Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Mheshimiwa Rais kasema tutumie akili zaidi kuliko nguvu kwenye kukusanya kodi, hilo lina tatizo kwako?! Anajua umuhimu wa kodi na haja sema zisikusanywe, nadhani tuendelee kuchapa kazi!
Kama una uhakika alisema hivyo, kwanini aseme uamuzi wake utasababisha mapato yapungue kwa miezi mwili au mitatu halafu tutakaa sawa. Tokea lini kuongeza wigo wa kodi kukapunguza mapato? Tukubali hapa mama kaingia kwenye mtego.
 
Nani kakwambia taifa halikusanyi kodi?
 
Moja naamini wewe sio mfanyabiashara ingekuwa kwene hii tasnia ungeelewa Nini maana ya Kodi ya dhulma wakati wa magufuli Kodi ya dhulma ilitawala, ndo Yale mtu kapewa tax clearance unakuja baada ya miaka mitano alete mahesabu ya miaka 10 wakati taasisi hyohyo impa clearence certificate...sikumbuki Kama Kuna awamu hii nchi iliacha kukusanya Kodi, wafanyabiashara wapo tayar kulipa Kodi ila watozwe kihalali kulingana na uwezo wao kitedha kihalali mbona wakati wa JK kulikuwa hamna bugudha nyingi pamoja na Kodi ilikuwa inapotea kwa rushwa za watendaji wa tra lakini Kodi ilikusanywa
 
Kama una uhakika alisema hivyo, kwanini aseme uamuzi wake utasababisha mapato yapungue kwa miezi mwili au mitatu halafu tutakaa sawa. Tokea lini kuongeza wigo wa kodi kukapunguza mapato? Tukubali hapa mama kaingia kwenye mtego.
Mama anataka atengeneze mfumo wa ulipaji Kodi mzuri na sio kutengeneza ukamuaji wa walipa Kodi kwa maslahi ya miradi wakati ur killing ur own people mbona Kuna nchi SA,Botswana wako mbali Sana angalia walivo namifumo mizuri yaulipa Kodi hukuti ubabe wakijinga Kama wanaofanya tra asa kwene awamu ya tano.....mama anataka atengeneze mfumo dhabiti wa walipa Kodi kwa moyo na kihalali
 
Hivi unapomgundua mtu alikua anakwepa kodi unatakiwa kumfanya nn? Hakuna nchi iliyoendelea inacheza na kodi wala kuchekeana na wafanyabiashara. Acheni ujinga, hii nchi tusipoangalia tutarudi tulipotoka. Mabarabara, miundombinu ilijengwa kila kona kwasbbu ya hizi kodi. Watanzania hatuna Shukrani
 
Kama una uhakika alisema hivyo, kwanini aseme uamuzi wake utasababisha mapato yapungue kwa miezi mwili au mitatu halafu tutakaa sawa. Tokea lini kuongeza wigo wa kodi kukapunguza mapato? Tukubali hapa mama kaingia kwenye mtego.
Yes kwa miezi michache itapungua kwasabab tra kawakataza kwenda kuwafungua watu account zao na kukwapua hela, kakataza kwenda kutishia case za uhujumu uchumi ili mtu aogope na atoe hela atakama anaonewa...unahisi mama hayo ayajui ww unayajua zaidi huyu mama kawa makamu wa raisi kwa miaka 6 anajua matatizo yte na namna ilivokuwa hata zaidi yako wewe
 
unajitekenya pumbavu ni mfanyabiashara gani atalipa kodi kwa kubembelezana
Wakati wa kikwete Kodi ilikuwa haikusanywi na ilikuwa inakusanywa vipi,wakati wa mkapa je? Yani njoo nikwambie wafanyabiashara Kodi watalipa tu ila tu mfumo wakulipa Kodi uwe huru na amani wakati wa jpm kulikuwa Kuna mambo yakijinga Sana ya tra ili mradi tu wa meet target walikuwa wanakamua wananchi..sio Siri Kodi wakati wa jpm ilikuwa inapanda kwasababu almost parefu haikuwa ya halali watu wanatishia kufunguliwa case, mtu ulipewa tax clearance leo baada ya mwaka unaitwa unaambiwa unadaiwa mil 400 haha tuseme ukweli maguful hakutaka kutengeneza mfumo wa ulipaji Kodi Tanzania ila alitaka hela ipatikane kwa namna yyte ile private sector wakati wa jpm ilidrop sana
 
Hatuhitaji fedha za kujenga chato tena fedha zitakazokusanywa zitatosha.
 
Umewaza vyema kabisa.
 
unapo mgundua mtu halipi kodi sheria ziko wazi nn kifanyike. TRA wanafahamu hili.
mama hajasema watu amabao hawalipi kodi waachwe hapana.
walipe kodi kwa haki na kwa sheria.

unless unajarib kusema sheria za ukusanyaji kido ni weak.
 
Ndio maana rais SSH katoa agizo wakaongeze wigo wa ukusanyaji kodi...kwa ustaarabu
Hakuna kodi ya ustaarabu dunia yote, bali kuna muda inabidi ubanane nao walipa kodi ingawa inatakiwa kujua hali halisi ya mlipa kodi kabla ya kumchukulia hatua.
 
Tutakopa. Deni letu bado ni stahimilivu.
 
Kwani nani kasema tusikusanye kodi? TRA wameambiwa waweke mazingira rafiki ya kuwafanya wafanya biashara waliokimbia nchi warudi ili walipe kodi. Waliopo wasinyanyaswe ili walipe kodi vizuri. Kwa sasa kodi inayokusanywa ni ndogo sana ndiyo maana mama analalamika. Hana hela zakutosha kuendesha nchi.
 
Kodi itakusanywa lakini si kodi kandamizi. Kodi kandamizi huua biashara.
 
Tutapata wapi pesa za kununua v8 na waunga juhudi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…