View attachment 2730513
ELIMU YA PADRE WA KANISA KATOLIKI
(Sehemu ya Pili)
Na. John-Baptist Ngatunga
___________________________
Baada ya kumaliza Malezi ya Seminari Ndogo yaani Pre-Form One hadi Kidato cha Sita na kupata Ufaulu wa Division I au II; Mseminari ataendelea na Masomo yake katika Seminari Kuu ambako atasoma Masomo ya Falsafa (Philosophy) kwa Miaka 3 na Miaka 4 Tauhidi (Theology) na Mwaka 1 wa Uchungaji (Pastoral Year) yaani Mwaka wa kupata Uzoefu wa Kichungaji (Field). Baada ya hapo atapata Ushemasi na kuwa Padre.
Mapadre wengi wa Majimbo husoma katika Seminari Kuu zifuatazo zilizopo chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC):
Philosophy (Falsafa):
1. St. Antony of Padua Ntungamo Senior Seminary (Bukoba)
2. Our Lady of the Angels Kibosho Senior Seminary (Moshi)
Theology (Tauhidi):
3. St. Paul the Apostle Kipalapala Senior Seminary (Tabora)
4. St. Karoli Lwanga Segerea Senior Seminary (Dar es Salaam)
Pia kuna Seminari Kuu ambayo hapo awali ilikuwa chini ya Watawa wa Mtakatifu Benedicto (OSB) wa Abasia ya Peramiho iliyoko Jimbo Kuu la Songea Mkoani Ruvuma anayopokea kwa kiwango kikubwa ana Waseminari wa Majimbo yaliyo chini ya Majimbo Makuu ya Songea na Mbeya:
5. St. Augustine Peramiho Major Seminary:
Philosophy (Falsafa) na Theology (Tauhidi)
Mseminari yeyote anayetaka kuendelea na Masomo yake ya Upadre katika Seminari Kuu ni lazima awe na sifa za Kitaaluma sawa na yule Mwenye sifa za kwenda kusoma chuo kikuu popote duniani. Ndio maana nimesema ni lazima Kidato cha Sita afaulu kwa kupata Division I au II.
Nje ya hapo, atatakiwa akasome kwanza Diploma ya Fani yoyote ile ili apate sifa sawa na yule anayeweza kusoma Shahada ya kwanza katika chuo kikuu au Taasisi yoyote ya Elimu ya Juu.
Kama ilivyo desturi ya Masomo ya Theology ambayo ili uwe na sifa ya kusoma Theology kwa kiwango cha kutaka kupata Shahada ni lazima kwanza usome na kumaliza Kozi za Falsafa basi. Kwa mantiki hii ieleweke pia kuwa hakuna Padre wa Kanisa Katoliki ambaye hajasoma Falsafa. Na maana rahisi ya FALSAFA ni "Elimu ya Elimu zote."
Na katika Miaka ya Falsafa, atawasoma Historia ya Falsafa (Ancient, Medieval, Modern na Contemporary). Atawasoma Wanafalsa mbalimbali kuanzia Wayunani wa Kale (Ancient Greek Philosophers) na wengine wote hadi Wanafalsafa wa Karne hii ya 21.
Atasoma Kozi zote za Falsafa unazozifahamu na usizozifahamu na kufaulu kwa kiwango kisichotiliwa Mashaka. Akishindwa kukidhi vigezo vya Ufaulu hawezi kuendelea na Masomo yake ya Upadre.
Akimaliza Falsafa kwa Miaka 3 na kupata Degree, ataendelea na Masomo ya Theology ambako atasoma Maandiko Matakatifu (Biblia) kwa undani, Sakramenti, Maisha ya Kiroho, Maadili ya Kanisa, Imani ya Kikristo na Imani za Dini nyingine, Uchungaji, Liturujia, Historia ya Kanisa, Sheria za Kanisa, Katekesi na mengine.
Licha ya Masomo hayo ya Darasani, Mseminari atajifunza mambo mengine mengi tu kama vile: Lugha mbalimbali, Muziki, Kompyuta, Sheria, Ujasiliamali, Ualimu, Ushauri na Unasihi, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Ufundi na mengine mengi yatakayomsaidia katika Utume wake katika Maisha ya Kichungaji.
Baada ya kumaliza Masomo yake ya Upadre katika Seminari Kuu, kunakuwa na utaratibu tofauti tofauti kutegemeana na Jimbo au Shirika la Kitawa. Lakini kikubwa ni kwamba wapo wanaomaliza Seminari Miaka yote 7 ya kukaa Darasani (Miaka 3 Falsafa na Miaka 4 Tauhidi) wakimaliza wanarudi Majimboni kupata Daraja ya Ushemasi ambao wanautumikia kwa Miezi isiyopungua 6 na kisha Kupadrishwa.
Lakini wengine wakimaliza Masomo yao ya Mwaka 3 wa Tauhidi sawa na Mwaka wa 6 (yaani Miaka 3 ya Falsafa Miaka 3 ya Tauhidi) wanaenda Mwaka wa Uchungaji ambao ni Mwaka 7.
Baada ya kumaliza Mwaka huo wa 7 hurudi Seminarini kumaliza Mwaka 4 wa Tauhidi ambao watasoma Miezi 6 watarudi kupata Daraja ya Ushemasi, kisha wanarudi tena Seminarini kuendelea na Masomo yao wakiwa Mashemasi. Baada ya hapo hurudi Majimboni kwao tayari kuipokea Sakramenti Takatifu ya Upadre.
Ndugu zangu; kuwa Padre sio mwisho wa kusoma kwa Padre wa Kanisa Katoliki. Baada ya Kupadrishwa, Padre anaweza kupelekwa tena Masomoni muda na wakati wowote kutegemeana na hitaji la Jimbo. Hapo atapelekwa kusomea chochote kile ambacho Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo husika ataona inafaa kwa kushauriana na Waandamizi wake.
Padre husika atapelekwa kwenye Chuo Kikuu chochote. Kumbuka mpaka hapa tayari anakuwa ana Degrees 2 (Falsafa na Tauhidi). Lakini ataendelea na Masomo hukoChuo Kikuu ili kuendelea kujipatia Maarifa. Elimu ni Moja ya Mapaji Saba ya Roho Mtakatifu pamoja na Akili. Hivo, Mapadre wanasoma soma kwa kiwango cha juu sana.
Na kama sikosei, nadhani kuanzia Mwaka 2012 kuna utaratibu hapa Tanzania kwamba kila Padre anayetakiwa kuteuliwa kwa nafasi ya Uaskofu ni lazima awe na Shahada ya Uzamivu yaani Shahada ya Juu kabisa ya Udaktari (Philosophiae Doctor-PhD) ya Fani au Taaluma yoyote.
Hapa tuelewe kuwa Udaktari ninaouzungumzia hapa sio Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) bali Udaktari wa Kitaaluma wa kukaa Darasani: kusoma na kufanya Tafiti.
Hapa naomba sana ieleweke vizuri sana kuwa zaidi ya 90% ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki hapa nchini ni Madaktari wa Falsafa katika Taaluma mbalimbali (They are Doctors of Philosophy in different Specializations).
Japo mara nyingi sana huwa wanatambuliwa tu kwa Cheo cha MHASHAMU ASKOFU MKUU.....au MHASHAMU ASKOFU....Laiti kama wangekuwa ni Watu wa kujikweza kama wafanyavyo baadhi ya walioheshimishwa kwa Udaktari wa Heshima pengine ilitakiwa tuwe tunawatambua kwa MHASHAMU ASKOFU DOKTA...........(PhD).
Ni Wasomi hawa watu lakini basi tu huwa hawaringi na hawajikwezi. Ila kiukweli kule 'ghorofani' kwao huwa kunafikiri ipasavyo. Wako vizuri sana hawa Mababa Maaskofu, Mapadre na Mashemasi. Kielimu Viongozi hawa wako mbali sana kuliko hata wanavyojionesha na tunavyowachukulia wengi wetu.
ITAENDELEA....... Sehemu ya Tatu