Uchaguzi 2020 Embu tuambizane ukweli, CHADEMA inatumia kigezo gani kusema itashinda?

Yani kabisa unamsikiliza huyo polepole aka alsahaf wa cxm?

Ahaaaa ahaaaa, halafu unakuta kuna watu wana notebook kabisa wakate Polepole anaongea eti wanachukua pointi!
 
Umejibu vizuri bila mihemko kama ya wenzio, lakini msijipe matumaini kuhusu hilo mkuu wana CCM wanakuwaga wamoja sana kwenye kipindi cha kampeni
Huo umoja ni wakinafiki 2 cz wanajua wasiposapoti baada ya uchaguzi wanaweza kutengwa na chama wasipate fursa za kijamii like ajira za watoto wao, vimikopo etc ila ndani ya mioyo yao wamekata tamaa na chama
 
Nilipoona tu hapo kuwa ccm ina wanachama 14m+ nikajua bandiko lote ni upuuzi mtupu. Magufuli ni bingwa wa kupika data, nakumbuka ule utapeli wake wa kutaja idadi ya samaki na mayai yake wakati akiwa waziri. Uhuni wa kitoto ile mbaya.
Mkuu tupe data, chadema inatumia kihezo gani kwamba itashinda urais?
 
Nilipoona tu hapo kuwa ccm ina wanachama 14m+ nikajua bandiko lote ni upuuzi mtupu. Magufuli ni bingwa wa kupika data, nakumbuka ule utapeli wake wa kutaja idadi ya samaki na mayai yake wakati akiwa waziri. Uhuni wa kitoto ile mbaya.
Kuna vijana waliamini zile namba asee. Samaki milioni 123.9,mayai milioni 700, ndege bilioni 3, ng'ombe, mbuzi kuku,bata milion 986
 
Kuna vijana waliamini zile namba asee. Samaki milioni 123.9,mayai milioni 700, ndege bilioni 3, ng'ombe, mbuzi kuku,bata milion 986

😁😁😁, Magufuli kweli alikuwa anatumia sisi ni vilaza wenzake.
 
Mkuu tupe data, chadema inatumia kihezo gani kwamba itashinda urais?
Kwa uhalisia tu kama Magufuli kaharibu kwa wakulima, wafanyabiashara, vijana na wafanyakazi ambayo ndo makundi makuu yaliyopo nchini Je kuna haja ya kuuliza kwa vigezo gani CHADEMA itashinda mwaka huu??
 
 
Hali ngumu ya maisha mitaani kwa sasa wakati tuna uchumi wa kati
 
Kwa uhalisia tu kama magufuli kaharibu kwa wakulima, wafanyabiashara, vijana na wafanyakazi ambayo ndo Makundi makuu yaliyopo nchini Je kuna haja ya kuuliza kwa vigezo gani Chadema itashinda mwaka huu??
Je, CHADEMA tangu kisajiriwe, viongozi wake wamefanya nini la kitaifa, ili waaminiwe kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii? Hao viongozi wapinga kila kitu? Hao viongozi wanaotafuta madaraka kwa lugha ya hadaa na kufitinisha Serikali na wananchi? Ati "Uhuru na Haki"?

Wapi sauti ya maskini husikika au kusikilizwa? Km mke tajiri hamsikilizi mme maskini, au mme tajiri humfanya mje kijakazi. Huo ndiyo uhalisia katika maisha. Mwenye nguvu mpishe.

Tunahitaji maendeleo ili kila mwananchi awe na nguvu kiuchumi. Ikifikia hapo, sauti ya kila Mtanzania itasikika au kusikilizwa.

WATANZANIA HAWADANGANYIKI, ila fisi wa madaraka watasubiri sana huo mkono wa madaraka udondoke wanyang'anyane. Na kama hujui, huko CHADEMA ni mashindano na mvurugano kuwa karibu na mgombea Urais wakiamini ndoto ya utawala wa nchi hii itakuwa kweli
 
Kwani TANU kabla ya Uhuru ilifanya nini hadi watanzania wakaiamini kwenye kuipa uongozi???

Maendeleo yapi unayasema wakati Magufuli alikuta sukari inauzwa 1800 saivi tunanunua 2800-3000??
 





Usibishane na vichaa! Majani ya Arusha yapo kochwani
 
Ukweli ni kuwa hakuna mwenye asilimia 100 ya kushinda au kushindwa; na ndiyo maana ya uchaguzi. Idadi ya wanachama si kigezo kikubwa sana maana hiyo idadi kuna wanachama hewa, pia hiyo idadi anaitamka yeye; unafikiri atasema ana wanachama milioni moja!!. Pia si lazima kila mwanachama wako akupigie kura, maana kuna watu wengine wana kadi za chamacha (iwe CHADEMA au CCM) kimkakati tu.
Utakumbuka kuna mtu aliwahi kusema ukitaka biashara yako ishamiri pandisha bendera!
 
Kwani TANU kabla ya Uhuru ilifanya nini hadi watanzania wakaiamini kwenye kuipa uongozi???

Maendeleo yapi unayasema wakati Magufuli alikuta sukari inauzwa 1800 saivi tunanunua 2800-3000??
Kwa majibu ya aina hiyo najiuliza kiwango cha uwezo wako wa kuchambua masuala. Unadokoa vijimambo visivyo hoja.

Kama hujui, basi nikwambie umaskini wetu ndio unatufanya tusiwe na sauti juu ya bei ya bidhaa na mazao yetu vivyo hivyo kwa bidhaa tusizozalisha.

Unajua fika kuwa tajiri haguswi. Uhuru na Haki za maskini hukanyagwa na tajiri. Lakini Mgombea Urais unayemsujudu anahubiri Uhuru na Haki wakati akitaka nchi iendelee kuwa tegemezi, nawe unaona hiyo ndiyo Sera.

Upumbavu na Ulofa uliokubuhu
 
Unajua sababu ya bei ya sukari kupanda kutoka 1800-2800/3000 ilikuwa nini???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…