Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi, tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Tutaenda kumpigia goti mzungu.

Ndio hapo tutapewa condition za ndoa ya jinsia moko.
 
Ni hivi ndugu:-
  1. Ni wapi Rais amesema hatokusanya kodi (kwa wingi) ?
  2. Tumeona TRA wamepewa target angalau wafikie TZS 2 Trillion kwa mwezi. Na hili limesisitizwa pia na Makamu wa Rais.
  3. Maagizo ya Rais ni kwamba kodi halali ikusanywe na sio kodi yenye mwelekeo wa dhuluma.
  4. Pia Rais alitoa maelekezo kwa TRA chini ya Wizara ya Fedha kuongeza wigo wa walipa kodi. Maana yake ni kuwa hii itapelekea idadi ya walipa kodi kuongozeka na hivyo kupanda kwa makusanyo ya serikali yanayotokana na kodi.
  5. Mwelekeo wa ukusanyaji wa kodi zisizo na dhuluma utaongeza imani ya wafantabiashara kwa serikali na kufanya biashara ziendelee kukua tofauti na kipindi cha nyuma ambacho watu walifunga biashara zao kutokana na harassments za ukusanyaji kodi.
  6. Sambamba na kipengele (5); approach anayoitaka Rasis kuhusiana na ukusanyaji kodi itavutia wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini.
Tuache kupiga ramli chonganishi zenye mwelekeo wa kumchonganisha Rais na wananchi/wafanyabiashara na kutaka kumwonyesha kama vile hana uwezo wa kuongoza.

Hii ni awamu na kipindi kipya; hivyo hamna budi kulikubali hilo.
 
Aliyekwambia kodi hazitakusanywa nani? mama atakachofanya atazuia pesa kwenda kwenye mamiradi yenu ya kipigaji kama ndege zinazotengeneza hasara, daraja la busisi, SGR, stiglaz hadi hapo upembuzi utakapofanyika upya tupate value for money.....
 
Nakumatt Imefunga takribani 80% ya shopping malls zake Kenya, je serikali ya Kenyatta pia wana chukua pesa za wafanya biashara katika account zao? hii nadharia ya kusema biashara Zilifungwa kwa sababu serikali kushika account za wafanya biashara ni uongo tena wa asubuhi, kusema Kodi ni kubwa pia ni fiksi nyingine kwani kama ni income 30% ni ile ile toka Enzo za mkapa .

Ulipaji wa Kodi kwa wafanya biashara wengi humu Wanaongea hata hawajui, wafanya biashara wengi wana uelewa mdogo Kahuku ulipaji wa kodi hapo ndipo kuna shida, binafsi TRA pia ni wazembe kutoa elimu hii na kuwa elimisha wafanya biashara jinsi ya kulipa kodi.

TRA iwaelimishe wananchi jinsi kodi Inavyopatikana na kukatwa katika biashara zao
 
Aliyekwambia kodi hazitakusanywa nani? mama atakachofanya atazuia pesa kwenda kwenye mamiradi yenu ya kipigaji kama ndege zinazotengeneza hasara, daraja la busisi, SGR, stiglaz hadi hapo upembuzi utakapofanyika upya tupate value for money.....
SGR haina faida?

Na mama mwaka huu anaanza ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Msalato
 
Naona makonda, musiba, jerry muro na sabaya pamoja na wahuni wenzenu mmejipanga kumkwamisha mama asitekeleze majukumu yake kwa kupotosha ukweli kuwa uwongo.

Hamta weza nchi sasa imepata Rais wa kweli. Nyie tulieni tu.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Sasa nani amekataa kodi isikusanywe. Watu wengine mbona akili kama hazipo vile?
 
Endapo hatutokusanya kodi kwa wingi Je tutapata wapi fedha za kuendeshea nchi?

Mfano naomba mnisaidie maswali haya...
Kodi ni wajibu wetu kuilipa. Ila kodi stahiki. Tusidhulumu watu kwa jina la kukusanya kodi
 
Duniani kote pale mheshimiwa rais nchi ili iweze kujiendesha lazima ikusanye kodi kwanamna yoyote ile kodi ilikuwepo tangu zama za mitume...
Umedanganywa na kulishwa tango pori. Ni heri kuwa na mfanyabiashara anaelipa nusu ya kodi kuliko kukosa anaelipa hata robo ya kodi. Mfanyabiashara anatoa ajira na kulipa mishahara kwa aliowaajiri.

Walioajiriwa wanalioa kodi ya mapato na kununua bidhaa zenye kodi kama VAT na kurudi Serikalini. Hivyo kuna kodi za moja kwa moja na kodi zilizojificha kutoka kwa muwekezaji.
 
Back
Top Bottom