Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Chadema watakuunga mkono mana hy n furaha yao, ila wenye akili hawatokuunga mkono ulichokiandika.
 
Tunajua sana kujustify ujinga tuliolishwa na sisiemu, leo hii ukitoka nje ya Tz utakuta watanzania wa kutafuta tena kwa shida kubwa na ni kwamba kwa sababu wanaogopa kusafiri kwa kuwa wanaogopa kuongea lugha za kigeni! Hatuna mchango wowote wa maana kwa dunia tangu iumbwe tunajustify uchawa tu eti Kiingereza sio kitu! Kiswahili kimetusaidia nini hadi sasa zaidi ya kupunguza usukuma na unyiramba tu! Huyo profesa wa kiswahili mwenyewe kafundishwa kiingereza hadi kapata PhD yake
Mbona wewe jamaa ni jinga hivi???

Kweli ujinga ni kipaji?

Haya uko nje kuna Waarabu, Wahindi, Wasomali ma Wacongo wengi.

Wanajua Kiingereza??
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Labda ni ma-prof. na ma-dr.wa Kiswahili,aijue English ili iweje sasa.Mimi sijaelewa hoja yako hapa
 
Mbona kiongozi wa Korea Kaskazini hajui Kingereza pamoja na marais wengi tuu, kwahy hata huko elimu yao ni mbovu?
 
Mbona wewe jamaa ni jinga hivi???

Kweli ujinga ni kipaji?

Haya uko nje kuna Waarabu, Wahindi, Wasomali ma Wacongo wengi.

Wanajua Kiingereza??

Hahahaah we mwerevu ulikutana nao wapi? Mpimbwe kijijini? So Trump yupo kwao anaongea nao kinyakyusa? Sikuiti mjinga mie jipime tu mwenyewe!
 
Hivu kuwa profesooo ni lazima ujue kiingereza? Huko Uingereza kwenyewe kuna wajinga wanaowaza kama wewe wanaongea kiingereza na hawajasoma hata darasa moja.

Kuna maprofesoo huko Ufaransa wanaongea kifaransa hawajui kiingereza

Kuna maprofesoo Ujerumani, Urusi, Hispania na hata Uchina na Japan hawajui kuongea kiingereza.

Komboa akili yako, toka kwenye utumwa wa akili itakusaidia maishani.
Mmmmh
 
Akili yako ndo ya kupima! Umewahi kufanya utafiti kujua ni wanazuoni wangapi wa kiwango cha ubobezi ambao wanatoka katika mataifa ambayo kiingereza si lugha yao mama na bado wakafanikiwa sana kwenye maeneo yao ya umahiri? Amka dude..kiingereza ni lugha tu kama kimakua,kindali na kisambaa!
lugha gani ya kufundishia Tanzania? Usimutukane mtoa mada bila kumwelewa.
 
Angeongea Kiswahili kibovu ndipo ingekuwa hoja!

Kwani maprofesa wa Uingereza wanajui Kiswahili!
Watanzania hatuna akili. Kule China na Japan Kuna ma profesa Ila hata English hawajui. Ukiwauliza kichina na Kijapani very competent. Tuache utumwa Huu. By the way kuandika anaandika Kwa kufikiria sentensi anaweza edit hadi mara 20. Lakini tit for tat speaking ni mtihani Kwa wengi. Sisi tunajua Kiswahili ndo lugha mama. Hiyo tu inatosha. Waingereza wao Kiswahili hawajui hata kama kipo why tuumize kichwa kwaajili ya lugha za watu.
 
Mbona kiongozi wa Korea Kaskazini hajui Kingereza pamoja na marais wengi tuu, kwahy hata huko elimu yao ni mbovu?
Elimu, elimu elimu...Kiongozi wa North Korea, Kim Jong-un. anaongea lugha tatu kwa ufasaha nazo ni Kikorea (Korean), Kiingereza (English) na Kijerumani (German)

Akiwa bado mdogo baba yake, Kim Jong 11, alihakikisha anampeleka Ulaya kusoma. Alisoma katika shule ya International School of Berne, Gümligen nchini Switzerland.

Kwa kuwa aliishi huko na mama yake tangu utotoni lugha mbili alizofanikiwa kuongea ni Kiingereza na Kijerumani na ilimchukua muda kuongea Kikorea kwa ufasaha.

Akiwa nchini kwake, Kim Jong-un anagoma kabisa kuongea lugha nyingine zaidi ya Kikorea kama wafanyavyo viongozi wengine kutoka mataifa yaliyo na misimamo kama ya kwake.
 
Tujiulize wenyewe kuanzia form 1 hadi 6 then chuo kikuu bachelor then Masters halafu PHd na maresearch yake na ualimu halafu mtu anapata uprofesa, anakuja kubofoa halafu mtu akisema elimu yetu ina shida watu wanamshambulia hapa eti English is nothing, ingekua nothing kwa nini tunapoteza miaka yetu tunajifunza??? Huu ni umbuzi yani au unyani! Hao wachina wanajifunza miaka michache na kumaster na kuanza kupambana na UK na US sisi tuna shida gani?
Mkuu shida kwenye mada kama hii tunachanganyana sana, kwa navyoelewa huwezi kusema english is nothing kwa sababu english ndio lugha dunia kama watu wasemavyo lakini pia si sahihi kupima elimu ya mtu au kutilia mashaka elimu ya mtu kwa kigezo cha kuangalia uzungumzaji wake wa kiingereza.

Navyoelewa mimi haiwezekani mtu kusoma kwa miaka yote hiyo kisha ukawa hujui lugha iliyotumika katika masomo ni suala ambalo haliwezekani ila inawezekana mtu akasoma miaka yote hiyo ila akawa hawezi kuzungumza kwa ufasaha kiingereza ila sio kwamba hajui kabisa kiingereza kama inavyochukuliwa humu.
 
Mwanangu wa miaka 5 Yuko kindergarten -2 anajua kingereza ila sio professor.

Wachina, warusi, wakorea hawajui kingereza ila ndio wababe wetu katika nyanja zote.

Btw huyo Professor kabobea kwenye nyanja ipi?
 
Hii lugha ndio watu wanaitumia shuleni kuanzia sekondari mpaka vyuo vikuu, ndio lugha rasmi kwenye elimu yetu.

Sasa kama hawaielewi huko shuleni watakuwa wameelewa kweli walichofundishwa na hiyo lugha?
Lugha wanaielewa mkuu bila hivyo ingekuwa kikwazo kwenye masomo yao ila shida ni kushindwa kuweza kuongea kiufasaha hiyo lugha hilo ndio tatizo letu.
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
North Korea wapo hawajui kabisa kengere Saa, vp nao mkuu?
 
Atakuwa amesoma takribani miaka 15 kupitia lugha ya kiingereza(Kuanzia sekondari).

PhD wanahitaji kiingereza(tena kizuri) kwenye kufanya, kuwasilisha na kutetea tafiti.

Tena wanafundishwa matumizi ya lugha kitaaluma.

Kwa kweli hili ni tatizo.

Labda kama hakutumia kiingereza kusoma tokea sekondari.
Hajasomea umahiri wa lugha ya kiingereza. Madakatari pia for 5 yrs ni ngeli kwa kila kona, lakini nitashangaa daktari (MD) mtanzania akaiongea ngeli kama mwingereza. Proceedings zote za kidakatari anapomtibu mgonjwa ni za ngeli na some latin and Greek, lakaini hajasomea kuwa na oratory skills za hizo lugha nje ya taaluma.
 
.Waingereza wao Kiswahili hawajui hata kama kipo why tuumize kichwa kwaajili ya lugha za watu.
Badilisheni sera ya lugha katika elimu muache kutumia lugha za watu kujifunzia. Tumieni Kiswahili au Kisukuma au Kiha. Ni aibu kutumia Miaka 20+ unasoma katika Kiingereza, umeandika tasnifu na journal articles, unafundisha katika Kiingereza, bado kukiongea huwezi. Huwa unafundishaje kama lugha ya kufundishia huimudu? Kuna tatizo mahali hata mtoe mapovu vipi? Eti Kiingereza ni lugha tu kama zingine. Sawa. Kwa nini sasa mmeamua kuitumia kama lugha yenu ya kufundishia? Kwa nini mnatumia lugha ambayo hata maprofesa wenu hawaifahamu vizuri?
 
Lugha wanaielewa mkuu bila hivyo ingekuwa kikwazo kwenye masomo yao ila shida ni kushindwa kuweza kuongea kiufasaha hiyo lugha hilo ndio tatizo letu.
Lugha ya taaluma ni tofauti na lugha ya kubishana mtaani mada tofauti na taaluma yako.
 
Back
Top Bottom