Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

Kwa mfano asingekuwa na mwitikio kabisa wa watu na akawa anasuasua, ungeuliza swali gani? Hivi kuna mtu anagombea kwa ajili ya kushindwa?
 
hao ccm watampigia kura Lisu kwani sera zake zimeeleweka kwa wote mpaka kwa uvccm, kwenye sanduku la kura ktk chumba cha siri magu anachinjiliwa mapema kabisa,Lisu ni mwamba anajua hoja za kisiasa,mbona hata magufuli anasema uchaguzi huu ccm itashinda au huko umeziba masikio kwa shibe husikii
 
Ndugu naomba utengue kauli yako Mimi sio mnufaika binafsi wa ccm Bali Mimi ni Kama wewe nanufaika na serekal ya ccm kwenye zile secta ambazo kila mtanzania ananufaika nazo kwa mfano barabara, hospital na huduma zingine za kijamii ila wanaufaika binafsi Ni hai wanao lipwa na sisiemu
 
Wanakwambia"watu wamelala barabarani ili Lissu asimame aongee wamsikie, kweli Lissu ni Rais", yani kwa watu kulala barabarani basi ndo kigezo cha Lissu kushinda urais.Chadema ndo matahira kweRi kweRi.
Lakini si tulishakubaliana kuwa upinzani ulishakufa? Sasa imekuwaje tena watu wanalala barabarani? Kulala kwao barabarani kunaashiria nini?
 
Maisha haya yalivyotuchapa awamu hii. Kweli mtu mzima unaenda kuipigia kura CCM. Bora umpe Lissu naimani ataleta na kuipitisha katiba mpya.
 
Ndugu na wewe unakubaliana na tume kuwa kuna waliojiandikisha 29Mil ??
yani kila kituo kina wapiga kura kati ya 300 to 400.
Hivi hawa watu 300 watatumia siku ngaoi kupiga kura kituo kimoja?
 
Kwa mjibu wa website ya CCM, na Kwa mjibu wa kauli ya mwenezi wa CCM ndugu Hamphuley Polepole, CCM inawanachama wa kudumu M.14+
Na kikawaida, ili uwe mwanachama wa Chama chochote, maana yake uwe umefikia umri wa miaka 18+
Polepole sisi ndio tulikuwa huko ila tulishatoka inaonekana hujui unachohesabu! Vilevile hesabu nyingi za hapo ni za 'kupika' ili kurahisisha ule 'mchezo wenu'
 
Kigezo ni kuwa chama chochote cha siasa kinachotambulika kina nafasi ya kuchukua uongozi kwa njia ya kura; hivyo lazima kiwe na imani hiyo. Vyama vingine vinatumia vigezo gani, ubwabwa maharage?
 
Lakini si tulishakubaliana kuwa upinzani ulishakufa? Sasa imekuwaje tena watu wanalala barabarani? Kulala kwao barabarani kunaashiria nini?
Hivi mtu mwenye akili anaweza kweli kulala barabarani,kama sio ujuha na sushamba?
upinzani haupo ushakufa waliopo ni waigizaji tu,upinzani ungekuwa hai ungeanza na tume wanayoilalamikia kila kukicha.
 
@mr mzumbe UMESAHAU KUWA MEAKA HUU TIGO FIESTA NA WASAFI FESTIVAL NI BURE KWA UDHAMIN WA CCM
 
wanaccm wengi moyoni ni wapinzani ingawa huvaa nguo za CCM usoni ili kulinda mali zao binafsi wasije kubambikiwa kesi na kuporwa mali zao
Kuna bro ni kada wa ccm sana juzi kaniambia dogo tafuta hela uwe mfanyabiashara ndo utajua ubaya wa serikali ya ccm hii, kaletewa kodi ya mwaka jana n tra milioni 34 kalipa,nw wanakuja tena eti anadaiwa milioni 20 bro kasanda
 
. Wewe ushabiki usikupeleke hivo mgombea wetu hashindi mwaka huu ila 2025 Njia nyeupe kabisa kwenda ikulu alafu mgombea wetu ameshapanic Sana yeye Hana Sera kabisa

Nije kwako wewe mwenzangu je wewe baba yako akinunua gari mpya nyumbani huwa unahoji? Kanunuaje? Kwa kipato kipi? Utagundua Lisu Hana uzalendo wowote
 
Wanakwambia"watu wamelala barabarani ili Lissu asimame aongee wamsikie, kweli Lissu ni Rais", yani kwa watu kulala barabarani basi ndo kigezo cha Lissu kushinda urais.Chadema ndo matahira kweRi kweRi.
Waliwahi kupiga deki lami hawawezi kushindwa kulala barabarani.
 
CCM

CCM wanaweza wakashinda lakini kwa wizi na dhulma.
Japo pia dhulma na wanaitengeza Mungu atawaangamiza kama Korona mana Mungu ameamua alipiganie taifa lake linalodhuliwa kutokana na upole,ujinga,umaskini unaotumiwa kama fimbo ya kuwaswaga watu wake huku waliodhulumu wakineemeka na dhulma zao hivyo kuwafanya watu wengi kutamani kujiunga na dhulma.
CCM kina kadi nyingi hewa mana wazee wengi ndio wanachama wa CCM . Wazee wengi wa umri wa Mkapa ndio wanachama wa CCM wasioyumba hata wakiona dhulma kubwa wanaisifia. Hao wengi wameshatangulia mbele za haki na wengine ni wagonjwa na uhakika wa kupiga kura hawana.
Lakini pia CCM kipindi hiki imepata wanachama wengi feki kama Alivyo Bashiru Ally , Mtatiro ,Ana Ngwira, Kafulila, Katambi, Nasari, na wengine wengi. Hao wangejua kuwa Lisu atarudi wasingejiunga na CCM . Hao adui yao alikua ni yule mlevi na Fisadi Mbowe aloyemleta Fisadi Lowasa.
CCM itapoteza kura nyingi sana kutoka kwa WanaCCM waliochoka siasa za kutishana ,kuuana ,kufitiniana, kukomoana, kudhulumiana, kuchafuana , kujipendekeza, kudhalilishana na kudharauliana .
Kura kwa Lisu , nyingi zitatoka kwa wale wanaojiita CCM lakini wapenda haki na usawa.
Kura nyingi kwa Lisu na Chadema zitatoka kwa watanzania wasiopenda kuona nchi hii inaingia kwenye ukabila wa wazi na kuona serikali ikiweka dini zote mfukoni kwake na kuwafanya watu wenye madaraka kuwa miungu ya kuabudiwa kwa sifa na shukrani huku wakipewa enzi na kutawala milele.

Kura nyingi zitatoka kwa wanaCCM wasiotaka kuona nchi hii inatawaliwa na mtu mmoja maisha yaani kuwa na Rais wa maisha eti kwa sababu amenunua ndege kwa kodi za wananchi.

Kura nyingi kwa Lisu zitatoka kwa Watanzania na wanachama wa CCM wasiopenda kuona ndugu zao na marafiki zao wanapigwa risasi na kupotea bila sababu ya msingi.

Kura nyingi kwa Lisu zitatoka Zanzibar kwa wanaCCM na Wana ACT .

Kura nyingi kwa Lisu zitatoka kwenye vijiji vilivyotengwa na kunyimwa mil.50 isipokuwa Chato pekee . Kura nyingi zitatoka kwa watanzania waliokos mgao wa Noah za makinikia.

Ni vita kati ya matajiri waliokwapua mali za umma na kujiuzia kila kitu mpaka nyumba za umma na sasa wanafanya kila hila kunakia madarakani huku wakitoa rushwa kwa tume na makada wengine wa CCM ndani ya vyombo vya dola.

Ushindi wa Chadema unaweza ukawa sio ndoto bali ni kweli.
Dhulma iondoke ili CCM ishinde au ishindwe kwa haki.
 
Wana CCM wengi watampa kura Lissu. Hata wao wanaccm vyuma vimewabana, kodi kubwa hata wao wanaccm inawatesa. Hata sukari bei ikifika 3000 na wao pia wanaathirika. Hata ukosefu wa ajira hauna ubaguzi hata wanaCCM wengi hawana ajira. Msimu huu kila Mtanzania pamoja na Mataga wote kura ni kwa Lissu.
 
Umejibu vizuri bila mihemko kama ya wenzio, lakini msijipe matumaini kuhusu hilo mkuu wana CCM wanakuwaga wamoja sana kwenye kipindi cha kampeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…