Endapo kuna mtu au kikundi cha watu kipo juu ya Sheria na Katiba, basi Taifa halipo huru

Hata chama kikiwa na mtu au kikund kipo juu ya sheria basi ni majanga
 
Hakuna ukweli zaidi ya propaganda. Na Mungu atupatie uzima, tutawataja tu wote ambao mko responsible pale Taifa litakapofikia.
Uzuri wa Mungu, anaona kilicho ndani ya mioyo ya waja wake, hivyo Mungu atasimama nao.



Better be safe than sorry,
Bora upige magoti, unyenyekee na kuishi utumwani, ukiwa hai, kuliko kushangiliwa na umati wa watu kwa kuitwa shujaa, marehemu, alikufa kishujaa!.

Between life and death, I've chosen life, to keep living.

P
 

Masikini
Pole sana Pascal
Hebu badili ID uwe huru zaidi.
Sisi hatuna shaka hata kidogo na Intellectual prowess yako, ila sasa unapoipindisha huko utumwani uliko unaidhulumu sana Intelect yako. Ni kweli unaweza kutafuta shibe ya mwili kwa kukubali utumwa na ukashiba kuuponya mwili, lakini sasa Intellect yako itazidi kudhoofika na kukonda kwa sababu unalazimisha ile chakula kisicho chake na unainyima uhuru wa fikra sahihi!!!.
Sasa basi, badiili ID uje anonymous Umkome Nyani giladi kama zamani kwa uhuru mpana.
Achana na hawa madhalimu wasio na haya wala aibu, ni makaburu tu, ila weusi wenzetu
 

Watu wauvu ukawia kufa
 
Mungu au aubadili moyo wako na wengine kama wewe, ili Taifa lipone. Otherwise, we’re doomed for failure.
 
Watu wauvu ukawia kufa
True, na wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana!.
P
 
 
Usishiriki uovu, utakuja kujuta kwasababu ya taaluma yako.
 
Hata chama kikiwa na mtu au kikund kipo juu ya sheria basi ni majanga
Utakuwa huelewi mambo. Katiba ya nchi inatosha. Huko kwenye vyama mtajuana wenyewe.

Katiba ya wananchi haijali kuhusu chama kinachoingoza nchi kwa wakati huo, ukileta ya kwenye vyama kama ni kinyume na katiba ya nchi, unasukumiwa ndani!

Wananchi wengi mmekosa maarifa, na Hilo litaliangamiza Taifa moja kwa moja.
 
Watu wema ufa mapema sababu Mungu uona Kama akiwaacha watatenda dhambi.Watu waovu waovu uchelewa kufa Mungu uwaacha uenda watatubu but wengi uzidi kuwa waovu Zaid
 
Mungu au aubadili moyo wako na wengine kama wewe, ili Taifa lipone. Otherwise, we’re doomed for failure.
Duh...!, hunitakii mema!, yaani unataka niendeleze ushujaa na kushangiliwa jf, halafu nimfuate Ben na Azory?, huku nyuma ibaki tuu kumbukumbu
"Tunamkumbuka sana Pasco wa JF..." and then what?.

Tanzania tuko kwenye vita vya ukombozi wa pili wa nchi yetu!. Kwenye vita hii, tuna wapiganaji mashujaa walioko mstari wa mbele wa mapambano, ambao wao kazi yao ni kupigana tuu, no matter what!. Na kuna wapiganaji makini ambao hawaamua kupigana pale tuu kwenye uhakika wa possibility ya kushinda vita!, lakini kundi kubwa zaidi ni kundi la watazamaji!. Hawa ndio determinant ya kundi lipi lishinde hii vita kwa sababu ushindi wa vita unaitegemea support ya hawa watazamaji na sio nguvu ya jeshi la adui!.

Wapiganaji Shupavu, Shujaa!.
Ndani ya vita hii kuna wapiganaji shupavu, hawa ni wale waliodhamiria kuingia vitani, na ni kweli wameingia vitani, na sasa wako vitani kupigana kufa na kupona, kuikomboa nchi yetu!. Wanapigana kwa ari kubwa huku "motto" yao ni "fight fight fight no matter what!", "no retreat!, no surrender!", hawa watapigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike, hata kama wanajua kabisa kuwa hawatashinda vita hii, na watashindwa tuu kutokana na kuwa na jeshi dogo na silaha duni kuliko adui yao, lakini wataendelea kupigana tuu, na mwisho wa siku, watashindwa and all will be wiped!, ila watakuwa declared "mashujaa wa ukombozi wa taifa" na majina yao, yataandikwa na kumbukwa milele!. Hawa ndio kina Ben Saanane, Wangwe, Mchungaji Mtikila, Azory Gwanda, etc.

Wapiganaji Makini!.
Wapiganaji makini, hawaingii vitani mpaka kwanza wajue nguvu ya jeshi la adui!, na wakijipima na nguvu yao, wanaamua kutopeleka kwanza majeshi vitani ili kuepuka a loosing battle!, yaani kushindwa!, hawa formula yao ni "never fight a loosing battle", na wakiwa kwenye uwanja wa mapambano, wakiona dalili za kushindwa, kuliko kuendelea kupigana na kushindwa, yaani just to fight na kuwa wiped out, watarudi nyuma, retreat, kwenda kujijenga upya, mpaka wawe na nguvu ya kutosha to hit back and win, or baada ya majaribio kadhaa ya kushindwa, then wanaamua to surrender kwa kanuni ya "if you can't beat them, join them" and learn their secrets of battlefields" kinachowafanya washinde!. Hawa watazomewa ni waoga, wanarudi nyuma!, wanakimbia vita!, That is me!, mimi niko kwenye kundi hili!.

Wengi wa wapinzani Tanzania ni wapiganaji mashujaa so does wengi wa wana jf, mimi ni miongoni mwa wale wachache tunaosema ukweli huu mchungu bila kumung'unya maneno, ili angalau watusikie, sometimes tunalazimika kutumia maneno makali kama hili la "ignorant!' tunaowaambia kuwa, upinzani Tanzania, bado sana!, kuliko kujiunga na upinzani, ni bora kusimama tuu na kuangalia kuepuka kupoteza muda!, hata kwenye urais wa 2025 ni CCM tena!, simply kwa sababu wapinzani bado hawajawa tayari kushika dola, au kutawala!, vyama vya upinzani Tanzania bado ni vyama vya kianaharakati wa ukombozi badala ya wanamikakati ya kutawala!. Wapinzani wakiambiwa ukweli huu mchungu, wanakasirika!, mimi nitaendelea kuusema ukweli huu mchungu no matter what, kwa sababu ndio ukweli wenyewe halisi!, kwenye urais 2025, wapinzani sio bado, bali ni hakuna kabisa wamekuwa wiped out!.

Kwenye makundi haya ya wapiganaji, wapo wana CCM ambao wao ni wapiganaji mashujaa, wako tayari kuifia CCM no matter what, ili CCM iendelee kutawala Tanzania milele, hata kama ni kwa kutumia rushwa, ufisadi na kila mbinu chafu ili kuendelea kutawala, watabariki mbinu hizi, ndio maana 2005 EPA kupitia kampuni ya Kagoda, ilitumika kuipatia CCM ushindi wa kishindo!.

Lakini ndani ya CCM hiyo hiyo, ndani yake wapo wapiganaji makini wachache ambao hawa ni kiukweli kabisa, wanakerwa umasikini wa taifa letu, wanakerwa na rushwa na ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM na viongozi wake!, hawa wanakerwa na madudu yanayofanywa na mawaziri wa JK ndio maana walidiriki kuwasema wazi wazi mchana kweupe tena kwenye kadamnasi ya watu, kuwa kina fulani na fulani ni mawaziri mizigo!, au fulani na fulani ni mafisadi, waondoke ndani ya chama chetu kwa kujivua gamba!, wawajibike!. Hawa Wanataka hata kama CCM itaendelea kushinda, ushinde kwa kuchaguliwa kwa haki na uhalali na Watanzania na sio ushinde kwa mbinu chafu!.

Na kwenye upinzani pia wapo wapinzani ambao ni wapigani shupavu, wao target yao ni Ikulu tuu, hata kama wanajua hawana askari wa kutosha kuwafikisha ikulu, wao ni kupigana tuu kuelekea ikulu hata kama wataishia njiani, ndoto yao ni ikulu tuu!.

Ndani ya upinzani, pia wako wapiganaji makini ambao tayari wameishajua mbinu zinazotumiwa na wapinzani haziwezi kuwapa ushindi wa vita hii!, wamegundua udhaifu wa makamanda wao, silaha zao duni na mbinu hafifu za medani zinazotumiwa na viongozi wao wachovu, haziwezi kuwaletea ushindi!, wamejaribu kuhamasisha mageuzi ya ndani, (internal reforms) ndani ya vyama vyao ili vyama vyao viongozwe na majemedari wa vita wenye uwezo wa kutumia mbinu zakisasa za medani, wameishia kuzomewa, kuitwa wasaliti na wengine kuhukumiwa vifo!. Hawa watafika mahali watakatishwa tamaa na upinzani, na mtawashuhudia wakirejea CCM, katika ile falsafa ya "if you cant beat them, join them".

Mimi nimechagua kuwa join, niko nao, ni mmoja wao!.

P
 
Usishiriki uovu, utakuja kujuta kwasababu ya taaluma yako.
When the law in use is the law of the jungle, then there are two options only, exist or extinct!. In order to survive, one has to struggle for existence, survival is for the fittest, to be fit to survive, one has to adapt to the changing environment, or face extinction.
JPM is a game changer, the political environment has changed, wapinzani wameshindwa ku adapt to the changing environment, now they face extinction.

Kama aliyepo ndio huyo huyo mmoja, kama unataka kupotea kama Ben Saanane, endeleza mapambano, humu jf, utasifiwa sana!, lakini mwisho wake....lakini kama unataka ku survive, you have to join him!.
I've chosen to survive, I have joined them!.
P
 
Wengi wenu mmesoma lakini matokeo bure kabisa! Nina wasiwasi sana na elimu ya Tanzania kama hali ni hii. Umefundishwa lakini umetoka kapa! #BureKabisa

Kujifunza hakuishi eti kwasababu tu umetoka darasani. Utajifunza hadi unaingia kaburini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…