Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

CDM imetumia kigezo kipi kuwaengua wagombea zaidi ya 1000 wa Udiwani??
 
Hata wenyewe wanajua hicho ndio kitakachowaangusha, lakini ukiwaambia wanasema eti "safari hii watapata kura nyingi sana kutoka kwa wana CCM waliomchoka JPM" sijui wanatumia vigezo gani kujua kuwa wana CCM wamemchoka Magufuli
 
CDM imetumia kigezo kipi kuwaengua wagombea zaidi ya 1000 wa Udiwani??
Hawakujaza fomu Sawa na ilivyotakiwa ukilinganisha na wenzao ambapo kabla ya kuijaza fomu, CCM huandaa semina kuhusu kujaza fomu, ama kutumia usaidizi wa wanasheria wa Chama Chao kujaza fomu za uchaguzi
 
Si kila aliyemwana-CCM basi atakipigia kura chama chake (CCM). Wengine ni wana-CCM lakini kura zao kwa wapinzani.
Alafu hizo takwimu za uwingi wa wanachama kwa CCM zimekuwepo tangu na tangu, lakini HAKUNA Mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM aliyewahi zidi ushindi wa kishindo kwa zaidi ya 85%.
Ila kwa Mwaka huu naona twakimu za ushindi zilishatengenezwa ili kuweka record mpya kwa Magufuli kama ndiye "Alfa Na omega".
 
Mama Samia, waziri mkuu wanajaza hata kuliko Lissu. JPM ndio balaa, watu mpaka wanataka kubebena vichwani. Mbowe, chama chako bado hakijaiva aisee.
 
Wanakwambia"watu wamelala barabarani ili Lissu asimame aongee wamsikie, kweli Lissu ni Rais", yani kwa watu kulala barabarani basi ndo kigezo cha Lissu kushinda urais.Chadema ndo matahira kweRi kweRi.
2015, watu walilala mpaka nje, walideki barabara, ili kipenzi chao lowasa apite na bado mliambulia upepo na kuzungusha kote mikono kule. Watanzania watawapa fundisho la karne mpaka vichwa vyenu vizime data. JPM tano tena.
 
Kigezo cha ccm kujaza wanafunzi kwenye mikutano yao
 
Kigezo Cha kuhongwa bajaji, bodaboda, mikopo na nguo sehemu walipochagua upinzani hata wewe utachagua upinzani ili uendelee kulipwa kupondea upinzani.
 
Kwenye suala la uanachama wa ccm Mimi na watu kadhaa kwny familia yangu tunazo kadi za ccm lakini hatutoipia kura kwa jinsi ilivyotutenda direct kupitia mwanafamilia mmoja,Sasa jiulize wanachama kama Mimi wako wangapi kwa vigezo vya;
1.wenye watoto waliosoma na hawajaajiriwa
2.waliotumbuliwa vyeti feki
3.waliobomolewa nyumba zao
4.ndugu zao waliobambikiwa kesi na kufungwa
5.waliokatwa kura ya maoni hata baada ya kuongoza kura za maoni
6.watumishi ambao wamepokwa haki yao ya nyongeza ya mshahara wa kila mwezi na madaraja
Hao wote wana familia,ndugu,jamaa na marafiki wanaonufaika kupitia wao
##october tuna Jambo letu##
 
Shetani ni baba wa uwongo..14+ watoke wapi..wanatengeneza njia ya kuiba kura..pita mtaani waulize vijana kumi utapata jibu
 
Kigezo wanachotumia ni kile cha kawaida cha ubinadamu - KUJIPA MOYO NA MATUMAINI!
 
Research umefanya wapi kwamba CCM wamejiandikisha mimi naenda na napigia kura CHADEMA asubuhi na mapema
Mkuu, Embu Twende tu kimahesabu ya kawaida kabisa ya darasa la Saba

Fanya hivi, CCM inawanachama na wapiga Kura, wanaolipia uanachama wao Kwa mwaka ni watu 14m+

Okey, Fanya wale ambao wataasi kuipigia Kura CCM pamoja na wale wanachama haohao ambao hawakujiandikisha wawe idadi ya M.4+, maana yake, wale wanachama M.10 ndio wawe wamejiandikisha na ndio watakaoipigia Kura CCM, Kati ya wapiga Kura wote nchini 29m+

Maana yake idadi ya wanaobaki 19m+ ndio pengine kuna wanachama wa Chadema m6+ hivi mfano, nao sio wote watakuwa wamejiandikisha, na sio kwamba wote hakuna wataoisaliti Chadema,

Idadi inayobaki ya wanabakia ni 13m+, ndio hao Vyama vinaingia kuwashawishi ili wawapigie Kura wagombea hao

Sasa Fanya hivi tena, Kampeni za CCM Kwa siku moja pengine zinawafikia watu laki tano tu katika kila mkoa wanakofanyia Kampeni, kuanzia Mgombea Uraisi, waziri mkuu, wabunge na madiwani kote nchini

Chukua hiyo idadi uzidishe Kwa siku zote za uchaguzi, Utaona kwamba, CCM itakuwa imewafikia watu zaidi ya m.30+ ukiondoa idadi ya watu ambao Wapo kibindoni kuipigia Kura CCM hata wasposikia Sera za ccm, wale wanachama m.10 wa uhakika

Sasa utaona kwamba, Kati ya watu watakaofikiwa na CCM hao therathini M. Fanya tu Hesabu za kawaida kabisa, yaani useme tu, Kati ya hao, CCM iwashawishi wapigakura wapya M7+ Tu ,Kati ya wapiga kura ambao hawako CCM Wala Chadema

Utaona kwamba, tayari CCM itakuwa inajumla ya idadi za Kura zisizopungua M17+ Kati ya wapiga Kura wote M29+, idadi ya wapiga Kura waliobaki ambao Chadema na Vyama vingine vitawashawishi ni M6+ Baada ya kuwaondoa wanachama wa kudumu wa CCM ambao ni M10, na Chadema wanachama M6


Huoni kwamba CCM itakuwa na idadi nyiiingi za Kura M17+ isiyofikiwa na Chama chochote?
 
Yani kabisa unamsikiliza huyo polepole aka alsahaf wa cxm?
 
Nilipoona tu hapo kuwa CCM ina wanachama 14m+ nikajua bandiko lote ni upuuzi mtupu. Magufuli ni bingwa wa kupika data, nakumbuka ule utapeli wake wa kutaja idadi ya samaki na mayai yake wakati akiwa waziri. Uhuni wa kitoto ile mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…