Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Ni kiingereza hajui au lafudhi yake ndio sio ya kiingereza!!?

Wachina wanajua kiingereza kama wazungu!!?

Acheni ushamba,msukuma lazima aongee kiingereza Cha kisukuma kama alivyo mchina anavoongea Kwa mother tongue yake!!

Wabongo washamba kinoma noma!!
 
Kama anajiita ni sawa. Kuna mtu pia anajiita Prof. Ndumilakuwili huyo kiingereza ni ziro. La amepewa huo uprof kwa vyeti kuna haja ya kujadili hapa
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Professor lazima awe kama Jacob Janabi,si vinginevyo mdau.
 
Angeongea Kiswahili kibovu ndipo ingekuwa hoja!

Kwani maprofesa wa Uingereza wanajua Kiswahili?
Kwani maprofesa wa uingereza huwa wanafundishwa kiswahili toka chekechea??Tanzania kama wewe profesa na hujui kingereza wewe ni SLOW tena kiande, maana umefundishwa kiswahili chekechea miaka miwili, primary miaka 7,secondary miaka 6,degree mitatu hadi 5,bado masters,PhD,kingereza bado kama kama ndalichako???
 
Samahani ni nje ya mada kidogo.
Leo nimeona na kusikiliza clip ya mke wa Lissu katika mkutano wa IDU huko Ubelgiji akiwasilisha kuhusu kukamatwa kwa Lissu na hatari ya hukumu ya kifo.

Ilikuwa ni kiingereza murua, chenye mpangilio mzuri kimantiki na kinachoma moyo wa msikilizaji sana.

Hata kama ungekuwa una chuki kupitiliza ile clip ina gusa.

Bila video nisingeamini kama yule ni Mtanzania.

Sipiganii watu wote wajue Kiingereza kwa ufasaha lakini nimevutiws na umahiri wa yule mama au dada.

Myonge mnyongeni haki yake mumpe.

Watakaosema so what sipendi ku-comment katika hilo.
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Kiingereza ndio uprofesa? Katafute maprofesa wa Urusi na Uchina au Scandinavian uone kiingereza Chao! Kiingereza ni lugha tu
 
yes sahihi kabisa
Sasa kama kiingereza kutumika katika masomo kunafanya mtu aweze kuongea kiingereza kwa ufasaha basi watanzania tungekuwa hatuna shida ya kukiongea kiingereza kwa ufasaha lakini uhalisia haupo hivyo.
 
Angeongea Kiswahili kibovu ndipo ingekuwa hoja!

Kwani maprofesa wa Uingereza wanajua Kiswahili?
Ni udhihirisho wa kiwango cha ujinga uliopo kwa baadhi ya watz kuamini kuwa kujua na kuongea kiingereza ndio usomi,...hovyo sana.
 
Umedandia bila kujua hoja. Sisi tunasoma kiingereza tangu darasa la kwanza,na kuanzia sekondari tunafundishwa kila kitu kwa kiingereza. Kwa nini usielewe na kuongea vizuri? (hapa sisemi uongee kama mzungu). Mbona watoto wa shule za kimataifa wanaongea vizuri? Wako London? Kenya watu ambao hawajaenda shule hawajui english. Tuache visingizio.
Neno mazingira unalielewaje? Watoto wa shule hizo walimu wao ni fluent na wengine wametoka nchi za ulaya, wanaonhea 24/7 lugha hiyo, kiufupi wako mazingira ya ulaya ila ndani ya tanzania, hao kuwa fluent katika lugha wala si ajabu. Sisi wengine hadi unafika level ya Phd sehemu pekee unaitumia lugha ni wakati wa official duties tena zingine zinaenda kwa kiswahili. Sio ajabu kuwa profesa na usimudu kiingereza vyema
 
Kiingereza ni lugha kama zilivyo lugha nyingine mf. Kimakonde, kinyakyusa, kikurya n.k, si lazima uijue lugha hiyo kinaga ubaga kama si mwenyeji wa maeneo ambayo lugha hiyo inazungumzwa. Tuache fikra duni.
Somo lifundishwe kwa kimakonde, ufaulu kwa kiwango cha juu kabisa lakini huwezi kuongea kimakonde!
 
Watu humu wana changanya kitu kimoja kikubwa nacho ni Kiingereza kama mfumo wa maisha na kiiingereza kama lugha ya kufundishia huyo mtaaluma kaangukia katika kiingereza kama lugha ya kufundishia ila kwenye kiingereza kama mfumo wa maisha hayupo na ndio maana inaonekana anacho kibovu.

Kama lugha ya kufundishia haina matumizi makubwa katika maisha yako hauwezi kuifanya vyema.
 
Watu wanajitoa ufahamu tu wakati wanasheria wetu wanapoenda nje wanashindwa kesi left and right kwa kushindwa lugha tu, tunalipa makampuni ya kigeni mamia ya mabilioni, tunasign mikataba mibovu na wakoloni kama kina mangungo for ages, tunapigwa kila siku, watanzania wanawaogopa wakenya kwenye biashara kama wamekutana na simba tumebaki tupo ndani tu na umachinga wetu halafu tunajidai kiingereza sio muhimu! Ni ujinga tu kujustify ujinga siku zote na tumerithishwa na sisiemu kwa kuwa inapata maslahi sana kwa ujinga wetu.

Watanzania hata confidence hatuna kwa kuwa hatuna knowledge na command ya language pia hatuna, jana tu tumeona mgombea wa WHO serikali ilivyopiga mabilioni kumsaidia ashinde, mpaka na Jk alitumwa akafanye mandingo kwa wapiga kura west Africa no confidence! Povu ruksa
 
Jambo la kuhoji hapo ni iwapo uprofesa wake ni halali ama la.

Kutojua kwake Inglishi hakuna uhusiano wowote na uprofesa wake.
Noooo hilo nalo ni la kuhoji
KWA NINI USISEME KWAMBA AWE ANAJUA KIFARANSA, KICHINA, KIRUSI AU KIBELGIJI AU KIJERUMANI?
Hapo ndo akili mbovu huzaa akili mbovu...
tuweni makini!
lugha si kipimo cha elimu, tusiwe vibaraka kupitiliza
huwez ukasomea mtaala wa english tokea msingi mpaka level ya prof na bado unayumba.
Kuna tatizo mahali
 
Machapisho ambayo huandikwa kwa kiingereza aliwezaje?

Maana mtu hadi anafikia kuwa profesa amefanya research za kutosha ambazo huandikwa kwa kiingereza.
Unachowasilisha kitaaluma ndio kinatizamwa. Machapisho hayo umahiri wa lugha sio kipaumbele. Hata hivyo wengi huandika na kuwapa wenzao kuifanyia proof reading na kunyoosha hapa na pale dosari za lugha
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Ulivyo na ujinga,nani alikwambia kuongea kiingereza ndio kipimo cha elimu?
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Sisemu mitano tena 😂😂😂
 
Back
Top Bottom