Elimu yetu inabidi kutazamwa upya. Haiwezekani mtu ajiite Prof huku hajui kiingereza

Kiswahili ni lugha ambayo haitoshelezi ndio maana hatutumii kufundishia sekondari na chuo. Hata shule ya msingi tunafosi tu.
Basi acha tujifunze kwa hicho kiingereza cha kuokoteza kisha tuongee kiswahili chetu
 
Unaposema hajui english unakusudia hawezi kusoma english na kuelewa? Hawezi kuandika kwa english? Akisikia english haelewi? Hajui kuzungumza kabisa english?

Kama hayo yote ndio unakusudia basi hata mimi inanipa maswali maana kawezaje kufika levo hiyo ya elimu?
 
Hoja ipo hapa: kama lugha ya kusomea mashuleni kuanzia sekondari mpaka chuo kikuu ni kiingereza inakuwaje sasa mhitimu hajui kiingereza?

Ingekuwa tunasoma kwa kiswahili kuanzia msingi mpaka vyuo vikuu hapo sawa watu wasingejua kiingereza ingekuwa sawa tu.

China, Urusi, Germany nk lugha za kufundishia ni lugha zao, hawa hata wasipojua kiingereza sio issue maana ajira zipo za kutosha kwao na official language ni lugha zao.

Tanzania mtu anakwenda kwenye interview anakuta kiingereza, matangazo ya kazi ni ya kiingereza, Sheria za nchi zipo kwa kiingereza, lugha ya kufundishia kuanzia sekondari mpaka chuo kikuu ni kiingereza, sasa msomi inakuaje hakijua hiki kiingereza?
 

Tunajua sana kujustify ujinga tuliolishwa na sisiemu, leo hii ukitoka nje ya Tz utakuta watanzania wa kutafuta tena kwa shida kubwa na ni kwamba kwa sababu wanaogopa kusafiri kwa kuwa wanaogopa kuongea lugha za kigeni! Hatuna mchango wowote wa maana kwa dunia tangu iumbwe tunajustify uchawa tu eti Kiingereza sio kitu! Kiswahili kimetusaidia nini hadi sasa zaidi ya kupunguza usukuma na unyiramba tu! Huyo profesa wa kiswahili mwenyewe kafundishwa kiingereza hadi kapata PhD yake
 
Lugha ya dunia?

Dunia gani hiyo.

Hebu vuka uende tu hapo Burundi na Rwanda uone kama hicho kiingereza chako kina mashiko.
 
Kuna Clip inasambaa mitandaoni ikimuonesha prof Mmoja akiongea kiingerereza kibovu.

Tuwe serious na aliwahi kutokea jamaa mwingine aliyekua Dr huyu nae kiingereza alikuwa hajui kabisa.

Nina mashaka.
Sio lazima Profesa mtanzania kwamba alisoma Tanzania. Wengine walikulia na kusomea Russia su China
 
Kwahiyo shida ni nini yenye kufanya watanzania wasijue kiingereza?
 
Utakuwa wewe ndiye prof wa mchongo na kingereza chako cha hovyo

Mbona umepaniki kama siyo wewe?
 
Fafanua hajui vp? Kwa sababu shida ni kushindwa kuongea kiingereza kwa ufasaha ila ukisema kiujumla hajui kiingereza nabaki najiuliza aliwezaje kuelewa masomo yake?
 
Hoja ipo hapa: kama lugha ya kusomea mashuleni kuanzia sekondari mpaka chuo kikuu ni kiingereza inakuwaje sasa mhitimu hajui kiingereza?
Umesema kusoma au kusomea shuleni.

Kwani huyo profesa kakwambia hajui kusoma kiingereza?

Tofautisha kusoma, kuongea na kusikia kilugha. Hicho kiingereza ni kilugha cha wazungu wenye asili ya Uingereza

Mtu anaweza kujua kuongea lugha vizuri lakini asijue kuiandika na kusoma. Mfano mtu anongea kiswahili lakini ukimtumia sms kwenye simu hawezi kusoma.

Mtu anaweza akasoma na akaelewa na akakujibu vizuri tu kwa maandishi lakini linapokuja suala la kuongea hawezi kuongea kwa ufasaha ukaelewa.

Mtu anaweza kusikia na kuelewa unamaanisha nini ukiongea lakini kuongea hiyo lugha kwa ufasaha akashindwa.
 
MKUU KUNA CHAKUONGEA NA CHAKUANDIKA..VIP HAWEZI VYOTE AU KIMOJA? ANAWEZA AKAWA HAWEZI CHA KUONGEA ILA KWENYE KUANDIKA ANAPANGILIA VIZURI AU CHAKUANDIKA HAWEZI VIZURI ILA KUONGEA ANAWEZA..AU AKAWA HAWEZI VYOTE HAPA NDO PAKUMUHOJI VIZURI HUO UPROFESA KAUPAJE?
 
Kwahiyo shida ni nini yenye kufanya watanzania wasijue kiingereza?
Tujiulize wenyewe kuanzia form 1 hadi 6 then chuo kikuu bachelor then Masters halafu PHd na maresearch yake na ualimu halafu mtu anapata uprofesa, anakuja kubofoa halafu mtu akisema elimu yetu ina shida watu wanamshambulia hapa eti English is nothing, ingekua nothing kwa nini tunapoteza miaka yetu tunajifunza??? Huu ni umbuzi yani au unyani! Hao wachina wanajifunza miaka michache na kumaster na kuanza kupambana na UK na US sisi tuna shida gani?
 
Fafanua hajui vp? Kwa sababu shida ni kushindwa kuongea kiingereza kwa ufasaha ila ukisema kiujumla hajui kiingereza nabaki najiuliza aliwezaje kuelewa masomo yake?
Huyo mleta uzi hajui nini anaongea
 
Kiingereza ni lugha tu ila haina madhara kwa material yaliyomo kichwani. Msomi hata kama hajui kabisa kiingereza kazi yake itamtambulisha. Madaktari wa huko Cuba wote wanajua kiingereza? Wachina na warusi je?
 
Kwani hao Wachina na Wahindi wanatumia Kiingereza kama lugha yao ya kufundishia? Wewe unaona ni sawa ufundishwe kwa lugha fulani zaidi ya miaka 20, uandike tasnifu 2 (Masters na Ph.D), uandike makala kwenye peer-reviewed journals mpaka uwe profesa, ufundishe na bado unafundisha kwa lugha hiyo hiyo...na bado uwe huwezi kuiongea vizuri hiyo lugha? Huoni kama hapo kuna tatizo kubwa?
 
Kiingereza ni lugha tu ila haina madhara kwa material yaliyomo kichwani. Msomi hata kama hajui kabisa kiingereza kazi yake itamtambulisha. Madaktari wa huko Cuba wote wanajua kiingereza? Wachina na warusi je?

Sasa kama huo Udaktari kajifunzia Kwa lugha ya kiingereza anakuaje haijui hiyo lugha, alielewa vizuri kweli huko shule alichosomea Kwa kiingereza?

China na Cuba hawatumii kiingereza shuleni kama lugha ya kufundishia.
 
Watu wengi wanasahau kuwa kiingereza ni lugha na ndio maana hata usipoenda shule kabisa unaweza ukakiongea vizuri tu, nadhani tungeshangaana au kuchekana kwa upande wa kiingereza kama somo na sio kama lugha katika kukiongea.

Hii lugha ndio watu wanaitumia shuleni kuanzia sekondari mpaka vyuo vikuu, ndio lugha rasmi kwenye elimu yetu.

Sasa kama hawaielewi huko shuleni watakuwa wameelewa kweli walichofundishwa na hiyo lugha?
 
Kwahiyo maprofesa wote wa uingereza ni wataalamu wa kiingereza kwa sababu ndio lugha ya kufundishia kwao?
Hatuongelei utaalamu hapa. Tunaongelea competence ya kawaida tu. Unaijua process ya mtu mpaka kuwa profesa? Mbali na kusomeshwa katika Kiingereza kwa miaka zaidi ya 20, profesa huyu anafundisha kwa Kiingereza na kusimamia wanafunzi wa shahada mbalimbali kwa Kiingereza. Kwa nini ashindwe kuongea Kiingereza? Huko darasani huwa anafundishaje? Akienda kwenye makongamano na consultancy huwa anaongea lugha gani?

Tubadilisheni tu lugha tuanze kufundishana kwa Kiswahili maana Kiingereza kilishashindikana; lakini ni aibu kwa mtu aliyesomeshwa kwa Kiingereza, Kichina, Kikurya...kwa zaidi ya miaka 20 na anaitumia lugha hiyo kufundishia kushindwa kuiongea lugha hiyo kwa ufasaha.
 
Alikuja na mama yake..baba yake ni mmatumbi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…