Elon Musk azikosoa vikali ndege vita za F-35 na mradi mzima wa utengenezaji wa ndege hizo

Elon Musk azikosoa vikali ndege vita za F-35 na mradi mzima wa utengenezaji wa ndege hizo

Tangu lini Elon Musk amekuwa authority kwenye fighter planes? Kutengeneza rocket na kuwa tajiri No 1 duniani hakukufanyi wewe ujue kila kitu.
Vipi na Pentagon nao hawana authority walipoitaka Lockheed na BAE wafanyie maboresho ya engine? Elon kazungumza ukweli ambao idara ya ulinzi ya Marekani inafahamu
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Una project gani ya tech ambayo umeshawahi kui innovate hapa nchini !? Ambayo Ina kubalika kiwilaya tu Achana na ngazi ya kitaifa, kama Ipo basi utakuwa Una Haki ya kumkosoa guru wa tech Kwa sasa Elon musk lakini kama hauna Hiyo project basi utakuwa unatupigia makelele tu hapa

Kumbuka Elon ni public figure ana ushawishi mkubwa kidunia mpaka anaongea Jambo la kukosoa sekta ya tech katika Serikali ya nchi yake hawezi kuwa amekurupuka , Kama hata Hilo pia unalipinga Anza kujitafakari mkuu inaweza kuwa Umechanganyikiwa ila haujijui
Musk akisema uolewe utaolewa kisa ni public figure na ana ushawishi?

Aliyekuambia duniani majeshi yanaongozwa na public figures na wenye ushawishi nani?
 
Mimi sijamuiga musk sababu hili suala musk kaliongelea juzi na Jana ila mimi nimeliongelea miaka zaidi ya mitano nyuma huko

Kwahio musk kaiga madini tokea kwangu ujue hili kwahio inatakiwa useme mimi nikisema ndoa haifai musk na yeye atasema haifai ingawaje siwezi kukata kitu kama kipo bora lazima niseme hakuna mpaka sasa na nahisi itachukua miaka mingi sana kuja kutokea ndege vita bora kabisa duniani kama f22 achana na hayo makopo kopo yanayoanguka yenyewe yakiguswa na kware tu chini F35 hakuna ndege ni project ya hovyo sana
F-22 Lightning imetengenezwa na Lockheed Martin ikaruka 1997, F-35 Lightning II imetengenezwa na Lockheed Martin pia ikaruka 2006.

Kwa akili yako unaona kampuni ileile, inatoa mwendelezo wa bidhaa kwa kurudi nyuma kiteknolojia? Yani ndege bora zaidi iwe imetoka LM alafu ndege mbovu sana iwe imetoka LM tena, na iliifuatia ile bora?
 
🤣🤣🤣

Kwa hiyo umekubali kuwa hilo kopo la Lockheed lina changamoto kwenye engine? Na mpaka leo imewashinda kuboresha si ndio?

Maana ulikuwa unalipa sifa lisilostahili.

Twende mdogomdogo kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake

Kasoro ya pili ni upande wa software. Hilo kopo lina shida sana upande huo tena. Unakubali au unakataa na hapo?
Quote comment nzima usitafute kipande chako tu, ulipoquote kuna hizi hoja.

Na kwa upande wa software hakuna ndege ina software bora kuzidi F-35. KAMA IPO ITAJE NA UWEZO WAKE
1. Taja ndege isiyo na changamoto au kasoro. F-35 injini zake zina protective coating ya joto kali inayoisha haraka hiyo ndio kasoro kubwa.

Wakati unatutafutia ndege isiyo na kasoro ngoja nikupe kasoro ya ndege nyinginezo zinazoshindana na F-35.

2. Su-57 mpaka leo haina injini yake, kwahiyo hata matatizo ya injini bado hayajulikani na yatakuwepo tu. Miaka nenda rudi Warusi wanaunda injini na hawafikii breakthrough.
3. J-20 ilianza inatumia injini ya AL-31 ya Urusi inayoendesha Su-27 (ya miaka ya 1970s uko). Ikaja ikatumia WS-10C ambayo ina underperformance sana, ndio inaiendesha hadi sasa. Ikabidi Wachina waunde injini kwa ajili ya stealth yao, wakaja na injini WS-15 ambayo hadi sasa hawajatumia hivyo matatizo yake bado.

Ndugu Mchina, kopo la Kichina halina hata injini. Hustahili kuwa kwenye mjadala huu.
 
Nilikupa majibu kule ukakimbia. Sasa naona unataka tuanze upya wakati siku zote hujawahi kuonyesha ni wapi F-35 zinapoteza maana. Unatoa maoni kama watoa maoni wengine, huonyeshi how F-35 ni mbovu. Ninazo sababu chungu nzima za kuonyesha ubora wa F-35 huna hata sababu moja ya kuipinga.

Elon Musk sio Mungu kwamba kila wazo lake ni sahihi.
kwamba wewe unajua ubora wa f-15 kumzidi Elon, a US defence contractor ?
utakua na matatizo makubwa sana kichwani kama unadhani unauelewa wa masuala ya defence ya US kumzidi Elon......

endelea ku-google mkuu
 
F-22 Lightning imetengenezwa na Lockheed Martin ikaruka 1997, F-35 Lightning II imetengenezwa na Lockheed Martin pia ikaruka 2006.

Kwa akili yako unaona kampuni ileile, inatoa mwendelezo wa bidhaa kwa kurudi nyuma kiteknolojia? Yani ndege bora zaidi iwe imetoka LM alafu ndege mbovu sana iwe imetoka LM tena, na iliifuatia ile bora?
Hata Samsung kama sijakosea kwenye s4 walilalamikiwa sana masimu yana hit kama majiko watu wakawa wana prefer s2 ilotoka miaka miwili ama mitatu nyuma kuliko s4 ambazo kwa wakati ule zilikua ndio toleo jipya hapa nimekuonesha tu ujue kama kuna muda makampuni yanajitahidi kutoa kitu bora ila bahati mbaya yanajikuta kwa bahati mbaya yanapoteana hata MB ama gari gani pale German zilionekana zinashida ukilinganisha na matoleo ya nyuma pia hata boeing alikutana na hii shida zile 377 kama sijakosea zilionekana za mchongo mpaka zikazuiwa na nyingi zikarejeshwa viwandani kufanyiwa ukarabati f22 ndio ndege bora kuwahi kuzinduliwa na marekani na ndio maana hata kwenye mission mingi wanapeleka hizi ndege za 70s yrs sio kwasababu ya nini sababu ya ubora wake F35 majamaa wamejitahidi kuipamba kuitengeneza iwe best hatimae ndio wameharibu mwisho usikariri kama kitu kadri kinavyokuja na toleo jipya ndio kinakua na ubora utafeli kama unavyofeli kwa hizo F35 hivi ziliwahi piga mission wapi hizi kopo kopo ukiacha kupiga vikundi vya wanamgambo pale iraq na Syria
 
Vipi na Pentagon nao hawana authority walipoitaka Lockheed na BAE wafanyie maboresho ya engine? Elon kazungumza ukweli ambao idara ya ulinzi ya Marekani inafahamu
J-20 inafanyiwa maboresho mpaka leo. Mbona hujawahi sema ni mbovu? Hapa ilipo iko inatafutiwa injini ya 3😂

Su-57 inatumia injini ya Su-35 na hujawahi sema ni mbovu. Mpaka leo haina injini yake.
 
Hata Samsung kama sijakosea kwenye s4 walilalamikiwa sana masimu yana hit kama majiko watu wakawa wana prefer s2 ilotoka miaka miwili ama mitatu nyuma kuliko s4 ambazo kwa wakati ule zilikua ndio toleo jipya hapa nimekuonesha tu ujue kama kuna muda makampuni yanajitahidi kutoa kitu bora ila bahati mbaya yanajikuta kwa bahati mbaya yanapoteana hata MB ama gari gani pale German zilionekana zinashida ukilinganisha na matoleo ya nyuma pia hata boeing alikutana na hii shida zile 377 kama sijakosea zilionekana za mchongo mpaka zikazuiwa na nyingi zikarejeshwa viwandani kufanyiwa ukarabati f22 ndio ndege bora kuwahi kuzinduliwa na marekani na ndio maana hata kwenye mission mingi wanapeleka hizi ndege za 70s yrs sio kwasababu ya nini sababu ya ubora wake F35 majamaa wamejitahidi kuipamba kuitengeneza iwe best hatimae ndio wameharibu mwisho usikariri kama kitu kadri kinavyokuja na toleo jipya ndio kinakua na ubora utafeli kama unavyofeli kwa hizo F35 hivi ziliwahi piga mission wapi hizi kopo kopo ukiacha kupiga vikundi vya wanamgambo pale iraq na Syria
F-35 zimeuzwa Israel, Uingereza, Japan, South Korea, Australia, Italy, Canada, Singapore, Finland, Poland, Germany, Denmark, Uholanzi, Ugiriki.

Ina maana wote hao ni wapumbavu hawana akili wamekosa ndege za kununua wakanunua F-35 ambayo imepoteza kodi za Wamarekani. Unaikashifu ndege ambayo Uturuki walilia wasiondolewe kwenye mradi, wakabembeleza. Ndege ambayo mpaka sasa units zilizotengenezwa ni zaidi ya 1,000 ndani ya miaka michache na order ni nyingi mpaka Lockheed Martin wamezidiwa?

F-35 ilishindanishwa kwenye tenda za nchi kadhaa kama Finland hao ndio walikuwa wawazi kabisa. Haijawahi shindwa na ndege yeyote.

Unachekesha.
Niliwahi kukuuliza hapa ukakimbia. Ungejibu leo basi
 
Niliwahi kukuuliza hapa ukakimbia. Ungejibu leo basi
Eidha swali sikuliona ama nililijibu ila naomba nilijibu kwenye hayo mataifa ukiacha hizi ndege ambazo unasema wamezinunua marekani nitajie silaha gani nyengine kubwa wamezinunua tokea labda Russia ama uchina ukitoa turkey na s4 hao jamaa wanauziana silaha wao kwa wao kwa mfano kama nato memba ukinunua silaha nje ya hapa wanaanza kumplain mfano turkey baada ya kununua s4 kutokea Russia marekani wakakata mipango ya kumuuzia F35 kwa madai kwamba s4 itachunguza na kujua madhaifu ya F35 nk nk
 
Na kwa upande wa software hakuna ndege ina software bora kuzidi F-35. KAMA IPO ITAJE NA UWEZO WAKE
Hilo hapo kopo F-35 likianguka kwa sababu ya software issues. Halafu nikusikie ukibwabwaja tena eti hakuna ndege ina software bora zaidi ya F-35

Hapa Lockheed waliingiza chaka Pentagon

Endless comedy of errors 🤣

Eidha swali sikuliona ama nililijibu ila naomba nilijibu kwenye hayo mataifa ukiacha hizi ndege ambazo unasema wamezinunua marekani nitajie silaha gani nyengine kubwa wamezinunua tokea labda Russia ama uchina ukitoa turkey na s4 hao jamaa wanauziana silaha wao kwa wao kwa mfano kama nato memba ukinunua silaha nje ya hapa wanaanza kumplain mfano turkey baada ya kununua s4 kutokea Russia marekani wakakata mipango ya kumuuzia F35 kwa madai kwamba s4 itachunguza na kujua madhaifu ya F35 nk nk
Nitajie Urusi au China au North Korea imenunua silaha gani ya Western. Kwanini unataka Ulaya inunue silaha Urusi, na Urusi hainunui silaha Ulaya.

Ulaya wasiponunua F-35 kwa Urusi, watanunua stealth fighter gani. Su-57 haina injini, Ulaya watanunua ndege haina injini???

J-35 ni ndege ya maonyesho mpaka sasa hata Wachina hawana hata moja jeshini.

J-20 haiuzwi, sasa Ulaya watanunuaje ndege haiko sokoni.

Zilizobaki ni 4th generation ambazo sio za China au Urusi tu, hata Saab JAS 39 Gripen ya Sweden huwa inashindwa tenda ikikutana na F-35.

Rafale ya Ufaransa ina bei kuzidi F-35 ila sio stealth, Eurofighter Typhoon ina bei kuzidi F-35 ila sio stealth na inazidiwa sana tech.

Kwa upande wa Uturuki, AD systems na fighters inabidi zitambuane kwa IFF ili zisishambuliane. Hivyo kulikuwa na ulazima S-400 na F-35 zifungiwe mifumo ya kusomana jambo ambalo halitakiwi. Uturuki ilikuwa na crew ya Warusi ndio watafunga mifumo na ndio watakuwa wanasoma data. Iambie Urusi mifumo ya S-400 isomwe na NATO uone kama itakubali. Common sense tu
 
Back
Top Bottom