Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Embassy Hotel na Motel Agip: Nini hasa kilitokea?

Wakuu kuna mwenye taarifa nini kinaendelea juu ya hoteli hizi kongwe? Hali ya majengo inasikitisha sana,nini kinaendelea maana ni miaka mingi mno!
Mkuu swali zito sana hili. Ngoja tusubiri majibu, naamini kabisa kuna watu wanadata na watazimwaga hapa soon!
 
Laiti mngejua kinachoendelea behind the walls hii nchi inasikitisha sana halafu kila kukicha nashangaa sana watu wanaosifu na kuishangilia CCM

Kunduchi Beach Hotel hii ni kama vile mwekezaji alipewa bure, serikali ya Iran ilikuwa inaidai Tanzania kwahiyo the best way ikawa ni kuichukua hiyo hoteli kama kufidia deni lao, vitu vingine vinasikitisha sana.

Hotel Agip aliyepewa hii hotel nayo inatia mashaka sana maana (Yuko Serikalini)

Embassy Hotel kapewa muhindi kama ilivyokuwa kwa New Africa Hotel
 
Finest,kuna vitu vingi sana pasua kichwa juu ya hizi hoteli! Cha kushangaza wanahabari wetu hawachokonoi kujua ukweli! Wanasubiri habari za matukio!!
 
hali ya yale majengo ni mbaya mno,miaka mingi majengo yanaota nyasi tu,tungewapa wanafunzi wakazifanya hosteli basi,tena pale IFM wanapata tabu bure huku majengo yanaoza!
 
kuna Wawekezaji Wazawa walinunua Embassy Hotel but awana pesa ata za kumalizia deni na ata la kuwalipa mafao wafanyakazi wake.
ununuaji similar na ule wa UDA na Simon Group.

nadhani hawakupewa miaka 5 ya tax holiday, pia hawakuwafisadi vizuri ccm kama wabara hindi na arabia
 
Laiti mngejua kinachoendelea behind the walls hii nchi inasikitisha sana halafu kila kukicha nashangaa sana watu wanaosifu na kuishangilia CCM

Kunduchi Beach Hotel hii ni kama vile mwekezaji alipewa bure, serikali ya Iran ilikuwa inaidai Tanzania kwahiyo the best way ikawa ni kuichukua hiyo hoteli kama kufidia deni lao, vitu vingine vinasikitisha sana.

Hotel Agip aliyepewa hii hotel nayo inatia mashaka sana maana (Yuko Serikalini)

Embassy Hotel kapewa muhindi kama ilivyokuwa kwa New Africa Hotel

kwa nini wanagawa ambazo tayari zilizopo badala ya kuwaambia wawekezaji kujenga mpya
 
Hoteli ya Embassy hotel ni mali ya KJ Motors asilimia 80 na Kibo hotel asilimia 20.Walishanunua toka siku nyingi.Nilichosikia kuna kesi mahakamani walishindwa kulipa wafanyakazi waliokuwemo mafao yao.
 
Hao wawekezaji wazawa si wanaziona hizi hoteli na miradi mingine inayotaka rasilimali ? mbona hawajihusishi ? haya mambo hayataki pesa tu , pia uzoefu na uvumilivu - sio leo unawekeza - kesho unataka faida mara mbili.

Ghrama za Hoteli kwa mteja hapa Tanzania ni ghali sana kwa kodi sababu mbali mbali sinazotozwa kiasi cha kufanya hizi 5 star hotels hazileti faida.
 
Kuna muhindi alinunua pale then kukawa na kesi between partners. Ingelikuwa ni mimi ningezichukua kwa serikali hoteli hizi mbili
 
embassy hotel ilikuwa na mgogoro kati ya wafanyakazi na mmiliki, wafanyakazi wakafungua kesi, ambapo mahakama iliamuru walipwe mafao yao. Hivyo yeyote anaetaka kuendeleza (mnunuzi mpya) inabidi alipe hizo stahili kwanza (tzs bn??) sijui nani atapatikana kuinunua na kulipa hayo madeni.
 
Pole sana jamaa yangu,
Hotel zote mbili zilishauzwa kwa owner wa Kunduchi Beach Hotel anayejulikana kwa jina Gulam Hussein huyu jamaa ndo mwenye maduka ya nguo ya Gomez pamoja na kampuni ya rangi... kinachongojewa ni yeye kupata mwekeza mwenza kutoka kwao India. Vilevile kulikuwa na kesi ilifunguliwa na wafanyakazi wa Embassy Hotel ambayo mpaka sasa haijaisha.
 
Wakuu kuna mwenye taarifa nini kinaendelea juu ya hoteli hizi kongwe? Hali ya majengo inasikitisha sana,nini kinaendelea maana ni miaka mingi mno!

Mhhhh! Mie pale Motel Agip nilikuwa napapenda sana walikuwa na vyakula yaani vilikuwa vinatengezwa vizuri sana. Hata sijui kilichojiri mpaka ile hotel ikafungwa. Kila nikipita mitaa ile na kukuta lile jengo likiendelea kuoza inanisikitisha sana
 
Wakuu kuna mwenye taarifa nini kinaendelea juu ya hoteli hizi kongwe? Hali ya majengo inasikitisha sana,nini kinaendelea maana ni miaka mingi mno!

Zina gundu! hata wawekezaji hawazioni wanapita tu.
 
Kuna muhindi alinunua pale then kukawa na kesi between partners. Ingelikuwa ni mimi ningezichukua kwa serikali hoteli hizi mbili
Atatokea msanii mwenye lugha laini atazichukua kiulaini.
 
Finest,kuna vitu vingi sana pasua kichwa juu ya hizi hoteli! Cha kushangaza wanahabari wetu hawachokonoi kujua ukweli! Wanasubiri habari za matukio!!

Kama hujui waandishi wengi wa habari wananunuliwa ili kuandika/kutoandika habari fulani.
 
Nimekuwa naangalia jengo la iliyokuwa Embassy Hotel kwa muda mrefu sana sasa imefungwa na hakuna hata dalili yoyote ya kufufuliwa au kutumika kwa shughuli nyingine ya kibiashara.

Jengo lipo mahali pazuri sana lakini linasikitisha sana linavyochakaa na sina hakika kama linalipiwa kodo stahili kwa jiji. Kitendo cha kuliacha jengo hilo katika hali ile ni hasara kwa Taifa.

Nimejiuliza sana kuwa ni kitendawili cha aina gani hicho kimeshinda wakuu wote wa mkoa wa Dar-es salaam na mawaziri wa ardhi na mawaziri wakuu kwa muda mrefu kiasi hicho?

Kama kuna mwenye habari zozote kuhusu Embassy Hoteli na hili jengo kwa ujumla tunaomba atuwekee hapa.

Natanguliza shukrani zangu.
Nimeona wameshaanza kuizungushia uzio wa Mabati nadhani kuna ukarabati kwani wameziba hadi barabara upande mmoja
 
Back
Top Bottom