengea Mwalimu kwa Watanzania, Afrika na dunia nzima, kwa Lissu kumwita ati ni tapeli sawa na kina Massawe au Papaa Msofe wa mitaani, ni tusi na kosa lisilosameheka kisiasa.
Na leo tamko hilo linamrudia Lissu, ati yeye ni msafi kuliko na kuzidi Mwalimu na anautaka urais!
Over my dead body.
Na naamini kuna wanasiasa watakuwa wameapa Lissu si lolote wala si chochote katika kugombea urais Tanzania.
Na pengine huko aliko aombe uraia na agombee Urais huko maana huko kuna demokrasia ya kutosha.