Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Hajasomea umahiri wa lugha ya kiingereza. Madakatari pia for 5 yrs ni ngeli kwa kila kona, lakini nitashangaa daktari (MD) mtanzania akaiongea ngeli kama mwingereza. Proceedings zote za kidakatari anapomtibu mgonjwa ni za ngeli na some latin and Greek, lakaini hajasomea kuwa na oratory skills za hizo lugha nje ya taaluma.
Hatutaki aongee kama muingereza, tunataka aongee kwa ufasaha na urahisi.

Lafudhi na mpandoshuko huathiri matamshi, lakini sio ufasaha.
 
Non sense, kwa sababu hicho cha kuongea eti wanataka kinyooke kama cha wazawa wa malkia.
Ndio maana nawaambia kama kutumia kiingereza tu kufundishia inatosha kufanya mtu aweze kuzungumza kiingereza fasaha basi watanzania tusingekuwa na shida ya kuongea kiingereza fasaha.

Huwa wanamsifia Mkapa kwamba ndio alikuwa anaongea kiingereza kizuri, kwahiyo kwao hiko ni kipimo cha ubora wa elimu kushindanisha na elimu za wengine.
 
Prof Janab amewashinda kwa kishindo hao jamaa wa wanaongea ngeli (ng'eng'e) nzuri kuliko yeye mara dufu, hapo vipi?
Unawaeleza uhalisia ulivyo wao wanasema et tunatetea ujinga.
 
Mkuu shida kwenye mada kama hii tunachanganyana sana, kwa navyoelewa huwezi kusema english is nothing kwa sababu english ndio lugha dunia kama watu wasemavyo lakini pia si sahihi kupima elimu ya mtu au kutilia mashaka elimu ya mtu kwa kigezo cha kuangalia uzungumzaji wake wa kiingereza.

Navyoelewa mimi haiwezekani mtu kusoma kwa miaka yote hiyo kisha ukawa hujui lugha iliyotumika katika masomo ni suala ambalo haliwezekani ila inawezekana mtu akasoma miaka yote hiyo ila akawa hawezi kuzungumza kwa ufasaha kiingereza ila sio kwamba hajui kabisa kiingereza kama inavyochukuliwa humu.
Unaposema lazima, ina maana hicho kiingereza ni mama yako?

Vipi kama alisoma Ufaransa au Urusi au alikulia na kusoma nchi za Scandnavia tangia utoto wake na akaamua kurudi Tanzania baada ya hapo.

Hebu msituchoshe na kushindwa kuwaza nje ya box. Hamna exposure kabisa, jaribuni kuwa mnatembelea japo hata Msumbiji wanapoongea Kireno au Burundi na Rwanda wanapoongea Kifaransa mtatupunguzia huu ushamba.
 
Mbona wanafunzi wanaopelekwa kusoma Kenya wanazungumza kiingereza kizuri sana. Nina watu wengi nawajua, wamesomesha watoto wao shule za primaries Kenya, wanazungumza vizuri sana kiingereza wakati kule wanakwenda shule tu. Kingine, Bongo mbona watoto wanaosoma Intenational school wanazungumza english nzuri? Wacheni visingizio. Tatizo ni elimu yetu.
Si kwa sababu ya mazingira wanazungukwa na watu waongeao kiingereza kucha kutwa. Lugha ni maongezi. Mtoto wa kisukuma ukimuweka london miaka miwili na waingereza ataongea kiingereza safi.
 
100%

Ndio maana wengi wanaokomaa na hoja za Kiingereza ni malimbukeni, na hawajawahi kugoka nje ya nchi.

Kwanza Wazungu walivyo *******, hata kama unajua English ukiongea lafudhi yako yanajifanya hayakuelewi.

Hata huko Uingereza watu wana lafudhi zao.
Hakika mkuu

Na kwa akili ya kipuuzi.kama hizi za mleta mada/uzi, CCM bado haijamaliza kazi yake. Iendelee kushikilia akili zao mpaka kizazi hiki cha kutukuza kila kitu cha wazungu kiishe.

Ndio maana kila uchao viongozi wa CCM wanajiita maprofesa, na wanaongea kiingereza safi ili wananchi wazembe kama hawa waamini watawala wao ni wasomi kweli kweli.
 
Prof Janab amewashinda kwa kishindo hao jamaa wa wanaongea ngeli (ng'eng'e) nzuri kuliko yeye mara dufu, hapo vipi?
VOTING RESULTS:
1. 🇹🇿 Prof Mohamed Janabi: 32
2. 🇨🇮 Dr N’da Konan Yao: 5
3. 🇬🇳 Mohamed Drame: 4
4. 🇹🇬 Prof Moustafa Mijiyawa: 4
 
Kama hajui kiingereza amewezaje kuelewa masomo yake? Kwa sababu hali ilivyo ni kwamba unaweza kukuta kuna msomi anasifika vizuri kwa taaluma yake ila siku akionekana kaongea kiingereza ambacho si fasaha tunaanza kusema elimu zetu mbovu na kuanza kutiliana mashaka na elimu zetu.
Nachoweza kukubalia ni kitu kimoja kuna watu waongeaji wazuri na wengine wanaweza kuwa sio waongeaji wazuri ila watendaji wazuri sana, ila tunategemea generally wasomi wetu waweze kuongea lugha kama kiswahili na english vizuri
 
sasa ndugu!!kwa mfumo wetu wa Elimu ,Mtu akifika level hii ya Elimu kama haijui hiyo lugha lazima kuwe na maswali,..Sasa anafundishaje vijana huko chuoni?
Angeongea Kiswahili kibovu ndipo ingekuwa hoja!

Kwani maprofesa wa Uingereza wanajui Kiswahili!
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Yeye ni prof wa ngeli/ linguistic?
Hicho kiingereza si kinaeleweka, sasa ajiumeme ili afanane na mzungu?, angeonekana ni msomi uchwara sana.
Ngeli ya kuongea mi nachochora ninavyotaka na ninaeleweka vizuri kwa sababu si language yangu, ya kuandika ni rahisi, kwa computer kuna tools zinakunyooshea lugha vizurii.
 
Angeongea Kiswahili kibovu ndipo ingekuwa hoja!

Kwani maprofesa wa Uingereza wanajui Kiswahili!
Hao maprofesa wa uingereza walifundishwa kwa kiswahili?

Kama unajiita dakatri huku lugha iliyotumika kukupa huo udaktari hauifahamu vizuri .

Maana yake wewe ni Daktari wa kukariri
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Nani mkuu? Prof. Lucas Mwashambwa nini? Ila Kiingereza kuu siyo lazima usomee. Ni lugha tu kama lugha zingine! Kwetu Watanzania siyo lazima uwe fluent, hicho hicho cha kuwasiliana kinatosha!
 
Sihitqji Hao maprofesa wa uingereza walifundishwa kwa kiswahili?

Kama unajiita dakatri huku lugha iliyotumika kukupa huo udaktari hauifahamu vizuri .

Maana yake wewe ni Daktari wa kukariri
Ukikariri (kama mistari ya singeli) school of medicine hutoboi, hatusomi ku perfect ngeli, tunasoma medicine, yenye language zingine pia, Greek na Latin, hizi zote hutaweza kuwa fluent lakini medical field utaitendea haki
 
Hao maprofesa wa uingereza walifundishwa kwa kiswahili?

Kama unajiita dakatri huku lugha iliyotumika kukupa huo udaktari hauifahamu vizuri .

Maana yake wewe ni Daktari wa kukariri
Hii hoja ni dhaifu!

Kujua maudhui na kujua lugha ni vitu viwili tofauti! Wengi humo tunaweza kusoma na kuelewa kiingereza, lakini kutunga essay ya maneno 100 kwa ufasaha ni mtihani, tusisiende kwenye Kiingereza cha kuongea!

Uzi ukiletwa kwa Kiingereza mnaangalia tu mnapita! Kaangalie forums za Kiingereza uone!
 
Hii hoja ni dhaifu!

Kujua maudhui na kujua lugha ni vitu viwili tofauti! Wengi humo tunaweza kusoma na kuelewa kiingereza, lakini kutunga essay ya maneno 100 kwa ufasaha ni mtihani, tusisiende kwenye Kiingereza cha kuongea!

Uzi ukiletwa kwa Kiingereza mnaangalia tu mnapita! Kaangalie forums za Kiingereza uone!
Elimu ya kukariri haiwezekani lugha iliyokupa degree ukose kuielewa .

Katazame watoto wanaosoma Shule bora Kama IST na ujilinganishe na wewe uliyepita shule za bure utaona kuwa upo dunia ya zamani
 
Back
Top Bottom