Elon Musk azikosoa vikali ndege vita za F-35 na mradi mzima wa utengenezaji wa ndege hizo

Marekani hataki watu wanunue silaha nje ya za kwake na ndio maana baada ya turkey kununua s4 kule Russia wakaanza kumpiga sana spana za kila namna walau kwa China anajua vikwazo kwake sio tatizo hao wengine hawawezi kuhimili vikwazo na ndio maana unaona kwa hila silaha za Russia zinapigwa kumbo na za Marekani mpaka leo Iran anashindwa kupewa silaha na Russia sababu ya vikwazo kadhaa kujitoa kwenye mradi ni mambo ya kawaida sana mbona hata Australia 🇦🇺 walijitoa kwenye mradi wa mabilioni ya dola ya nyambizi za ufaransa mpaka ukataka leta mgogoro wa kidiplomasia baina ya marekani na ufaransa au na wao Australia 🇦🇺 waliona kama hizo nyambizi hazina injini ndio maana wakajitoa
 
Hizo ndege za kichina siziongelei sababu siijui lolote kuzihusu kwahio usinihusishe nazo pia kwa F35 tunaongelea kuanguka kwake sio kua ndege zaidi ya 29 zilizo rekodiwa na ndege zaidi ya 21 zimeanguka mwaka mmoja F35 wajitathmini sana
 
Kinachozungumziwa ni F-35, wewe unataja F-15.

Wanajadili Mark X unataja Fuso. Wewe una akili?
typoo,
still hoja iko palepale, wewe unamzidi Elon kiufahamu kuhusu F-35?
unafahamu huyo ana clearance ya level gani huko pentagon?

kuna vitu vingine sio vya kujifanya mjuaji sana kuwazidi waliopo ndani.....
 
kumbe unaelewa sasa kwanini hayo madude wanauziana wenyewe NATO?

kiufupi silaha ni biashara, awe mrusi, mchina au us, wote wanafanya biashara!

US alichowazidi wenzake ni soko kubwa la silaha zake, ana NATO inanunua silaja zake hata kama 'mbovu' ikiwemo hiyo f-35, ana waarabu, korea, japan, ausie na NZ.... hata akiunda 'bomu' hao watanunua tu

ubora wa silaha usiupime kwa kuangalia nani kanunua, ipime uwanja wa vita!
 
Hapa ndiyo umetoa jibu technically kabisa nafikiri kuongeza au kupunguza itakuwa ni ukosefu.
 
Nishakupa sababu kwanini hawanunui, Ulaya hawawezi nunua Su-57 na haina injini. Su-57 probably haina bei ya kutisha wateja wakuu wa Urusi kama Misri, Algeria, India wanaimudu ila bado sio ndege ya kununua sio kamilifu.

Uwanja wa vita utaipimaje Su-57 na haiendi, angalau F-35 inafanya sorties. J-20 utaipimia wapi uwanja wa vita gani.

Kwa kipimo chenu cha uwanja wa vita ni ndege gani hapo mnayotetea imeenda vitani.

Utengeneze ndege mbovu ulalamike watu hawanunui kisa US ina wateja. Mbona Mig-21 ni ya Urusi ukouko na ndio 3rd generation fighter iliyouzwa zaidi karne ya 20.
 
T14 Armata
 
Ana hoja.

Asikilizwe
Hoja anaweza kuwa nayo.

Ila usisahau kuwa ni mfanyabiashara na kushiriki kwake kwa kampeni za Trump ni calculated move.

Hii kauli ni mwanzo wa kuvizia tenda za kutengeneza silaha.

Itakuwa ana projects zake anataka kuzipenyeza.
 
Haache dharau..........yeye mwenyewe hayo madude yake ya kwenda Mars yana impact gani kwa maisha ya sasa .........ikiwa mida sio mrefu atakuwa jivu eli mauti...........haya ndio Russia kareta vita huko marekani atachukua satellite yake akamzuie asilipue marekani.......huyu ni tajiri ila punguani kujifanya yeye ndio mwenye akili kuliko watu wengine........anajua hao Lockheed wamefanya miradi mingapi ya kuilinda marekani na yeye mwafrika mwenye rangi ya kidhungu??............kama hao Lockheed wasinge kuwa na project kali hata yeye asingetoka kwa wazulu kwenda kushangaa marekani .........hili ni tajiri jinga kabisa kuwahi kutokea hapa duniani
 
Alichosema ni cha kweli au kaisingizia Lockheed?
 
Na zote hizi mbili unazitaja zinatakiwa ziwe power ya J-35 ambayo ni ndege ya maonyesho. Lini J-35 imekabidhiwa jeshini ianze kutumika mpaka uanze taja injini zake ziko kazini?
Unataka J-35 izinduliwe mara ngapi?
 
Hamna anachojua kuwazidi wamarekani wenyewe kwanza yure muhamiaji tu.........ikipitishwa sera ya kurudi ulikotoka atakuwa hana tofauti na mange kimambi
Haujajibu swali
 
Mbona Lockheed kwenye kutengeneza engine ya F-35 waliwatumia contractors wengine kama Pratt & Whitney na kampuni nyingine zilihusika kama Rolls Royce, Hamilton na Woodward
 
Wewe unataka nijibuje ? Au unataka nijibu kama unavyotaka wewe ?maana umeuliza nimekujibu kwa nilivyoelewa au ulikuwa na jibu lako?? Liweke nione nimekosea wapi mkuu
Alichosema ni kweli au uongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…