Elon Musk azikosoa vikali ndege vita za F-35 na mradi mzima wa utengenezaji wa ndege hizo

Ni beef hilo Mzee siasa mchongo mchafu uzuri huko hutosikia Elon Musk katekwa na wasiojulikana watajulikana ndani ya nusu dakika
Hawawezi

Hata Pentagon ilishawahi kuwataka contractors wa F-35 waziboreshe hitilafu za hayo makopo hasa upande wa engine

Lakini Lockheed na wenzake wakapotezea kwa sababu ya gharama na wakati wamepiga vibunda vya maana kwenye huo mradi

Elon Musk amekuja kulifufua hilo suala. Pesa za walipa kodi wa Marekani zimeishia kwa defense contractors pockets
 
80% ya products za US ni overpriced kwakua kodi yao nikubwa kwenye materials
Licha ya hayo Marekani kuna upigaji sana ni vile wengi hawajui hasa huwa wanafanya cost plus contracts kwenye construction, defense n.k

Halafu kuna lobbying, non-profit projects

Pentagon kwa mwaka wa saba mfululizo wamefeli kwenye financial audit ndio ujue MIC (Military Industrial Complex) ya Marekani kuna upigaji

Kuna kipindi Pentagon audit waligundua kuwa Boeing wanai-overcharge Air Force wanapoiuzia parts au spare za madege yao makopo. Hebu imagine screw tu walipandisha bei kwa 10,000%
 
Hawawezi

Hata Pentagon ilishawahi kuwataka contractors wa F-35 waziboreshe hitilafu za hayo makopo hasa upande wa engine

Lakini Lockheed na wenzake wakapotezea kwa sababu ya gharama na wakati wamepiga vibunda vya maana kwenye huo mradi

Elon Musk amekuja kulifufua hilo suala. Pesa za walipa kodi wa Marekani zimeishia kwa defense contractors pockets
Defense contractors wa Marekani wameajiri Wamarekani milioni 2 na wanauza hisa zao katika masoko ya hisa ya Marekani.
 
Licha ya hayo Marekani kuna upigaji sana ni vile wengi hawajui hasa huwa wanafanya cost plus contracts kwenye construction, defense n.k

Halafu kuna lobbying, non-profit projects

Pentagon kwa mwaka wa saba mfululizo wamefeli kwenye financial audit ndio ujue MIC (Military Industry Complex) ya Marekani kuna upigaji

Kuna kipindi Pentagon audit waligundua kuwa Boeing wanaiovercharge Air Force wanapoiuzia parts au spare za madege yao makopo. Hebj imagine screw tu walipandisha bei kwa 10,000%
Defense contractors wa Marekani wameajiri Wamarekani milioni 2 na wanauza hisa zao katika masoko ya hisa ya Marekani.
 
Nilikua namueleza sana hili swahiba wangu T14 Armata kwamba F35 pale marekani kapuyanga narudia tena kumwambia katika ndege ambazo marekani kapotena basi ni hayo makopo hayo madege ni buuurree kabisaa ingawaje wamarekani wa jf watapingana mpaka na Elon
Unajua T14 Armata humwambii kitu kuhusu Marekani? Ukitaka jamaa akuandikie magazeti humu, basi mbishie kuhusu Amerika. Hapo lazima utalia tu. Nadhani anakula posho ndefu sana ya Joe na Kamala.
 
Unategemea asifie wakati anataka kandarasi hiyo hiyo? Lazima ajifanye kuonesha madhaifu ili awe considered. Wafanyabiashara sio wa kuamini when it comes kuwania kazi.
Kwa hiyo wote ni wajinga kwamba hawaoni ukweli wa hoja? Mbona mnaandika mambo kisongombingo sana nyie? As if mtu mwenye akili ni Musk pekee?

Anachofanya Musk kwa sasa katika kuonesha madhaifu, ni kupaza sauti ileile ambayo muda mrefu watu wakweli wamekuwa wakisema. Wala hajazungumza jambo jipya hapo.

Ndiyo maana tukawaambieni kwamba Marekani ilitamani vita hivi ili iuze silaha zake na pia kufanyia majaribio silaha zingine. Hapo bado sijatacha uchafu na ukatili wa kibinadamu unaoendelea Ukraine. Marekani kwa asili ni bepari mfanyabiashara. Lengo lake huwa ni moja tu - kujitanua na kutawala kwa gharama yoyote.
 
Umesema vyema

Ni vile wengi walikuwa wanaogopa kupaza sauti juu ya issue ya F-35 ni project ya hovyo sana yenye upigaji
 
Ndiyo maana tukawaambieni kwamba Marekani ilitamani vita hivi ili iuze silaha zake na pia kufanyia majaribio silaha zingine. Hapo bado sijatacha uchafu na ukatili wa kibinadamu unaoendelea Ukraine. Marekani kwa asili ni bepari mfanyabiashara. Lengo lake huwa ni moja tu - kujitanua na kutawala kwa gharama yoyote.
Urusi na Putin wamefanikisha lengo la Marekani?
 
Wachina nao walishatoa kama f35 kumuonyesha hazina uspesho wowote

1732562324385.png
 
Nilikua namueleza sana hili swahiba wangu T14 Armata kwamba F35 pale marekani kapuyanga narudia tena kumwambia katika ndege ambazo marekani kapotena basi ni hayo makopo hayo madege ni buuurree kabisaa ingawaje wamarekani wa jf watapingana mpaka na Elon
Nilikupa majibu kule ukakimbia. Sasa naona unataka tuanze upya wakati siku zote hujawahi kuonyesha ni wapi F-35 zinapoteza maana. Unatoa maoni kama watoa maoni wengine, huonyeshi how F-35 ni mbovu. Ninazo sababu chungu nzima za kuonyesha ubora wa F-35 huna hata sababu moja ya kuipinga.

Elon Musk sio Mungu kwamba kila wazo lake ni sahihi.
 
Unajua T14 Armata humwambii kitu kuhusu Marekani? Ukitaka jamaa akuandikie magazeti humu, basi mbishie kuhusu Amerika. Hapo lazima utalia tu. Nadhani anakula posho ndefu sana ya Joe na Kamala.
Wewe na ndugu yako ungana mseme F-35 ina ubaya gani na inazidiwa na 5th generation gani.

Badala ya ngonjera leta facts.
 
Back
Top Bottom