Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 15,096
- 8,914
Mimi naona kama kuna vitu vinachanganywa, kushindwa kuongea kabisa kiingereza hilo ni jambo na kuongea ila sio kwa ufasaha hilo ni jambo lengine.Hatuongelei utaalamu hapa. Tunaongelea competence ya kawaida tu. Unaijua process ya mtu mpaka kuwa profesa? Mbali na kusomeshwa katika Kiingereza kwa miaka zaidi ya 20, profesa huyu anafundisha kwa Kiingereza na kusimamia wanafunzi wa shahada mbalimbali kwa Kiingereza. Kwa nini ashindwe kuongea Kiingereza? Huko darasani huwa anafundishaje? Akienda kwenye makongamano na consultancy huwa anaongea lugha gani?
Tubadilisheni tu lugha tuanze kufundishana kwa Kiswahili maana Kiingereza kilishashindikana; lakini ni aibu kwa mtu aliyesomeshwa kwa Kiingereza, Kichina, Kikurya...kwa zaidi ya miaka 20 na anaitumia lugha hiyo kufundishia kushindwa kuiongea lugha hiyo kwa ufasaha.
Shida yetu sisi ni kushindwa kuongea kiingereza kwa ufasaha, kama ingekuwa kusoma masomo kwa kiingereza inatosha kufanya mtu ajue kuongea kiingereza kwa ufasaha basi watanzania tungekuwa tunaongea kiingereza kwa ufasaha ila haipo hivyo.