Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
1747633727168.png
 
Hivi engineering, Medicine, Agriculture huko university unaafundishwa ku perfect ngeli, au unafundishwa taaluma?
So wewe uko hivi:BanHammer:kwa ngeli, na ndyo imekuinua sana??

OK tuna hao wataalam na hadi leo tunaita wachina watujengee madarasa, madaktari wetu hata wanasiasa tu hawaamini kila siku wanaenda nje kutibiwa na kila mtu akienda hospitali anakuja hapa jf kulalamika huduma mbovu kwa kilimo ndio hadi leo tuna njaa kila mwaka na pia wakulima wetu wanalima kwa jembe la mkono kwa traditional ways miaka na miaka, hao wasomi wetu wana mchango gani hadi sasa, so tunasema elimu ina tatizo kwa kuwa huwenda wana vyeti tu na wamekariri kwa kuwa lugha ilikua tatizo, hadi leo wanashindwa kutafsiri elimu yao kuwa mali hata iwalipe wao tu! Mkubwa kusema waende Veta hakukurupuka yani, anaona kabisa wasomi wetu wana vyetu vya degree nyingi tu lakini ufahamu wao haufikii hata wa VETA.

Wakisikia Martha Karua anakuja wanatamani kufunga mipaka kabisa hahaha😛😛😛
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
hivi huwezi pata uprofesa kwa kiswahili lugha ya taifa
 
Maprofesa wenyewe ndio hawa wanamuweka mchina "inside" yani ndani (mahabusu yani)!

Wa namna hii hata siwezi kumwachia mwanangu amfundishe sio lugha ya English tu hata kiswahili hajui

Neno mazingira unalielewaje? Watoto wa shule hizo walimu wao ni fluent na wengine wametoka nchi za ulaya, wanaonhea 24/7 lugha hiyo, kiufupi wako mazingira ya ulaya ila ndani ya tanzania, hao kuwa fluent katika lugha wala si ajabu. Sisi wengine hadi unafika level ya Phd sehemu pekee unaitumia lugha ni wakati wa official duties tena zingine zinaenda kwa kiswahili. Sio ajabu kuwa profesa na usimudu kiingereza vyema
Unanitania wewe. Mtu awe umefika Phd level halafu unatumia kiingereza kwenye official duties tu! Tangu darasa la kwanza ulikuwa husomi english? Sekondari je? Chuo kikuu je? Hebu acheni kutetea uzembe! By the way umekubaliana na hoja yangu kuwa tatizo ni elimu yetu kwa sababu umeonyesha kuwa waalim wetu hawako fluent kwenye english na pia mazingira ya shule sehemu kama vyuo yamejaa uswahili.
 
Mazingira yetu hayakuwafanya au kuwajenga kuongea lugha mara kwa mara kama sisi wengine unafanya kazi sehemu au unasoma lazima uongee hiyo lugha maana hakuna mswahili au mngindo karibu yako leo utakosea baadae utaenda sawa na hizi lugha zote zinataka confidence kwanza na kuongea mara kwa mara sasa Watanzania wengi wanajua kuandika ila kuongea alichoandika ndio tatizo Wazambia wanajua kuongea ila hawajui kuandika wanachoongea..
Watanzania hata kuandika hatujui. Na mbaya zaidi siku hizi hata kiswahili cha kuandika kinatushinda. Tatizo ni elimu! BTW huwezi kujua kuandika halafu kuongea ushindwe. Wewe unazungumzia ujuzi wa kukariri majibu ya maswali wakati wa mtihani tunayokariri na kuandika tulichokariri.
 
Unanitania wewe. Mtu awe umefika Phd level halafu unatumia kiingereza kwenye official duties tu! Tangu darasa la kwanza ulikuwa husomi english? Sekondari je? Chuo kikuu je? Hebu acheni kutetea uzembe! By the way umekubaliana na hoja yangu kuwa tatizo ni elimu yetu kwa sababu umeonyesha kuwa waalim wetu hawako fluent kwenye english na pia mazingira ya shule sehemu kama vyuo yamejaa uswahili.
Wewe binafsi unajiweka wapi ni mahiri wa lugha kama benjamin mkapa ama sogea twende ili tuwasiliane tu? Unafikia English C2 level? Wewe ulisoma Tanzania? Shule za kawaida ama za kimataifa? Experience yako ikoje? Walimu wa biology na physics ama history walikuwa wanafundishaje? Kipindi kizima kwa kiingereza ama 75 %kwa kiswahili katika kufafanua mada, sasa tokea huo msingi umahiri wa kiingereza mwanafunzi atautolea wapi? Mahiri wa lugha ya kiingereza Tanzania ni mawili ama amesoma shule nzuri sana hizo za kimataifa ama ana kipawa cha asili cha kukamata lugha za kigeni kwa wepesi na hawa ni wachache sana. Ila wengi wetu tunaweza kuwasiliana bila shida kwa kiingereza ila hatuna ule umahiri wa lugha.
 
Sasa unabishana nini wakati mimi nasema hilo hilo? Kuwa elimu yetu ndiyo tatizo? Kumbe umedandia gari mbele tu! Unakubali kabisa kuwa waalim hawana viwango halafu hapo hapo unabisha jambo usilolijua. Tanzania hatuko comfortable kabisa kwenye kuongea english na unakuta profesa anaongea madudu. Sasa kuna ulazima gani wa kutumia english kufundishia somo wakati 75% ya mada unazungumza kiswahili? Huoni ni tatizo hili?
 
Yaani upepo unakopiga nawe hukohuko unaelekea. Hoja zako zote hazikuwa na mlengo huu. Ila ni vyema kama umeamua kuwa upande wetu
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Kuna mmoja nilimuita mdumavu wa akili na mwili humuhumu.Amenichukia ile mbaya.
 
Kiingereza ni lugha tu mkuu, ila uwanja wake wa uprofesa naamini Yuko vizuri. By the way Kuna watu ni waandishi wazuri lakini sio waongeaji wazuri.
 
Akili yako ndo ya kupima! Umewahi kufanya utafiti kujua ni wanazuoni wangapi wa kiwango cha ubobezi ambao wanatoka katika mataifa ambayo kiingereza si lugha yao mama na bado wakafanikiwa sana kwenye maeneo yao ya umahiri? Amka dude..kiingereza ni lugha tu kama kimakua,kindali na kisambaa!
Tukikubali hii hoja yake siku nyingine atakuja kusema "kwa nini Wema Sepetu siyo professor wakati anaongea kiingereza kizuri?"

#tumpinge kabisa!
 
Hoja ipo hapa: kama lugha ya kusomea mashuleni kuanzia sekondari mpaka chuo kikuu ni kiingereza inakuwaje sasa mhitimu hajui kiingereza?

Ingekuwa tunasoma kwa kiswahili kuanzia msingi mpaka vyuo vikuu hapo sawa watu wasingejua kiingereza ingekuwa sawa tu.

China, Urusi, Germany nk lugha za kufundishia ni lugha zao, hawa hata wasipojua kiingereza sio issue maana ajira zipo za kutosha kwao na official language ni lugha zao.

Tanzania mtu anakwenda kwenye interview anakuta kiingereza, matangazo ya kazi ni ya kiingereza, Sheria za nchi zipo kwa kiingereza, lugha ya kufundishia kuanzia sekondari mpaka chuo kikuu ni kiingereza, sasa msomi inakuaje hakijua hiki kiingereza?
Cha kuandika anakijua ila kuongea anashindwa kwa sababu mdomo unaujauzito.
 
Kwani hao Wachina na Wahindi wanatumia Kiingereza kama lugha yao ya kufundishia? Wewe unaona ni sawa ufundishwe kwa lugha fulani zaidi ya miaka 20, uandike tasnifu 2 (Masters na Ph.D), uandike makala kwenye peer-reviewed journals mpaka uwe profesa, ufundishe na bado unafundisha kwa lugha hiyo hiyo...na bado uwe huwezi kuiongea vizuri hiyo lugha? Huoni kama hapo kuna tatizo kubwa?
Kwani lengo la kiingereza kutimika kufundishia hapa Tanzania ni nini?
Ni kwamba ili tujue kuongea kiingereza au kile kinachofundishwa kieleweke kwa wanaofundishwa.

Naomba jibu langu tafadhali.
 
Back
Top Bottom